Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya biashara kwa wajasiliamali wanawake yaliyoendeshwa na Benki ya Exim kutoka kulia ni Upendo Shoo ambaye ni mfanyabiashara Kariakoo, Caroline Mmbaga mfanyabiashara wa madini na Evelyne Masawe ambaye ni mfanyabiashara ya maduka ya dawa ya jumla wakifurahi kwa pamoja baada ya kukabidhiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo hayo ya wajasilimali wa kike yaliyofanyika kwa siku mbili katika Hoteli ya Golden Tulip. Exim bank wameamua kutoa mafunzo hayo ili wanawake wajue namana ya kuendesha biashara zao hasa kujua namna ya kuweka kumbukumbu za biashara hizo (Women Enterprenuers Training).
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Christina Manyenye kulia akimkabidhi cheti za ushiriki wa mafunzo ya biashara kwa wanawake Caroline Mmbaga baada ya kumalizikia kwa mafunzo hayo katika hoteli ya Golden Tulip.
Meneja masoko na Mawasiliano Christina Manyenye akiwaelezea njinsi ya kuweza kujua shughuli za benki ya Exim wakati wa semina ya wajasiliamali wa kike iliyoandaliwa na benki hiyo ikiwa na lengo la kuwafanya wanawake waweze kujua namna ya kuweza kuhifadhi kumbukumbu zao za kibiashara na namna ya kujua kukopa katika mabenki.
Msomaji
Dar es salaam
No comments:
Post a Comment