Wednesday, April 27, 2011

TAREHE YA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA TAWI

Ndugu Wanachama wa Chama cha mapinduzi,
Ufuatao ni utaratibu wa mwisho katika kukamilisha mchakato mzima wa uchaguzi wa viongozi wa Tawi letu;

Siku ya Mwisho ya kuchukua na kurudisha fomu za maombi ya uongozi ni Jumapili, Tarehe 8 may 2011.

Na siku ya uchaguzi wa viongozi ni Jumapili, tarehe 22 may 2011.

Tafadhari hakikisha umepata kadi na umelipia ada yako ya mwaka kabla ya siku ya uchaguzi, kwani ni wanachama hai tu watakaoruhusiwa kushiliki katika uchaguzi huu.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI,

ABDALLAH NYANGASA,

KAIMU KATIBU MKUU

TAWI LA CCM MAREKANI.

Saturday, April 9, 2011

UCHAGUZI WA VIONGOZI WA TAWI LA MAREKANI

Kidumu Chama Cha Mapinduzi!!

Habari za leo ndugu wanachama,

Wakati muhimu katika kulijenga na kuliendeleza Tawi letu umewadia. Uchaguzi wa viongozi wa Tawi watakaosukuma mbele maendeleo ya tawi na chama chetu umekaribia. Fomu za uchaguzi zitaanza kutolewa leo, zoezi hili la kuchukua na kurudisha fomu litakuwa kwa muda wa wiki mbili kuanzia leo. Tarehe ya uchaguzi itatangazwa ndani ya kipindi hiki cha uchukuaji na urudishaji fomu.

Nafasi zitakazogombewa nikama ifuatavyo:

1. Mwenyekiti wa CCM wa Tawi

2. Wajumbe kumi wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Tawi

3. Katibu wa CCM wa Tawi

4. Katibu wa Siasa na Uenezi wa Tawi

5. Katibu wa Uchumi na Fedha wa Tawi

Ili kuweza kushiliki kikamilifu katika uchaguzi huu kwa kugombea au kupiga kura, hakikisha kwamba una kadi yako ya chama,pia uwe mwanachama hai kwakulipia mchango wa kadi wa kila mwaka kama kadi yako ina muda wa zaidi ya mwaka. Kwa wanaohitaji kadi, kadi zinapatikana kwa kiasi cha $10, na mchango wa kadi wa kila mwaka ili kuwa mwanachama hai ni $25. Malipo yanaweza kufanyika kupitia uongozi wa muda.

Fomu za uchaguzi zipo tayari na zinapatikana kutoka kwa viongozi wa muda kupitia njia za mawasiliano hapo chini ya habari hii.

Anwani ya muda:

7447 Harwin drive ste 220B, Houston, TX 77036.

Namba za simu za viongozi wa muda wa Tawi:

Novastus Simba – Mwenyekiti 832-208-8344

Abdalla Nyangasa – Katibu Mkuu 832-537-11694

Misso Temu - Katibu wa Uchumi na Fedha 281-995-0019

Salum Rajabu – Katibu muenezi wa Tawi 832-524-9608



Salum Rajabu
Katibu wa Siasa na Uenezi wa Tawi