Wednesday, December 31, 2008

KHERI YA MWAKA MPYA.

Ndugu watanzani,
kwa niaba yangu, viongozi wenzangu pamoja na wanachama wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) tawi la Marekani napenda kuwatakia kheri na baraka kwa mwaka ujao wa 2009, na kwamba uwe ni mwaka wenye mafanikio makubwa kwa kila mmoja wetu na hatimae taifa kwa ujumla wake.
Aidha mwaka ujao uwe ni mwaka ambao sote kwa pamoja tutaunganisha nguvu zetu kama wananchi wa taifa moja makini kabisa bila kujali umbali toka tulipo mpaka Tanzania, itikadi zetu kidini, kichama au hata kikabila katika kuwasaidia viongozi wetu kutimiza malengo tuliyojiwekea kwa maendeleo yetu kama taifa tukiamini kwamba Tanzania kwanza mimi baadae.
Mwisho nawaomba watanzania sote kila mmja kwa imani yake kumuomba mwenyezi MUNGU kuliepusha taifa letu Tanzania katika majanga na dhoruba mbalimbali na kwamba nchi yetu iendelee kuwa yenye amani, utulivu na upendo miongoni mwa mataifa duniani.

MUNGU IBARIKI AFRIKA,
MUNGU IBARIKI TANZANIA
.

Asanteni sana,
Ndejembi Michael,
M/kiti.
Ni haki ya kila mmoja kukijua na kujivunia, kabla hata ya kwenda shule kile anachokiona kuwa ni cha maana kwake na kwa taifa lake. Pichani ni Mtoto Raphael akiwa amevalia tshirt yenye bendera ya marekani kama fahari kwake pia inaarifiwa kwamba mtoto huyu anazitambua rangi zote tatu zilizomo katika bendera ya nchi yake ingawa hajaanza shule bado.

Msomaji.
Houston tx.

Monday, December 29, 2008

Pichani mwenye mtoto ni Bi. Bristol Polin binti wa kwanza wa Governor wa Alaska Salah Polin aliyekuwa mgombea mwenza wa McCain akiga picha na moja wa jamaa zake wa karibu muda mfupi baada ya kujifungua. Bi Briston mwenye umri wa miaka 18 amepata mtoto wa kiume baada ya kujifungua jana na inaripotiwa kwamba mtoto huyo alizaliwa akiwa na uzito wa 7 pounds.

msomaji.
DC.

Picha nyingine iliyopigwa na Bw. J. Ayub- hili ni moja kati ya madaraja makubwa kabisa hapa nchini marekani kupata kujengwa katika miaka ya themanini.
Hii ni picha ya Governor wa Alaska Bi. Salah Polin aliyeteuliwa na Bw. McCain kuwa mgombea mwenza wa nafasi ya umakamu wa urais. Picha hii ilipigwa na Mtanzania Bw. Julias Ayub wa Ohio na kutumiwa katika kurasa ya mbele ya moja ya magazeti ya Ohio, tunakupongeza bwana Julias kwa kitendo chako cha kushujaa.

J. Ayub
Ohio.

Saturday, December 27, 2008

Moja kati ya nyenzo kuu na muhimu za maendeleo ya mwanadam ni elimu ambayo humuwezesha mwanadamu kuyatawala mazingira yake. pichani ni sanamu ya nyumba inayoonyesha eneo lilipangwa kujengwa nyumba litakavyoonekana mara baada ya ujenzi kukamilika.

Ndejembi Michael.
Hii ni moja kati ya picha nyingi zilizobandikwa nchini Ufaransa wakati wa kipindi cha uchaguzi zilizokuwa zikimuelezea Rais mteule wa Marekani Bw. Baraka Obama, (tafsiri ya maneno aliyoandikwa katika picha hii yanauliza, 'Obama ni nani'). Watabiri wa mambo wanadai kwamba rais Obama anaweza kuwa ndiye mtu maarufu na aliyetangazwa sana na vyombo vya habari duniani kote kwa mwaka 2008.

Ndejembi Michael.


Hata katika mabonde na miamba migumu jamaa wameweza kupitisha reli kama moja ya njia kuu za ushafirishaji wa bidhaa na abiria.

Ndejembi michael.
Hili ni moja kati ya moja ya madaraja ya reli hiyo ambayo yako katika ya moja ya mto iliko nchini korea. juu ya hili daraja ni barabara na chini ya hili daraja kuna kivuko.

Ndejembi Michael.
hata hivyo kukabiliana na ujenzi wa njia za usafiirishaji na hasa reli si kazi rahisi na hasa ikiwa eneo husika liko kwenye mabonde na vilima kwani reli inapaswa kuwa katika eneo ambalo ni tambarale.
lakini wakisukumwa na dhamira za dhati wa-korea wameweza kujenga reli zao kama picha hii inavyoonekana.
Ndejembi Michael.
Maendeleo ya kiuchumi katika nchi au jamii yeyote duniani hutegemea mambo mengi muhimu na moja kati ya hayo ni usafirishaji. Hii ni moja kati ya njia kuu za isafirishaji nchini korea ambazo zimesaidia sana ukuaji wa uchumi wa taifa hilo ambalo kwa sasa ni moja kati ya mataifa yenye nguvu kubwa za kiuchumi duniani.

Ndejembi Michael.

Friday, December 26, 2008

Salamu za mwaka mpya kutoka Chicago


Hivi ndivyo linavyoonekana jiji la Chicago-nyakati za usiku kipindi hiki cha sikukuu. Picha hizi zimepigwa jana usiku na mwakilishi wa jimbo la Illinois, Chicago. Ukitaka kuona vizuri bonyeza kwenye picha.
(Ahsante sana ndugu Johnson kwa salamu na picha hizi)

Wednesday, December 24, 2008

Uwe ni wakati mnzuri wa kutafakari yaliyopita, yaliyopo na yajayo kabla ya kuamua kipindi kijacho tuwe katika mtazamo gani.
Kwa niaba yangu, viongozi wenzangu na wanachama wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hapa Marekani tunapenda kuwatakia kila la kheri na baraka ya sikukuu hii ya Christmas watanzania wote popote pale walipo tukiwaombea afya njema, sikuku yenye amani na utulivu na furaha vitawale mnaposherehekea sikukuu hii

Mwenyekiti.

Tuesday, December 23, 2008

Mjumbe wa halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na naibu spika wa Bunge mama Anna Makinda akiwa katika picha ya pamoja na mlezi wa Chama Cha Mapinduzi upande wa Marekani Bw. juma Maswanya. Hii ilitokea muda mfupi baada mama Makinda kufanya mazungumzo na viongozi wa CCM Marekani wiki chache zilizopita jijini Houston - Texas.

Ndejembi Michael.
Haya ni majengo ya BOT, tumepokea email toka kwa mmoja wa wasomaji wetu akiomba yeyote anaejua haya majengo yanafanana na majengo gani duniani amjulishe kupitia matandao huu, ili kuondoa ubishi kati yake na wenzake.

Msomaji.

Monday, December 22, 2008

Kenya, Uganda fail US aid test again, Tanzania passes

Kenya and Uganda have once again been deemed ineligible for a special US development aid programme that is providing Tanzania with nearly $700 million over the next five years.According to “scorecards” issued last week, Kenya fails to qualify for the Millennium Challenge assistance because it falls short of an anti-corruption standard for the fourth consecutive year.That finding will have disappointed Foreign Minister Moses Wetang’ula.He stated in an interview during a September visit to the United Nations that US Secretary of State Condoleezza Rice had assured him that Kenya would soon be approved for a Millennium Challenge grant.In addition to failing the anti-corruption test that countries must pass in order to qualify for the aid, Kenya was judged to be lagging in regard to rule of law, immunisation rates, health expenditures and fiscal policy.The country was given passing grades on 12 criteria, including political rights and government effectiveness.Uganda is not entitled to receive Millennium Challenge funds because it meets one less than the minimal number of standards for potential eligibility.Uganda fails on measurements of political rights, civil liberties, immunisation rates, health expenditures, girls’ completion of primary education and fiscal policy.Tanzanian and American officials are meanwhile completing preparations for a Millennium Challenge programme aimed at greatly improving the country’s road and electricity networks.The scope of this initiative suggests that Kenya and Uganda could also receive substantial infrastructure aid if they were to pass the performance tests established by US monitors.The $698 million development assistance compact with Tanzania is the largest package of aid among 16 that have so far been approved for developing countries.The agreements total $5.5 billion, with more than half that amount going to eight countries in black Africa: Benin, Cape Verde, Ghana, Lesotho, Madagascar, Mali, Mozambique and TanzaniaFor more than a year, Kenya and Uganda have both been getting help from US officials on how to meet the necessary aid criteria.The two countries were accepted into a “threshold programme” designed to address problems that have prevented selected countries from qualifying for a full Millennium Challenge compact.Kenya was awarded $12.7 million for efforts to reduce corruption in the public procurement system.The Kenyan government had previously identified the Ministry of Health and its Kenya Medical Supplies Agency (Kemsa) as being “particularly susceptible to waste, fraud and abuse throughout the procurement and delivery process,” according to a Millennium Challenge report.The threshold programme has thus involved a series of workshops on public procurement reforms in which 43 Kenyan procurement entities have so far taken part.A review of Kemsa’s procurement practices has also been carried out.A Millennium Challenge status report on Kenya published last month says this assessment of Kemsa “marks a giant step forward in transparency.”Also as part of the Millennium threshold initiative, Kenyan procurement overseers took part earlier this year in a study visit to the Tanzania Public Procurement Regulatory Authority.The Tanzanians offered advice on how Kenya might improve its performance in this realm.Uganda’s $10.4 million threshold programme is focused on procurement reforms as well, with the added aim of improving the effectiveness of investigations by the National Fraud Squad.“Progress was sustained in mobilising civil society and the private sector in the fight against corruption,” according to a Millennium Challenge status report on Uganda.Tanzania has been undergoing its own threshold programme even though it has qualified for full Millennium Challenge assistance.This initiative “has provided critical assistance to sustain Tanzania’s anti-corruption reform movement,” a Millennium Challenge report says.It notes that 77 districts in the country have established public expenditure tracking systems while 360 villages now have notice boards on which residents can see income and expenditure information for their local areas.More than 150 prosecutors have recently been hired through the threshold programme as part of Tanzania’s efforts to pursue corruption cases more vigorously.

Msomaji.

CHRISTMAS IN WASHINGTON, D.C.

Horse drawn carriage ride
The Washington Monument (aka the Giant Pencil)
Night time view of the Lincoln Memorial from the Washington Monument
Night time view of the White House and the National Christmas tree from the Washington Monument
Night time view of the Capital from the Washington Monument
In case you were wondering this is not the White House
The National Christmas tree
The National Christmas tree and the Washington Monument (aka the Giant Pencil)
District of Columbia tree
The White House
The nativity by the National Christmas tree
Hivi ndivyo linavyoonekana jiji la D.C-nyakati za usiku na hasa kipindi hiki cha sikukuu. Picha hizi zimepigwa jana na mwakilishi wetu wa D.C.
JAMES-WASHINGTON, D.C

Sunday, December 21, 2008

ZANZIBAR NA UPEPO WAKE MUURUWA.

Hivi ndivyo inavyoonekana maadhari ya Zanzibar hasa kipindi hiki cha kuelekea sikukuu, aliyetutumia picha hii anadai kwamba hali ya uchumi inayoikabili dunia kwa sasa imeathiri hali ya mambo nchini Tanzania na kwamba inawalazimu kutegemea uvuvi badala ya kutegemea utalii pia ili kujikimu kimaisha.
Jumbe Ismail - Zanzibar.

UKAIDI HUU SI WAKUVUMILIWA.

Huu ni upande wa mbele wa kiwanda cha Brookside kilichopo Arusha - Tanzania kinachodaiwa kuwa ni cha kusindika maziwa, hata hivyo habari za kuaminika zinasema kwamba kiwanda hiki si cha kusindika maziwa na kwamba kimekuwa na kawaida ya kukusanya maziwa na kuyapeleka Kenya ili yasindikwe na kisha kuyarudisha Tanzania ili kuyatafutia masoko. Hivi karibuni waziri wa viwanda na biashara Dr. Mary Nagu alikipiga marufuku kiwanda hicho kwa madai hayo hayo hata hivyo agizo hilo lilipuuzwa kwa kile kilielezwa kwamba serikali ya Tanzania haiwezi kufanya chochote kwa kuwa kiwanda hicho kinamilikiwa na familia ya rais wa zamani wa Kenya Bw. Jomo Kenyatta. Mama Nagu upo?

Ndejembi Michael.

Saturday, December 20, 2008

JIJI LA NEW YORK, SIKU KABRA YA SEPITEMBA ILEVENI

Hivi ndivyo lilivyokuwa likionekana jiji la Manhattan NY, siku moja kabla ya tukio la september eleven wakati wa usiku . Picha hii imetumwa na msomaji wetu kutoka New York ambaye siku ya tukio alikuwa katika jengo la sita kulia kwa majengo mawili marefu kuliko yote yaliyoangushwa. Ukitaka kuona vizuri jengo alilokuwemo msomaji bonyeza kwenye picha.

Msomaji.

BAADA YA KUTUNUKIWA SHAHADA JK AREJEA

Rais Dr. Kikwete akiteta jambo na makamu wa kwanza wa rais Dr. Mohamed Shain alipokuwa akirejea toka Nairobi - Kenya. Kushoto kwa Dr. Shain ni mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Kandoro.

Ndejembi Michael.

MISS EAST AFRIKA HUYU HAPA.

Claudia Nuyimana akivishwa taji la Miss East baada kutwaa taji hilo jana ijumaa huko Burundi.

Msomaji.

BAHATI HAIKUWA YAKO.

Huyu ndiye bi. Lynette Lwakatale aliyeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss East Afrika, hata hivyo mambo hayakuwa mazuri kwake.

Msomaji.
Rais mteule wa Marekani Bw. Baraka Obama anaekabiliwa na changamoto ya kuinua uchumi wa taifa kubwa kabisa dunia la Marekani, hali ya mambo bado si shwari ndani ya Marekani na dunia nzima kwa ujumla kutokana na hali mbaya ya kiuchumi inayoikabili dunia kwa sasa.

Ndejembi Michael.

HIZI NDIZO ATHARI ZA KUPOROMOKA KWA UCHUMI

Hizi ndizo athari za kiuchumi zinazoikabiri dunia kwa sasa na inadhaniwa kuwa hari ni mbaya zaidi kwa nchi za dunia ya tatu ikiwemo Tanzania. Hiki ni moja kati viwanda vikubwa kabisa vya kutengeneza magari kilichopo Houston - Texas kikiwa na idadi kubwa ya magari bila kuwa na wanunuzi, idadi kubwa ya wamarekani kwa sasa wamepunguza kununua magari kutokana na wegi wao kupoteza kazi ama moja ya wanakaya kupoteza ajira.

Ndejembi michael.

HA! HA! HAAAA!, HII NDIO ATLANTA BWANA.

Hivi ndivyo linavyoonekana jiji la Atlanta - GA nyakati za usiku na hasa kipindi hiki cha sikukuu. Picha hii imepigwa jana usiku na mwakilishi wa Atlanta.

kisingino-Atlanta.

Friday, December 19, 2008

SIJIUZURU NG'OO - GOVERNOR BLAGOJEVICH.

Gov. Rod Blagojevich wa Illinois amekataa kujiuzuru kwa madai kuwa hana hatia, gov Blagojevich anayetuhumiwa kuhusika na kashfa ya rushwa katika kumtafuta mrithi wa senator Obama aliyechaguliwa kuwa rais wa Marekani amedai kuwa hana hatia na kwamba atapiganaia haki yake mpaka dakika ya mwisho.

Msomaji - Dallas.

KIKWETE ATUNUKIWA SHAHADA - NAIROBI

Rasi wa jamuhuri ya muunganowa Tanzania Mh. JK Kikwete akitunukiwa shahada ya heshima toka chuo kikuu cha Kenyatta kilichopo Nairobi nchini Kenya. Mkuu wa chuo hicho Dr. Harris Mulee ndie aliyemtunuku shahada hiyo katika mahafali ya 25 ya chuo hicho yaliofanyika leo chuoni hapo.
Ndejembi Michael.

KIKWETE AWAGEUKIA ATCL

Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete amerishutumu vikali shirika la ndege Tanzania (ATCL) kwa uzembe uliopelekea shirika hilo kufungiwa, na pia amemtaka waziri wa miundo mbinu Mh. Shukuru Kawambwa kukutana na menejiment ya shirika hilo ili kutatua tatizo hilo

Msomaji wetu.
Rais JK Kikwete akisalimiana na waziri mkuu Mh. Mizengo pinda jana mara baada ya kurejea toka msumbiji alikokwenda kwa ziara ya siku mbili, kulia kwa Mh. Pinda ni makamu wa rais Dr. shein na anayefuata baada ya Dr. shein ni Tanzania first lady mama Salma Kikwete.

Ndejembi Michael.
Hili ndilo jiji la dallas ndugu, kipindi kama hiki cha sikukuu jiji hili huonekana kama hivi hasa kipindi cha jioni

Masanja, Dallas.

Hatimae aliyekuwa katibu mkuu wa Wizara ya Fedha Mh. Gray Mgonja ameachiwa kwa dhamana jana katika mahakama ya Kisutu baada kutimiza masharti yaliyotolewa na mahakama hiyo. Kesi itaendelea kusikilizwa hapo baadae, katibu huyo mstaafu alitoa hati ya nyumba kadhaa pamoja na godauni linalokadiliwa kuwa na thamani ya Tsh 6.1 bilion.
Msomaji.

Thursday, December 18, 2008

Kansas city Power & light district

Hapa ni mjini Kansas City asubuhi ya leo kwenye kitongoji cha Kansas City Power & Light District. Kwa matukio zaidi kwenye hiki kitongoji bonyeza hapa http://www.powerandlightdistrict.com/ , tunakushukuru sana ndugu yetu kwa picha hii

Houston asubuhi hii.
Haya ndo mambo ya houston, huu ni moja kati ya minara mirefu hapa htown maarufu kama San Jacinto Monument.

HERRY MAKANGE AFARIKI DUNIA.

Mtangazaji na mpiga picha maarufu wa channel Ten na Dtv Bw. HERRY MAKANGE amefariki dunia kwa ajari ya pikipiki iliyotokea jana Kibaha - Pwani. Bwana Herry alikumbwa na mauti hayo alipokuwa njiani akitokea Nyumbani kwake Kibaha kuelekea maeneo ya Posta Mpya Jijini Dar es salaam jirani na ziliko ofisi za DTV anakofanya kazi.
Uongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Tawi la Marekani unatoa pole nyingi kwa ndungu jamaa na marafiki wa bwana HERRY MAKANGE, na MUNGU ailaze pema peponi roho ya marehem. Amen.
Ndejembi Michael.

Wednesday, December 17, 2008


Hawa ndio wamatumbi walionitumia picha, wanadai wao ni wamarekani wenye asili ya tanzania ndio maana wanazo picha nyingi tu zinazoihusu tanzania. Na wanasema watakuwa wadau wakubwa wa blog hii ya CCM.
Na nyingine hii hapa, hawa jamaa wanatembea na hizi picha na nyingine nyingi tu za mambo mbalimbali ya bongo. Sijui kama hata wabongo wenyewe wanaweza kufanya hivyo sio kwa aajiri ya kuwaonyesha watu mbalimbali bali kama fahari yao iwe kwenye simu za mkononi, screen sever au mahala pengine popote.
Msomaji.