Wednesday, January 7, 2009

UVCCM WAWATISHA VIGOGO MAFISADI

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umepitisha azimio la kuwataka wanachama na viongozi wake wote kushiriki kikamilifu kuisaidia serikali kuwafichua viongozi wa CCM, jumuiya zake na serikali wanaojihusisha na vitendo viovu, ikiwamo kutumia madaraka vibaya.
Azimio hilo, ni katika maazimio saba yaliyopitishwa na Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Taifa la UVCCM katika kikao chake kilichofanyika chini ya Mwenyekiti wake, Hamad Masauni, mjini Zanzibar, Januari 2, mwaka huu.

Katibu Mkuu wa UVCCM, Francis Isack, alisema kupitia taarifa ya Umoja huo iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana kuwa maazimio hayo yalipitishwa baada ya kamati hiyo kujadili mambo mbalimbali yanayohusu Umoja huo.

Wanachama na viongozi wote wa UVCCM nchini kote washiriki kikamilifu kuisaidia serikali ya awamu ya nne chini ya uongozi shupavu wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, kuwafichua watu wote wanaojihusisha na vitendo viovu kama vile utumiaji mbaya wa madaraka kwa viongozi wa CCM, jumuiya za CCM na serikali,`` alisema Isack.

Alisema katika azimio hilo, wanachama na viongozi wa UVCCM pia, wametakiwa kuisadia serikali kuwafichua wanaojihusisha na mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi, maarufu kama maalbino.

Isack alisema kamati hiyo pia iliazimia kwamba, UVCCM itashirikiana na CCM mkoa na wilaya ya Mbeya wakati wote wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbeya Vijijini, unaotarajiwa kufanyika Januari 25, mwaka huu.

Katibu Mkuu huyo alisema katika maazimio hayo, UVCCM inaunga mkono kauli iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni ya kulaani mauaji yanayofanywa na majeshi ya Israeli dhidi ya Wapalestina wasio na hatia katika Ukanda wa Gaza, nchini Palestina kwa kisingizio cha kuwasaka, kupambana na kuwaangamiza wanamgambo wa kikundi cha Hamas.

UVCCM inatambua kuwa kila binadamu ana haki sawa na mwingine yeyote ya kuhakikishiwa uhai wake na kulindwa kwa gharama yoyote pale kunapokuwa na tishio lolote dhidi ya maisha yake, hivyo hata katika mazingira gani Israeli haina haki ya kufanya mauaji hayo ya kikatili dhidi ya raia yeyote wa Kipalestina,`` alisema Isack.

Alisema katika maazimio hayo, UVCCM inatoa salamu za rambirambi kwa Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, kutokana na kifo cha aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magogoni Zanzibar na pia inatoa mkono wa pole kwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusufu Makamba, kutokana na kifo cha Katibu wa chama hicho wilaya ya Uyui, mkoani Tabora na kuwaombea marehemu wote Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi.

Alisema kamati pia iliazimia kuandaa mkakati wa kujadili changamoto zinazoikabili taifa kutokana na maelekezo rasmi yaliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume kupitia hotuba zao za kufungua na kufunga Mkutano Mkuu wa Saba wa Vijana Taifa ili kuhakikisha UVCCM inatekeleza kikamilifu majukumu yake ya msingi.

Baadhi ya majukumu hayo, ni pamoja na kuwatumikia vijana wote nchini kwa vile UVCCM, ni jumuiya ya chama kilichopo madarakani na pia ndiyo nguzo kuu ya maendeleo ya nchi kisiasa, kiuchumi, kiulinzi, kijamii na kiutamaduni.


SOURCE: Nipashe

8 comments:

Anonymous said...

Corruption poses a serious development challenge. In the political realm, it undermines democracy and good governance by flouting or even subverting formal processes. This is a problem my country tanzania is facing.


Ngosha

Anonymous said...

Changing a few people and bringing new people in that look better than their predecessors, who have better abilities and better biographies, will be another solution. We need to change the faces of our political leaders. I always hear the same names and faces in our government and most are corrupted.

Anonymous said...

I can say nothing. But one thing is important. We brought many of our laws under pressure to bring them as fast as possible, and then we often use the method of imitation. We need to let our laws work as planned that is the only way we will overcome corruption in tanzania

Yunusu

Anonymous said...

Here there are great risks of corruption and from that comes the danger. Lets say, we have privatization processes, selling state assets, real estate and land, significant companies. Here, a single motion of a pen decides on values worth millions, if somebody will get rich, can depend on free will. Here i mean fisadi's for those who did not understand my writing.

Kagoda

Anonymous said...

Certainly, in tanzania the issue is that we retrospectively saw that in the past we made mistakes and that the mistakes were mainly that the procedure of privatization was hidden from the public, or at least not understandable for the public. Just remember the largest privatizations in tanzania, from banks to public companies. Here one thing is very clear, regardless if everything was totally clean or not

Anonymous said...

We will have to admit at one point that despite many illegalities, absolute immorality and bad politics in that view, we are faced with the fact that the times has passed to some polician and that we have to count on new faces.

Jk u'r doing good and i am sure you will suport me on this. You are vision is good but some people your working with are out of ideas and you need new faces with new and creative mind

Anonymous said...

sio wawatishe wadeal nao maana wanatuharibia chama. ndejembi we don't need dis people at all! unajua wanaweza kuwa walikisaidia chama kwa kipindi flani sasa hivyo vimisaada ndio vinavyowapa kiburi.
sasa please we can not be slaves just becouse ya hivyo vimisaada bt tukiendelea kuwakumbatia tuta haribu nchi nzima.

Maswega,
virginia
USA

Anonymous said...

wapitishe maazimio ya kuwakamata wote waliohusika ktk epa, kwanza watu hao ni wahujumu wa uchumi na ni wasaliti wa nchi kwa tafsiri ya mw. Nyerere kwamba tuliyemsomesha anapaswa kufanya kazi kwa manufaa ya taifa hawa wameyafanya hayo kwa manufaa yao binafsi, ndugu ndejembi hembu tumieni busara zenu bwana mdogo kukinusuru chama ninyi ndio vijana wenye nguvu na si tu kwamba mna elimu bali pia mmeelimika na pia mmejionea changuzi na utendaji wa vyama kama republican na democratic hapa usa

Uncle Steve.
Rome
Italy