Thursday, May 28, 2009

SALAAM KUTOKA KWA MSOMAJI WETU DAR ES SALAAM

Msomaji wetu wa dar anatuma salaam kwa watanzania wote waliopo nje na ndani ya nchi na anependa kwa wote waliopo nje ya jiji la dar es salaam wajionee jii kulivo kwa sasa. Pia amehaidi kuwa ataendele na utaratibu huu wa kuwatumia picha za jiji la dar hili mkumbuke nyumbani

BONYEZA KWENYE PICHA HILI UJIONEE VIZURI

Makutano ya barabara pale maeneo ya nyumba ya Sana karibu na hotel ya Movenpic a.k.a
Shellaton Hotel

Hii ni hotel ya Movempick hiliyopo jijini dar zamani hilikuwa inaitwa shellaton hotel

Maeneo ya pakingi mjini
Hili jengo linaitwa JMMALL a.k.a Harbour View kwa mbele Hili jengo linaitwa JMMALL a.k.a Harbour View kwa pembeni
Maeneo ya Msaki
Uwanja wa ndege wa kimataifa wa jijini dar es salaa "Julius Nyerere International Airport"
Hii inaitwa new world Cinema karibu na maeneo ya maji machafu
Hili ndio lile jengo la Peugeot House
Hapa ni Ohio Street pale dar sio u.s.a
Hili ni Jengo la PPF Tower lilipo karibu na jengo la Air Tanzania (nitawatumi picha zake siku nyingine hili mkumbuke shilika lenu la ndege)
Hapa ni mitaa ya karibu na Sulender
Hii ndio Shopers Plaza Pale maeneo ya zamani Driven Cinema

Hili ndio jengo la Ubungo Plaza
Jengo hili lipo maeneo ya mjini
Jengo hili lipo maeneo ya karibu na kivukoni upande wa mjini
Majengo ya Quality Plaza
Hii ni Mimani city hiliyopo maeneo ya mwenge
May Fair Plaza Shopping Centers ya Dar hiliyopo karibu na maeneo ya Tanesco kuelekea Mikocheni
Jengo hili linaitwa Mkapa Tower a.k.a Mafuta House lipo maeneo ya posta Mpya
CCM nchini Marekani inatoa shukrani kwa niaba ya wasomaji na watanzania wote kwa ujumla
Mwenyekiti
Michael Ndejembi

MAMA ANNA KILANGO APOKEA ZAWADI KWA WINGI!!!

Mama Anna Kilango Malecella akipokea kikombe kutoka kwa Mohamed Raza
Mbunge huyu Mahariki Anne Kilango Malecela, akiendela kunemeka baada ya watu mbalimbali kuendelea kumtuza tuzo Mama Kilango akikabidhiwa traksuti.
Mama Malecella akiondoka kwa furaha baada yakupewa zawadi.


Mbunge wa Jimbo la Same Mahariki Anne Kilango Malecela, ameendelea kunemeka baada ya watu mbalimbali kuendelea kumtuza tuzo mbalimbali kwa ajili ya kuwa mwanamke Mbunge anayepambana na mafisadi ambao wanaifilisi nchi kwa kutoa hoja zinazohusu utetezi wa wanyonge Bungeni.
Leo Mbunge huyo amepokea vifaa vya michezo vyenye thamni ya Shilingi milioni 1.5 toka kwa mfanyabiashara maarufu wa Zanzibar na Mpenda michezo Mohamed Raza akimkabidhi vifaa hivyo alisema kuwa yeye anaungana na wengine wakiwamo Wamarekeni walio mtuku tuzo ya mama jasili wa kupambana na Ufisadi vifaa hivyo ni pamoja na Trakisuti, soksi , jackets, mipira 20 nk. Msaada huo ulikabidhiwa katika ukumbi wa idara habari na Maelezo leo asubuhi majira ya Saa 5. Raza alisema kuwa vifa hivyo ni mali yake mbunge huyo wa Same Mashariki na wananchi wake.
Msomaji

Tuesday, May 26, 2009

WAZIRI WA JINSIA AWAPONGEZA WANAWAKE WALIOSHINDA BUSANDA NA MAGOGONI ZANZIBAR

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mh. Magreth Sita

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mh. Magreth Sita akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo wakati alipotoa pongezi leo kwa wabunge wawili wanawake wa CCM walioshinda katika majimbo ya uchaguzi ya Busanda mkoani Shinyanga Frolensia Bukwimba na Magogoni Zanzibar Asha Muhamed Hillar.

Amesema ushindi wa wabunge hao unawapa faraja wanawake wote na kuonyesha kuwa sasa jamii inaanza kuwakubali wanawake na mchango wao kwa taifa letu, hivyo akawataka wanawake wote kuwa kitu kimoja na kujituma zaidi katika kazi ili waweze kuaminiwa kama wabunge hawa wawili walioshinda katika majimbo ya uchaguzi ya Busanda Tanzania Bara na Magogoni Zanzibar.
Msomaji
Dar es salaam

Monday, May 25, 2009

RAIS JAKAYA KIKWETE AREJEA KUTOKA MAREKANI

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na viongozi mbalimbali katika uwanja wa ndege wa mwalimu J. K. Nyerere mara baada ya kurejea akitokea nchini Marekani alikokwenda kwa Ziara ya wiki Moja ya kikazi waliopo katika picha kuanzia kushoto ni Waziri mkuu Mizengo Pinda na Makamu wa Rais Dr. Ally Mhamed Shein.

Msomaji


BREAKING NEWS!!!!!!!!

CCM WASHINDA UCHAGUZI BUSANDA
Mgombea wa CCM, Lolensia Bukwimba ameibuka kidedea



Matokeo Rasmi
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukwimba, Dan Mollel ametangaza matokeo rasmi ya Uchaguzi mdogo. Mgombea wa CCM, Lolensia Bukwimba ameibuka kidedea.

Matokeo ni kama ifuatavyo:
Waliojiandikisha............. 135,000 na ushee
Waliojitokeza ....................55,000 na ushee
CCM ............................29,242
CHADEMA...................22,764
CUF..................................827
UDP..................................327

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Shughuli haikuwa mchezo Busanda!!!!

Upigaji kula ulikuwa ni wawazi kwa kila mwanachama
Mh. John Pombe Magufuli akifanya vitu vyake
Maelfu Ya Wanachama Wa CCM mikono juuMamia ya wanachama wa vyama vya upinazani nao walikuwepo kushuudia tukio zima Helikopta Ya CCM nayo ilikuwepo

JIONEE ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NCHINI MAREKANI MH.MIRAJI MALEWA- WASHINGTON DC ILIVYOKUWA

Katibu alikutana na mama yake Hasheem Thabeet pamoja na mwanae. Pia watanzania wengine walifanikiwa kukutana na katibu akiwemo mkurugenzi wa blog ya jamii, bwana Issa Michuzi
waTanzania wakiwa na katibu ( kulia) . Pia mkurugenzi wa blog ya jamii bwa.Issa Michuzi (pili kulia) naye alikuwepo
Nyota wa filamu Chris Tucker (kati) alipokutana na katibu mkuu Miraji Malewa(kushoto) ambaye tayari ameisharejea makao makuu ya chama Houston Teaxas kuendeleza shughuli za chama.

HAFLA YA CHAKULA CHA JIONI KWA WASHIRIKI WA MKUTANO MKUU WA TANR.

Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo akitoa hotuba yake.
Kundi la wamaasia wakicheza ngoma ya kimila ya kwao. Huyu anaruka utafikiri anadanki mpira, hata Kobe Bryant na LeBron James hawaoni ndani
Wazungu ambao wanahudhuria katika mkutano wa 34 wa Tanzania National Reinsurance Corprotation TAN-RE , wakifuatilia kwa makini mchezo wa wamasai ambao walikuwa wakitumbuiza kwa sanaa yao.
Waziri wa Fedaha na Uchumi Msatafa Mukuro akiteta jamboa na baadhi ya washiriki wa mkutano wa 34 wa Tanzania National Reinsurance Coproration (TAN-RE) wakati wa hafal ya chakula chanjioni iliyofanyika katika Hoteli ya Moven Pick, (kushoto) Mohamed Sumar (watatu) ni Mwenyekiti wa Crown Holdings Limited Abubaker Ibrahim na Makamo Mwenyekiti wa Tanzania National Reinsurance Coopration Wilson Ndesanjo.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa 34 wa Tanzania National Reinsurance Corproration (TAN-RE) wakila dunia na kubadilishana mawazo wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichofanyika katika Hoteli ya Moven Pick , jiji Dar es Salaam, Mkutano huo umezinduliwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda leo katika ukumbi wa Hoteli ya Ubungo Plazza.


Msomaji
Dar es salaam

CEO ROUNDTABLE YATOA MILIONI 17.5 KUSAIDIA MAFUNZO YA KUPAMBANA NA UHALIFU KWA KUTUMIA MTANDAO

Afisa Mtendaji mkuu wa CEO Roundtable of Tanzania Ally Mufuruki kushoto akikabidhi mfano wa cheki yenye thamani ya shilingi milioni 17.5 kwa Kamishna Samson Kasala ambaye ni msaidizi wa DCI kwa ajili ya kusaidia mafunzo ya askari wapelelezi 20 watakaopata mafunzo jinsi ya kupambana na uhalifu kwenye mtandao kwa kutumia kompyuta, makabidhiano hayo yamefanyika katika makao makuu ya Wizara ya mambo ya ndani leo hii, katikati ni Mkurugenzi wa Tanconsurt Ltd George Ally
Mkurugenzi wa Tanconsurt ambaye pia ni miongoni mwa viongozi wa juu wa tasisi ya CEO Roundtable of Tanzania akiongea na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika Wizara ya Mambo ya Ndani wakati taasisi hiyo ilipokabidhi mfano wa cheki yenye thamani ya shilingi milioni 17.5 kwa ajili ya kusaidia mafunzo ya maafisa wa upelelezi katika kupambana na uhalifu wa kutumia Mtandao katika kompyuta yaani Cyber Crime katikati ni afisa mtendaji mkuu wa CEO Roundtable of Tanzania na mwisho ni Kamishna Samson Kasala msaidizi wa DCI.

Saturday, May 23, 2009

Tanzania to get more United States of America support

US has reaffirmed its support to Tanzania in health, education and agriculture. It has also pledged to work with other partners to solve conflicts in Africa.

Those were among issues discussed President Jakaya Kikwete met and his host President Barack Obama in Washington on Thursday. Mr Kikwete becomes the first African head of state to meet the US President.

Mr Obama was elected president last year and was sworn in on January 20 this year. A short statement about the meeting between the two leaders made available by the US embassy in Dar es Salaam yesterday, noted that the two presidents had "a valuable discussion on a range of issues."

"President Obama expressed his appreciation for the close bilateral relationship the United States shares with Tanzania,� reads part of the statement emailed to The Citizen.

The two presidents exchanged views on approaches to enhance US-Tanzania partnership on improving development policy.

According to the statement, the two leaders expressed desire to work together to solve common problems in future. Earlier, President Kikwete met US Secretary of State Hillary Clinton.

In her remarks, Mrs Clinton described Tanzania as �a country that has made so much progress and has an extraordinary potential that we wish to partner with and assist in every way possible.

" President Kikwete thanked the US for continued support, saying: "I'm here to reaffirm our commitment for continued cooperation and friendship.

" He said Tanzania and US had excellent relations on political and bilateral levels as they "see eye-to-eye on many international issues.

" The meeting between the two presidents had, however, attracted both optimism and caution from across sections of business, political and civil society officials in Tanzania.

Opinion on the expectations from the highly publicised meeting was sharply divided, with some interviewees viewing it as an opportunity for the country to exploit for prosperity while others felt the nation should not expect much from the meeting.

The executive director of the Tanzania Investment Centre, Mr Emmanuel ole Naiko, said the country stood to benefit from the investor confidence that was likely to be boosted by the meeting between Mr Kikwete and Mr Obama.

He said Mr Kikwete's recent trips to the US had helped raise the levels of American investments in the country.

Friday, May 22, 2009

President Barack Obama meets with Tanzania President Jakaya Kikwete in the Oval Office Thursday, May 21, 2009. This was the President's first meeting with an African Head of State. Right is US Secretary of State Sen, Hilary Clinton




Tanzania President Jakaya Mrisho Kikwete waves as he leaves the White House in Washington,DC, after meeting with US President Baraka Obama

HII INAMAANA GANI KWA TANZANIA NA WATANZANIA?

Rais JK akiwa katika picha ya pamoja na watanzania waishio LA- CA
Jumanne wiki hii rais JK aliwasili hapa Marekani kwa ziara ya kikazi ya wiki moja
rais alianza ziara yake jiji Los Angeles ambako pamoja na mambo mengine alipata nafasi ya kuzungumza na watanzania waishio hapo na maeneo ya jirani ingawa kuna taarifa kwamba baadhi ya watanzania walisafiri kutoka miji ya mbali kabisa kwenda LA kumsikiliza Mh. kikwete.
Akiongea na watanzania hao rais alizungumzia suala linalowasumbua vichwa watanzania wengi nalo si lingine ila ni lile la kuwa na uraia wa nchi mbili kwa watanzania wanaoishi nje ya tanzania.


Mh. Kikwete alipokuta na waziri wa mambo ya nje wa Marekani sen Hilary Clinton

Ingawa rais alizungumzia mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuwataka watanzania waishia nje kujishughulisha zaidi kuzisaidia familia zao zilizoko Tanzania na masuala ujenzi wa shule na shughuli nyingine za maendeleo kuiachia serikali suala la kuwa na uraia wa nchi mbili kwa watanzania waishio nje ya nchi limeonekana kupewa uzito zaidi kutokana na ukweli kwamba linawakosesha fursa nyingi watanzania wengi waishio nje ya Tanzania ambao kwa namna moja au nyingine wangeweza kuzitumia nafasi hizo za maendeleo kuisaidia nchi yao.


rais wa Marekani bwana Baraka Obama akimsikiliza Mh. Kikwete.
Rais alisema kwamba suala hilo halikupokelewa vizuri na baadhi ya watanzania walioko Tanzania ikiwa na pamoja na wasomi ambao kwa namna moja au nyingine walitegemewa kuwa kwanza kuuona mchango ambao ungetolewa na watanzania hao walioko nje ikiwa watazitumia vyema fursa hiyo ya kuwa na uraia wa nchi mbili.

Lakini haya yote sio yaliyonifanya kuandika makala hii ila dhana nzima iliyobeba dhamila ya dhati ya ujio wa Mh. JK Kikwete kama rais wa Tanzania hapa Marekani.
JK amekuwa rais wa kwanza toka Afrika kupata mwaliko toka kwa Bw. Baraka Obama ambae ameingia ikulu ya Marekani akiwa kama rais takribani miezi minne hivi na akiwa bado na mambo mengi muhimu ya kufanya ameweza kuikumbuka Tanzania na kumwita rais Kikwete ikulu hapo. Hii inaonyesha kwamba suala kukutana na JK lilikuwa ni moja kati ya mambo muhimu kwake na serikali yake ndio maana amefanya hivyo.


Baraka Obama pamoja na Hilary Clinton wakipata maelezo toka Kikwete.
Ingawa ndani ya Tanzania kuna baadhi ya watanzania bila kujali idadi yao wala itikadi zao kichama wanaulaumu kwa namna moja au nyingine utawala wa rais JK kikwete na Chama tawala nje Tanzania inaonekana ni nchi ya kuigwa na nchi nyingine za Afrika na kwingineko. Labda tu niulize mwonekano huu wa Tanzania na heshima kubwa kama hii inatokana na nini hasa kama si utawala bora na wenye tija kwa taifa la Tanzania?


Rais Kikwete akikaribishwa ikulu ya Marekani na bw. Baraka Obama jana.
Tanzania kama nchi nyingine yoyote ile inamatatizo tena mengi tu ambayo kimsingi hata atawale nani katu hatoweza kuyamaliza, japo yapo pia matatizo ambayo ni kwa uzembe tu wa baadhi ya watendaji wa serikali wameshindwa kuyatatua. Watanzania lazima tujivunie heshima tunayopewa na mataifa mengine ya nje kama Marekani. Tutambue kwamba mwaliko aliopewa Mh. rais kikwete ni heshima kwa kikwete mwenyewe, Chama Cha Mapinduzi ambacho kikwete ndie mwenyekiti wake, Tanzania na watanzania.

Michael Ndejembi.