Tuesday, July 7, 2009

JIONEE ZIARA YA RAIS KIKWETE NCHINI ZAMBIA ILIVYOKUWA

Rais Kikwete (kati kushoto) mkutanoni na Rais Rupiah Banda wa Zambia (kati mstari wa kulia) kushoto kwake ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko Dr. Mary Nagu na kulia kwake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Seif Ally Idd. Katika mkutano huo walijadili kuhusu Reli ya Tanzanzia na Zambia (TAZARA). Rais Kikwete alikuwepo katika ziara ya kikazi Nchini Zambia kwa mda wa siku tatu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kati) akiwa kwenye mkutano na Rais wa Zambia Rupiah Bwezani Banda (hayupo pichani) kushoto kwake ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko Dr. Mary Nagu na kulia kwake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Seif Ally Idd. Lengho la mkutano huo ilikuwa kujadili kuhusu Mamlaka ya Reli ya Tanzanzia na Zambia (TAZARA).
Rais Jakaya Kikwete akipeana mkono na mmoja wa wazee wa mila wa Kabila la Lwiindi Gonde, mara baada ya yeye na Mwenyeji wake Rais wa Zambia, Rupiah Banda (katikati), kukabidhiwa zawadi za mikuki wakati wa sherehe za kimila zilizofanyika katika eneo la Monze, kusini mwa Zambia .
pamoja na kuhudhuria sherehe za aina hii rais Kikwete ambaye alikuwa katika ziara ya kiserikali ya siku tatu walizungumza na mwenyeji wake suala linalohusu urithi wa Nyerere na Kaunda, reli ya Tazara na kuagiza madeni yaangaliwe namna ya kulipwa na miundo mbinu iangaliwe kwa kuongea na China ambayo ipo tayari kusaidia.

Msomaji
Zambia

No comments: