Friday, July 24, 2009

BLOG HII YA CCM KUANZA TENA KUPOKEA MAONI

Ndugu wajumbe,
Baada ya kupokea maombi mengi ya wasomi na wachangiaji wa habari na picha kwamba wangependa kuona na kusoma maoni mbali mbali kwenye mtandao huu tunapenda kuwa taarifu kwamba kuanzia sasa tutaanza tena kupokea maoni mbalimbali.

Hivyo watumaji wa maoni mnaombwa kuendelea kutuma maoni yenu kama kawaida.

ILANI:
Tunaomba kusisitiza kwamba lugha zisizo na maadili hazikubariki, na kwamba tushirikiane kulinda maadili ya mtandao wetu ambao unatizamwa na watu wengi wenye lika tofauti.

Nawakaribisha tena kutoa maoni.

UONGOZI
CCM - TAWI LA MAREKANI

4 comments:

Anonymous said...

Ninafurahi kuona kuwa kitendo cha kuzuia maoni ya watu mlichokuwa mnakitekeleza ni kinyume na sera za CCM, kimsingi mlikuwa mnakiuka haki za kimsingi za binadamu.
I am not happy kabisa na jinsi hii blog inavyofanya kazi. Mfumo wa uendeshaji kwa maana ya habari zinazowekwa humu haziitofautishi na blog zingine ambazo tayari zina-exist na zina mafanikio makubwa. Ni vema hii blog ingetafuta nafasi yake katika jamii ili iweze kupata mafanikio zaidi. Mafanikio hayawezi kuja kirahisi kama wahusika hawatakuwa wabunifu, bidii na kuweza kuleta mabadiliko yanayotarajiwa. Kimsingi sijaona mchango wowote ambao ninaweza kujivunia hii blog imefanya as far as kueneza siasa ya chama cha mapinduzi inahusika.
Hii ni changamoto,vinginevyo hii blog haina maana kuitwa blog ya CCM.

Anonymous said...

Asante sana viongozi wa CCM kwa kuanza tena kuruhusu maoni.
ila nasisitiza kwamba lugha chafu na matusi lazima tuzikemee vikali sana.
Ningependa kuwataka waratibu wa huu mtandao kuanza kuwa na mbinu tofauti za kutupatia habari kwani mnayoyafanya sasa ni kama marudio ya mitandao mingine ingawa kwa dhati mnastahili pongezi japo kwa kutufikisha hapa.

Iddy
DC

Anonymous said...

Ndejembi ulikuwa umeanza udicteta nashukuru kwamba umelitambua hilo na sasa umejirekebisha, asante kwa hilo. Sasa una jipya jipya kwa ana CCM Marekani?


Agwe
Singapore

Anonymous said...

Sasa mlipozuia maoni yetu imewasaidia nini?, kama kweli mnapenda demokrasia basi wacha mtandao wazi kwa wote, sio baada ya siku mbili tena mnazuia maoni