Tuesday, February 8, 2011

Kauli ya Kamati Kuu ya CCM kuhusu Suala la Katiba Mpya

Kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichofanyika Dar es Salaam tarehe 20/1/2011 chini ya Uenyekiti wa CCM Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, ilijadili kwa makini suala la mahitaji ya Katiba mpya na imetoa kauli ifuatayo

Kamati Kuu ina mpongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano Dr. Jakaya M. Kikwete kwa kuzingatia ukweli kwamba Katiba iliyopo imefanya kazi vizuri kwa miaka 50, na hivyo kuelekeza kwamba ni kipindi kizuri cha kuitazama upya ili hatimaye ipatikane Katiba itakayotupeleka miaka 50 mingine ijayo.



Aidha, Kamati Kuu ina muunga mkono Mhe. Rais kwa hatua anayotarajia kuichukua ya kuunda Tume ya Kikatiba itakayokusanya maoni ya wananchi kuhusu masuala ya Katiba (Constitutional Review Commission). Kamati Kuu imesisitiza kwamba Tume hiyo ya Katiba iwe na mchanganyiko wa wananchi wa aina mbalimbali kama: wasomi, wakulima, wafanyakazi, Wafanyabiashara, Madhehebu ya dini, Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), pia makundi maalum kama vijana, wanawake, watu wenye ulemavu n.k. Aidha wakati ukifika wa Tume kuanza kazi itafaa ipewe muda wa kutosha ili ikusanye maoni mengi iwezekanavyo kutoka kwa wananchi wengi iwezekanavyo.

Kamati Kuu ilisisitiza mambo mengine yafuyatayo:-

· Kwamba elimu kwa umma kuhusu Katiba ya sasa itolewe ya kutosha ili kuwawezesha wananchi waelewe na ndipo watoe maoni wakiwa na uelewa kuhusu yaliyomo katika Katiba ya sasa.

· Kwamba Serikali itazame uwezekano wa kulishirikisha Bunge ili litunge sheria itakayoongoza utendaji kazi wa Tume ya Katiba, pamoja na kuelekeza Hadidu za Rejea za kazi ya Tume hiyo.

· Zoezi la kutoa elimu kwa umma kuhusu Katiba, na lile la Tume kukusanya maoni ya wananchi yapewe muda wa kutosha ili wananchi wengi iwezekanavyo watoe maoni yao kuhusu mambo gani yawemo katika Katiba ijayo.

· Kwamba mjadala kuhusu mambo gani mapya yaingie katika Katiba ijayo, na mambo gani yaliyomo katika Katiba ya sasa yaondolewe na yepi yabaki, sharti ufanywe kwa makini sana, bila jazba na bila ya vitisho wala mashinikizo kutoka kwa mtu yeyote au kikundi cho chote.

Kwa kifupi Kamati Kuu inawataka wananchi wajiandae kushiriki kwa ukamilifu katika mchakato wa mjadala kuhusu Katiba. Hii ni haki yao ya msingi. Jambo la kuzingatia ni kwamba mjadala huu uendeshwe katika hali ya amani na utulivu kama ilivyo jadi ya nchi yetu.

Imetolewa na:-


Capt. (Mst) John Z. Chiligati (Mb.),

KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,

ITIKADI NA UENEZI


Kwa habari hii zaidi na nyingine nyingi bofya hapa chini.
http://www.cms.ccmtz.org/index.php?section=news&cmd=details&newsid=122
Salum Rajabu
Katibu wa muda: Itikadi na Uenezi CCM-Marekani


Monday, February 7, 2011

SHEREHE YA KUAZIMISHA MIAKA 34 YA CCM. HOUSTON, TX.

Picha ya pamoja ya Wanachama wa Tawi na Viongozi wao Katibu akimkabidhi kadi mwanachama mpya.


Katibu wa Muda wa Itikadi na Uenezi akitoa nasaha zake


Katibu mkuu wa Muda akitoa kadi kwa mwanachama mpya
Viongozi wa Muda wa TAwi na Viongozi wa Shina no 1 Houston

Katibu wa Tawi wa Muda akimpongeza Mwenyekiti wa shina no 1 Houston Cassias Pambamaji mara tu baada ya ufunguzi wa shina hilo katika sherehe hizo

Da Zainab pia alikuwepo
Hongera mwanachama mpya
Hongera sana kwa kujiunga na CCM
Uongozi wa Shina na Tawi

Tuko Juu!
Juu zaidi!
CCM Oyee!
OYeee!
Mwenyekiti wa muda wa Tawi Novatus Simba akimpongeza mwanachama mpya mara baada ya kuchukua kadi yake
Kaka Juma Maswanya pia alikuwepo
Wanachama wakiwa na sura za Furaha
Ilikuwa ni furaha tupu
Hongera saaana!
Mwanachama mpya na Viongozi wa MudaMaswanya,Simba, Kitogo
Secky Adadi akichukua kadi kwa furaha tele

Kila mtu alikuwa happy!
Chacha Mussa Akipokea kadi yake
Hongera LBT!
Da zainab akiwa mwenye furaha tele
Katibu akitoa kadi kwa mwanachama mpya huku viongozi wengine wakiangalia
Green and Yellow!
Karibu sana kundini!