Wednesday, September 30, 2009

Taarifa Rasmi: Maamuzi ya Halmashauri Kuu ya Taifa

MAAMUZI YA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA TAIFA (NEC)

Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM katika kikao chake cha leo (7/3/2009) kilichofanyika chini ya Uenyekiti wake Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete imefanya maamuzi yafuatayo:-

Kuhusu Kura za Maoni Kuwapata Wagombea Nafasi katika Vyombo vya Dola (Ubunge/Uwakilishi/Udiwani)

Kwa kutimiza azma ya kupanua demokrasia ndani ya Chama, na pia kwa lengo la kumshirikisha kikamilifu kila mwana CCM katika kupiga kura za maoni za kuwapata wagombea viti vya Ubunge, Baraza la Wawakilishi na Udiwani, Halmashauri Kuu ya Taifa imeamua kwamba kila mwana CCM atakuwa na haki ya kupiga kura za maoni kupitia Tawi lake.

Utaratibu huu utaanza kutumika katika Uchaguzi Mkuu wa mwakani (2010) na unafuta utaratibu wa zamani ambapo kura za maoni zilikuwa zinapigwa na wajumbe wachache kupitia mikutano mikuu ya Majimbo.

Utaratibu wa kura za maoni utakuwa kama ifuatavyo:-

(a)Kabla ya kura za maoni, wagombea watapata fursa ya kutembelea matawi yote na kukutana na wana CCM kwa lengo la kujitambulisha na kuomba kura.

(b) Ziara hizi zitaandaliwa na CCM ngazi ya Wilaya na wagombea watasafiri kwa pamoja kwa usafiri ulioandaliwa na kugharamiwa na CCM. Hatua hii ina lengo la kutoa haki sawa kwa kila mgombea kutembelea matawi yote na kujitambulisha.

(c) Baada ya ziara ya kujitambulisha kukamilika itapangwa siku moja ambapo wanachama wote watapiga kura kwenye matawi yao. Upigaji kura utaanza saa 2 asubuhi hadi saa 8 mchana Kamati ya Siasa ya Tawi itaweka utaratibu wa kuhakiki zoezi hili. Kura zitahesabiwa katika kituo husika na matokeo kutangazwa siku hiyo hiyo. Nakala ya matokeo itabadikwa hadharani nje ya ofisi ya Tawi, au mahali ambapo kura zitapigiwa ili yawe wazi. Kila mgombea atakuwa na haki ya kuweka wakala wa kusimamia upigaji kura, na zoezi la kuhesabu kura. Wilaya itaweka wasimamizi wa uchaguzi katika kila Tawi.

(d) Baada ya kura kuhesabiwa katika kituo na matokeo kutangazwa, msimamizi wa kituo atatakiwa kupeleka matokeo hayo kwa Katibu wa CCM (W) kwa njia yo yote ya haraka kwa mfano simu, fax, pikipiki, n.k.

(e) Baada ya matokeo kutoka matawi yote kufika wilayani, Katibu wa CCM (W) akisimamiwa na Kamati ya Siasa ya Wilaya atajumlisha kura za kila mgombea. Wakati wa zoezi la kujumlisha kura, kila mgombea atakuwa na haki ya kuwepo mwenyewe au mwakilishi wake.

(f) Baada ya zoezi la kura za maoni kukamilika, vikao vya ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa vitakaa kuchambua kwa undani zaidi sifa za wagombea na kuzingatia kura za maoni walizopata, na hatimaye kuteua wagombea. Majina ya wagombea hatimaye yatawasilishwa kwenye Tume ya Uchaguzi kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi na ratiba ya Tume ya Uchaguzi.

Halmashauri Kuu ya Taifa inaamini kuwa utaratibu huu unatoa nafasi kwa kila mwana CCM kushirikishwa katika mchakato wa kuwapata wagombea na pia watashiriki kuwaunga mkono wagombea wa CCM ili wapate ushindi kwenye Uchaguzi Mkuu. Vile vile utaratibu huu utaondoa tabia mbaya iliyojitokeza huko nyuma ya baadhi ya wagombea kutoa rushwa kwa wapiga kura ili kujipatia ushindi kwani kwa utaratibu huu haitakuwa rahisi kuwahonga wana CCM wa matawi yote Jimboni bila ya kubainika.

Aidha, Halmashauri Kuu imeagiza Kamati za Usalama na Maadili katika ngazi zote ziwe macho wakati wa kura za maoni ili kubaini vitendo vya rushwa. Mgombea ye yote atakayebainika kujihusisha na vitendo vya kutoa rushwa au kukiuka kanuni za uchaguzi, ataenguliwa katika kugombea, na iwapo atajihusisha na rushwa atafikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Kuhusu Utaratibu wa Kuongeza Wabunge/Wawakilishi Wanawake Kufikia Lengo la Asilimia 50
Halmashauri Kuu ya Taifa baada ya kuchambua njia mbalimbali za namna bora ya kuwapata Wabunge/Wawakilishi Wanawake ili kufikia lengo la asilimia 50 lililowekwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM, imeamua kama ifuatavyo:-

(a) Halmashauri Kuu ya Taifa imependekeza kwa Serikali kuwa idadi ya Wabunge katika Bunge la Muungano iwe na ukomo wa viti 360. Hivyo fomula yo yote ya kuongeza idadi ya Wabunge Wanawake sharti izingatie ukomo huu.

(b) Kwamba tuendelee na utaratibu uliopo sasa wa kuwapata Wabunge/Wawakilishi wa Viti Maalum Wanawake. Isipokuwa kwamba idadi yao katika kila chombo ipatikane kutokana na asilimia 50 ya Wabunge/Wawakilishi wote wa majimbo yaliyopo (232).

(c) Kwa kuzingatia kwamba Bunge litakuwa na ukomo wa viti 360 na kwamba idadi ya majimbo ya uchaguzi yaliyopo sasa ni 232, idadi ya Wabunge Wanawake itakayopatikana ni 116 sawa na asilimia 50 ya Wabunge wote wa Majimbo. Hata hivyo kuna Wabunge Wanawake 7 watapatikana kwa mujibu wa Katiba ya nchi; hivyo kwa utaratibu huu, Wanawake 109 ndio watakaopatikana kupitia Viti Maalum.

(d) Kwa upande wa Zanzibar, inapendekezwa kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iweke ukomo wa idadi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi iwe wajumbe 86. Kwa kuwa hivi sasa Baraza lina viti 50 vinavyotokana na majimbo ya uchaguzi, idadi ya Wawakilishi Wanawake watakaopatikana kwa njia hii itakuwa 25, yaani asilimia 50 ya Wawakilishi wote wa kuchaguliwa katika majimbo yaliyopo kwa kuwa Wawakilishi Wanawake 5 watapatikana kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar; hivyo Wanawake 20 ndio watakaopatikana kutokana na Viti Maalum.

(e) Katika kuandaa orodha ya wagombea Wanawake kwa nafasi 109 za Bunge la Muungano, na nafasi 20 za Uwakilishi zitakazogombaniwa, watapigiwa kura na vikao vya UWT. Kwa hiyo wagombea Ubunge/Uwakilishi watapigiwa kura na Mkutano Mkuu wa UWT wa Mkoa. Vivyo hivyo wagombea Udiwani wa Viti Maalum Wanawake watapigiwa kura na Mkutano Mkuu wa UWT wa Wilaya.

(f) Halmashauri Kuu ya Taifa pia imezielekeza Serikali zote mbili zikuchukue hatua zifuatazo:-

(i)Serikali ya Muungano irekebishe Katiba ya nchi na sheria ya Uchaguzi ili kuweka ukomo wa idadi ya Wabunge katika Bunge la Muungano kuwa 360, na pia kuhalalisha kisheria utaratibu huu mpya wa kuwapata Wabunge Wanawake kupitia Viti Maalum.

(ii) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, pia ibadilishe Katiba, na sheria ya Uchaguzi ili kuweka ukomo wa idadi ya Wawakilishi kuwa 86 na pia kuhalalisha kisheria utaratibu mpya wa kuwapata Wabunge Wanawake kuptia Viti Maalum.

(iii) Ili kuongeza idadi ya Wanawake katika Baraza la Wawakilishi, Katiba ya Zanzibar ifanyiwe marekebisho ili kumwezesha Rais wa Zanzibar ateue Wanawake wasiopungua watano (5) miongoni mwa nafasi kumi alizonazo kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar.

NEC inawahimiza na kuwahamasisha wanawake wajitokeze kwa wingi kugombea nafasi za Ubunge, Uwakilishi na Udiwani kupitia Majimboni badala ya kutegemea viti maalum. Aidha, vyama vyote vya siasa vinahamasishwa na kuhimizwa viteue Wanawake wengi zaidi kugombea nafasi majimboni.Mwisho, Halmashauri Kuu ya Taifa imeipongeza Kamati Maalum iliyoongozwa na Dr. Bilal kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya katika kukusanya maoni haya ambayo yamekubaliwa rasmi na sasa yatawasilishwa Serikalini kwa utekelezaji.Kuhusu Uteuzi wa

Mwisho wa Majina ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya za UVCCM na UWT

Halmashauri Kuu ya Taifa imefanya uteuzi wa majina ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Vijana na Wanawake.

Waliofanyiwa uteuzi ni:-
1. Ndugu Martin Reuben Shigela - UVCCM
2. Ndugu Hasna Sudi Mwilima - UWT

Majina haya yatafikishwa katika Baraza Kuu la UVCCM na la UWT kwa ajili ya kupigiwa kura za uthibitisho.


Imetolewa na:-
Capt. (Mst) John Z. Chiligati(Mb),
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
ITIKADI NA UENEZI

Sunday, September 20, 2009

Rais kikwete ameondoka nchini leo kuelekea Marekani kuhudhuria kikao cha 64 cha UN

RAIS Jakaya Kikwete ameondoka nchini leo jioni kwenda New York, Marekani kuhudhuria kikao cha 64 cha Baraza la Umoja wa Mataifa (UN) ambalo atalihutubia Alhamisi ijayo.
Mbali na kuhudhuria baraza hilo litakalofunguliwa rasmi Jumatano, Rais Kikwete anatarajiwa kuhudhuria mikutano mbalimbali iliyoandaliwa na UN kwa ajili ya viongozi wakuu wa nchi watakaokuwepo nchini humo.

Baadhi ya mikutano ni pamoja na unaohusu mabadiliko ya hali ya hewa unaoandaliwa na Katibu Mkuu wa UN, Ban Ki Moon.

Taarifa ya Ikulu pia imesema Rais atahudhuria kikao cha uzinduzi wa mpango wa pamoja wa viongozi wa Afrika kupambana na malaria Afrika ambao Tanzania ni mwenyekiti mweza na imeshirikiana na umoja huo kuuandaa.

Katika kikao kingine, Kikwete pamoja na Waziri Mkuu wa Uingereza, Gordon Brown kwa pamoja wataongoza kikao cha viongozi kuzungumzia malengo ya milennia namba 4 na 5, malengo yanayohusu kupunguza vifo vya watoto wachanga na wajawazito

Saturday, September 19, 2009

SALAMU ZA IDD-EL-FITRI KWA WATANZANIA WOTE

Ndugu Watanzania wenzetu, CCM-Nchini Marekani inayo furaha kubwa kuwatumia Mkono wa Idd El-fitri, mwaka huu wa 2009. Kwa niaba ya wanachama wote wa CCM nchini marekani, na kwa niaba ya viongozi wote wa CCM nchini Marekani, tunapenda kuchukua fursa hii kuwapongeza kwa kumaliza salama mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Tunawatakieni nyote kila la kheri wakati huu wa sikukuuu.

Idd Mubarak

Friday, September 18, 2009

Ngeleja: Matumizi ya nishati mbadala huleta maendeleo endelevu

Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja.
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, amesema matumizi ya nishati mbadala, nishati isiyoharibu mazingira na magari yatumiayo nishati isiyoharibu mazingira ni kichocheo cha maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi duniani kinachohifadhi na kutunza mazingira.

Waziri Ngeleja ameyasema hayo katika Mkutano wa Dunia wa kujadili nishati mbadala na matumizi ya magari yanayotumia nishati isiyoharibu mazingira ‘clean vehicles’ pamoja na nishati isiyoharibu mazingira ‘clean fuels’, unaofanyika mjini Stockholm nchini Sweden kuanzia Septemba 16 hadi 18 mwaka huu.

“Tanzania imekuwa ikipiga hatua katika kuzalisha nishati za umeme zitokanazo na maji, upepo, gesi asilia, jua na umeme unaozalishwa kwa kutumia makaa ya mawe ‘geothermal’ lakini rasilimali kama upepo, umeme wa makaa ya mawe, madini ya uranium na nishati ya mawimbi hazijaanza kushughulikiwa”, alisema.

Kwa mujibu wa Waziri Ngeleja, asilimia 90 ya nishati itumiwayo Tanzania inatokana na mimea mfano kuni na mkaa wakati asilimia nane hutokana na nishati ya kuagiza nje inayotokana na petroli huku asilimia 1.5 hutokana na nishati ya umeme inayozalishwa kwa kutumia maji, gesi asilia na makaa ya mawe.

Alisema kuwa asilimia 0.5 ya nishati inayotumiwa hapa Tanzania hutokana na upepo, umeme wa jua na rasilimali nyingine zitoazo nishati.

Mbali na hayo, Waziri Ngeleja ameueleza mkutano huo kuwa Tanzania ina fursa ya kuwa na maendeleo endelevu yatokanayo na matumizi ya nishati mbadala kwa sababu ina hali ya hewa nzuri inayoruhusu kustawi kwa mimea inayotoa nishati, ipo katika ukanda unaoruhusu biashara ya nishati hiyo kwa sababu inatumia Bahari ya Hindi kwa pamoja na nchi nane jirani.

Pamoja na mafanikio yanayopatikana kutokana na matumizi ya nishati mbadala, Waziri Ngeleja alisema kuna changamoto ambazo zinaikabili Tanzania ikiwa ni nchi changa katika matumizi ya nishati hii ya kisasa.Aliitaja changamoto ya kwanza ni kuwa ni mdororo wa kiuchumi ulioikumba Dunia na kuathiri sekta ya uwekezaji.Mbali na hilo, anasema utunzaji wa mazingira na uendelezaji wa nishati mbadala unahitaji mipango na mikakati ya uhakika ambayo Tanzania inaichukua kwa umakini mkubwa

Msomaji
Dar es salaam

Thursday, September 17, 2009

Tanzania's President to Participate in U.S - Africa Business Summit

Washington, DC — The Corporate Council on Africa (CCA) announces that President Jakaya Mrisho Kikwete of the United Republic of Tanzania will attend the 7th Biennial U.S.–Africa Business Summit: Realizing the Investment Power of Africa, to be held at the Walter E. Washington Convention Center in Washington, D.C., September 29 – October 1, 2009.

“President Kikwete’s leadership has been crucial to Tanzania’s success,” said Stephen Hayes, president and CEO of CCA. “With a continued eye toward the development of the nation, Tanzania will be in a position to grow rapidly as the world economy emerges from the current downturn.” According to a December 2008 report by the Economist, Tanzania, in 2009, will have the world’s 9th fastest growing economy, just behind China and ahead of India.

President Kikwete will be joined by Tanzania’s Minister for Agriculture Food Security and Cooperatives Stepen Masato Wasira, who will participate in the Heads of State and African Leaders Roundtable on Agribusiness Development. President Kikwete will also be joined by Minister of Trade Mary Nagu, who will partake in the trade plenary Navigating Bilateral, Regional, and Global Trade Agreements in Turbulent Times.

The Tanzanian economy has seen average real GDP growth of six percent over the past seven years as the government continues to privatize key industries. The government has taken steps to promote foreign investment and create a welcoming environment for capital including an overhaul of the tax code, licensing foreign banks, and establishing an investment promotion center. Tanzania is the third-largest producer of gold in Africa and has vast amounts of natural resources including diamonds, coal, iron ore, uranium, nickel, chrome, tin, platinum, coltan, niobium and other minerals. Commercial production of natural gas commenced in 2004.

Sector ministers will also be represented from South Africa; Rwanda; Nigeria; Kenya; Senegal; Ghana; Uganda; Malawi; Mozambique; Namibia; Sudan; and Liberia. “For companies interested in operating in Africa, interacting with these ministers and government officials is necessary for understanding how to conduct business in their respective countries,” said Hayes.

For more information and to register for the 7th Biennial U.S. – Africa Business Summit, visit: http://www.africacncl.org/. All working media must be credentialed to cover the summit. Please open the following link: 09 Summit Media Credential Form and submit media form to: summit@africacncl.org.

About The Corporate Council on Africa:
Established in 1993, The Corporate Council on Africa is a nonpartisan 501 (c) (3) membership organization of nearly 180 U.S. companies dedicated to strengthening the commercial relationship between the U.S. and Africa. CCA members represent nearly 85 percent of total U.S. private sector investments in Africa. The organization is dedicated to bringing together potential business partners and to showcase business opportunities on the continent.
CONTACT: Nicole Amarteifio, (202) 263-3538, namarteifio@africacncl.org

Msomaji
U S A

Dkt. Diodorus Kamala atembelea kiwanda cha East African Cable

Waziri wa Afrika Mashariki Dkt. Diodorus Kamala (wa pili kulia) akipata maelekezo kutoka kwa Charles Ngachwelwa Meneja ubora wa Kiwanda cha East African Cable kuhusu mtambo wa kutengeneza nyaya za kusukia motor na transfoma wakati alipotembelea kiwanda hicho kilichopo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Joseph Kamau Meneja uzalishaji akifuatiwa na Muriithi Ndegwa Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda. Waziri huyo alitembelea kiwanda hicho leo kwa lengo la kuona bidhaa zinazozalishwa kiwandani hapo ili aweze kuzitangaza kwa wanachama wa Afrika Mashariki.
Waziri wa Afrika Mashariki Dkt. Diodorus Kamala (katikati aliyevaa koti yeupe) akipata maelekezo kutoka kwa Muriithi Ndegwa ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha East African Cable (kulia kwa waziri) kuhusu roll ya waya wa shaba ambayo inaingizwa katika mashine na kutolewa katika ukubwa wa aina tofauti wa nyaya. Kulia ni Charles Ngachwelwa Meneja ubora wa Kiwanda akifuatiwa na Joseph Kamau Meneja wa uzalishaji. Waziri huyo alitembelea kiwanda hicho leo kwa lengo la kuona bidhaa zinazozalishwa kiwandani hapo ili aweze kuzitangaza kwa wanachama wa Afrika Mashariki.

Msomaji
Dar es salaam

WAZIRI MKUU AKIZUNGUMZA NA KIONGOZI WA JIMBO LA GUJARAT INDIA

Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Kayanza. Peter Pinda akizungumza na Waziri Kiongozi wa Jimbo la Gujarat nchini India, Narendra Modi kwenye hoteli ya Gateway katika jimbo hilo, jana wakati wa ziara yake nchini humo.

Msomaji
India

Wednesday, September 16, 2009

Msimamo wa Spika Samueli Sitta Safi-Mwakilishi UNDP..

Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania, Samuel Sitta,ambaye amepewa sifa kwa kutetea maslahi ya nchi kwa njia ya kidemokrasia akiingia bungeni.


Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alain Noudehou, amepongeza msimamo wa spika wa Bunge,Samuel Sitta bungeni,akisema unawakilisha demokrasia ya kweli katika kutetea maslahi ya wananchi.
Noudehou alisema hayo jana alipokuwa akizungumza katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya demokrasia iliyoandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania(TCD)na kufanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

“Pamoja na mambo mengine alisema Mh. Spika wa bunge amefanikiwa kukamilisha Mpango wa Maendeleo ya Bunge ambao umetoa picha kamili ya Bunge madhubuti linalowajibika kwa watu wake. UNDP iko tayari kumsaidia kutekeleza mkakati huo,”alisema Noudehou.

Kwa mujibu wa Noudehou kama Tanzania inataka kuendelea kujimarisha kidemokrasia, haina budi kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na changamoto zinazohusu uwajibikaji, uwakilishi na usawa.

“Hali hiyo itawezesha kujenga jamii ambayo itajihakikishia maendeleo ya watu,kupatikana kwa haki na ukombozi wa kiraia kwa Watanzania wote,alisema.Aliongeza kuwa ili Tanzania iweze kukabiliana na changamoto hizo inahitaji kuegemea kwenye kuimarisha asasi za kidemokrasia katika kuunga mkono chaguzi,kulinda utawala wa sheria na kuhamasisha mazungumzo ya ndani ya vyama vya siasa.

“Kuimarisha uwezo wa taasisi za kidemokrasia kama Bunge,Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa(Takukuru),vyombo vya usimamizi wa chaguzi na kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari kutaendelea kuleta mabadiliko ya kidemokrasia,” alifafanua.“Haya mazungumzo ya vyama vya siasa kwa sasa ni muhimu sana kwa Tanzania katika kipindi hiki cha kuingia kwenye uchaguzi.Mazungumzo hayo yanapanua utamaduni na uvumilivu wa kisiasa.”

Msomaji
Dar es salaam

Pius Aloysius ateuliwa Mkurugenzi wa Bodi ya NBAA!!

Waziri wa Uchumi na Fedha Mh. Mustafa Mkulo
Waziri wa Fedha na Uchumi Mh..Mustafa Mkulo amemteua Bwana Pius Aloysius Maneno kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu kuanzia tarehe 22 mwezi wa nane mwaka 2009 Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ingiaedi Mduma imesema kuwa uteuzi huo ni kwa mujibu wa kifungu cha 6 cha sheria namba 33 ya mwaka 1972 na kurekebishwa na sheria namba 2 ya mwaka 1995 iliyoanzisha NBAA. Hapo awali Bwana Pius alikuwa Meneja wa Corporate Service na alikuwa anakaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA.

Msomaji
Dar es salaam

Tuesday, September 15, 2009

Mafunzo ya Wiki Mbili Kwa Makatibu Wakuu Yalivyofunguliwa

Katibu Mkuu kiongozi Philemon Luhanjo akiongea na waandishi wa habari kuhusu mafunzo ya uongozi yanayofanyika katika hoteli ya Movenpick jijini Dar es Salaam.Mafunzo hayo ya wiki mbili ambayo yameandaliwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma yanatolewa kwa Makatibu wakuu, Manaibu Katibu wakuu pamoja wakurugenzi walioteuliwa hivi karibuni kushika nyadhifa hizo.Picha Zote na Anna Nkinda - Maelezo
Washiriki wa mafunzo ya uongozi kwa Makatibu wakuu,Manaibu Katibu wakuu pamoja na wakurugenzi walioteuliwa hivi karibuni kushika nyadhifa hizo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunguliwa kwa mafunzo hayo ya wiki mbili.Waliokaa mstari wa mbele katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo kulia kwake ni Katibu Mkuu Utumishi George Yambesi na kushoto kwake ni John Odebiy ambaye ni Mwezeshaji wa mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Msomaji
Dar es salaam

Baba wa taifa, Mwalimu. Nyerere Atunukiwa Tuzo ya 'World Hero of Social Justice'

Rais wa baraza kuu la 63 la Umoja wa mataifa,father Miguel d'Escoto Brockman,akitoa maelezo kwa Mama Maria Nyerere kuhusu tuzo ya 'World Hero of Social Justice' ambayo rais huyo amemtunuku kwa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius K.Nyerere katika hafla iliyofanyika jijini New York,Marekani na kuhudhuriwa na mabalozi mbalimbali kutoka nchi za Afrika na mabara mengine wanaoziwakilisha nchi zao katika umoja wa mataifa.Picha zote kwa Hisani ya Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa.
Mabalozi wa wanaoiwakilisha Tanzania nchini Marekani, Brazil na Umoja wa mataifa nao walikuwapo kumpa Tafu Mama katika hafla hiyo kutoka kulia Joram Biswalo(Brazil)Omben Sefue( Washngton )Tuvako Manongi(ofisi ya Naibu Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa)na mwenyeji wao Augustine Mahiga (Umoja wa Mataifa) katika picha ya pamoja na Mama Maria Nyerere

Msomaji
U S A

Thursday, September 10, 2009

Taarifa Rasmi: Kuhusu Kikao Cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM

Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imefanya Mkutano wa kawaida tarehe 16-17 Agosti, 2009 chini ya Uenyekiti wa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Katika mkutano huu Halmashauri Kuu imejadili masuala mbali mbali kuhusu hali ya kisiasa nchini, maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, zoezi la uboreshaji wa daftari la wapiga kura, pia imefanya uteuzi wa wagombea katika nafasi mbalimbali.

Baada ya kujadili masuala hayo, Halmashauri Kuu ya Taifa imefanya maamuzi yafuatayo:-

1. MAANDALIZI YA UCHAGUZI

(a) Serikali za MitaaHalmashauri Kuu ya Taifa imepitisha ratiba ya CCM kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa; kwa mujibu wa ratiba hiyo muda wa kuchukua na kurudisha fomu kwa wagombea wa CCM kwa uongozi wa Vitongoji, Serikali za Vijiji na Mitaa ni toka tarehe 10/8/2009 hadi 20/8/2009.

Halmashauri Kuu ya Taifa imetoa wito kwa wana CCM na wapenzi wa CCM katika ngazi ya Vitongoji, Vijiji na Mitaa wajiandae kushiriki kwa ukamilifu katika mchakato wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu kwa kuzingatia ratiba ya CCM na pia ratiba ya wasimamizi wa Uchaguzi huu (TAMISEMI).

Aidha, Halmashauri Kuu ya Taifa imewahimiza wana CCM na wapenzi wa CCM wajitokeze kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura kuanzia tarehe 4/9/2009 hadi 25/9/2009 na kwamba muda ukiwadia wajitokeze kuwapigia kura wagombea wa Chama Cha Mapinduzi hapo tarehe 25/10/2009.

(b) Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura - Pemba
Halmashauri Kuu ya Taifa baada ya kupokea taarifa kuhusu zoezi la uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Kisiwani Pemba, imetoa wito kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ihakikishe zoezi hilo linasimamiwa kwa makini, na liendeshwe kwa haki na kwa utulivu; na kwamba Serikali ya Mapinduzi ihakikishe kwamba kila mwenye haki na sifa ya kujiandikisha anapata haki hiyo, na wale wasio na sifa wasiruhusiwe kujiandikisha.Kimsingi zoezi hili sharti liendeshwe kwa kuzingatia sheria ya Uchaguzi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na sio vinginevyo.


2. KUONGEZA IDADI YA WANAWAKE KATIKA VYOMBO VYA UWAKILISHI

Halmashauri Kuu ya Taifa imetafakari upya mapendekezo yake ya awali kuhusu utaratibu wa kuongeza idadi ya wanawake katika Bunge la Muungano na katika Baraza la Wawakilishi. Mapendekezo mapya ni kama ifuatavyo:-

(a) Kwamba kwa kuwa idadi ya Wabunge wote kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 66(1)(b) ni 249, viti asilimia arobaini (40%) itengwe kwa ajili ya wanawake, yaani viti 100.

(b) Kwamba ukomo wa viti Bungeni ubaki 360, hivyo pendekezo hili litaongeza idadi ya viti kutoka 323 vya sasa hadi 349, na vitabaki viti 11 kufikia ukomo wa viti (360) Bungeni. Hali hii inawezesha Tume ya Uchaguzi kuongeza idadi ya majimbo mapya 11.

(c) Utaratibu wa asilimia 40 utakapotumika utawezesha kupatikana kwa Wabunge Wanawake 100 kwa viti maalum pekee, idadi ambayo ikijumulishwa na wa kuchaguliwa ambao kwa sasa ni 18, watano wa kuteuliwa na wawili kutoka Baraza la Wawakilishi, tutapata Wabunge wanawake 125. Kiwango hiki ni sawa na asilimia 50 ya Wabunge wote waliotajwa kwenye Ibara ya 66(1) (b) ya Katiba.

(d) Ili kufikia lengo la kupata wabunge wanawake 50%, wanawake hawana budi kushindana kwa bidii katika majimbo. Kwa hali hii Halmashauri Kuu ya Taifa imeagiza CCM katika ngazi zote zifanye uhamasishaji wa Wanawake wengi kwenda kugombea katika majimbo ya uchaguzi mwaka 2010 ili kuongeza Wabunge zaidi ya 18 waliopo hivi sasa.

3. UTEUZI WA WAGOMBEA UENYEKITI WA WILAYA

Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, imepitisha wana CCM walioomba kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM katika Wilaya za Rorya, Tarime na Arumeru.Nafasi za Tarime na Rorya zimetokana na kugawanywa kwa wilaya ya Tarime na kuwa wilaya mbili na ile ya wilaya ya Arumeru imetokana na kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Wilaya hiyo, Ndugu Lucas Lobulu aliyefariki Mei 6, 2009. Waliopitishwa kugombea nafasi hizo ni:-

Wilaya ya Arumeru
1.Ndugu Jeremiah Saruni Kaaya
2. Ndugu Gabriel Kilale Nnko
3.Ndugu Joseph Ole Loning’o Saivoiye

Wilaya ya Tarime
1.Ndugu George Mkama Chacha
2.Ndugu Bogomba Rashid Chichake
3.Ndugu Peter Keba Wangwe

Wilaya ya Rorya
1.Ndugu Leonard Yodal Ambonya
2.Ndugu Jomoko Mjee Kateti
3.Ndugu Ramadhan A. Nyanganira

Wilaya husika zitafanya uchaguzi kwa ratiba itakayoandaliwa baadaye.

4. CHAGUZI NDOGO BUSANDA, MAGOGONI NA BIHARAMULO

Baada ya Halmashauri Kuu ya Taifa kujadili tathmini ya chaguzi ndogo katika majimbo ya Busanda, Magogoni na Biharamulo, imewashukuru na kuwapongeza wale wote waliofaikisha ushindi wa CCM katika Uchaguzi mdogo wa Majimbo ya Ubunge ya Busanda (Mwanza) na Biharamulo Magharibi (Kagera) pamoja na Uchaguzi mdogo wa Uwakilishi wa Jimbo la Magogoni, Zanzibar.

Aidha, Halmashari Kuu pia imetoa pongezi za dhati kwa wana-CCM, wapenzi wa CCM na wananchi kwa ujumla kwa ushindi waliokipatia Chama Cha Mapinduzi katika chaguzi hizo ndogo za Ubunge, Uwakilishi na za Udiwani katika Kata 10 za Tanzania Bara.Kutokana na ushindi huo, kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa kiliwaomba wana-CCM, wapenzi wa CCM, wakereketwa na wananchi kwa ujumla kuendelea kukipa ushindi Chama Cha Mapinduzi ili kiendelee na majukumu ya kumkomboa Mtanzania na kudumisha amani na utulivu.

5. MAHAKAMA YA KADHI

Halmashauri Kuu ya Taifa imeridhika na hatua zinazochukuliwa na Serikali za kulipatia ufumbuzi suala la Mahakama ya Kadhi Tanzania Bara. Moja ya hatua hizo ni uundaji wa Kamati ya mazungumzo baina ya viongozi wa dini ya Kiislam na Serikali kuhusu mchakato wa uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi nje ya mfumo wa Serikali.

Aidha, Halmashauri Kuu imesisitiza kwamba iwapo wapo Waislam wanaona haki zao hazikamiliki bila ya kuwa na chombo cha aina hiyo, wasizuiliwe. Waruhusiwe kuanzisha Mahakama ya Kadhi wao wenyewe na Serikali isijihusishe kuiendesha mahakama hiyo kwani kwa kufanya hivyo itakuwa imejiingiza katika shughuli za kidini; na kwamba Mahakama hiyo isihusike na kesi za jinai wala madai, bali ihusike na masuala ya ndoa, talaka na mirathi.

6. WARAKA WA BARAZA LA MAASKOFU (RC)

Baada ya Halmashauri Kuu ya Taifa kuzingatia waraka wa Maaskofu, na hasa malumbano na hisia tofauti zilizojitokeza kuhusu waraka huo, imeelekeza kwamba viongozi wakuu wa nchi wafanye mazungumzo na viongozi wa dini zote ili kutafuta njia tulivu ya kusafisha hali ya hewa na kujenga umoja na utengamano katika jamii yetu.

7. MALUMBANO YA VIONGOZI

Kuhusu tabia iliyozuka hivi karibuni ya baadhi ya Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Viongozi wa Chama kutoa matamshi hadharani yenye mwelekeo wa kuchafuana majina, na yanayoashiria kuvunjika kwa umoja na mshikamano ndani ya CCM na Serikali zetu, na pia yenye mwelekeo ya kudhoofisha muungano wetu, Halmashauri Kuu ya Taifa pamoja na kukemea vikali tabia hii, imetoa maagizo yafuatayo:-

(a) Kwamba kuanzia sasa viongozi wote wa CCM warejee katika nidhamu ya Chama ya kuzungumzia masuala ya Chama katika vikao rasmi vya Chama na sio vinginevyo.

(b) Kamati za Wabunge wa CCM, na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CCM zitumike kujadili masuala yahusuyo CCM ndani ya vyombo hivyo.

(c) Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar watumie taratibu zilizopo katika kushughulikia kero za Muungano badala ya kufanya kwa suala la mafuta kwa upande wa Zanzibar.

d) Viongozi watakao vunja maadili haya watakuwa wamejibainisha kwamba hawana nia njema na CCM, na watahesabiwa ni wasaliti wa CCM hivyo Chama hakitasita kuwapa adhabu kali, ikiwa ni pamoja ya kuvuliwa uongozi na hata kufukuzwa katika Chama.

(e) Halmashauri Kuu ya Taifa imetoa wito kwamba mapambano dhidi ya rushwa na maovu mengine ni jukumu la wana CCM wote na raia wema wote kwa mujibu wa Katiba ya CCM Ahadi 4 ya Wana CCM. Halmashauri Kuu ya Taifa imeonya kuhusu dhana inayojengeka kwamba vita dhidi ya rushwa na ufisadi inahusu kikundi kidogo tu cha wana CCM, usahihi ni kwamba vita hii ni ya wana CCM wote kwa mujibu wa Katiba ya CCM vita hivi lazima iendelee kuhusisha wana CCM wote na wananchi wote wenye mapenzi mema na nchi yetu.

(f) Kwa kutambua kuwepo matatizo ya matamshi na vitendo visivyoridhisha katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi, Halmashauri Kuu ya Taifa imeamua kuunda Kamati Ndogo ya kutafuta undani wa matatizo hayo na kupendekeza kwa Kamati Kuu njia za kuyatatua. Aidha, Kamati hiyo pia itaangalia utendaji kazi wa Kamati za Chama katika Bunge na Baraza la Wawakilishi kwa nia ya kubaini upungufu uliopo ili kupendekeza kwa Kamati Kuu kuhusu njia za kurekebisha. Pia, Kamati itaangalia masuala ya uendeshaji wa shughuli za Bunge na Baraza la Wawakilishi na kushauri namna ya kuimarisha, pale panapostahili.

Kamati hiyo itaongozwa na Mzee Alli Hassan Mwinyi Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Wajumbe wengine ni Mzee Pius Msekwa Makamu Mwenyekiti CCM (Bara) na Ndugu Abdulhaman Kinana.

8. KUHESHIMU VIONGOZI WASTAAFU

Halmashauri Kuu ya Taifa imewakumbusha wana CCM, Viongozi na Watanzania kwa jumla kuhusu umuhimu wa kudumisha utamaduni wa kuwaheshimu na kuwaenzi viongozi wastaafu, hususan Marais wastaafu.

Aidha, Halmashauri Kuu ya Taifa imesikitishwa sana na hali iliyojitokeza Bungeni ya kutoa maneno ya kejeli dhidi ya Mzee Benjamin W. Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu.

Halmashauri Kuu ya Taifa imesisitiza kwamba Mzee Mkapa katika kipindi chake ameliongoza Taifa letu kwa ufanisi mkubwa, aliinua hali ya uchumi, aliendeleza miundombinu, aliendeleza huduma za kijamii hasa elimu, afya, maji na kwa jumla alilijengea heshima kubwa Taifa letu.

Mzee Mkapa anastahili pongezi sio kejeli, anastahili heshima na sio dharau, anastahili kuenziwa na sio matusi.

Kwa kuzingatia hayo, Halmashauri Kuu ya Taifa inatoa wito kwa wana CCM na Watanzania wote wenye nia njema na nchi yetu waache mara moja kumchafua na kumkejeli Mzee Mkapa na badala yake apewe heshima anayostahili na aachwe apumzike kwa amani.

9.UTEUZI WA MAKATIBU WAPYA WA MIKOA

Halmashauri Kuu ya Taifa imewateua wafuatao kuwa Makatibu wa Mikoa:-

(1) Ndugu Sauda Mpembalyoto (Katibu wa Wilaya ya Hai)
(2) Capt. (Mst) Frarten Kiwango (Katibu wa Wilaya ya Kibaha Mjini)

Hawa wanajaza nafasi zilizoachwa wazi na Ndugu Amina Makilai aliyekuwa Katibu wa Mkoa wa Pwani na sasa ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa UWT, pia Ndugu Salum Msabah aliyekuwa Katibu wa Mkoa wa Kigoma na sasa amerejeshwa Makao Makuu ya CCM kuongoza Kitengo cha Propaganda.

10. UCHAGUZI WA MJUMBE WA NEC KUPITIA JUMUIYA YA WAZAZI

Nafasi hii iliachwa wazi na marehemu Richard Nyaulawa na ilikuwa inawaniwa na wagombea watatu.Kutokana na kura za wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa aliyechaguliwa ni Ndugu Jasson Rweikiza aliyepata kura 88.

Wengine waliogombea nafasi hii ni Ndugu Ramadhani Maneno kura 85 na Ndugu Sifa Swai kura 46.

Imetayarishwa...11:50:20 17.08.2009.
MAKAO MAKUU,
CHAMA CHA MAPINDUZI
DA ES SALAAM

KWELI RAIS JAKAYA AMEANDIKA HISTORIA MPYA TANZANIA

Mh Rais Jakaya Kikwete akiongea moja kwa moja na wananchi kupitia Luninga na Redio kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC Tido Muhando.

Hivi ndiyo ilivyokuwa wakati Rais Jakaya alipoongea na watanzania (Live) moja kwa moja kupitia Redio na Televisheni na kuulizwa maswali mbalimabli na wananchi ili kupata ufafanuzi wa mambo kadhaa yahusuyo utendaji wa serikali na matarajio ya watanzania.
Utaratibu huu umebuniwa kwa mara ya kwanza na Rais Jakaya na ni kwa mara ya kwanza toka tujipatie uhuru kutoka kwa wakoloni, Mh Rais alizungumzia mengi na kujibu maswali mengi kutoka kwa wananchi

Lakini moja ya mambo aliyozungumzia ni uhuru wa wananchi kuzungumzia na kukosoa utendaji wa serikali na akazungumzia pia uhuru wa vyombo vya habari na kusisitiza vyombo hivyo kufuata maadili ya kazi zao bila kuandika habari za uongo na uchochezi, hili ni jambo jema sana kwani tunahitaji habari nyingi zaidi lakini pia tunahitaji habari za kweli na zenye upembuzi yakinifu ili jamii iweze kupata habari zilizo sahihi

Tunakupongeza sana Mh Rais kwa uamuzi wako wa kuongea na wananchi huku ukiulizwa maswali mabalimbali na kuyajibu, kwa kutendo hiki umeandika historia mpya ya uhuru wa umma kupata habari na kutoa maoni yao juu ya uendeshaji na uboreshaji wa maendeleo ya nchi na wananchi kwa ujumla tunakupa Heko kwa uamuzi wako huu na tunadhani utazaa matunda, tunakutakia mafanikio mema katika kazi zako za kila siku katika kujenga Taifa letu Tanzania.

Saturday, September 5, 2009

Benki ya Wanawake Yazinduliwa nchini Tanzania.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akichapa kazi wakati wa uzinduzi wa benki ya wanawake jana hapo anachukua moja ya vitu muhimu vilivyokuwa vikiongelewa na waziri sita wakati alipokuwa akisoma speech.
Mama Salma Kikwete akisakata rusha roho wakati wa uzinduzi wa benki ya wanawake, iliyopo jijini DAR ES SALAAM mtaa wa Salamanda.karibu na posta ya zamani.
Mkurugenzi mkuu wa benki ya wanawake Tanzania Margaret Chacha akisoma hotuba ya maendeleo ya benki hiyo.
Mbunge wa Viti maalum Mchungaji wa kanisa la Assembless of God Mama Rwakatale akicheza mziki wa kidunia (rusha roho) iliyokuiwa ikipigwa na bendi ya TOT .wakati wa uzinduzi wa benki ya wanawake ilipozinduliwa na Rais Kikwete jana, wengine walioshambulia jukwaa hilo ni Mke wa Rais mama Salma Kikwete, Mke wa spika Mama Margaret Sitta (kushoto) Mke wa Rais Mstaafu awamu ya pili mama Mwinyi na Waziri Sophia Simba.



HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, KWENYE UZINDUZI WA BENKI YA WANAWAKE TANZANIA SIKU YA IJUMAA YA TAREHE 04 SEPTEMBA, 2009, DAR ES SALAAM

Mheshimiwa Margaret Sitta, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto;Waheshimiwa Mama Salma Kikwete, Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo- WAMA;

Mama Sitti na Mama Khadija;Waheshimiwa Mawaziri na Naibu Mawaziri mliopo hapa;Dr. Lucy Nkya, Naibu Waziri, Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto;

Mheshimiwa William Lukuvi, (Mb), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam;

Bibi Mariam Mwaffisi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto;
Bwana Daniel Ole Sumayan, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Wanawake Tanzania;
Waheshimiwa Wabunge; Wajumbe wa Bodi ya Benki ya Wanawake Tanzania; Wageni Waalikwa; Mabibi na Mbwana:

Utangulizi
Niruhusuni nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kutujaalia uzima na hasa bahati ya kushuhudia tukio hili la kihistoria la uzinduzi wa Benki ya Wanawake Tanzania. Nakushukuru sana Mheshimiwa Margareth Sitta, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, na uongozi wa Benki ya Wanawake Tanzania kwa kunialika kushiriki katika shughuli hii adhimu.

”Hayawi hayawi leo yamekuwa.” ”Walisema hawapati mbona wamepata”? Hayo ndiyo maneno ninayopenda kuanza nayo katika hotuba yangu ya ufunguzi wa Benki ya Wanawake Tanzania. Maneno hayo yanaelezea kwa ufasaha na usahihi ukweli kwamba leo ni siku ya aina yake katika historia ya nchi yetu na hasa kwa maendeleo ya wanawake hapa nchini. Ni siku ambayo ndoto ya miaka mingi ya wanawake wa Tanzania ambayo ilionekana kama haiwezekani hatimaye imewezekana. Tumekusanyika hapa kuwa shuhuda wa kutimia kwa ndoto hii.

Kilio cha Siku Nyingi cha Wanawake
Mheshimiwa Waziri, Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana;Kuwepo kwa benki ya wanawake nchini ni maombi na kilio cha wanawake wa nchi yetu tangu uhuru. Ni kilio kilichotolewa na Jumuiya ya Umoja wa Wanawake tangu wakati wa TANU na hata baada ya CCM kuzaliwa. Ni kilio cha Bibi Titi Mohamed na Mama Sofia Kawawa wakati wa uhai wao wakiwa Wenyeviti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT). Ni kilio cha Mheshimiwa Anna Abdallah wakati akiwa Mwenyekiti wa UWT na ni kilio cha Mheshimiwa Sophia Simba akiwa Mwenyekiti wa sasa wa UWT. Hakuna Mwenyekiti wa UWT ambaye hakusemea jambo hili. Ni kilio cha wanachama wao na wanawake wote nchini.

Kilio hicho cha wanawake wa Tanzania kilifikishwa kwa viongozi wote Wakuu wa nchi yetu tangu uhuru. Kilitolewa kwa Rais wa Kwanza Mwalimu Julius Nyerere, kwa Rais wa Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, kwa Rais wa Tatu, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa na hata kwangu pia. Kwetu sisi viongozi wote maombi yalipofikishwa, ahadi yetu ilikuwa ni kuyafanyia kazi. Kila mmoja wetu kwa wakati wake alichukua hatua mbalimbali na sasa tumehitimisha.

Ndugu Wananchi;
Waswahili wana misemo miwili ambayo napenda kuinukuu; ”safari ni hatua” na ”kila jambo kwa wakati wake”. Hatimaye wakati umetimia kwa jambo hili kukamilika kama tunavyoshuhudia leo.

Hatuna budi kumshukuru kwa namna ya pekee Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa kwa maono yake ya mbali na uamuzi wake wa busara na kishujaa wa kukubali uanzishaji wa Benki ya Wanawake uwemo katika Ilani za Uchaguzi za CCM za mwaka 2000 na ile ya 2005. Ibara ya 120(g) ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2005 inaagiza kuwa: ”Kukamilisha taratibu na hatimaye kuunda Benki ya Wanawake”.

Nasema ulikuwa ni uamuzi wa kishujaa kwa sababu kukubali jambo hili ambalo kwa miaka ya nyuma halikuweza kutekelezwa liwe ahadi bayana ya Chama Cha Mapinduzi kunahitaji moyo wa ujasiri na kuthubutu. Nampongeza kwa uwezo wake wa kuona mbali na imani yake kwamba katika awamu ya nne ya uongozi wa nchi yetu jambo hili litawezekana. Na kweli limewezekana. Naomba kwa mara nyingine tena tumtambue na kumpongeza Mzee wetu Benjamin William Mkapa.

Ndugu Wananchi;
Napenda kuitumia nafasi hii kuwatambua na kuwashukuru wenzangu wote katika Serikali ninayoiongoza kwa utendaji kazi wao mzuri uliowezesha ndoto ya wanawake na ya wananchi wetu wa Tanzania kutimia. Niruhusuni niwataje watu wanne kwa niaba ya wenzao wote waliohusika, moja kwa moja, katika kufanikisha kuwepo kwa Benki ya Wanawake Tanzania tunayosherehekea uzinduzi wake leo.

Wawili wa kwanza ni kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, na Watoto, yaani Mheshimiwa Sophia Simba aliyekuwa Waziri wangu wa kwanza wa Wizara hiyo na Mheshimiwa Margareth Sitta ambaye ndiye Waziri wa sasa. Waziri Sophia Simba ndiye aliyepanda mbegu na Waziri Margareth Sitta ndiye aliyemwagilia maji mpaka mti ukakua, ukakomaa na kutoa matunda tunayoyachuma sasa.

Wawili wengine ni Mheshimiwa Zakhia Meghji aliyekuwa Waziri wangu wa kwanza wa Fedha na Mheshimiwa Mustapha Mkullo, Waziri wa sasa. Mheshimiwa Zakhia Meghji aliunga mkono uamuzi wangu kuwa Serikali ichangie fedha zake kuwezesha Benki hii kuanza. Wakati ule Waziri Sophia Simba alikuwa ameanzisha mchango wa kuanzisha Benki hiyo na makusanyo hayakuwa yanaenda kwa kasi iliyoniridhisha.

Nilipomwambia Waziri wa Fedha,
Mheshimiwa Zakhia Meghji wakati ule kuwa Serikali itenge pesa kwenye bajeti yake kuchangia Benki ya Wanawake hakusita, akakubali na kuanzisha mchakato. Mheshimiwa Mustapha Mkullo amekuja kuukamilisha mchakato huo na matokeo yake ni Serikali kutoa shilingi bilioni 2.9 na kuwezesha kuwepo kwa Benki hii hivi leo.

Mchango huu siyo mwisho, Serikali itaendelea kuchangia mtaji wa benki hii kadri itavyowezekana. Wakati tukiwashukuru viongozi hao wa kisiasa hatuna budi kuwashukuru watendaji mbalimbali waliokuwa chini yao kwa kazi yao nzuri iliyowezesha mambo kukamilika vizuri kama tunavyoshuhudia leo.

Umuhimu wa Kuanzisha Benki ya Wanawake
Mheshimiwa Waziri, Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana,Kuanzishwa kwa Benki ya Wanawake Tanzania ni kitendo cha kihistoria kinachotambua nafasi ya mwanamke nchini na kumtendea haki. Wanawake ni wengi kuliko wanaume hapa nchini. Ni asilimia 50.8 ya watu wote Watanzania. Hivyo basi wanaume ni asilimia 49.2.

Wanawake ndiyo wanaobeba mzigo mkubwa wa kazi ya uzalishaji mali mashambani pamoja na ile ya kutunza familia nyumbani. Lakini, wanawake hao wanaotoa mchango mkubwa sana kwa uchumi wa familia na jamii kwa jumla, wengi wao ni maskini. Ukweli ni kwamba, hapa nchini pamoja na wananchi wengi kuwa maskini (asilimia 33.3 kwa takwimu za 2007) lakini kati yao wanawake ni wengi zaidi kuliko wanaume.

Wanawake wapo katika hali hiyo kwa sababu ya mazingira maalum wanayoishi nayo. Baadhi ya mila na desturi za makabila yetu mengi zinamfanya mwanamke awe hivyo. Bahati mbaya pia baadhi ya sheria zetu zinaendeleza na kuendekeza unyanyasaji na ukandamizaji wa wanawake. Kiserikali tumezirekebisha baadhi ya sheria hizo na kazi bado inaendelea.

Kwa upande wa mila na desturi baadhi ya sheria tulizotunga zimesaidia kuzirekebisha na tutakazotunga siku za usoni zitasaidia zaidi. Hata hivyo, hatuna budi kuendeleza juhudi katika jamii zetu na makabila yetu nchini za kubadili mila na desturi zinazoathiri vibaya haki na maendeleo ya wanawake na kuwafanya wengi wao kuwa maskini.

Pamoja na hayo ambayo mafanikio yake yameanza kuonekana bado imekuwepo na bado ipo haja ya kuwepo mipango ya kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa mikopo ili waweze kujinasua kutoka katika lindi la umaskini. Kukosekana kwa asasi ya fedha yenye uwezo na mtaji mkubwa wa kuwawezesha wanawake kupata mikopo mikubwa zaidi ambayo wataitumia kama mitaji ya kuendeleza shughuli zao kiuchumi umekuwa upungufu mkubwa. 

Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana;
Hivyo basi kuanzishwa kwa Benki ya Wanawake Tanzania ni hatua muafaka ya kutatua tatizo hili katika dhamira azizi ya kuwawezesha wanawake kiuchumi. Ni ushahidi mwingine kwamba Serikali yetu inawajali wanawake wa Tanzania na inayo dhamira ya dhati ya kuinua hali zao za maisha. Kuwepo kwa Benki hii na kuanza kazi rasmi kunatoa fursa kwa wanawake wa Tanzania kutumia huduma zake kujiletea maendeleo na kuondokana na umaskini.

Nimefarijika sana kusikia kwamba wanawake wengi na wanaume pia wamejitokeza kutumia huduma za Benki hii tangu ifungue milango yake tarehe 28 Julai, 2009. Ni matumaini yangu kwamba, watu wengi zaidi na hasa wanawake watajitokeza kufungua akaunti katika Benki hii.
Natoa wito kwa wanawake wote Tanzania, ambao benki hii ipo kwa ajili yao, wawe mstari wa mbele kufungua akaunti na kununua hisa.

Wakifanya hivyo watakuwa wamiliki halisi wa benki na kufaidi zaidi matunda yake. Hivyo basi, napenda kusisitiza umuhimu wa wanawake wa Tanzania kujitokeza kwa wingi na kuwa mstari wa mbele katika kuistawisha Benki yao. Lazima muonekane mkifanya hivyo, vinginevyo vilio vyenu vya huko nyuma vitakuwa havieleweki na juhudi zetu wengine zitakuwa sawa na kilio nyikani. Zitakuwa zimepotea bure. Siamini kuwa mtaacha hayo yatokee.

Pamoja na kusema hayo kuhusu wanawake, ni vizuri nikasisitiza ukweli kwamba benki hii ipo kwa ajili ya watu wote: wanawake na wanaume. Hivyo napenda kutumia nafasi hii pia kutoa wito kwa wanaume wenzangu kote nchini kujitokeza kufungua akaunti na kununua hisa katika Benki hii.

Lazima tujitokeze kuwaunga mkono mama zetu, wake zetu, dada zetu na mabinti zetu. Hatuna budi kukumbuka ule msemo maarufu kuwa ‘’kila kwenye mwanamke aliyefanikiwa, nyuma yake kuna mwanaume anayejali.’’ Sasa ni wakati wetu wanaume kuonyesha tunajali kwa kusaidia Benki ya Wanawake Tanzania istawi na kufanikiwa katika malengo yake.

Mchango wa wanaume ni muhimu kama watu wenye wajibu kwa maendeleo ya wanawake kama vile ambavyo wanawake huchangia kwa maendeleo ya wanaume. Vile vile, ni ukweli ulio wazi kwamba katika jamii wanaume ndiyo wenye uwezo mkubwa kiuchumi kuliko wanawake. Hivyo basi, lazima wanaume wawe mstari wa mbele kununua hisa na kufungua akaunti katika Benki ya Wanawake.

Pia wanaume wasaidie kuwashawishi wanaume wenzao, marafiki zao, wake zao, watoto wao na ndugu zao wanunue hisa na kufungua akaunti zao katika Benki hii. Aidha, niwaombe wafanyabiashara na makampuni makubwa na madogo nao kufanya hivyo hivyo. Ningefurahi sana pia kama asasi za Serikali na zisizo za kiserikali nazo zikafungua akaunti katika Benki hii. Kama haya yote yatafanyika Benki ya Wanawake Tanzania itapata mafanikio makubwa tunayoyatarajia sote katika muda usiokuwa mrefu.Tujenge Benki

Mheshimiwa Waziri, Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana;Wakati huu tunapozindua rasmi Benki ya Wanawake Tanzania, napenda pia kuwakumbusha msemo ambao wanawake wanaujua sana maana yake. Nao si mwingine bali ni ule usemao ‘’kuzaa si kazi, kazi kulea”. Ni kweli tumehangaika sana kwa miaka mingi, tangu uhuru, mpaka leo tunapopata bahati ya kuwa na hii benki. Haikuwezekana huko nyuma sasa tumeweza. Lakini, kazi kubwa inaanza sasa. Kazi hiyo si nyingine bali ile ya kuhakikisha kuwa Benki hii inajengeka na inaendeshwa vizuri ili kiwe ni chombo cha fedha kilicho kizuri, imara, kinachojengeka, kukua na kuendeshwa kwa kuzingatia misingi stahiki ya weledi wa kibenki.

Haya yote yatapatikana kwa kuwa na menejimenti nzuri inayojua vizuri kazi yake ya uendeshaji na kutambua vyema wajibu wake na kuutekeleza ipasavyo kwa kuzingatia kanuni za weledi wa shughuli za kibenki. Pia kwa kuwa na watumishi wenye ujuzi wa kutosha wa kazi za kibenki, wachapa kazi hodari, waaminifu na waadilifu.

Mfanikio ya benki hii yatategemea kuwa na Bodi ya Wakurugenzi nzuri inayotambua vyema wajibu wake wa uongozi wa benki. Bodi ambayo wajumbe wake ni watu makini, wabunifu, waaminifu na waadilifu. Mambo haya ni sharti muhimu sana kwa kukua na kuimarika kwa Benki yetu hii sasa, miaka mingi ijayo na kwa wakati wote wa uhai wake.

Pengine, haya niyasemayo sasa ni muhimu zaidi hapa mwanzoni kwani ukianza vizuri unajihakikishia mafanikio mazuri baadae na hatma njema. Nayasema haya kusisitiza umuhimu wa kuzingatia kanuni za uendeshaji na uongozi mzuri wa taasisi ya fedha kama hii. Naomba kamwe nisieleweke kuwa nina mashaka na Menejimenti au Bodi iliyopo. Sina mashaka kabisa. Nina imani nao sana kwamba wana uwezo wa kutuvusha na kutupeleka kwenye neema. Nayasema haya kusisitiza umuhimu wake na kutaka yazingatiwe wakati wote.

Mheshimiwa Waziri, Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana;Jambo lingine muhimu sana kwa maendeleo ya benki hii ninalopenda kulisisitiza ni kuwa na sera ya mikopo iliyo nzuri. Aidha, hakikisheni kwamba mnakuwa makini katika ukopeshaji na ulipaji wa mikopo. Nimefahamishwa kuwa Benki hii ambayo ni maarufu kwa jina ”Benki Pekee Kwa Wote” itatoa mikopo kwa wanawake na wananchi wote kwa ujumla, wenye biashara kubwa, za kati na ndogondogo. Hii ni sahihi kabisa.

Hata hivyo, ili benki hii iendelee kukua na kustawi na iwe na maendeleo endelevu na kutimiza malengo yake kama ilivyokusudiwa lazima mikopo itolewe kwa uangalifu na hakikisheni inalipwa kwa wakati. Vile vile, muwe na msimamo thabiti katika kuwabana na kuwawajibisha wasiolipa mikopo yao kwa mujibu wa masharti ya mikopo.Natoa wito kwa wale watakaokopa katika Benki ya Wanawake waitumie vizuri na walipe mikopo yao kwa wakati ili waepukane na madhara yanayosababishwa na kushindwa kurejesha mikopo kwa wakati stahiki.

Kwa upande wa Benki lazima kuzingatia taratibu za kutoa mikopo kabla ya kutoa na kuhakikisha kuwa wakopaji wanafuatiliwa vizuri ili kupunguza hasara. Hii itaiwezesha benki kuwa na msingi imara ulio endelevu na kuweza kuwafikia wadau wake (wanawake) wengi mijini na vijijini kama lilivyo lengo la Benki hii. Narudia kusisitiza kuwa ni muhimu kwa wanawake kujijengea tabia na utaratibu wa kuweka akiba zao katika benki hii.

Licha ya kuwahakikishia usalama, benki inatoa fursa nyingi za kiuchumi. Nakuomba Mheshimiwa Waziri na viongozi wenzako Wizarani na katika UWT kufanya juhudi za makusudi za kutoa elimu kwa wanawake wote nchini. Katika kufanya hivyo muwaelimishe pia kuwa, huwa rahisi kwa benki kuwakopesha watu wenye akaunti na ambao hufanya shughuli zao za mapato na malipo kupitia benki hiyo.

Ni matarajio yangu na ya wanawake wote nchini kuwa huduma za Benki hii zitawafikia kwa urahisi. Hii ina maana ya Benki kuwa na matawi maeneo mengi nchini. Hili ni jambo la msingi ambalo Benki yetu hii haina budi ilipatie jibu sawia. Nimefurahi kusikia kwamba katika mpango mkakati wake, benki hii imejipanga kufanya hivyo siku za usoni. Naomba Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ishirikiane kwa karibu na Menejimenti ya Benki katika utekelezaji wa shabaha hii ya kufungua matawi katika mikoa hapa nchini.

Naomba pia nitahadharishe kuwa, ufunguzi wa matawi katika mikoa ufanyike baada ya kuimarika kwa Benki. Jambo hili lisifanyike kwa nia ya kupendezesha wadau bila kujali uwezo wa Benki kumudu kufanya hivyo. Msipozingatia kanuni hiyo ya msingi benki itadhoofika baada ya muda si mrefu na uhai wake utakuwa hatarini. Angalieni mifano ya Benki nyingine nchini, hususan zile za kigeni ambazo zilichukuwa muda kabla ya kufungua matawi nje ya Dar es Salaam. Walifanya hivyo ili kujipa muda wa kukua na kujijenga. Msikubali kufanya kinyume chake.
Jitihada Nyingine za Kuwawezesha Wanawake
Mheshimiwa Waziri, Wageni Waalikwa, Mabibi na MabwanaNi muhimu nikaeleza pia kwamba, jitihada za kuwawezesha wanawake kiuchumi hazianzi leo kwa uanzishaji wa hii Benki.
Serikali imekuwa inachukua hatua mbalimbali kwa nia ya kuwawezesha wananchi kiuchumi, hususan wanawake na vijana. Kumekuwepo na mipango na programu kadhaa kwa lengo hilo. Kwa mfano, kuna Mfuko wa Maendeleo wa Wanawake (WDF), ambao umekuwa unatoa mikopo ya masharti nafuu kwa wanawake kupitia Halmashauri za Wilaya na Miji nchini. Wanawake zaidi ya 300,000, wamefaidika na mfuko huu na wengi zaidi watanufaika.

Upo mfuko wa Rais wa Kujitegemea na Mfuko wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi unaojulikana kama mabilioni ya JK, ulioanzishwa mwaka 2006 ambapo wanawake wengi wamenufaika. Serikali pia, imewezesha mashirika kadhaa yasiyokuwa ya Kiserikali kufanya kazi nchini na kunufaisha wanawake wengi. Tutaendelea kuongeza fedha katika mifuko hiyo na kurahisisha mazingira ya kazi kwa NGO’s zinazosaidia wanawake nchini. Pia tutaendelea kuongeza mtaji wa Benki hii mara kwa mara.

Aidha, wanawake wamewezeshwa kushiriki katika maonyesho mbalimbali ya biashara ambapo wamewezeshwa kupata masoko ya bidhaa zao na kuwa kichocheo cha kuongeza bidhaa wanazozalisha. Wanawake, pia, wamekuwa wakipatiwa mafunzo ya ujasiriamali kwa madhumuni ya kutumia vizuri mitaji pamoja na mikopo wanayopatiwa.

Serikali katika awamu hii imetoa msukumo mkubwa wa wananchi kuanzisha Vyama vya Ushirika vya Kuweka na Kukopa yaani SACCOS. Kwa ajili hiyo SACCOS nyingi zimeanzishwa nchini na kuwa chombo cha kifedha ambacho wanawake wengi wameweza kupata mikopo ya kufanya shughuli zao. Benki ya Wanawake tunayoizindua leo inaweza kuwanufaisha wanawake wengi zaidi kama itaweka mkakati mahususi wa kufanya kazi na SACCOS hapa nchini. Kufanya hivyo pia kutasaidia benki kusogeza huduma zake karibu na walipo wadau wake. Itasaidia kujijenga na kutanua huduma zake. CRDB ni mfano mzuri wa benki iliyotumia mfumo wa SACCOS kujijenga, kujitanua na kuwa karibu na watu.

Kilimo Kwanza
Ndugu Wananchi;
Kabla ya kumaliza hotuba yangu ningependa kutoa ombi maalum kwa uongozi na menejimenti ya Benki yetu hii mpya kuwa, katika kutengeneza sera ya mikopo wasisahau mikopo kwa sekta ya kilimo. Naelewa hisia na hasa hofu za mabenki kukopesha sekta ya kilimo. Nawaomba msizipuuzie hofu hizo hata kidogo ila msitishike mno wala kuendekeza hofu hizo na zikawafanya muinyanyapae sekta ya kilimo.
Zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania wanaishi vijijini na wanategemea kilimo kwa maisha yao na kwa maendeleo yao. Na, wengi wa hao ni wanawake. Hivyo mkitoa mikopo kwa sekta ya kilimo mtawanufaisha wadau wenu wengi na kuwafurahisha. Jambo muhimu ambalo hamna budi kulizingatia ni kuwa makini kwa upande wa mtu na shughuli mnayoitolea mkopo.

Nawaomba mchague sekta ndogo au shughuli za kilimo ambazo hatari za kupata hasara si kubwa, mtoe mikopo kwa kina mama wanaojihusisha nazo. Mkifanya hivyo, pia mtakuwa mmechangia katika utekelezaji wa mkakati mpya wa kusukuma kilimo kwa kasi mpya, maarufu kwa Kilimo Kwanza.

Namalizia kwa kuwapongeza tena wanawake wote nchini kwa mafanikio makubwa waliyopata ya kuweza kuwa na benki yao. Nawaomba mdumishe na kuendeleza umoja na mshikamano wenu ili kuhakikisha kuwa benki yenu hii muimiliki na kuiendesha vizuri kwa maslahi ya wanawake na maendeleo yao. Baada ya kusema hayo, natamka kuwa Benki ya Wanawake Tanzania imezinduliwa rasmi.

Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Ibariki Afrika,
Mungu Wabariki Wanawake Wote Nchini,
ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.

Thursday, September 3, 2009

KIBAKI NA PINDA WAKUTANA KWA MAZUNGUMZO JIJINI NAIROBI

Rais Mwai Kibaki wa Kenya akiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu Mizengo Pinda katikati na Deodorous Kamala kulia wakati wa mzungumzo yao yaliyofanyika jijini Nairobi.

Msomaji
Nairobi

KATIBU MKUU JINSIA NA WATOTO AKIKABIDHI BENKI YA WANAWAKE GARI

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bibi Mariam Mwaffisi (kulia) akimkabidhi funguo za gari Mkurugenzi wa Tanzania Women's Bank Bibi, Magreth Chacha (Kushoto) . Gari hiyo imekabidhiwa kwa ajili ya shughuli za Benki hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho tarehe 4 Septemba,2009, saa 3:00 na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete .

Msomaji
Dar es salaam

Wednesday, September 2, 2009

Rais Jakaya Kikwete akiongea na mwenyeji wake Kiongozi wa Libya Muamar Gadafi ambaye pia amesherehekea miaka 40 ya utawala wake hivi karibuni rais pia alihudhuria mkutano wa AU nchini Libya.