Thursday, December 31, 2009

RAIS JAKAYA AKITANGAZA RASMI KIFO CHA SIMBA WA VITA IKULU LEO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitangaza Rasmi kifo cha Mzee Rashid Mfaume Kawawa mapema leo, Rais pia ametangaza siku saba za maombolezo kwa nchi nzima na bendera zitapepea nusu mlingoti kwa muda wa siku hizo saba mipingo mingine ya Serikali inaendelea juu ya utaratibu wa mazishi na wakati wowopte itatangaza utaratibu huo.

Rais Kikwete alipomtembelea Mzee Kawawa Hospitali ya Muhimbili

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakimjulia hali Mzee Rashid Mfaume Kawawa aliyelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili jana jioni

SALAMU ZA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE ZA MWAKA MPYA KWA WANANCHI

SALAMU ZA MWAKA MPYA ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, KWA WATANZANIA,
TAREHE 31 DESEMBA, 2009


Utangulizi
Ndugu Wananchi;
Kama ilivyo ada naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uhai na kutuwezesha kufika siku ya leo ya kuuaga mwaka 2009 na kuukaribisha mwaka 2010. Wapo wenzetu wengi tulioanza nao mwaka lakini hawakujaaliwa kuwa nasi siku hii ya leo kwa kuwa wametutangulia mbele ya haki. Tunamuomba Mwenyezi Mungu awape mapumziko mema. Kwa wenzetu wanaougua tuwaombee awape nafuu ya haraka ili waendelee kutoa mchango wao katika maendeleo yao, jamii zao na taifa zima kwa jumla. Aidha, tuendelee kuomba rehema za Mola wetu atujaalie afya njema na umri mrefu ili tuweze kuushuhudia mwaka wote wa 2010 na miaka mingine mingi ijayo.

Ndugu Wananchi;
Kama wote mlivyosikia, leo, siku ya mwisho ya mwaka 2009, Taifa letu lilipata msiba mkubwa wa kuondokewa na Mzee wetu, Mzee Rashid Mfaume Kawawa, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu.

Kama nilivyoeleza wakati nalitangazia taifa kifo chake, huu ni msiba mkubwa kwa Taifa letu. Tumepoteza mmoja wa viongozi mashuhuri. Marehemu alijitoa muhanga kupigania uhuru na maendeleo ya nchi yetu. Wakati wote wa uhai wake alitumia uwezo wake na vipaji vyake alivyojaaliwa na Mola wake kujenga, kuendeleza na kutetea maslahi ya Taifa lake na Chama chake CCM na TANU kabla yake. Mzee Kawawa alikuwa mhimili mkubwa kwa Taifa letu na Chama cha Mapinduzi hata baada ya kustaafu uongozi. Sote tutaendelea kumkumbuka kwa moyo wake wa ubinadamu na mchango wake usiokuwa na kifani kwa nchi yetu na watu wake. Tuendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amin.

Nchi Salama na Tulivu
Ndugu Wananchi,
Ni jambo la faraja na kuonea fahari kwamba tunaumaliza mwaka 2009 taifa letu likiwa salama na kwamba amani na utulivu viliendelea kutawala. Aidha, taifa letu limeendelea kuwa moja na watu wake wameendelea kuwa wamoja, licha ya kuwepo kwa changamoto za hapa na pale zilizotokana na harakati za vyama vya siasa na kauli za baadhi ya wanasiasa na viongozi wa kijamii wakiwemo wale wa dini. Wakati mwingine, matendo na kauli zao zimekuwa na mwelekeo wa kuwagawa Watanzania katika makundi yenye mifarakano na uhasama.

Napenda kutumia nafasi hii kuwapongeza na kuwashukuru kwa dhati Watanzania wenzangu kwa ukomavu wa kisiasa, moyo wao wa uzalendo na busara waliyotumia ya kukataa kuwa wahanga wa njama hizo ovu. Badala yake mmechagua kufuata na kufanya mambo yenye maslahi kwa umoja, maendeleo na usalama wa taifa letu. Hakika ni moyo huo na ufahamu huo ndiyo umeliweka taifa letu kuwa moja na lenye amani na utulivu tulionao tangu uhuru wa Tanganyika, mapinduzi ya Zanzibar na baadae Muungano mpaka leo. Nawaomba ndugu zangu tushikilie msimamo huo hasa katika mwaka ujao wa uchaguzi ambapo haya yaliyofanywa mwaka huu yanaweza kufanywa maradufu.

Tusiwape nafasi wakafanikiwa wale watu wabaya wanaotaka kutugawa kwa dini, kabila, rangi, Bara na Visiwani au Unguja na Pemba. Pia tusiwape nafasi wale wote wanaotaka kuleta machafuko nchini. Kamwe tusikubali kuwa kama wale wenzetu tuliowapa hifadhi hapa kwetu au tunaowaona kwenye luninga na kuwasikia katika redio na kuwasoma katika magazeti wakiuana, kuumizana na kuharibiana mali huko nchini kwao. Nina imani kubwa kwamba hatutaiacha nchi yetu ifike hapo.

Mazungumzo Baina ya CUF na CCM

Ndugu Wananchi;
Wakati nikitahadharisha na kuwataka Watanzania wenzangu tuendelee kudumisha amani na utulivu wa nchi yetu sina budi kutambua matumaini mema yanayojitokeza Zanzibar. Hatua ya Mheshimiwa Amani Abeid Karume, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kukutana na kuzungumza na Maalim Seif Sharif Hamad, Katibu Mkuu wa CUF inazidi kuleta matumaini ya amani na utulivu kuendelea kustawi Zanzibar na kote nchini sasa na katika uchaguzi ujao. Tuendelee kuwaunga mkono na kuwapa moyo viongozi wetu hawa ili wakamilishe kwa salama kazi waliyoianza kwa maslahi ya Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla.

Uhalifu Unadhibitiwa
Ndugu Wananchi:
Katika mwaka huu tunaoumaliza leo tumeshuhudia kuimarika kwa juhudi za kupambana na uhalifu na maovu katika jamii. Matokeo ya juhudi hizi yameonekana katika kudhibitiwa kwa uhalifu. Wahalifu wengi wamekamatwa na kufikishwa Mahakamani. Njama kadhaa za uhalifu zimezuiliwa. Watuhumiwa wengi wa makosa ya rushwa wamefikishwa mbele ya vyombo vya sheria. Nawapongeza sana wenzetu wa Jeshi la Polisi na Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini kwa kazi nzuri walioifanya. Nawaomba mwaka 2010 waongeze juhudi maradufu. Mimi naendelea kuwaahidi msaada na ushirikiano wangu na wa Serikali.

Mauaji ya Albino
Ndugu Wananchi;
Mwaka 2009, matukio ya mauaji ya ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino yamepungua. Kumekuwepo na vifo 7 ikilinganishwa na 27 vya mwaka 2008. Hata hivyo, watu 7 kuuawa bado ni wengi mno. Haitakiwi auawe hata mtu mmoja.

Katika mwaka ujao tutaendeleza juhudi za kupambana na uhalifu huu mpaka tuutokomeze. Bahati nzuri taarifa zilizopatikana wakati wa zoezi la kura ya maoni lililofanyika mapema mwaka huu zinasaidia sana vyombo vyetu vya dola katika kuwafuatilia watu wanaoshukiwa kujihusisha na vitendo hivi viovu vya aibu. Ni jambo la kuleta faraja kwamba tayari kesi tatu zimesikilizwa na kuamuliwa na Mahakama. Wahusika wametiwa hatiani na baadhi kuhukumiwa kifo. Haki imetendeka.

Ndugu Wananchi,
Nasikitika kwamba bado hatujafanikiwa kudhibiti ajali za barabarani licha ya wito wangu wa kila mwaka katika salamu kama hizi na ule wa viongozi wenzangu kila zitokeapo ajali mbaya za magari barabarani.
Mwaka huu, hadi mwezi Septemba jumla ya ajali zilizotokea ni 15,798 ikilinganishwa na 13,405 zilizotokea katika kipindi kama hicho mwaka jana. Ajali hizo zimesababisha vifo 2,685 ikilinganishwa na vifo 2,040 vilivyotokea mwaka 2008. Idadi ya majeruhi imeongezeka kufikia 15,508 ikilinganishwa na majeruhi 12,508 mwaka 2008.

Kwa mara nyingine tena narudia wito wangu kwa watumiaji wa barabara hasa madereva kuzingatia Sheria ya Usalama barabarani waendeshapo magari. Ningependa kuona mwaka 2010 ukiwa mwaka wa mabadiliko mema kwa maana ya kupungua kwa ajali za barabarani.

Narudia wito wangu kwa Askari wa Usalama Barabarani kuwa makini katika kusimamia Sheria ya Usalama Barabarani na kuwawajibisha ipasavyo madereva wazembe. Aidha, naomba wahakikishe kuwa ukaguzi wa ubora wa magari yatembeayo barabarani unafanywa kwa dhati na siyo wa kurashiarashia. Na, kwa magari ya abiria ukaguzi ufanywe mara kwa mara. Pia, nawahimiza Wizara ya Mambo ya Ndani kukamilisha mchakato wa kuongeza adhabu kwa madereva wazembe. Nawaomba SUMATRA watafute namna ya kuwawajibisha wamiliki wa magari wasiojali uimara wa magari yao yatembeayo barabarani.

Hali ya Uchumi wa Taifa

Ndugu Wananchi;
Mwaka uliopita ulikuwa mgumu sana kwa ustawi wa uchumi wa nchi yetu. Matarajio na malengo yetu makuu kuhusu ujenzi na maendeleo ya uchumi wetu hatukuweza kuyafikia. Mauzo yetu ya nje ya bidhaa na mazao ya kilimo, mifugo, viwanda na madini yalipungua kwa kukosa masoko katika nchi za Ulaya, Marekani na Asia. Bei za mazao na bidhaa zetu hizo iliporomoka sana. Watalii walipungua na mapato ya utalii kushuka pia. Wawekezaji wameahirisha uamuzi wa kuwekeza nchini. Biashara ya uchukuzi wa mizigo iendayo na itokayo nchi jirani ilipungua sana. Mapato ya Serikali yakapungua kwa asilimia 9. Jumla ya yote kasi ya kukua kwa uchumi inatarajiwa kushuka kutoka lengo la asilimia 7.8 na kuwa asilimia 5. Hii ni athari kubwa sana kwa taifa letu.

Pamoja na kuwepo kwa sababu nyingine, hali hiyo imechangiwa kwa kiasi kikubwa na matatizo makubwa na ya aina yake yanayoukabili uchumi wa dunia kuanzia mwaka 2007 na kuwa mbaya zaidi tangu mwaka 2008 hadi sasa.

Kama mtakavyokumbuka Juni 10, 2009, mjini Dodoma, nilitangaza Mpango Maalum wa Dharura wa Taifa wa kuhami na kuimarisha uchumi wa nchi yetu. Kama nilivyoeleza mpango huo umekadiriwa kugharimu takriban shilingi bilioni 1,600 (au shilingi trilioni moja na bilioni mia sita).

Ndugu Wananchi;
Kwa hakika hii ni gharama kubwa mno kwa nchi maskini kama yetu kubeba lakini ilikuwa hapana budi kufanya hivyo. Kufanya kinyume chake kungeifanya hali ya uchumi wa nchi yetu kuwa mbaya zaidi. Utulivu tulionao katika uchumi mkuu ungetoweka na mambo mengi yangeparaganyika. Kama tungeiacha hali ifikie hapo huenda hata utulivu wa kisiasa tunaojivunia nao ungetetereka pia. Kutofanya chochote isingekuwa uamuzi wa busara kuchukua pamoja na ukweli kwamba kwa kupeleka kiasi kikubwa cha fedha kama hiki kwa ajili ya kunusuru uchumi kumepunguza fedha ambazo zingetumika kwa ajili ya shughuli nyingine za maendeleo na Serikali.

Ndugu zangu, Watanzania Wenzangu;
Katika Mpango wetu wa Dharura, miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ni ile ya Serikali kubeba mzigo wa madeni ya Benki ya makampuni, na watu waliopata hasara kutokana na kupungua kwa mauzo nje na kuanguka kwa bei za mazao na bidhaa wanazouza katika soko la dunia. Nia yetu ilikuwa kuzuia wasifilisike na mabenki yaliyowakopesha yasiathirike. Pia tulichukua uamuzi wa kufidia bei ya pamba kwa shilingi 80 kwa kilo ili kumpunguzia mkulima mzigo wa hasara na kuwapa moyo waendelee na kilimo cha pamba msimu unaofuata. Tulifidia zao la pamba kwa kuwa ndilo zao lililoathirika zaidi kuliko mazao mengine yote.

Ndugu Wananchi;
Katika mpango wetu huo pia tulianzisha mfuko maalum wa uwekezaji ili kuyapa imani mabenki ambayo yalipata hofu ya kukopesha yaendelee kutoa mikopo kwa wafanyabiashara na wawekezaji. Kwa upande wa Serikali yenyewe mpango huo ulilenga kukabiliana na tatizo la kupungua kwa mapato ya Serikali.

Nafurahi kusema kuwa utekelezaji wa Mpango wetu wa Dharura wa Kuhami na Kuimarisha Uchumi unakwenda vizuri na takriban malengo yote tuliyojiwekea yametekelezwa kama tulivyokusudia. Ni matumaini yangu kuwa utekelezaji wa Mpango huu utafanikiwa ili kuzuia kudidimia zaidi kwa uchumi wa nchi yetu na kusaidia kuuimarisha.

Ndugu zangu, Watanzania Wenzangu;
Mwaka 2010 tunaouanza kesho hautakuwa mwepesi ingawaje tunatarajia kuwe na nafuu kiasi kuliko mwaka huu. Yapo mambo mawili yananifanya niwe na matumaini hayo. Kwanza, kasi ya kuporomoka kwa uchumi katika mataifa makubwa tajiri kulikochimbuka matatizo haya inaelekea kudhibitiwa. Pili, hatua za dharura tulizozichukua zinaelekea kufanikiwa kwa kiasi fulani kuzuia uchumi usididimie na baadhi ya sekta zimeonyesha dalili za kuimarika ikiwemo sekta yetu kuu ya utalii.
Hali ya Mvua na Chakula Nchini

Pamoja na msukosuko wa uchumi wa dunia na kushinda, sina budi kukumbusha kuwa safari yetu bado ni ndefu na kuna vikwazo vingi vya kuvuka. Hatuna budi kutambua wajibu wetu wa kufanya kazi kwa makini zaidi, bidii zaidi na maarifa ili tuweze kukabiliana sawasawa na athari zake

Ndugu Wananchi;
Waswahili wana msemo usemao “kila msiba una mwenzake”. Hali hiyo imekuwa kweli kwetu sisi hapa nchini kwa mwaka huu. Wakati tunakabiliwa na athari za msukosuko mkubwa wa uchumi wa dunia unaotishia kufuta mafanikio yote tuliyopata katika mageuzi na ujenzi wa uchumi wetu, ukame umezua changamoto nyingine inayoongeza ugumu katika juhudi zetu za kujinusuru.

Kwa miaka miwili mfululizo sasa mikoa yote inayopata mvua za vuli na masika na baadhi ya mikoa inayopata mvua moja imekuwa na upungufu mkubwa wa mvua. Mikoa hiyo ni Pwani, Dar es Salaam, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Mara, Mwanza, Shinyanga na Dodoma. Matokeo yake ni kuwepo kwa upungufu wa chakula katika mikoa hiyo na nchi nzima kwa jumla.

Ndugu Wananchi;
Katika msimu wa mwaka 2008/09 nchini kulikuwa na upungufu wa tani 860,000 za nafaka na katika msimu wa 2009/10 inatarajiwa kutakuwa na upungufu wa tani 1.3 milioni za nafaka. Kwa sababu hiyo, watu wengi katika wilaya kadhaa hapa nchini wamelazimika kutegemea msaada wa Serikali kwa ajili ya kujipatia usalama wao wa chakula. Kwa mfano, mwaka 2008 Serikali ilitoa tani 11,610 za nafaka kama msaada wa chakula kwa watu 425,313 Katika wilaya 30 nchini. Hadi kufikia tarehe 22 Desemba, 2009 Serikali imeshatoa tani 115,837.1 za nafaka katika wilaya 59 nchini, na matarajio yetu ni kutoa zaidi. Napenda kuwahakikishia Watanzania wenzangu kuwa tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha chakula kinapatikana kwa wanaohitaji. Hatutakubali kuona Mtanzania hata mmoja anakufa kwa njaa, labda tusipate taarifa mapema. Iwapo itatokea hatutapata chakula cha kutosha hapa nchini, tupo tayari kutatafuta popote duniani.

Bahati mbaya sana kwa baadhi ya wilaya za Mikoa ya Arusha na Manyara ukame ulikuwa mkali sana na kusababisha mifugo mingi kufa. Familia nyingi za ndugu zetu wafugaji zimejikuta kwenye umaskini mkubwa kwa sababu ya kupoteza mifugo yao. Nilitembelea wilaya ya Longido na kuona kwa macho yangu athari za ukame. Napenda kuwahakikishia ndugu zetu hao kuwa Serikali imeona na imesikia. Tutatafuta namna ya kuwasaidia waanze maisha mapya. Hatuwezi kufanya makubwa lakini madogo tunayaweza. Aidha, tutaendelea kuwapatia msaada wa chakula.
Kilimo Kwanza

Ndugu Wananchi;
Mwaka huu wa 2009 umekuwa mwaka wa mafanikio ya kutia moyo katika mchakato wetu wa kuleta mapinduzi ya kilimo nchini au mapinduzi ya kijani kama watu wengine wanavyopenda kuyaita. Mambo mengi tuliyopanga kufanya yametekelezwa na kutoa mwelekeo mzuri katika safari yetu ya kuboresha kilimo chetu. Mara baada ya kuingia madarakani tuliamua kuchukua hatua za dhati za kuanzisha mchakato thabiti wa kuleta mapinduzi ya kijani nchini. Mwaka mmoja baadaye tulizindua Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo au Agriculture Sector Development Programme maarufu kama ASDP kwa kifupi.

Madhumuni ya Programu hii ni kuondoa vikwazo vinavyozuia maendeleo ya haraka ya kilimo chetu na kusababisha tija kuwa ndogo na hivyo uzalishaji kuwa mdogo. Vikwazo hivyo pia vinasababisha ubora na thamani ya mazao yetu ya kilimo kuwa ya kiwango cha chini. Kwa sababu hiyo, hali ya usalama wa chakula kwa watu wengi na nchini kwa ujumla kuwa ya mashaka. Sababu hiyo pia imechangia kuwafanya watu wengi nchini kuwa maskini kwani asilimia 80 ya Watanzania huishi vijijini na wanategemea kilimo hicho hicho kwa maisha yao na maendeleo yao. Katika Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo tunayoendelea kuitekeleza hivi sasa, vikwazo vimetambuliwa na kutengenezewa mipango ya kuvitatua

Ndugu Wananchi;
Mwaka huu tumefikisha miaka mitatu ya utekelezaji wa Programu hii na nafurahi kusema kuwa mambo yanakwenda vizuri. Tumeongeza maradufu bajeti ya sketa ya kilimo na kufikia shilingi 721.3 bilioni ambayo ni sawa na asilimia 7.5 ya bajeti ya Serikali kwa mwaka huu wa fedha. Ni kweli kwamba kiasi hicho ni chini ya lengo la asilimia 10 lililowekwa na Umoja wa Afrika na SADC. Hata hivyo, hapa tulipofikia mwaka huu ni pakubwa sana ikilinganishwa na tulipokuwa miaka ya nyuma.

Ndugu Wananchi;
Tumeweza kupata mafanikio ya kutia moyo katika kukabiliana na vikwazo katika kilimo nchini. Kwa mfano, tumepanua kilimo cha umwagiliaji na kazi inaendelea. Tumeongeza uagizaji wa matrekta kwa nia ya kupunguza matumizi ya jembe la mkono. Kila Halmashauri ya Wilaya nchini, kwa kuanzia imeagizwa kununua matrekta yasiyopungua 50.

Kwa upande wa upatikanaji wa mbegu bora, tumechukua hatua za dhati za kuongeza uwezo wetu wa uzalishaji wa mbegu bora nchini. Tumeongeza fedha kwa shughuli za utafiti nchini jambo ambalo litanufaisha utafiti wa mbegu nchini. JKT na Jeshi la Magereza yameanza uzalishaji wa mbegu bora kama wakala wa Wakala wa Taifa wa Mbegu. Wakati huo huo juhudi zinaendelea za kufufua mashamba ya mbegu ya Serikali na kuhusisha kwa upana zaidi sekta binafsi katika shughuli hii muhimu.

Upatikanaji wa Mbolea

Ndugu Wananchi;
Jambo lingine ambalo tumepata mafanikio ya kutia moyo mwaka huu ni la upatikanaji wa mbolea na pembejeo za kilimo. Tumefanikiwa kuongeza fedha za mfuko wa ruzuku ya mbolea na pembejeo nyingine za kilimo kutoka shilingi billion 7 mwaka 2005 hadi shilingi 118 bilioni mwaka huu. Mwaka wa jana katika ugawaji wa mbolea na pembejeo za kilimo za ruzuku, tulianzisha mpango wa vocha ili kuhakikisha kuwa kweli mbolea inawafikia walengwa.

Matokeo ya hatua hizo ni kuongezeka kwa mbolea na pembejeo za kilimo za ruzuku pamoja kwa wakulima na kuongezeka kwa idadi ya wakulima wanaopatiwa pembejeo hizo. Kwa upande wa mazao ya mahindi na mpunga, mwaka huu, wakulima 1,500,000 watanufaika na ruzuku ya mbegu na mbolea kutoka wakulima 750,000 wa mwaka wa jana.

Tumeanzisha pia utaratibu wa ruzuku ya dawa na mbegu kwa zao la pamba mwaka huu, ambapo wakulima wapatao 500,000 watanufaika. Kwa upande wa zao la korosho, ruzuku inayotolewa ni kufidia asilimia 50 ya bei ya dawa. Kwa upande wa mazao ya kahawa na chai, Serikali inatoa ruzuku na kuyawezesha mashirika ya utafiti ya TACRI na TRITI kuuza miche kwa nusu ya bei waliyokuwa wanawauzia wakulima.

Ndugu Wananchi;
Mwaka huu tumeanzisha mkakati maarufu kwa jina la Kilimo Kwanza. Natambua kuwa wapo watu hawajaelewa ipasavyo dhana iliyobebwa na mkakati huo. Lakini, wapo wenzetu wengine ambao wamediriki hata kubeza kuwa Kilimo Kwanza si lolote si chochote, hata kabla utekelezaji wake haujaanza kwa ukamilifu.

Ndugu Wananchi;Naomba nirudie kwa kifupi kusema kuwa mkakati wa Kilimo Kwanza si badala ya ASDP bali upo kwa ajili ya kuongeza nguvu na kutoa msukumo zaidi katika utekelezaji wa malengo ya programu yetu hiyo muhimu. Katika Kilimo Kwanza tunatekeleza malengo ya ASDP ila tunataka kuzitumia rasilimali na maarifa ya wenzetu wa sekta binafsi kuleta ufanisi zaidi. Tunataka ndugu zetu wa sekta binafsi wawekeze katika shughuli za kuendeleza kilimo nchini, yaani walime mashamba makubwa na wawekeze katika biashara na viwanda kwa ajili ya kukipatia kilimo chetu mahitaji yake ya zana na pembejeo. Aidha, tunataka wawekeze katika viwanda vitakavyosindika mazao ya kilimo na kuzalisha bidhaa kwa kutumia malighafi zinazotokana na kilimo. Nafurahi kwamba wenzetu wa sekta binafsi ambao walihusika kwa ukamilifu katika matayarisho ya mkakati huo wapo tayari. Tena wengine wameshaanza kuwekeza katika viwanda hivyo.

Kuendeleza Mifugo

Ndugu Wananchi;
Katika kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo, nimejifunza kuwa shughuli za ufugaji hazipewi fursa sawa kama zile za ukulima wa mazao. Nimeagiza kuwa ili kuitendea haki shughuli ya mifugo, tutayarishe programu maalum kwa ajili ya kuendeleza ufugaji. Hivyo basi, katika mwaka ujao tutegemee kuona shughuli za mifugo zikipewa fursa zaidi ya ilivyo sasa.

Maendeleo ya Miundombinu

Ndugu Wananchi;
Katika mwaka 2009, tumeendelea kupata mafanikio katika uendelezaji wa miundombinu hasa ya barabara. Mafanikio hayo yamewezekana kutokana na Serikali kuendelea kutenga fedha nyingi kila mwaka katika bajeti ya sekta hiyo. Mwaka huu kwa mfano, tumetenga shilingi bilioni 1,096 ambazo ni sawa na asilimia 11.5 ya bajeti nzima ya Serikali.Hii ndiyo bajeti ya pili kwa ukubwa baada ya ile ya Elimu.

Kwa sababu hiyo, barabara nyingine zimekamilika na nyingine zimeendelea kujengwa kwa kiwango cha lami na changarawe. Aidha, tumeshuhudia uzinduzi wa ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara nyingine kadhaa hapa nchini. Kwa kuongeza fedha katika Mfuko wa Barabara, barabara nyingi za Mikoa na Wilaya zimeimarishwa na zinaendelea kuimarishwa kwa kujengwa kwa kiwango cha changarawe.

Ndugu Wananchi;
Katika mwaka ujao tunategemea mambo kuwa mazuri zaidi. Kama kila kitu kitakwenda kama ilivyopangwa zile barabara za Tanga – Horohoro, Tunduma – Sumbawanga na Namtumbo – Songea – Mbinga zitaanza kujengwa. Mchakato wa ujenzi wa barabara hizo zinafadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia mfuko wa Millennium Challenge Account, hivi sasa imefikia hatua ya uteuzi wa makandarasi wa barabara hizo. Kazi hiyo ya uteuzi inatarajiwa kukamilika robo ya kwanza ya 2010 na ujenzi kuanza katikati ya mwaka. Ratiba ni hiyo hiyo kwa miradi mingine inayofadhiliwa na MCC.

Ndugu Wananchi;
Jambo lingine la faraja kuhusu ujenzi wa barabara ambalo napenda kulitaja leo ni kule kukamilika kwa ujenzi wa daraja la Umoja katika mto Ruvuma linalounganisha nchi zetu mbili rafiki za Msumbiji na Tanzania. Hatimaye ndoto ya hayati Rais Julius Nyerere wa Tanzania na hayati Rais Samora Machel wa Msumbiji imetimia. Tena jambo zuri na la heshima kuhusu daraja hili ni kwamba nchi zetu zimetumia fedha zake bila msaada wa wafadhili. Hii inadhihirisha kuwa pamoja na ukweli kwamba tunahitaji misaada kutoka nchi zilizoendelea, yapo mambo tunayoweza kuyafanya wenyewe pale tunapokosa misaada kama ilivyokuwa kwa daraja hili.

Bandari, Usafiri wa Anga na Reli

Ndugu Wananchi;
Kwa upande wa huduma za reli, bandari na usafiri wa anga, mwaka 2009 ulikuwa wa matatizo. Kiini cha matatizo yaliyozikabili sekta hizi tatu muhimu ni udhaifu katika uendeshaji na uwekezaji mdogo katika maendeleo ya miundombinu hii muhimu.

Kwa upande wa bandari, tatizo la mlundikano wa meli zinazosubiri kupakua au kupakia mizigo bandarini limepungua sana. Hii imeletwa na ununuzi wa vifaa vipya vya upakuaji na upakiaji wa makontena bandarini na matengenezo ya vifaa vilivyokuwepo ambavyo vilikuwa vimeharibika. Bado lipo tatizo la kasi ya kuyaondoa bandarini makontena yaliyokwishapakuliwa kutoka kwenye meli. Natambua juhudi zinazoendelea kupata ufumbuzi wa tatizo hili. Nawasihi wahusika wote kuongeza kasi, ari na nguvu ya kupata jawabu la kudumu kwa tatizo hili.

Baada ya Serikali kufanikiwa kuondoa ukiritimba wa kampuni TICTS sasa fursa ipo ya kuleta wabia wengine kuendeleza bandari ya Dar es Salaam. Nawaomba wahusika katika Mamlaka ya Bandari kuchangamka kutafuta wawekezaji kwa ajili ya upanuzi wa Bandari yetu.

Usafiri wa Anga

Ndugu Wananchi;
Kwa upande wa usafiri wa anga mwaka huu Serikali imeendelea na jitihada za kuimarisha utendaji na uendeshaji wa Shirika la Ndege la Tanzania. Pamoja na hayo, pia Serikali imeendelea na mchakato wa kupata mbia wa kushirikiana nae kuendesha shirika hilo. Ni matumanini yangu kuwa mchakato huo utakamilika mapema mwaka 2010 ili shirika letu tulipe matumaini mapya ya uhai na maendeleo.

Serikali imeendeleza juhudi za ujenzi na uimarishaji wa viwanja vya ndege nchini. Shughuli za ukarabati na upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere zimeendelea kufanyika. Mwaka huu tunatarajia kazi hiyo kuendelezwa kwa upana na kina zaidi. Aidha, kazi ya kuimarisha viwanja vya ndege vya Arusha, Mwanza, Mpanda, Bukoba na Mafia imeendelea kama ilivyopangwa. Katika mwaka huu, kwa msaada wa wabia wetu wa maendeleo matengenezo makubwa yatafanywa kwa viwanja vya Tabora, Kigoma, Bukoba na Mafia. Naomba Wizara ya Miundombinu na hasa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege wamsimamie kwa karibu mkandarasi anayejenga Uwanja mpya wa ndege wa Kimataifa wa Songwe ili uanze kutumika mwaka 2010.

Reli

Ndugu Wananchi;
Kwa upande wa reli zetu mbili, yaani Reli ya TAZARA na ya Shirika la Reli la Tanzania, mwaka huu umekuwa wa misukosuko iliyohusu matatizo ya uendeshaji na uchakavu wa miundombinu ya reli hizo. Kwa upande wa TAZARA mazungumzo yaliyomalizika hivi karibuni mjini Beijing, China baina ya nchi zetu tatu, yaani Zambia, Tanzania na China yemeleta matumaini mapya kuhusu kupata ufumbuzi wa matatizo ya miundombinu ya reli na vyombo vya uchukuzi. Bado tutaendelea kulitafutia ufumbuzi tatizo la menejimenti.

Kwa upande wa Shirika la Reli Tanzania, fedha za kukabiliana na tatizo la miundombinu chakavu ya reli, mabehewa na vichwa vya treni ipo tayari. Kinachochelewesha kuzipata na kuzitumia ni migogoro inayoelekea kuwa sugu ya menejimenti na uendeshaji. Serikali inaendelea kushughulikia tatizo hilo na ni matumaini yangu kuwa mapema mwaka 2010 tutapata ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hili, ufumbuzi ambao utakuwa wa maslahi kwa taifa letu.

Elimu
Ndugu Wananchi;
Kwa upande wa elimu mwaka huu umeendelea kuwa wa mafanikio kwa upanuzi wa elimu ya awali, msingi, sekondari na elimu ya juu. Kwa sababu hiyo, tunao wanafunzi wengi katika ngazi zote na aina zote za elimu kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya nchi yetu.

Mafanikio haya yameleta changamoto zake na hasa ile ya kupata fedha za kutosha kukidhi mahitaji ya ajira na huduma kwa walimu, majengo na vifaa vya kufundishia kama vile vitabu na vinginevyo. Kupata ufumbuzi kwa matatizo ya sekta ya elimu nchini imekuwa ni moja ya kipaumbele cha juu tangu tuingie madarakani. Kila mwaka tumeongeza bajeti ya elimu na kuifanya bajeti hiyo kuwa ndiyo kubwa kuliko zote. Kwa mfano, mwaka huu tumetenga shilingi bilioni 1,743.9 ikilinganishwa na bilioni 1,430.4 mwaka wa jana na bilioni 669.5 tulipoingia madarakani mwaka 2005.

Pamoja na nyongeza kubwa kiasi hicho, bado tunayo mahitaji makubwa ambayo bado hayajatoshelezwa. Miongoni mwa hayo ni upungufu wa walimu, vitabu, vifaa vingine vya kufundishia, madarasa, maabara, nyumba za walimu pamoja na mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu. Ninachowaahidi ni kuwa katika mwaka ujao tutaendelea kuiangalia kwa upendeleo bajeti ya elimu ili tuendelee kupunguza vikwazo vinavyozuia elimu yetu kuendelea kustawi.

Ndugu Wananchi;
Kwa upande wa matokeo ya mtihani wa darasa la saba kwa mwaka huu, sina budi kukiri kuwa hayakunifurahisha na kwa kweli yamenishtusha. Nimesikia maelezo mengi ya kila aina kuhusu sababu zilizochangia ufaulu wa watoto wetu kuwa wa chini kiasi hicho mwaka huu. Pamoja na yote yaliyosemwa nimewataka viongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wakae chini na wenzao wa TAMISEMI, Maafisa Elimu wa Wilaya na Wawakilishi wa Walimu kujadili tatizo hili kwa dhati na kutafuta ufumbuzi wake ili lisijirudie tena.

Huduma ya Afya
Ndugu Wananchi;
Mwaka huu tumeendelea kupiga hatua katika kuimarisha huduma ya afya nchini. Vituo vya huduma ya afya kwa maana ya zahanati, vituo vya afya na hospitali vimeongezeka kutoka 5,800 mwaka 2008 hadi 6,240 mwaka 2009. Hali kadhalika tumeendelea kuboresha upatikanaji wa dawa, vifaa vya tiba na watumishi wa afya. Pamoja na mafanikio hayo, bado zipo changamoto nyingi zikiwemo za baadhi ya dawa kuwa pungufu pamoja na uhaba mkubwa wa vifaa vya tiba na watumishi hasa wauguzi na madaktari.

Tumeendelea na juhudi za kukabiliana na matatizo hayo. Tumeongeza bajeti ya afya kwa kiasi kikubwa ili kujenga uwezo wa kukabiliana na changamoto hizi na nyinginezo. Tumeweka msisitizo maalum katika kupambana na maradhi yanayoua watu wengi kama vile malaria, kifua kikuu na UKIMWI. Kwa upande wa UKIMWI tunaendelea na juhudi za kutoa elimu kwa umma ili watu wajikinge na UKIMWI. Na, tunatoa dawa za kurefusha maisha kwa walioathirika.
Kwa upande wa malaria, pamoja na juhudi tuzifanyazo sasa kukabiliana na maradhi hayo, tumeamua kuchukua hatua za kufuta maradhi hayo hapa nchini. Tumefanikiwa Zanzibar, hivyo naamini hata Bara tutafanikiwa. Tunataka kukata mzizi wa fitina kwa kutumia vyandarua vilivyotiwa dawa na kupulizia dawa majumbani na mazalia ya mbu. Tayari tumepata vyandarua vya kumuwezesha kila mtoto mwenye umri wa chini ya miaka 5 kupata chandarua chake. Kazi ya kugawa inaendelea kote nchini. Hivi sasa matayarisho yanaendelea ya kuiwezesha kila kaya kupata vyandarua viwili. Matayarisho yatakapokamilika tutaarifiana.

Jambo lingine kubwa tunaloendelea nalo ni jitihada za kupunguza vifo vya kina mama waja wazito kutokana na matatizo ya uzazi. Tumetengeneza mkakati kabambe ambao tunaendelea kuutekeleza. Nina imani kuwa tutafanikiwa katika dhamira yetu hii njema. Si haki hata kidogo kwa mama kupoteza maisha wakati wa uzazi.

Umeme
Ndugu Wananchi;
Kwa upande wa umeme, mwaka huu tumeongeza kasi ya kutekeleza maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi katika kufikisha umeme kwenye miji mikuu ya wilaya. Umeme tayari umefika Mbinga, Simanjiro, Ludewa, Mkinga na Kilolo. Wakati wowote mwezi Januari mwaka 2010 umeme utawaka Kilindi, Uyui na Bahi. Mchakato wa kununua genereta mpya 17 ili kuzipatia umeme Wilaya za Ngorongoro, Kasulu, Kibondo, Kigoma na Sumbawanga unaendelea vizuri. Fedha zimekwishatengwa na mkandarasi amekwishapatikana.

Wilaya ya Bukombe itapata umeme kwa msaada wa Benki ya Maendeleo ya Afrika na mchakato unaendelea juu ya kupata fedha za utekelezaji wa mradi huu muhimu. Mji wa Longido utapata umeme kutoka Namanga na matayarisho ya ujenzi wa njia yanaendelea. Kwa wenzetu wa Kigoma mjini, nafarijika sana kwamba mitambo miwili ya umeme tuliyonunua mwaka huu imeanza kufanya kazi na tatizo la umeme limepungua. Ufumbuzi wa kudumu utapatikana tutakapofunga mashine nyingine mpya 5 ambazo zimeshaagizwa. Kwa mji wa Songea, Serikali imekwishatenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa mtambo mpya ili kuimarisha upatikanaji wa umeme mjini hapo wakati tunasubiri umeme wa gridi.
Ndugu Wananchi;
Mwanzoni mwa Oktoba, mwaka huu, mikoa, wilaya, miji na vijiji vinavyopata umeme wa gridi vilikabiliwa na tatizo la mgao wa umeme. Tatizo hili lilitokana na kuharibika kwa mitambo ya Songas na ya Kituo cha Umeme cha Kihansi. Matengenezo ya mtambo wa Songas ulikamilika na Kihansi bado mpaka Januari 2010. Tatizo hilo limesisitiza haja ya kuongeza uzalishaji wa umeme na kuwa na akiba ya kutosha. Kwa sasa hatuna uwezo huo ndiyo maana hitilafu ndogo ikitokea inakuwa ni tatizo kubwa. Kuongeza uzalishaji wa umeme ndilo lengo letu mwaka ujao na mingine ijayo.
Huduma ya Maji
Ndugu Wananchi;Kuhusu huduma ya maji, katika mwaka wa 2009 tulijitahidi kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma ya maji nchini. Mnamo mwezi wa Mei mwaka huu nilizindua mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria ambao umewapatia maji watu zaidi ya milioni 1 katika miji ya Shinyanga na Kahama na vijiji 54 vya wilaya za Misungwi, Geita, Shinyanga na Kahama. Mradi huu ulitugharimu shilingi 252 bilioni ambazo ni fedha zetu wenyewe. Katika mwaka ujao wa 2010, tutaendelea na jitihada hizi za kuboresha huduma ya maji kote nchini. Kwa ajili hiyo, katika bajeti ya mwaka 2009/2010, tumetenga jumla ya shilingi billion 65 kwa utekelezaji wa miradi mingine ya maji.

Ushirikiano wa Kimataifa
Ndugu Wananchi;
Katika mwaka huu unaoishia leo, nchi yetu imefanikiwa kuimarisha uhusiano na mataifa mengine duniani na mashirika ya kimataifa. Tanzania imeendelea kuheshimiwa katika medani za kimataifa. Kwa ajili hiyo, tumeshirikishwa katika masuala mengi makubwa ya kimataifa. Tumetembelewa na viongozi mashuhuri wengi waikiwa Wakuu wa Nchi kadhaa. Viongozi wakuu wa nchi yetu nao wamealikwa na kutembelea nchi nyingine duniani. Mahusiano hayo yamekuwa na manufaa ya kusaidia maendeleo na ustawi wa nchi yetu. Tumeendelea kupata masoko ya bidhaa na mazao yetu pamoja na misaada ya maendeleo na mitaji ya uwekezaji.

Ndugu Wananchi;
Pengine katika heshima kubwa na muhimu tuliyoipata mwaka huu ni ile ya kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa wa kimataifa wa masuala ya kiuchumi Barani Afrika uitwao World Economic Forum on Afrika. Hii itakuwa mara ya kwanza kwa mikutano hyo kufanyika nje ya Cape Town, Afrika Kusini. Ni heshima kubwa kwa Tanzania, hivyo nawaomba Watanzania wenzangu na hasa wananchi wa Dar es Salaam kuwapokea vizuri wageni wetu wazito kwa utajiri na maarifa. Tuoneshe ukarimu wetu wa kawaida kwa wageni wetu ili wapende kurudi tena Dar es Salaam na Tanzania kwa mikutano mingine au matembezi na shughuli nyingine.
Uchaguzi Mkuu wa 2010

Ndugu Wananchi;
Kwa upande wa kukuza na kuendeleza demokrasia, mwaka 2009 kulifanyika uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mafanikio makubwa. Napenda kuitumia nafasi hii kuwapongeza viongozi na wananchi wote kwa jumla kwa mafanikio haya ya kutia moyo. Inathibitisha, kwa mara nyingine tena, kuwa demokrasia inazidi kuota mizizi Tanzania. Kwa niaba ya CCM naomba niwashukuru Watanzania wenzetu kwa kuendelea kukiamini Chama chetu. Imani huzaa Imani. Hatutawaangusha.

Mwaka 2010 ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani. Ni matumaini yangu kuwa tutaidumisha sifa ya nchi yetu ya nchi ya demokrasia ya kweli iliyojengeka juu ya msingi wa uhuru na haki. Hiyo ndiyo siri ya kudumishwa kwa amani na utulivu Tanzania. Sisi, Serikalini tumejipanga vizuri kuhakikisha kuwa mahitaji yote ya rasilimali yanayotakiwa na Tume ya Uchaguzi yanapatikana kwa ukamilifu na kwa wakati. Tumetenga fedha za kutosha katika bajeti ya mwaka huu na tutamalizia katika bajeti ijayo. Aidha, tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha kuwa uchaguzi unakuwa huru na wa haki na unafanyika katika mazingira ya utulivu na amani.

Ndugu Wananchi;
Wito wangu kwenu wananchi wenzangu ni kuwa mjitokeze kwa wingi kushiriki katika mchakato wa uchaguzi katika hatua zake zote. Kwa wale ambao hawajajiandikisha kwenye daftari la wapiga kura wajiandikishe wakati ukifika. Wakati wa uchaguzi ukifika wajitokeze kupiga kura kuchagua viongozi wanaowapenda.
Kwa viongozi, wanachama na wafuasi wa vyama vya siasa nawaomba tushiriki katika mchakato wa uchaguzi tukizingatia taratibu na sheria za nchi. Nataka uchaguzi ujao uwe ni fursa ya kuimarisha zaidi demokrasia yetu na kupata viongozi walio bora. Kamwe tusiruhusu uchaguzi uwe chanzo cha migogoro, chuki, mivutano na uvunjifu wa amani ndani ya vyama, baina ya vyama na kwenye jamii kwa ujumla. Kila mmoja wetu anayo nafasi yake katika kuhakikisha kwamba haiwi hivyo.

Hitimisho

Ndugu Wananchi;
Watanzania Wenzangu;Napenda kumalizia salamu zangu za mwaka mpya kwa kumshukuru tena Mwenyezi Mungu kwa rehema zake alizotujalia mwaka 2009. Tumuombe atuzidishie maradufu yale yaliyo mema na kutunyooshea yasiyokuwa na maslahi mema kwetu katika mwaka ujao 2010. Nawashukuru tena Watanzania wenzangu wote kwa imani yenu kwangu na kwa ushirikiano wenu kwangu na kwa Serikali yetu. Umoja na juhudi za kila mmoja wetu kwa nafasi yake ndivyo vilivyotuwezesha kumaliza mwaka, taifa letu likiwi tulivu, lenye umoja na mshikamano. Ndiyo siri ya mafanikio tuliyoyapata. Tunajali na kuthamini michango yenu na ushirikiano mnaotupatia katika utekelezaji wa majukumu mliyotukabidhi.

Kesho, tunapouanza mwaka mpya, napenda kuwahakikishia kuwa mimi na wenzangu wote serikalini tutaendelea kuwatumikia kwa moyo wetu wote na nguvu zetu zote katika kuyatafutia majawabu matatizo yanayolikabili taifa letu. Naamini kwa umoja wetu, juhudi na maarifa tutafanikiwa.

Nawatakieni nyote heri na fanaka tele katika mwaka mpya 2010.Mungu Ibariki Afrika!Mungu Ibariki Tanzania!Asanteni kwa kunisikiliza!

Mungu Ibariki Afrika!
Mungu Ibariki Tanzania!
Asanteni kwa kunisikiliza!

Monday, December 21, 2009

President Kikwete Marks His Fourth Year As Great Peace Maker

AS President Jakaya Kikwete marks his fourth year in office today, the pillar of reconciliation of the Zanzibar longstanding political rivalry between his ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) on the island and the Civic United Front (CUF) stands boldly behind him as a sterling achievement.

The recent glorious hand shakes of the CUF's strongman Seif Sharif Hamad and Zanzibar President Amani Abeid Karume, political rivals hitherto blinded by fierce animosity for each other, may not have produced a tangible peace agreement, but their posture is no longer that of daggers drawn.

President Kikwete being the national chairman of CCM, it is unthinkable that such a national feat could have been pulled without his knowledge or involvement albeit remote. The meaning is that the doors, which were slammed shut and remained closed in the hostility time, have once more been flung open for progressive and friendly discussions.

The national political future is brighter and Mr Kikwete deserves accolades for the hopeful turnaround. The fight between CCM and CUF in Zanzibar has been raging for years, torn and stained by mistrust between the two parties.

Since the last general elections in 2005 the two camps have been looking daggers at each other, the chief bone of contention being the alleged flawed polls that CUF alleges put the CCM presidential candidate Amani Abeid Karume in power.

This accusation did not start with the 2005 General Election and a couple of Kikwete's predecessors had to reckon with it. The third-phase president Mr Benjamin Mkapa did his best to reconcile the Tanzania Indian Ocean political rivals, but only made a little dent if ever his efforts had any results at all, in the fight.

Mkapa's predecessor Ali Hassan Mwinyi, successor of Tanzania's founding president Mwalimu Julius Nyerere also had, so to speak, some brush with the acrimonious political situation as well. He merely slid down like one striving to climb a slippery hill.

Notably, both Mwinyi and Mkapa scored no remarkable effects on the matter. Kikwete's assumption of power made no indication for a solution to the dispute.

That, however, does not mean all hope had been lost since with the coming of a new leader, new hope and the people's expectations also grow. President Kikwete's youth may have been one element that generated hope for a solution to the Zanzibar's political impasse. His charisma too may have shone some light into the political future of the nation.

Yet to some other political players of the day the president must have appeared too young to bring a relief in the fight and if they gave him any chance to try, it was very little and they did it with much impatience.

Soon Doubting Thomases began hurling political stones at him as a failure because, given what they must have set as the deadline for a solution, peace between the two wrangling parties was long over due.

The isles political reconciliation has been to most political observers on the island, belated. So belated it has been that the country's chief opposition party CUF blamed the lack of reconciliation on the president, writing it off as a weakness signature of the presidency.

The CUF National Chairman Prof Ibrahim Lipumba could not hide his feelings for how Kikwete was handling the matter and got it off his chest when on 28 September this year he said: "President Kikwete has neither the desire nor the ability to resolve Zanzibar's political impasse."
The professor spoke as a disappointed politician and dismissed the President's remark on the issue as misguided. What President Kikwete has said was that he had not failed to resolve the Zanzibar's political quarrel. It had to be approached with keen diplomacy.

However, keen political observers will remember that with hardly a year in office the president said the government was working around the clock underground to resolve the Zanzibar's political deadlock and bring about peace to the islanders.

Given comments like those of Prof. Lipumba and others, only a few people must have believed that the government was working hard to resolve Zanzibar's political crisis. But now, and in retrospect specifically, what President Kikwete told the UN Secretary General Mr Ban Ki-moon at the UN Chief's office in New York recently that an amiable solution to the Zanzibar crisis was within the two parties power, can only be underscored by Mr Hamad and President Karume's meet and the resultant hearty handshake.

The inimical political state between CUF and CCM no doubt polarized the insular Tanzania and there can be no gainsaying that acrimony, which gained a global stature has done much harm to the Zanzibar government, particularly hurting the twin island of Pemba, CUF's stronghold.

Think of the EPA scandal. He has applied the rule of law. Talk of Richmond. The rule of law was left to govern. Now talk of the Zanzibar political impasse that left his predecessors gasping. He applied diplomacy even as he remained so much in the background.

Signing a tangible agreement of sorts is therefore neither here nor there as of now. Most material is that the ground for further peaceful negotiation has been prepared and the spirit that pulled the antagonistic parties of Hamad and Karume together appears to be growing stronger for not only more warm handshakes but likewise for a communal better tomorrow.

When Kikwete begins the race for a second term he can move around the country with his chest forward, his head held high in the pride of ability to bring peace. Peace is conducive for prosperity.

JE KIFANYIKE NINI KULETA MAENDELEO YA NCHI ??

Bonyeza kwenye picha!!

Waziri Ngelleja aongea na waandishi wa habari kuhusu kurudiwa kwa zabuni ya ununuzi wa mitambo ya umeme

Waziri wa Nishati na Madini William Ngelleja akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uamuzi wa serikali wa kuona busara ya kurudiwa kwa zabuni ya ununuzi wa mitambo miwili ya uzalishaji umeme na kuwataka wazabuni wote waliofuzu kwenye mchujo na kuthibitika kuwa wanauwezo wawasilishe takwimu za kuwezesha kufanyika kwa tathimini ya gharama za ununuzi wa mitambo, ujenzi na uendeshaji. Zabuni hiyo inahusu Mitambo miwili yenye uwezo wa kuzalisha Megawat 100 katika mkoa wa Dar es Salaam na Megawat 60 katika mkoa wa Mwanza. Kulia ni naibu waziri wa wizara hiyo Adam Malima.
Msomaji
Dar es salaam

Friday, December 18, 2009

RAIS JAKAYA ATIA SAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO YA MAREHEMU GAMA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha Maombolezo Nyumbani kwa Marehemu Gama Mbezi beach jijini Dar es Salaam, aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwemo Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa na Katibu Mkuu wa CCM
Msomaji
Dar es salaam

Rais Kikwete atembelea Chuo Cha wanayamapori mweka

Mwanafunzi wa Chuo cha Wanyamapori na uhifadhi, Mweka, Moshi vijijini Bi.Zawadi Mahinda akimwonesha Rais Jakaya Kikwete mbegu ya mti aina ya Msandali wakati Rais Kikwete alipokitembelea chuo hicho jana kujionea shughuli mbalimbali za masomo na tafiti zinazofanywa chuoni hapo.
Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza kwa makini mwanafunzi katika chuo cha wanyamapori Mweka, Bwana Gumbo Mbelwa Mhandeni alipokuwa akitoa maelezo ya tafiti juu ya uhifadhi wa pembe za wanayama mbalimbali wakati Rais Kikwete alipokitembelela chuo hicho

Msomaji
Moshi

Thursday, December 17, 2009

RAIS JAKAYA AWAKARIBISHA WAREMBO MISS EAST AFRICA KWA CHAKULA CHA JIONI

Rais Jakaya Kikwete na Mkewe mama Salma wakiwa katika picha ya pamoja na warembo wa Miss East Africa na kamati nzima ya mashinfdano hayo mara baada ya chakula cha jioni alichowaandalia Ikulu jana, warembo hao kutoka mataifa saba wanatarajia kupanda jukwaani kesho katika kinyang'anyiro kitakachofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam, mshindi wa shindano hilo atajinyakulia gari aina ya Toyota Celica Sports yenye thamani ya dolla 24.000.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na warembo kutoka mataifa mbalimbali wakati alipowakaribisha Ikulu jana kwa chakula cha jioni, waremb walipata nafasi ya kumuuliza rais maswali mbalimbali kuhusu mambo mbalimbali ya jamii uchumi michezo na mengine mengi.

Msomaji
Dar es salaam

Tuesday, December 15, 2009

DR. SHEIN ALIVYOWASILI DENMARK KWA MKUTANO WA MABADILIKO YA TABIA NCHI

Wakati jana mkutano wa mazingira huko Denmark ulipata kwikwi kwa muda baada ya nchi za Dunia ya tatu zikiongozwa na Africa kugomea kutoa ushirikiano, leo viongozi mbalimbali wameanza kuwasili kwaajili ya mkutano wa viongozi wa dunia kuhusu mabadiliko ya tabia nchi ambao utafanyika kesho.Tanzania inawakiliswa na Makamu wa Rais Dr Ali Mohamed Shein ambaye ndo anawasili muda huu.

Msomaji
Denmark

Monday, December 14, 2009

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Clement Mshana akifafanua jambo kuhusu matumizi ya Tovuti ya Wananchi katika kujibu hoja za wananchi wakati wa mafunzo ya tovuti kwenye kikao kazi cha makatibu wakuu wa wizara leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya makatibu wakuu wa wizara mbalimbali wakifuatilia kwa makini maelezo juu ya Tovuti ya Wananchi katika kujibu hoja mbalimbali za wananchi zinazowasilishwa serikalini wakati wa mafunzo ya tovuti kwenye kikao kazi cha makatibu wakuu wa wizara leo jijini Dar es salaam
Msomaji
Dar es salaam

Thursday, December 10, 2009

Jakaya Kikwete ateta na Mzee Kawawa Viwanja vya ikulu

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mzee Rashid Mfaume Kawawa katika viwanja vya ikulu jana usiku wakati wa hafla maalum ya kusherehekea miaka 48 ya Uhuru.
Msomaji
Dar es salaam

RAIS KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI IKULU

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha baraza la mawaziri ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi

Msomaji
Dar es salaam

Wednesday, December 9, 2009

Kikwete aongoza Watanzania kuadhimisha miaka 48 ya Uhuru uwanja wa Uhuru

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam walijitokeza katika uwanja wa taifa kusherehekea miaka 48 ya uhuru
Amiri jeshi mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua majeshi ya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 48 ya Uhuru yaliyofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama Jenerali Davis Mwamunyange wakati wa maadhimisho ya miaka 48 ya uhuru yaliyofanyika katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam leo asubuhi.
Mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliohudhuria maadhimisho ya miaka 48 ya Uhuru katika uwanja wa taifa leo.
Msomaji
Dar es salaam

Tuesday, December 8, 2009

Madereva watakiwa kutoa ushirikiano kwa kampuni ya majembe

Mkurugenzi mkuu SUMATRA Israel Sekilasa.
Benjamin SaweMaelezo Dar es Salaam .Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini imesema wakala wa ukusanyaji madeni sugu kampuni ya Majembe Auction Mart inafanyakazi chini ya Sheria ya utekelezaji wa masharti ya leseni za usafirishaji ya mwaka 2007.
Meneja wa Ufundi na Usalama wa SUMATRA Aron Kisaka alisema wameichagua Majembe Auction Mart ili kuimarisha usimamizi wa utoaji huduma za usafiri Dar es Salaam na kuwataka madereva wa daladala kutoa ushirikiano kwa taasisi hiyo
Bwana Kisaka alisema hayo hivi karibuni katika mkutano uliondaliwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Said Mwema uliokuwa na lengo la kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sekta ya usafiri nchini.
Aidha wadau na wananchi kwa ujumla wanaombwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa mamlaka zinazosimamia usafiri pamoja na Kampuni ya Majembe kwa lengo la kuimarisha usimamizi na kuboresha huduma hii muhimu kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam .
Bwana Kisaka alisema Majembe kazi yao ni kufuatilia utekelezaji wa masharti ya leseni ya usafirishaji abiria na si utozaji wa faini ambapo kazi ya utozaji wa faini hufanywa na SUMATRA .
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Said Mwema alisema utendaji wa kazi wa Majembe ni wa kitaalamu kwani Jeshi la Polisi liliwapa semina ya siku moja juu ya utendaji kazi na linaendelea kuwafunza zaidi kwa vitendo
Pia Bwana Mwema alisema Jeshi la Polisi limejiandaa vema katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka katika sehemu mbalimbali ikiwa ni pamoja na nchi kavu,hewani,majini,na mipakani katika kulinda usalama na amani nchini.
Kampuni ya Majembe Auction Mart ambayo imeteuliwa kufanya kazi hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja itatekeleza majukumu waliyopewa kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani.
Msomaji
Dar es salaam

Monday, December 7, 2009

Rais Jakaya Kikwete alivyorejea Nyumbani

Makamu wa Rais Dr.Ali Mohamed Shein akimpokea Rais Jakaya Kikwete muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jioni hii akitokea Trinidad na Tobago pamoja na Cuba ambapo alihudhuria Mkutano wa Jumuiya ya Madola na kufanya ziara kikazi nchini Cuba na Jamaika.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na waandishi wa Habari katika uwanja wa JK Nyerere leo Pembeni ni Makamu wa Rais Dr.Ali mohamed Shein.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifafanua jambo wakati alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa Mwalimu JK Nyerere akitokea katika visiwa vya Trinidad na Tobago ambapo alihudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za jumuiya ya Madola papoja na kufanya ziara ya kikazi nchini Cuba.Kushoto ni Makamu wa rais Dr.Ali Mohamed Shein

Msomaji
Dar es salaam

MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA KUMI YA BONDE LA MTO NILE

Makamu wa Rais Dr. Ally Muhamed Shein akifungua rasmi mkutano wa siku tatu ambao unaambatana na sherehe za miaka kumi ya bonde la mto Nile (Nile Basin Initiative) mkutano huo unakutanisha Mawaziri wa maji na wajumbe mbalimbali kutoka nchi ambazo bonde la mto nile limepitia na utajadili mmambo mbalimbali kuhusu jinsi ya kulinda na kuhifadhi mazingira pamoja na changamoto zinazojitokeza juu ya uhifadhi wa bonde hilo na unafanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais Dk.Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na mawaziri wa maji wa Bonde la Mto Nile mara leo baada ya kufungua mkutano wa siku tatu wa Nchi Shiriki za Bonde la Mto Nile (Nile Basin Initiative) ulioambatana na sherehe za kutimia miaka 10 tokea kuundwa kwa Ushirika huo, mkutano huo utajadili juu ya mafanikio yaliyopatikana tokea kuanzishwa kwake, changamoto pamoja na matarajio ya baadae katika kituo cha mikutano cha Mlimani City jijini.
Msomaji
Dar es salaam

Friday, December 4, 2009

Take skills back home, President Jakaya Kikwete tells Tanzanians studying abroad!!!

President Jakaya Kikwete has called on Tanzanians pursuing studies abroad to return home after finishing their courses so they can use their skills to improve the country’s socio-economic development.

Kikwete made the call on Wednesday at Melia Santiago Hotel here at a luncheon with students pursuing different studies in Santiago de Cuba province. Among the students, six are pursuing degrees in medicine, two in engineering and one in economics.

He urged the students to study hard so that at the end of their courses they returned home with full knowledge and skills that would help the country.

The president said the country was in dire need of medical doctors and other experts.
According to Tanzania’s Ambassador to Cuba Peter Kallaghe, there were about 43 students studying in different universities in Cuba.

In the afternoon, President Kikwete visited the Granjita Siboney Memorial House where Cuban revolutionary leader Alejandro Castro Ruz and his colleagues planned the failed revolution in 1953.

The said house was also visited by Mwalimu Julius Nyerere when he visited the region on September 20, 1974. Kikwete is the second Tanzanian president to visit Cuba.

Later in the evening Kikwete visited the Moncada Barracks, which was built in 1859, and was briefed about the history of the 1959 Cuban revolution.

President Kikwete is in Cuba for a three-day official visit following an invitation by his host, Cuban President Raul Castro Ruz.

President Kikwete was expected to complete his visit yesterday

Msomaji
Cuba
Jenista Mhagama Kamanda wa UVCCM Ruvuma !!
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi wa Fedha na Uchumi,Amos Makala(kulia),akimwapisha Jenista Mhagama kuwa Kamanda wa UVCCM wa Mkoa wa Ruvuma katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea. Katikati ni Katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma,Emmanuel Mteming'ombe na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM wa mkoa huo, Benedict Ngwenya.

Msomaji
Ruvuma

Balozi wa Marekani Akutana na Rais Karume

Balozi Mpya wa Marekani Nchini Tanzania Mhe Alfonso Lenhardt jana alimtembelea ikulu Rais wa Zanzibar Mh Amani Abeid Karume na kumweleza jinsi serikali ya nchi ya Marekani imeridhishwa na utaalamu unaotumika katika uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura linaloendelea visiwani Zanzibar. Balozi huyo pia alisifu jinsi zoezi hilo linavyoendelea kwa amani na utulivu katika maeneo mbalimbali katika vituo kadhaa alivyovitembelea alipowasili visiwani Unguja kabla ya kwenda ikulu kuonana na rais.

Msomaji
Zanzibar

AfDB lends Tanzania $245 mln for road upgrades

The African Development Bank (AfDB) approved a $245 million loan for a road project in Tanzania aimed at boosting the east African country's economy, the bank said on Thursday.
The work involves upgrading a 260-kilometre long road between Iringa and Dodoma, and another 193 kilometre stretch from Namtumbo to Tunduru, as well as strengthening Tanzania's road management, the AfDB said in a statement.
"The two roads are part of the regional corridor and will improve cross-border trade with neighbouring countries as well as enhance tourism and regional integration," it said.
The Tunis-based bank's shareholders include Africa's 53 nations and 24 non-African donor countries. It lends commercially to Africa's richest nations and at concessionary rates to poor ones.
The bank has stepped up lending during the global financial crisis, taking a lead on key projects to ensure countries press ahead with their long-term development while commercial lenders avoid committing new funds.
Msomaji
Rabat

Balozi wa Rwanda aishukuru Tanzania

Balozi wa Rwanda nchini Tanzania Bi. Fatuma Ndangiza akitoa tamko rasmi la Rwanda kujiunga na Jumuiya ya Madola na pia kushukuru mchango wa Tanzania kusaidia kufanikisha zoezi hilo leo jijini Dar es salaam. Rwanda sasa ni mwanachama wa 54 wa Jumuiya ya Madola kufuatia kukubaliwa na wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola katika mkutano uliofanyika Trinidad na Tobago.

Msomaji
Dar es salaam

maadhimisho wa siku ya walemavu nchini tanzania kwenye viwaja vya Mnazi Mmoja yalivyofana!!

Mkuu wa wilaya ya Ilala Evance Balama akimuangalia Abdala Nyangala ambaye ni mlemavu wa macho kutoka Mbagala Kibondemaji jinsi anavyochomeka uzi wa sherehani kwenye cherehani yake ambayo anaitumia kushona nguo za aina mbalimbali za jinsia ya kike na kiume. Mkuu wa wilaya huyo alikuwa mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya siku ya walemavu Duniani yaliyofanyika leo katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti ugonjwa wa UKIMWI (TACAIDS) Fatma Mrisho akiangalia batiki zilizotengenezwa na wanawake wajasiliamali wenye ulemavu wa aina zote wakati wa maadhimisho ya siku ya walemavu Duniani yaliyofanyika leo katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Wasanii wa kikundi cha sanaa cha walemavu wa aina zote cha Upendo kilichopo mkoani Dar es Salaam wakitoa burudani wakati wa maadhimisho ya siku ya walemavu Duniani yaliyofanyika leo katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Msomaji
Dar es salaam

Thursday, December 3, 2009

Balozi Mpya wa Rwanda amtembelea Spika Mhe Samuel Sitta

Balozi Mpya wa Rwanda Nchini Bi.Fatuma Ndagiza akimweleza Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta baadhi ya Mambo ambayo nchi yake ingependa kujifunza kutoka Bunge la Tanzania wakati alimpomtembelea kujitambulisha Ofisi kwa Spika jana . Balozi huyo wa Rwanda alimweleza Spika wa Bunge kuwa pamoja na mambo mengine Nchi yake inatarajia kuleta ujumbe Tanzania kwa lengo la kujifunza maswala ya Ushirika Nchini.
Msomaji
Dar es salaam

Kigoma Nao Pia Wagoma !!

Wasafiri wakiwa katika stesheni ya Kigoma wakisubuli usafiri wafanyakazi wamegoma hadi wapewe malipo yao na kampuni mpya ya kuendesha shirika hilo.Treni ya abiria ya kwenda Mwanza, Kigoma na Mpanda ikiwa imesimama katika stesheni ya Salanda mkoani Singida ili abiria wajipatie chakula juzi. Treni hiyo iliingia mkoani Kigoma jana baada ya madereva wake kuwa na mgomo katika vituo vya njiani mara kwa mara.
Jamani wafanyakazi wa Reli ya kati wanananyanyasika sana kwa kuchelewaeshewa malipo yao ya mishahara. hadi wamefikia uamuzi wa kugoma kushinikiza walipwe stahili zao
Baadhi ya abiria waliokuwa wakisafiri kuelekea Kigoma na Mwanza wakiwa wamezonga stesheni ya Manyoni baada ya dereva wa treni kugoma wakati walipofika eneo hilo wakidai kuwa hadi shirika hilo liwalipe mshahara wa mwezi wa November.
Huku hakuna magari ya kutoa upepo kama vile mgoma wa Dar.
vurugu kwenda mbele.
Abiria wakiwa ndani ya mabehewa wakisubiri hatima yao ya safari yao.

Msomaji
Kigoma

Utiaji wa Saini makubaliano kati ya Norway na Tanzania kusaidia Bonde la Mto Nile !!

Balozi wa Norway nchini John Lomy akiweka saini hati ya makubaliano ya kutoa dola za kimarekani milioni 3.4 kwa ajili ya upembuzi yakinifu wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Singida kupitia Arusha hadi Nairobi. Kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa Uendelezaji wa Bonde la mto Nile Bi. Henrietha Ndombe
Balozi wa Norway nchini John Lomy (kushoto) akibadilishana hati za makubaliano ya kutoa dola za Kimarekani milioni 3.4 na Mkurugenzi mtendaji wa Uendelezaji wa Bonde la mto Nile (NBI) Bi. Henrietha Ndombe kwa ajili ya upembuzi yakinifu wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Singida kupitia Arusha hadi Nairobi. Makubaliano hayo yalifanyika jana jijini Dare salaam.

Msomaji
Dar es salaam

Wednesday, December 2, 2009

2010 General Election set to cost 134 billion/-

NEC Election Director Rajab Kiravu

The National Electoral Commission (NEC) announced yesterday it would spend nearly 70bn/- in updating the Permanent Voters’ Register (PVR) and additional 64bn/- in organizing the 2010 General Election.
The planned spending reflects over 30bn/- increment compared to the last election held in 2005, where the spending structure was 38bn/- for the establishment of the PVR and 58bn/- for the presidential, parliamentary and councillors’ elections.
Both the NEC Election Director Rajab Kiravu and the commission’s vice-chairman Omar Makungu told editors from different media outlets at a special briefing held in Dar es Salaam that preparations for the General Election were going on as planned.
On NEC election spending in particular, Kiravu said his commission was optimist that a large portion of the money would come from local sources through next year’s National Budget.
“The government covered most of the costs in previous General Elections. Its contribution against donor funding accounted for 84 per cent in 2000 and 87 per cent in 2005. We hope that it will continue reducing donor dependency in next year’s elections,” he explained.
According to Kiravu, ballots would be cast at 55,000 polling centres throughout Tanzania mainland and Zanzibar and each one of them would be served by four commission staff members.
Regarding the updating exercise, he said the commission planned to reach a total of 21 million people and would apply a digital technology in mapping election areas and process.
On the election law, he said NEC was, among other things, seeking to push for the changing of the law allowing presidential and running mates to pull out from elections to avoid unnecessary inconveniencies and embarrassments.
Kiravu said the commission was still considering various options for subdividing some constituencies and results would be made public in future.
“We are still consulting various stakeholders and final results will be released when we are done with it,” he said, adding that the exercise is done routinely after a period of 10 years. The last time NEC subdivided constituencies was in 1995.
He explained that one of the important criteria under consideration was the size of the parliamentary debating chamber in the country’s designated capital, Dodoma. Any plan to add more constituencies should take into consideration the ability of the chamber to accommodate more lawmakers, Kiravu reminded.
Another criterion, he said, was the government commitment to increased women representation in accordance with the Southern African Development Community (SADC) protocol requiring signatories to ensure 50 per cent women representation in key decision-making bodies, including the Parliament.
He said NEC would not rush into subdividing the constituencies until it gets the exact position of the government on the matter for it to make clear calculations on the number of special seats and thereby determine the number of seats to be added.
Responding to a question on media endorsement of certain presidential candidates, he said with exception of state-owned media, which NEC is required to ensure give all candidates equal opportunity in their coverage, other media “are free” to endorse candidates of their choice.
Msomaji
Dar es salaam

Katibu mkuu wa CCM Mhe Yusufu Makamba akazia wito wa harambee ya uchaguzi wa CCM

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, ndugu Yussuf Makamba (Mb) ametoa ufafanuzi wa Kauli ya Katibu wa NEC Uchumi na Fedha, ndugu Amos Makala kutokana na habari iliyochapishwa na gazeti la Majira la Desemba Mosi, 2009 lenye Kichwa cha habari “Kauli ya fedha za kampeni moto CCM”.

Makamba alisema hapingani na Mkakati sahihi wa Idara ya Uchumi na Fedha wenye nia nzuri ya kukipatia Chama fedha kwa njia ya uwazi usiotia shaka yoyote. Kwa kuhofia mwandishi kupotosha jambo kubwa kama hili alimtaka awasiliane na Makala mwenyewe ili aweze kupatiwa ufafanuzi wa kina kwani ndiye Mkuu wa Idara mwenye Mamlaka ya kuelezea mipango na mikakati yote iliyo chini yake.

Alisema mwakani tuna uchaguzi mkuu wa Dola, moja ya kazi ya idara yake ni kubuni mikakati na mbinu halali za kukitafutia Chama fedha, ikiwa ni katika kutekeleza awamu ya tatu ya mradi wa kuimarisha Chama.

Mbinu hizo ni pamoja na kila mwanachama, wapenzi na wakereketwa wa CCM wanatakiwa kukichangia Chama, kuanzisha harambee katika ngazi zote za chama ili kutunisha mifuko ya uchaguzi katika ngazi hizo na kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano kupitia ujumbe mfupi (SMS) . Huo ni utaratibu wa kawaida ambao hutumiwa pia na taasisi za mbali mbali.

Makamba anasema Mpango huo wa Idara umetangazwa huko Ruvuma, na Kibaha na Mkuu wa Idara mwenyewe, anawaomba watu wenye mapenzi mema na CCM walione hili kwamba ni jambo jema na waliunge mkono kwani linatia matumaini.

Anakubaliana na nukuu ya Makala toka kwa mwana mapinduzi wa China, Mao Tsetung ya kwamba ukifanya jambo lolote na ukapingwa na mpinzani wako ujue umepatia endelea nalo na ukifanya jambo na ukaungwa mkono au kupongezwa na mpinzani wako jua kwamba umekosea mahali, acha mara moja mpango huo.

Kwa ufafanuzi huu Makamba anawataka wanachama wa ngazi zote wajiandae kukichangia chama chao na wao wanasubiri kwa hamu mapendekezo hayo ya Idara ili wayatafakari na kupeleka katika ngazi za juu kwa kuyapitisha.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI !!!
Imetolewa na:
Ofisi ya Katibu Mkuu
CCM,Lumumba
1/12/2009

MAADHIMISHO YA MIAKA 10 YA USHIRIKIANO WA NCHI ZINAZOTUMIA MTO NILE

Katibu mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Christopher Sayi kulia na kushoto ni Rayson Muhabuki Lake Victory Basin Water Officer.
Katibu mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Christopher Sayi akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo mchana wakati alipozungumzia maadalizi ya maadhimisho ya miaka kumi ya Bonde la Mto Nile kwa chi zote zinazoshiriki katika kuutumia mto huo ambayo yatafanyika nchini kuanzia Novemba 6-8 mwaka huu kwenye ukumbi wa Mlimani City.
Bwan Sayi amesema nchi hizo zimeichagua Tanzania kuwa mwenyeji wa maadhimisho haya kwakuwa pia ndiyo ilikuwa mwanzilishi wa ushirikiano huu ambao ulizaliwa hapahapa nchini Februari 22 mwaka 1999.
Msomaji
Dar es salaam

Tuesday, December 1, 2009

Wanafunzi wa shule za sekondari watakiwa kuzijua haki zao za msingi!!

Makamu Mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu na utawala Bora Mahfoudha Alley Hamid katika moja ya mikutano aliyowahi kuifanya na waandishi wa habari.

Wanafunzi wa shule za Sekondari hapa nchini wametakiwa kuzijua haki zao za msingi ambazo zitawasaidia kupata mahitaji yao ya muhimu bila ya kunyanyaswa na watu wachache ambao hawapendi kuzifuata haki za binadamu na utawala bora.

Wito huo umetolewa jana na Mary Massay ambaye ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya haki za Binadamu na Utawala bora wakati wa mdahalo wa wananafunzi wa shule za sekondari kutoka mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kuhusu haki za binadamu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa tume hiyo uliopo jijini Dar es Salaam.

Massay alisema kuwa ofisi za tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora imekuwa ikichapisha vitabu, majarida na vipeperushi mbalimbali vinavyoelezea haki za binadamu katika makundi mbalimbali hivyo basi kama wanafunzi hao watakuwa na bidii ya kusoma machapisho hayo yatawasaidia kujua haki zao.

Alisema, "Hivi sasa tume ya haki za binadamu na utawala bora imeamua kutokuwaacha nyuma watoto kwani nao ni wanajamii na ni sehemu ya haki za binadamu hivyo basi inawafundisha mambo ya muhimu kuhusiana na haki za binadamu ili nao watakaposhika madaraka hapo baadaye wajue la kufanya".

Aliendelea kusema kuwa wananchi wengi katika miaka ya hivi karibuni wamekuwa na uelewa mkubwa kuhusu haki za binadamu na utawala bora jambo la muhimu lililopo ni kuzilinda na kuzitetea haki hizo."Ni jukumu la watanzania wote kujua haki za binadamu ni zipi kwani katika maisha tunayoishi kila siku haki za binadamu zipo.

Kwa mfano unaweza kujiuliza Je shuleni watoto wanapewa nafasi ya kuchangia? Wazazi wanawashirikisha watoto wao katika mambo mbalimbali ya familia?, kama hakuna ushirikishwaji wa watoto basi haki za binadamu hazifuatwi hapo", alisema Massay.

Msomaji
Dar es salaam