Friday, May 22, 2009

HII INAMAANA GANI KWA TANZANIA NA WATANZANIA?

Rais JK akiwa katika picha ya pamoja na watanzania waishio LA- CA
Jumanne wiki hii rais JK aliwasili hapa Marekani kwa ziara ya kikazi ya wiki moja
rais alianza ziara yake jiji Los Angeles ambako pamoja na mambo mengine alipata nafasi ya kuzungumza na watanzania waishio hapo na maeneo ya jirani ingawa kuna taarifa kwamba baadhi ya watanzania walisafiri kutoka miji ya mbali kabisa kwenda LA kumsikiliza Mh. kikwete.
Akiongea na watanzania hao rais alizungumzia suala linalowasumbua vichwa watanzania wengi nalo si lingine ila ni lile la kuwa na uraia wa nchi mbili kwa watanzania wanaoishi nje ya tanzania.


Mh. Kikwete alipokuta na waziri wa mambo ya nje wa Marekani sen Hilary Clinton

Ingawa rais alizungumzia mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuwataka watanzania waishia nje kujishughulisha zaidi kuzisaidia familia zao zilizoko Tanzania na masuala ujenzi wa shule na shughuli nyingine za maendeleo kuiachia serikali suala la kuwa na uraia wa nchi mbili kwa watanzania waishio nje ya nchi limeonekana kupewa uzito zaidi kutokana na ukweli kwamba linawakosesha fursa nyingi watanzania wengi waishio nje ya Tanzania ambao kwa namna moja au nyingine wangeweza kuzitumia nafasi hizo za maendeleo kuisaidia nchi yao.


rais wa Marekani bwana Baraka Obama akimsikiliza Mh. Kikwete.
Rais alisema kwamba suala hilo halikupokelewa vizuri na baadhi ya watanzania walioko Tanzania ikiwa na pamoja na wasomi ambao kwa namna moja au nyingine walitegemewa kuwa kwanza kuuona mchango ambao ungetolewa na watanzania hao walioko nje ikiwa watazitumia vyema fursa hiyo ya kuwa na uraia wa nchi mbili.

Lakini haya yote sio yaliyonifanya kuandika makala hii ila dhana nzima iliyobeba dhamila ya dhati ya ujio wa Mh. JK Kikwete kama rais wa Tanzania hapa Marekani.
JK amekuwa rais wa kwanza toka Afrika kupata mwaliko toka kwa Bw. Baraka Obama ambae ameingia ikulu ya Marekani akiwa kama rais takribani miezi minne hivi na akiwa bado na mambo mengi muhimu ya kufanya ameweza kuikumbuka Tanzania na kumwita rais Kikwete ikulu hapo. Hii inaonyesha kwamba suala kukutana na JK lilikuwa ni moja kati ya mambo muhimu kwake na serikali yake ndio maana amefanya hivyo.


Baraka Obama pamoja na Hilary Clinton wakipata maelezo toka Kikwete.
Ingawa ndani ya Tanzania kuna baadhi ya watanzania bila kujali idadi yao wala itikadi zao kichama wanaulaumu kwa namna moja au nyingine utawala wa rais JK kikwete na Chama tawala nje Tanzania inaonekana ni nchi ya kuigwa na nchi nyingine za Afrika na kwingineko. Labda tu niulize mwonekano huu wa Tanzania na heshima kubwa kama hii inatokana na nini hasa kama si utawala bora na wenye tija kwa taifa la Tanzania?


Rais Kikwete akikaribishwa ikulu ya Marekani na bw. Baraka Obama jana.
Tanzania kama nchi nyingine yoyote ile inamatatizo tena mengi tu ambayo kimsingi hata atawale nani katu hatoweza kuyamaliza, japo yapo pia matatizo ambayo ni kwa uzembe tu wa baadhi ya watendaji wa serikali wameshindwa kuyatatua. Watanzania lazima tujivunie heshima tunayopewa na mataifa mengine ya nje kama Marekani. Tutambue kwamba mwaliko aliopewa Mh. rais kikwete ni heshima kwa kikwete mwenyewe, Chama Cha Mapinduzi ambacho kikwete ndie mwenyekiti wake, Tanzania na watanzania.

Michael Ndejembi.

1 comment:

Anonymous said...

Kwanza naanza kwa kuwalaumu waendeshaji wa huu mtandao kwa kutoruhusu maoni yetu kama mlivyokuwa mkifanya hapo mwanzo.

Pili nawapongeza kwa juhudi zenu maana sisi tulio wengi tumendeleea kupata habari kupitia huu mtandao wenu.

Tatu kuhusu mjadala wako bwana Ndejembi, binafsi nakubaliana na wewe kwamba Tanzania sasa hivi inapewa heshima kubwa ulimenguni lakini ninachopendekeza ni kwamba tutumie nafsi hii kuwaendeleza watanzania walio wengi sio tu wale waliopo madarakani.

Nne nampongeza Mh. rais Kikwete kwa juhudi zake katika kuendeleza utawala bora na kulitangaza taifa letu.