Waziri wa afya Mh. David Mwakyusa akikaribishwa na mganga mkuu wa Hospitali ya Amana Dr. Willy Sangu. Waziri Mwakwisa alifika Hospitalini hapo kuzindua maabara ya kisasa iliyojengwa na mfuko wa Abbot Fund kwa niaba ya wananchi wa Marekani.
Waziri David Mwakyusa ambae ni waziri wa afya na na Ustawi wa Jamii akizindua rasmi maabara mpya na ya kisasa iliyojengwa kwa msaada wa mfuko wa Abbot Fund katika Hospitali ya Amana jijini Dar es salaam.
Mwandaaji wa uzinduzi huo Matina Nkurlu kushoto akizungumza na mmoja wa wageni waliokuwepo katika uzinduzi huo aliyekuwa akipiga picha tukio hilo FULLSHANGWE haikufanikiwa kunasa jina lake mara moja lakini ilivutiwa na uratibu wake jinsi alivyokuwa akipanga mikakati ya upigaji picha wakati wa zoezi hilo ili kuhakikisha matukio yote yanapatikana katika kumbukumbu.
Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Maabara ya kisasa iliyojengwa kwa msaada wa shirika la Abbott Fund la Marekani Prof. David Mwakyusa akizungumza na wageni mbalim bali waliohudhuria katika uzinduzi huo. Waziri wa afya Mh. David Mwakyusa akikagua moja ya vifaa vilivyomo katika maabara mpya ya Hospitali ya Amana jijini Dar es salaam.
Makamu wa rais wa Abbott Fund Tanzania Bi. Christy Wistar akizungumza katika uzinduzi huo ambao ulifanyika katika Hospitali ya Amana.
Mganga mkuu wa Hospitali ya Amana Dk. Willy Sangu akiongozana na waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii pamoja na Mbunge wa Ilala Mh. Mussa Azan Zungu kwenda kuzindua rasmi maabara hiyo.
Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa wamekaa tayari kwa kushuhudia uzinduzi huo
Brass Band ya Polisi nao walikuwepo wakifanya vitu vyao kabla ya kuanza rasmi kwa shughuli za uzinduzi wa maabara hiyo ya kisasa iliyojengwa katika Hospitali ya Amana kwa msaada wa shirika la Kimarekani la Abbott Fund nchini leo

Msomaji
No comments:
Post a Comment