Sunday, May 3, 2009

WAHANGA WA MABOMU WAANDAMANA NA MABANGO, WAMTAKA WAZIRI MKUU!!

Wakazi wa Mbagala kuu wakiandamana na mabango yao baada ya kutoridhishwa na ugawaji wa vifaa hivyo kwa wahanga wa mabomu, kutokana na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa katika eneo hilo kushindwa kushirikiana vizuri katika kusimamia zoezi hilo, wakazi hao wamesema katika hali isiyo ya kawaida kuna hata baadhi ya viongozi wa kitaifa wa wametembelea eneo hilo na kugeuza ni sehemu ya kampeni, badala ya kusaidia wananchi wenye matatizo kwa wakati huu, katika eneo hilo wajumbe wengi wa nyumba kumi wanatoka chama cha CUF wakati Diwani wa kata hiyo anatoka CCM hivyo wakazi hao wanasema ushirikiano umekuwa mdogo kutokana na kila mtu anavutia kwake lakini sisi wananchi tunahitaji huduma kwa sasa hiyo siasa haitusaidii kwa kipindi hiki zaidi ya kutuumiza tu ukizingatia kuwa mvua inanyesha kwa wingi
Kijana mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja akifoka mbele ya Polisi na kusema "magodolo yanapelekwa kijichi badala ya kutupatia sisi wenye matatizo" kama unavyoona mabango waliyoshika jinsi yalivyandikwa.
watu mbalimbali wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe unaomuomba Waziri mkuu Mizengo Pinda kwenda tena katika eneo hilo, kutokana na ufisadi unaofanywa na viongozi wa mtaa na kata yao kwa vifaa mbalimbali vilivyotolewa kama msaada kwa wahanga wa tukio hilo watu hao wamesea vifaa vinapelekwa kwenye majumba na kusiko julikana badala ya kuwapatia watu walioathirika ili viweze kuwasaidia.
Wafanyakazi wa chama cha msalaba mwekundu wakiwa katika eneo la tukio kwa ajili ya kutoa misaada mbalimbali kwa wahanga wa tukio hilo. Mahema yakiwa yamejengwa katika maeneo ambayo wakazi wa mbagala kuu wameathirika na mabomu baada ya nyumba zao kuteketea kutokana na milipuko hiyo iliyotokea siku tatu zilizopita chama cha msalaba mwekundu kimeendelea na zoezi la kutoa misaada katika maeneo hayo japokuwa limekuwa gumu kwa kiasi fulani matatizo ya baadhi ya viongozi wa vyama na serikali katika kata hiy .

Msomaji
Dar es salaam

No comments: