Thursday, July 30, 2009

Exim Bank Watoa Mafunzo Kwa Wajasiriamali wa Kike !!

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya biashara kwa wajasiliamali wanawake yaliyoendeshwa na Benki ya Exim kutoka kulia ni Upendo Shoo ambaye ni mfanyabiashara Kariakoo, Caroline Mmbaga mfanyabiashara wa madini na Evelyne Masawe ambaye ni mfanyabiashara ya maduka ya dawa ya jumla wakifurahi kwa pamoja baada ya kukabidhiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo hayo ya wajasilimali wa kike yaliyofanyika kwa siku mbili katika Hoteli ya Golden Tulip. Exim bank wameamua kutoa mafunzo hayo ili wanawake wajue namana ya kuendesha biashara zao hasa kujua namna ya kuweka kumbukumbu za biashara hizo (Women Enterprenuers Training).
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Christina Manyenye kulia akimkabidhi cheti za ushiriki wa mafunzo ya biashara kwa wanawake Caroline Mmbaga baada ya kumalizikia kwa mafunzo hayo katika hoteli ya Golden Tulip.
Meneja masoko na Mawasiliano Christina Manyenye akiwaelezea njinsi ya kuweza kujua shughuli za benki ya Exim wakati wa semina ya wajasiliamali wa kike iliyoandaliwa na benki hiyo ikiwa na lengo la kuwafanya wanawake waweze kujua namna ya kuweza kuhifadhi kumbukumbu zao za kibiashara na namna ya kujua kukopa katika mabenki.
Meneja masoko na mawasiliano wa Exim bank Christina Manyenye akimkabidhi cheti Evelyne Masawe wakati wa kuhitimu mafunzo ya kujua kutunza pesa na namna ya kuweza kuanzisha biashara.
Mtaalamu wa ushauri wa kibiashara (financial literacy) Issaya Lwechungura akigawa karatasi kwa wajasiliamali zenye maelekezo namna ya kujua kutunza mahesabu ya biashara wakati wa makutano wa mafunzo.

Msomaji

Dar es salaam

Tuesday, July 28, 2009

Moto ulivyoteketeza meli ya Bakhresa

Moto ulivyoteketeza meli ya bakhresa ilikuwa ya mizigo ni ya mv pemba, ilikuwa ikikaribia kutia nanga.
Harakati za kuuzima moto zikiendelea

Msomaji

Idadi ya watalii wanaoingia nchini Tanzania yazidi kuongezeka

Dk Ladislaus Komba
Pamoja na mtikisiko wa uchumi unaoendelea duniani, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk Ladislaus Komba amesema tathmini ya awali ya biashara ya utalii nchini inaonyesha kuwa idadi ya watalii inaongezeka hapa nchini kama ilivyopangwa.
Dk Komba alisema hali hiyo inaweza kuendelea kuwa nzuri ikiwa huduma na miundombinu katika maeneo ya utalii itaboreshwa na kutoa unafuu kwa watalii. Alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.
Alisema tathmini inaonyesha kuwa idadi ya watalii inazidi kuongezeka na kwamba kinachotakiwa kufanywa na serikali kwa sasa, ni kuondoa baadhi ya kasoro za huduma kwenye sekta hiyo. "Watalii wengi wanaokuja Tanzania kwa sasa ni kwa ajili ya mapumziko na wengi wanatoka Marekani, Uingereza, Ujerumani na Italia", alisema.
`Watalii wameongezeka kwa asilimia 11.6 katika (kipindi cha mwaka 2007/2008) na pato linalotokana na matumizi ya kitalii nalo limeongezeka kwa asilimia 26, ukilinganisha na mwaka 2006,`` alisema Dk Komba wakati akiwa anahudhuria mkutano wa wadau wa sekta ya utalii katika kujadili tafiti mbalimbali zilizofanywa na wataalamu serikalini.
Maelezo ya Dk Komba yamekuja wakati ambapo Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga akisema serikali inatathmini mfumo wa utalii kwa ujumla ili kuangalia kama kuna uwezekano wa kupunguza gharama za kitalii au la.
Hii ilitokana na shinikizo kutoka kwa baadhi ya wadau wa sekta binafsi wa utalii kuitaka serikali kupunguza gharama hizo kama ilivyofanya
Kenya hivi karibuni ili kuwavutia watalii wanaoshindwa kuja kutokana na kuathirika kifedha baada mtikisiko wa kiuchumi duniani. Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Tafiti, Mafunzo na
Takwimu wa wizara hiyo, Ibrahim Mussa alisema maboresho mengine yanayopaswa kufanywa ni kuweka mashine za kutoa fedha kwa njia ya viza, kwenye vituo vya utalii.
''Unajua mara nyingi watalii hawapendi kutembea na fedha taslimu, wanataka hata wakifika kwenye mahoteli baada ya kutumia wakae na fedha zo kwenye kadi zao,`` alisema Mussa.
Msomaji
Dar es salaam

Tanzania launches bank for women

Tanzania has launched a bank aimed specifically at women in what officials say will be an empowering move.

The bank says women need only an ID card or passport to open an account, unlike other banks which require title deeds or other proofs of wealth.

And applicants need only 3,000 Tanzanian shillings ($2) in savings - much less than other banks.
Although the bank, which is based in Dar es Salaam, targets women with its services, men can also open accounts.

The bank's management says it will give women expert help and advice.
'Too shy'

Margareth Mattaba Chacha, the managing director, said: "We know some women hesitate to come forward - they are too shy and think they don't know anything.

"But here we're going to have a big group of professionals to take women through step-by-step until we really reach our women."

The BBC's Zuhura Yunus, in Dar es Salaam, says 110 people had opened accounts at the Tanzania Women's Bank by the end of the morning.

Officials hope there will be 200 more people coming in every day and say the Dar es Salaam branch is just the beginning of a countrywide network.

Margaret Sitta, Minister of Community Development, Gender and Children, said the bank would empower women, but stressed that the accounts were open to all.

Msomaji
Dar es salaam

Two Americans among passengers killed in road accident in northeastern Tanzania

Two Americans were among the passengers killed in a road accident when a bus crashed into a truck in northeastern Tanzania on Sunday afternoon, local media reported on Tuesday.

One of the dead Americans has been identified as Kathryin Baxter, holder of passport number 089355273 issued in New Orleans,the United States, in December 2000. But the other dead American has not been identified, the local daily the Citizen reported.

Around 30 were killed when the accident took place in Korogwe, about 210 km northwest of the Dar es Salaam as the speeding bus was traveling to Dar es Salaam from the northwestern town of Arusha. The police are holding the driver of the bus, Samwel Paulo, 34, for questioning.

Most of Tanzanians rely on buses as their daily public transport between towns and high speed is usually blamed for the road accidents.

Nearly 3,000 people were killed in road accidents last year in Tanzania, the traffic police authority had said.

DAR ES SALAAM, July 28

Monday, July 27, 2009

33 killed in Tanzania bus accident

The state-owned broadcaster is reporting that a bus has crashed into a truck in northeastern Tanzania, killing 33 people. Tanzania Broadcasting Corp. is quoting unnamed police officials as saying the accident happened Sunday afternoon in Korogwe, about 210 kilometers (130 miles) northwest of the commercial capital, Dar es Salaam. The bus was traveling to Dar es Salaam from the northwestern town of Arusha, the station reports.

Five people remain at the hospital at Korogwe. Other passengers had minor injuries and were discharged from the hospital after being treated, the station says.
Buses are Tanzania's main public transport between towns and many bus drivers exceed the speed limit.

Msomaji
Arusha

WAGONJWA TARAFA YA KATERERO MKOANI KAGERA WALALA NA MAITI WODINI

Katoro Wagonjwa wa kijiji cha Katoro kata ya Katoro Tarafa ya Katerero wilaya ya Bukoba vijijini wanaolazwa katika kituo cha afya Katoro wanakabiliwa na tatizo la kulala na maiti wodini kutokana na kituo hicho kutokuwa na chumba cha kuhifadhia maiti.

Hayo yamesemwa jana na daktari Mfawidhi wa kituo hicho Augustine Mnyamukama wakati akisoma risara ya watumishi kwa mke wa Rais Mama Salma Kikwete aliyefika kituoni hapo kwa ajili ya kutoa vitanda vya kujifungulia viwili, vitanda vya kawaida vitano na mashuka kumi.

"Kama mgonjwa akifariki katika kituo chetu hakuna mahali pa kuhifadhia maiti jambo ambalo linawafanya wagonjwa wa wodi husika kulala na maiti hadi ndugu wa marehemu watakapokuja kuichukua maiti na kwenda kuizika", alisema.

Dk. Mnyamukama aliyataja matatizo mengine yanayoikabili kituo hicho kuwa ni upungufu wa watumishi, upungufu wa madawa muhimu pamoja na vifaa, vitanda vya kuzalishia na vya kawaida, hakuna wodi maalum ya akina mama wajawazito na wanaume, kutokuwepo kwa huduma ya upasuaji wa dharula , nyumba za watumishi, umeme na maji. Aliendelea kusema kuwa pamoja na matatizo hayo jitihada za pamoja zinafanyika kati ya wananchi na Serikali ili kuweza kutatua matatizo hayo.

"Hivi sasa tumefanikiwa kupata gari la kusafirisha wagonjwa wa dharula hali iliyosababisha kupungua kwa vifo wa watoto na kina mama wajawazito, tunatoa huduma ya Ugonjwa wa UKIMWI pia Halmashauri ya wilaya ya Bukoba kwa kushirikiana na wafadhili (JRF) wamewezesha kukarabatiwa kwa wodi ya watoto", alisema.

Aliyataja magonjwa yanayowasumbua wananchi wa eneo hilo kuwa ni maralia, magonjwa ya nayoshambulia mfumo wa hewa, kuharisha, minyoo, upungufu wa damu, vichomi na magonjwa yanayosababishwa na virusi vinavyosababisha Upungufu wa Kinga Mwilini.

Akikabidhi vifaa hivyo Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) aliwataka wananchi wa eneo hilo kuvitunza vifaa hivyo ili viweze kutumika kwa muda mrefu kwa vizazi vijavyo. "Katika maeneo mengine wananchi wamekuwa wakiharibu na hata kuiba vifaa mbalimbali vinavyotolewa na wafadhili jambo ambalo limekuwa likikatisha tamaa na kurudisha nyuma maendeleo ya nchi", alisema.

Kituo hicho kipo umbali wa kilomita 58 kutoka Hospitali ya mkoa kilijengwa mwaka 1947 kikiwa zahanati na ilipofika mwaka 1974 kilipandishwa hadhi na kuwa kituo cha Afya kinahudumia zaidi ya wakazi 13,574 pamoja na kuhudumia zahanati za Kishogo, Butainamwa, Kaibanja, Ruhunga, Kihumulo na Kyamulaile.

Kwa upande wa tiba kituo hicho kinatoa huduma ya wagonjwa wanaotibiwa nyumbani na kurudi (OPD), kutibu wagonjwa kwa wastaini 90 kwa siku na kulaza wagonjwa wa wastani kumi na tisa kwa siku. Pia kituo kinatoa huduma za kinga kwa mama na mtoto, uzazi wa mpango, elimu ya afya kwa jamii, huduma ya mkoba, kuzuia maambukizi ya Virusi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na upimaji wa virusi kwa hiari.

Mama Kikwete yuko katika ziara ya kikazi ya siku tatu katika mkoa wa Kagera yenye lengo la kuchangia juhudi za kupunguza vifo vya kinamama vinavyotokana na uzazi kwa kutoa vifaa vya huduma ya afya ya uzazi, hususan katika wodi za wazazi. Kuhamasisha juhudi za maendeleo kwa wanawake kupitia vikundi vya SACCOS na benki za vijijini- VICOBA.

Kuhamasisha juhudi za kupunguza matukio ya mimba na utoro mashuleni, kuhamasisha vikundi vya SACCOS na benki za vijijini- VICOBA na kuhamasisha juhudi za kupunguza matukio ya mimba na utoro mashuleni.

Msomaji
Kagera

Saturday, July 25, 2009

ZITTO KABWE WA CHADEMA AANZA KULAUMIWA.

Mbunge wa Jimbo la Kigoma kaskazini bwana zito kabwe ameanza kulaumiwa na wapiga kura wake kwa madai kwamba hana msaada naona kwamba hajawatembelea tangu achaguliwe miaka minne iliyopita. habari zilizotufikia mchana wa leo zinadai kwamba wapiga kura hao walitoa shutuma hizo walipokuwa wakizungumza na wajumbe wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa kigoma ambao alikuwa katika vijiji kadha vya jimbo hilo la kigoma kaskazini.
Msomaji
Dar es salaam.

Friday, July 24, 2009

MAREKANI YASEMA IKO TAYARI KUIUNGA MKONO GEORGIA

Makamu wa kwanza wa rais wa Marekani bwana Joe Biden amesema kwamba nchi yake iko tayari kuiunga mkono Georgia katika vita yake na Urusi. Biden ametoa kauli hiyo akiwa mjini Tbilisi ambao ni mji wa Georgia, Urusi na Georgia zimekuwa na mapigano na malumbano kwa muda mrefu sasa hali inayosababisha kupotea kwa amani katika eneo hilo. Marekani ilikwisha iagiza serikali ya Urusi kuondoa majeshi yake katika eneo la mapigano lakini Urusi ilipuuza na kwamba bado majeshi ya nchi hiyo yapo katika maeneo ya Abkhazia na Ossetia ambayo ni maeneo ya Georgia.

Msomaji
Rusia



BLOG HII YA CCM KUANZA TENA KUPOKEA MAONI

Ndugu wajumbe,
Baada ya kupokea maombi mengi ya wasomi na wachangiaji wa habari na picha kwamba wangependa kuona na kusoma maoni mbali mbali kwenye mtandao huu tunapenda kuwa taarifu kwamba kuanzia sasa tutaanza tena kupokea maoni mbalimbali.

Hivyo watumaji wa maoni mnaombwa kuendelea kutuma maoni yenu kama kawaida.

ILANI:
Tunaomba kusisitiza kwamba lugha zisizo na maadili hazikubariki, na kwamba tushirikiane kulinda maadili ya mtandao wetu ambao unatizamwa na watu wengi wenye lika tofauti.

Nawakaribisha tena kutoa maoni.

UONGOZI
CCM - TAWI LA MAREKANI

Monday, July 20, 2009

GRIZZLIES SIGN THABEET TO $7.7M CONTRACT

First-round draft pick Hasheem Thabeet has signed with the Memphis Grizzlies

The 7-foot-3 center from Connecticut was the second pick in the draft. Thabeet is due to make about $7.7 million over two years under the rookie salary scale.

Thabeet is the first Tanzanian-born player drafted by an NBA team. He averaged 13.6 points, nearly 11 rebounds and 4 blocks per game at UConn last season and was named Big East co-player of the year.

Thabeet is also second on the Big East's all-time blocked shots list behind Patrick Ewing.

Msomaji
U S A

SALAAM KUTOKA KWA MSOMAJI WETU DAR ES SALAAM

Kituo kikubwa cha Basi yaendayo mikoani maeneo ya ubungo jijini dar es salaam
Kituo kikubwa cha dala dala maeneo ya ubungo
Msomaji wetu wa dar amendelea kutuma salaam kwa watanzania wote waliopo nje na ndani ya nchi na anependa kwa wote waliopo nje ya jiji la dar es salaam wajionee jii kulivo kwa sasa. Pia amehaidi kuwa ataendele na utaratibu huu wa kuwatumia picha za jiji la dar hili mkumbuke nyumbani
CCM nchini Marekani inatoa shukrani kwa niaba ya wasomaji na watanzania wote kwa ujumla

Tanzania’s Simba Omit Key Striker Musa Hassan Mgosi For The Up-coming Season

The player is heading for Norway for trials which he must now pass or face the whole season without a club

A source within the TFF confirmed that Mgosi has been dropped from the Msimbazi Street club’s list for the next Premier League season.

The source said that Mgosi, who is reportedly going for trials at Norway’s Kongsvinger, has been replaced by Mtibwa Sugar’s budding striker Zahoro Pazi.

“Mgosi brought the letter signed by Simba chairman Hassan Dalali, confirming that the club has decided to cut off his name in the list of player who will feature for the club next season,” said the source.

Saturday was the deadline for the Premier League teams to submit their lists of players for next season's league. When asked to pass comment, Mgosi was shocked by the report that his name has been removed. However, he confirmed that he would be leaving for Norway soon.

“I’ve not been informed about the cut-off. I don’t think Simba's officials could do such a thing. I’ll go for trials in Norway and you cannot be sure whether you will pass or not. It’s gambling,” the shocked Mgosi said. “If the deal fails to go through, I’ll have to rejoin Simba.”

If he is successful, Mgosi will join former team-mate Henry Joseph, who recently signed a four-year deal with the Norwegian club, as well as Nigerian youngster Emeh Izuchukwu

Msomaji
Dar es salaam

Tanzania says Zain to give up state telco shares

Zain Tanzania, part of Kuwait's Zain (ZAIN.KW), plans to give up its 35 percent stake in state-run Tanzania Telecommunication Co (TTCL), the east African nation's technology minister said on Monday.

"Recently, Celtel has shown interest in exiting. But there's need for consultation before that happens," said Peter Msolla, minister for communications, science and technology.

Msolla made the remarks while presenting his ministry's budget in Dodoma. Zain was originally known as Celtel when the then-Dutch firm bought its stake in TTCL in 2004, and the Tanzanian government has retained that name in its records.

Msolla said Zain, TTCL and Consolidated Holdings Corp, which holds shares in state-run corporations on the government's behalf, met late last week over the matter.

"In principle, they have agreed to end the partnership and Celtel exits. Celtel's 35 percent shareholding will revert to the government. We will continue talks on how to offload those shares," he said.
The government holds the other 65 percent of TTCL. Zain is in talks with potential buyers for a stake in its African operations, but it denied earlier this month that it had reached a deal to sell the unit to Vivendi (VIV.PA.

TTCL had a monopoly in fixed-line phone services that ended in 2005. It has long been plagued by complaints from customers over inefficient services.

After peaking at 236,493 fixed-line users in 2007, its customers fell to 116,265 by end of 2008 before picking up to 170,021 in March, according to data from regulator Tanzania Telecommunications Regulatory Authority.

TTCL started mobile phone services in 2008, picking up 105,804 customers in the first year. As of March, it had 121,233 mobile users.

Tanzania, a nation of 40 million people, had 13.1 million phone subscribers at the end of 2008. This had jumped to 14 million by the end of March, with 99 percent of them being mobile customers.

Last week the government said it had reached an amicable agreement with SaskTel International, a subsidiary of Canada's SaskTel, to end a three-year contract to manage TTCL. The pact, entered into in 2007, was worth up to $5 million.

"They left officially on July 12, so now it's like TTCL is starting afresh and is under interim leadership," Msolla said.

DAR ES SALAAM, July 20 (Reuters) -

Sunday, July 19, 2009

RAIS JAKAYA KIKWETE AMEMTEUA MSAIDIZI WAKE KATIKA DIPLOMASIA

Rais Jakaya Kikwete amemteua, Zahra Mwanasharif Nuru, kuwa Msaidizi wa Rais wa masuala ya diplomasia. Taarifa iliyotolewa alhamisi wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, na Katibu Mkuu, Ikulu, Michael Mwanda, kwa niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi, ilisema kuwa uteuzi huo ulianzia juzi (Jumanne).

Taarifa hiyo ilisema kuwa Zahra Nuru anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Andrew Daraja ambaye alihitimisha mkataba wake wa utumishi wa umma.

Ilisema Zahra Nuru amepata kuajiriwa na Umoja wa Mataifa. Kabla ya kuhitimisha mkataba wake na Umoja wa Mataifa, Zahra Nuru alikuwa mtaalam na Mshauri Mwandamizi wa Katibu Mkuu Msaidizi na Mshauri Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Afrika.

Msomaji
Dar es salaam

Tuesday, July 14, 2009

Waziri wa nishati na madini Mhe William Ngeleja akizindua mtambo wa kusindika gesi asilia Ubungo jijini Dar es Salaam

Waziri wa Nishati na Madini Mhe William Ngeleja (wa pili kulia) akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mtambo wa kushindilia gesi asili uliofanyika leo huko Ubungo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo Ethur Mwakapugi na kushoto kwa waziri ni Meneja Mkuu wa PanAfrican Energy (T) Ltd Pierre Raillard.
Waziri William Ngeleja akiweka gesi katika gari wakati wa uzinduzi wa mtambo huo wa kushindilia gesi asili uliofanyika leo huko Ubungo jijini Dar es Salaam. Aliyesimama nyuma ya waziri ni Meneja Mkuu wa PanAfrican Energy (T) Ltd Pierre Raillard.
Msomaji
Dar es salaam

RAIS JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA MKUU WA MAJESHI WA AFRIKA KUSINI

Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa majeshi ya Tanzania na Afrika Kusini na maafisa wengine wa nchi hizi mbili wakati walipoonana na rais Ikulu jijini dar es salaam, kushoto ni Jenerali Godfrey Ngwenya Mkuu wa majeshi Afrika kusini na kulia ni Jenerali Davis Mwamunyange Mkuu wa majeshi wa Tanzania.
Rais Jakaya Kikwete akimkaribisha Ikulu Mkuu wa Majeshi ya Afrika ya kusini Jenerali Godfrey Ngwenya wakati alipomtembelea ikulu jijini Dar es salaam


Msomaji
Dar es salaam

Monday, July 13, 2009

Waziri wa mambo ya nchi za nje Mh. Bernard K. Membe Kumwakilisha Rais Jakaya Kikwete Kwenye Mkutano wa NAM,Misri..

Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM) unatarajiwa kufanyika Sharm El Sheikh,Misri tarehe 15 hadi 16 Julai, 2009.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mhe. Bernard K.Membe atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete katika mkutano huo.

Mkutano huo utatanguliwa na mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za NAM unaofanyika tarehe 13 na 14 Julai,2009.Maudhui ya mkutano huo ni pamoja na Mtikisiko wa Kiuchumi Duniani;Mageuzi katika Vyombo vya Fedha Duniani; Mageuzi katika Umoja wa Mataifa na Migogoro ya Kisiasa Duniani.

Aidha, mkutano huo unategemewa kupitisha maazimio mbalimbali yaliyopendekezwa na mkutano wa Mawaziri huko Tehran, Iran mwaka 2008 na ule wa Havana,Cuba mwezi Mei, 2009.Mhe.Waziri Membe ataambatana na Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, Mhe. Dkt.Augustine Mahiga Na Balozi wa Tanzania nchini Misri,Mhe.Ali Shauri Haji.

IMETOLEWA NA:
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO
WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM

M-PESA yaja Tanzania !!

Mkuu wa wa maswala ya kibiashara wa Benki ya Afrika Wasia Mushi (kulia) akiongea wakati wa hafla ya makubaliano ya ushirikiano huo baina ya Benki ya Afrika na Vodacom kuhusiana na M-pesa. Wateja wa benki ya BAO watapata huduma ya kutuma pesa na kupokea pesa kupitia simu zao za mikononi, M-PESA. kushoto ni Mkuu wa Udhamini na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza.akimsikiliza kwa makini katika hafla iliyofanyika katika ofisi za benki hiyo jijini. Mtaalamu wa M-pesa Magesa Wandwi akielezea jinsi ya huduma za M-pesa zinavyoendeshwa wakati wa uzinduzi wa ushirikiano wa kutoa huduma hiyo kati ya benki ya Afrika BOA na Vodacom , ambapo BOA wanakuwa wakala wa Kwanza wa Kampuni ya Vodacom kutoa huduma hiyo M-PESA kupitia benki yao ,(katikati)Mkuu wa udhamini na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza,na Mkuu wa maswala ya kibiashara wa Benki ya Afrika Wasia Mushi.
Mkuu wa Udhamini na mawasiliano wa Vodacom George Rwehumbiza akipongegezana na Mkuu wa maswala ya benki ya Afrika (Head of Commercial Banking Wasia Mushi , baada yakumalizikika hafla ya makubaliano ya ushirikiano wa kutoa huduma ya M-pesa ambapo benki hiyo itakuwa wakala mkuuwa utoaji wa huduma hiyo katikati ni Head of risk and credit Erick Ouattara.
Mkuu wa Udhamini na mawasiliano wa Vodacom George Rwehumbiza akipongegezana na Mkuu wa maswala ya benki ya Afrika (Head of Commercial Banking Wasia Mushi , baada yakumalizikika hafla ya makubaliano ya ushirikiano wa kutoa huduma ya M-pesa ambapo benki hiyo itakuwa wakala mkuuwa utoaji wa huduma hiyo katikati ni Head of risk and credit Erick Ouattara
Mkuu wa udhamini na mawasiliano wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza(kushoto)akiwapa maelekezo namna ya matumizi ya M-PESA. Maafisa wa Benki ya Afirika(BOA) Selemani Ponda Head of Finance , Patrick Maleo, Head of Legal and Administion na Wasia Mushi Head of Commercial Baking namna ya huduma ya M pesa inayotolewa na Vodacom mara baada ya Benki hiyo kuwa ya kwanza inchini Tanzania inayoshirikiana na Vodacom kutoa huduma hiyo.
Msomaji
Dar es salaam

Sunday, July 12, 2009

Mama Kikwete kijijini SOS nchini Zambia

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa amembeba mtoto Monde Muteka anayelelewa katika kijiji cha watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha (SOS) kilichopo katika mji wa Livingstone nchini Zambia . Mama Kikwete alitembelea katika kijiji hicho hivi karibuni ili kuona jinsi watoto hao wanavyolelewa kituoni hapo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (katikati) na Mke wa Rais wa Zambia Mama Thandiwe Banda (kulia) wakiangalia chumba wanacholala baadhi ya watoto wanaolelewa katika kijiji cha watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha (SOS) kilichopo katika mji wa Livingstone nchini Zambia . Kushoto ni Esther Balengu ambaye ni mama mlezi wa nyumba hiyo. Wake hao wa Marais walitembelea katika kijiji hicho hivi karibuni ili kuona jinsi watoto hao wanavyolelewa kituoni hapo.

Msomaji

Tuesday, July 7, 2009

JIONEE ZIARA YA RAIS KIKWETE NCHINI ZAMBIA ILIVYOKUWA

Rais Kikwete (kati kushoto) mkutanoni na Rais Rupiah Banda wa Zambia (kati mstari wa kulia) kushoto kwake ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko Dr. Mary Nagu na kulia kwake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Seif Ally Idd. Katika mkutano huo walijadili kuhusu Reli ya Tanzanzia na Zambia (TAZARA). Rais Kikwete alikuwepo katika ziara ya kikazi Nchini Zambia kwa mda wa siku tatu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kati) akiwa kwenye mkutano na Rais wa Zambia Rupiah Bwezani Banda (hayupo pichani) kushoto kwake ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko Dr. Mary Nagu na kulia kwake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Seif Ally Idd. Lengho la mkutano huo ilikuwa kujadili kuhusu Mamlaka ya Reli ya Tanzanzia na Zambia (TAZARA).
Rais Jakaya Kikwete akipeana mkono na mmoja wa wazee wa mila wa Kabila la Lwiindi Gonde, mara baada ya yeye na Mwenyeji wake Rais wa Zambia, Rupiah Banda (katikati), kukabidhiwa zawadi za mikuki wakati wa sherehe za kimila zilizofanyika katika eneo la Monze, kusini mwa Zambia .
pamoja na kuhudhuria sherehe za aina hii rais Kikwete ambaye alikuwa katika ziara ya kiserikali ya siku tatu walizungumza na mwenyeji wake suala linalohusu urithi wa Nyerere na Kaunda, reli ya Tazara na kuagiza madeni yaangaliwe namna ya kulipwa na miundo mbinu iangaliwe kwa kuongea na China ambayo ipo tayari kusaidia.

Msomaji
Zambia

RAIS JAKAYA KIKWETE NDANI YA SABA SABA

Rais Jakaya Kikwete akiongozana na Mkewe Mama Salma Kikwete walipotembelea Maonesho ya saba saba jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na mmoja wa wajasiliamali waliopo kwenye banda la shirika lisilokuwa la kiserikali linalotoa mikopo kwa wafayabiashara ndogondogo Pride Tanzania wakati alipotembelea katika banda hilo jioni hii katika maonyesho ya 33 ya biashara ya kimataifa yanayofanyika kwenye viwanja vya saba saba Kirwa jijini Dar es alaam, wa pili kutoka kulia ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na katikati ni Meneja mkuu wa Shirika la Pride Shimimana Ntuyabaliwe.


Msomaji
Dar es salaam

Monday, July 6, 2009

UCHAGUZI BIHARAMULO, CCM YASHINDA KWA KISHINDO !!!

Wanachama wa CCM wakisherehekea ushindi walioupata katika uchaguzi ndogo wa mbuge wa wilaya ya Biharamulo Magharibi kuziba nafasi ya ubunge iliyoachwa wazi kutokana na kifo cha mbunge wake Phares Kabuye.
Wapigaji kura wa Biharamulo mkoani Kagera, wakitumbukiza kura zao katika kituo cha shule ya msingi Umoja Biharamulo ili kuziba nafasi ya ubunge iliyoachwa wazi kutokana na kifo cha mbunge wake Phares Kabuye.



Habari kutoka Biharamulo nikwamba CCM imeshinda kwa kishindo uchaguzi mdogo katika wilaya ya Biharamulo Magharibi katika kujaza nafasi ya ubunge iliyoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa wilaya hiyo marehemu Phares Kabuye aliyefariki dunia mwanzoni mwa mwaka huu. Mgombe wa ubunge tiketi ya CCM Mh. Oskal Mukasa ameibuka kidedea kwa ushindi wa jumla ya kula 17,561 ambazo ni zaidi ya asilimia 51 ya kula zote zilizopigwa. Idadi ya wapigakula waliojitokeza inakadiliwa kuwa ni 34,000 kati ya 87,000 ya waliojiandikisha kupiga kura

Msomaji
Biharamulo

KIWANDA CHA KUTENGENEZA MAGARI TANZANIA CHATENGENEZA MAGARI YANAYOENDANA NA SOKO LA DUNIA

Jeshi la wananchi ( JWTZ )Kiwanda cha NYUMBU wametengeneza Roli aina ya NYUMBU linalovutia hata kwa kulitazama na ambalo pia ni Imara sana, hii ni hatua kubwa kwa jeshi letu. Hapa ni kwenye maonesha ya saba saba yanayofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere Barabara ya Kirwa. Tunajionea Teknolojia nchini Tanzania inavyokuwa kila mwaka, nifaraja kubwa kwa upande wa Teknolojia yetu hasa katika kutengeneza Magari

Msomaji
Dar es salaam

Waziri Mkuu Mh. Mizengo Peter Pinda ndani ya saba saba

Waziri Mkuu Mh. Mizengo Peter Pinda akisalimiana na mmoja wa wajasiliamali wanaowezeshwa kwa mikopo na shirika la Pride Tanzania, wakati alipotembelea banda lao kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika hilo, katika kuwakopesha wafanya biashara ndogondogo kwenye maonyesho ya 33 ya biashara ya kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya saba saba jijini Dar es alaam.

Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akisalimiana na viongozi wa shirika la Prida Tanzania wakati alipotembelea banda lao tayari kwa kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na wajasiliamali wa shirika hilo, kutoka kulia ni Meneja mkuu wa shirika hilo Tanzania Bi Shimimana Ntuyabaliwe na kushoto ni mwenyekiti wa bodi ya Pride Tanzania Mzee Idd Simba

Msomaji
Dar es salaam

Saturday, July 4, 2009

Tanzanian President Jakaya Kikwete, center leaves after attending the closing session at the third day of the 13th African Union summit of heads of state and government in Sirte, Libya Friday, July 3, 2009. African Union leaders were debating Friday a hotly contested draft declaration that could deal a heavy blow to efforts by the International Criminal Court to prosecute war criminals from the continent.

Friday, July 3, 2009

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania na Rais Jakob Zuma mkutanoni nchini Libya

Rais Jakaya Kikwete akiongea na Rais wa South Afrika Jacob Zuma Kwenye Mkutano wa Umoja wa Afrika uliofanyika katika jiji la Sirte nchini Libya .
Mama Salma Kikwete (katikati) akiwa na wake wa viongozi katika mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika nchini Libya.

Thursday, July 2, 2009

Tanzania's President Jakaya Kikwete (C) talked with unidentified officials at the Southern African Development Community (SADC) special summit on Madagascar in Johannesburg on June 21, 2009. The summit, called over the army-backed ouster of Marc Ravalomanana, also resolved to expediate mediation efforts and facilitate talks. Madagascar, which was suspended from the bloc in March, had no official representation but fallen leader Ravolamanana held informal bilateral talks with several participants.

Msomaji