Monday, July 6, 2009

UCHAGUZI BIHARAMULO, CCM YASHINDA KWA KISHINDO !!!

Wanachama wa CCM wakisherehekea ushindi walioupata katika uchaguzi ndogo wa mbuge wa wilaya ya Biharamulo Magharibi kuziba nafasi ya ubunge iliyoachwa wazi kutokana na kifo cha mbunge wake Phares Kabuye.
Wapigaji kura wa Biharamulo mkoani Kagera, wakitumbukiza kura zao katika kituo cha shule ya msingi Umoja Biharamulo ili kuziba nafasi ya ubunge iliyoachwa wazi kutokana na kifo cha mbunge wake Phares Kabuye.



Habari kutoka Biharamulo nikwamba CCM imeshinda kwa kishindo uchaguzi mdogo katika wilaya ya Biharamulo Magharibi katika kujaza nafasi ya ubunge iliyoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa wilaya hiyo marehemu Phares Kabuye aliyefariki dunia mwanzoni mwa mwaka huu. Mgombe wa ubunge tiketi ya CCM Mh. Oskal Mukasa ameibuka kidedea kwa ushindi wa jumla ya kula 17,561 ambazo ni zaidi ya asilimia 51 ya kula zote zilizopigwa. Idadi ya wapigakula waliojitokeza inakadiliwa kuwa ni 34,000 kati ya 87,000 ya waliojiandikisha kupiga kura

Msomaji
Biharamulo

No comments: