Sunday, November 7, 2010

HONGERA MH RAIS JAKAYA KIKWETE




TAWI LA CCM MAREKANI LINAUNGANA NA WATANZANIA WOTE KATIKA KUKUPONGEZA KWA KUCHAGULIWA TENA KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA MUHULA MWINGINE WA MIAKA MITANO. USHINDI ULIOPATIKANA NI USHINDI WA WATANZANIA WOTE NA NI ISHARA YA IMANI TULIYONAYO KATIKA UONGOZI WAKO BORA.


TUNAKUOMBEA KWA MWENYEZI MUNGU AKUPE AFYA NJEMA, AKUONGEZEE ZAIDI HEKIMA, BUSARA NA UVUMILIVU ILI TUENDELEE KUFAIDI MATUNDA YA UONGOZI WAKO ULIOJAA MAPENZI KWA WANANCHI WAKO NA NCHI YETU.

Monday, November 1, 2010

Shein Rais mpya wa Zanzibar






Tuesday, 02 November 2010 02:23

Dk Shein akizungumza na wananchi wa Zanzibar mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya UraisFidelis ButaheCCM jana ilifanikiwa kunyakua tena kiti cha urais baada ya mgombea wake, Dk Ali Mohamed Shein kuibuka mshindi kwenye uchaguzi uliofanyika Jumapili akimshinda mgombea wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad.Dk Shein, ambaye anamalizia kipindi chake kama makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano, sasa anakuwa rais wa saba wa Zanzibar, ambayo inaundwa na visiwa vya Pemba na Unguja akimbadili Abeid Amani Karume pia wa CCM.Lakini Dk Shein atakuwa na changamoto kubwa ya kuwa kiongozi wa kwanza kuongoza Serikali ya Umoja wa Kitaifa na atashirikiana na Maalim Seif, ambaye kwa mujibu wa marekebisho ya katiba baada ya kufikiwa kwa maridhiano, anakuwa makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar.Akitangaza matokeo hayo, mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (Zec), Khatib Mwinyichande alisema Dk Shein alipata kura 179,809 ambazo ni sawa na asilimia 50.1.Kwa mujibu wa matokeo hayo, Maalim Seif, ambaye amegombea urais kwa mara ya nne, alipata kura 176,338 ambazo ni sawa na aslimia 49.1 ya kura zote 358,815.Alisema kuwa vyama vilivyosimamisha wagombea urais katika uchaguzi huo ni pamoja na AFP, CCM, CUF, Jahazi Asilia, NCCR-Mageuzi, NRA na Tadea."Matokeo yanaonyesha kuwa mgombea wa NRA amepata kura 480 sawa na asilimia 0.1, wa CCM kura 179,809 sawa na asilimia 50.1, wa CUF kura 176,338 sawa na asilimia 49.1, Jahazi Asilia kura 803 sawa na asilimia 0.2, NCCR kura 363 sawa na asilimia 0.1, NRA kura 525 sawa na asilimia 0.1 na Tadea kura 497 sawa na asilimia 0.1," alisema Mwinyichande.Tofauti na ilivyokuwa kwenye chaguzi zilizopita, jana hali ilikuwa shwari wakati mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (Zec) akitangaza matokeo ya urais. Shangwe zilizofuata baada ya Dk Shein kutangazwa kuwa mshindi, hazikunakshiwa kwa vijembe vya kuudhi wapinaani kama ambavyo imekuwa ikifanyika kwenye chaguzi zilizopita.Hata Maalim Seif alikuwepo wakati wa hafla hiyo na akakubali kwenda mbele kutoa hotuba ya kukubali matokeo ambayo ilijaa hekima na busara ikieleza umuhimu wa makubaliano yaliyofikiwa baina ya pande hizo mbili kuu, huku ikitaharidha kuhusu vitendo vinavyoweza kuvuruga maridhiano hayo."Kwa mara ya kwanbza uchaguzi umefanyika kwa amani, bila ya vitisho. Kampeni ziliendeshwa kiungwana na kwa ustaarabu," alisema Maalim Seif ambaye aliwahi kuwa waziri kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ)."Nachukua nafasi hii kumpongeza kwa dhati kabisa Dk Ali Mohamed Shein kwa kupata ridhaa ya Wazanzibari atuongoze kwa miaka mitano inayokuja."Dk Shein ana uwezo, uzoefu na mahaba kwa nchi yake. Tunatumaini ataongoza kwa busara na hekima kwa lengo la kuunganisha nchi yetu. Naamini kuwa Wazanzibari walifanya maamuzi sahihi Julai 31. Tarehe hiyo waliamua kuunda serikali shirikishi."

Dk Shein na Mr Seif wakipongezana mara baada ya tume ya uchaguzi kutoa matokeoSeif, ambaye alikuwa akizungumza kwa utulivu, alisema uamuzi huo umeweka enzi mpya ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kwamba Wazanzibari wamempa Dk Shein jukumu la kuongoza kwa mara ya kwanza serikali ya umoja.Lakini mkongwe huyo wa siasa visiwani Pemba na Unguja hakusita kutoa tahadhari kwa Dk Shein na CCM wakati akitaja mambo makuu matatu muhimu."Kwanza ni shukrani kwa Tume ya Uchaguzi kwa kuendesha uchaguzi ambao ulikuwa na afadhali kulinganisha na chaguzi nyingine," alisema."Lakini kuna dosari ambazo ni lazima zirekebishwe. Mwenye matatizo si wewe mkurugenzi... ni baadhi ya maofisa wako."Alieleza matatizo ambayo maofisa wa uchaguzi wamekuwa wakiyafanya akisema yanasababisha watu wasiwe na imani na tume."Jambo la pili ni kwamba Dk Shein ni rais mteule. Ametangazwa tu kuwa mshindi, lakini hakuna mshindi. Washindi ni Wazanzibari wote na Shein ni mteule tu."Dk Shein alionya katika suala lake la tatu kuwa baada ya matokeo hayo kusiweo na siasa za kubezana."Siasa za kubezana zitachafua hali ya hewa kabisa," alionya Maalim Seif akimtaka Dk Shein afikishe ujumbe huo kwa viongozi wenzake wa CCM na wanachama wao.Naye Dk Shein, ambaye huzungumza kwa utaratibu na mpangilio, alimshukuru Maalim Seif kwa hotuba yake, aliyoielezea kuwa ilijaa busara na hekima na kuahidi kutekeleza yote ambayo kiongozi huyo wa CUF aliyazungumzia."Nafahamu fika kuwa kazi hii ni nzito... Mungu anisaidie, anipe hekima na busara ili niifanye kwa uadilifu," alisema Dk Shein.Shein sasa atakuwa na changamoto jipya la kuwa rais wa kwanza kuongoza Zanzibar akishirikiana na chama kikuu cha upinzani, CUF baada ya pande hizo mbili kufikia maridhiano ambayo yalilifanya Baraza la Wawakilishi kuridhia kupitisha sheria inayoruhusu kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.Kwa mujibu wa muundo mpya wa Serikali ya Zanzibar, mshindi wa uchaguzi mkuu ndiye ataingia Ikulu akiwa rais na mgombea aliyeshindwa atakabidhiwa nafasi ya makamu wa kwanza wa rais.Muafaka huo ulifikiwa baada ya viongozi wakuu wa vyama hivyo viwili, Rais Amani Abeid Karume kukutana kwa faragha Ikulu na katibu mkuu wa CUF, Seif Sharrif Hamad Novemba 4, 2009.
Taarifa iliyotolewa baada ya faragha hiyo ilieleza kuwa wawili hao walizungumzia haja ya kudumisha amani na utulivu pamoja na kuwa na maelewano na ushirikiano baina ya wananchi wote wa Zanzibar.


Source: Mwananchi

Monday, October 18, 2010

CCM to tap skills from Tanzanians in diaspora


CCM to tap skills from Tanzanians in diaspora
From MARC NKWAME in Arusha, 17th October 2010 @ 12:06 , Total hits: 73

THE CCM Union presidential running mate, Dr Mohamed Gharib Bilal, said here that his government intends to tap skills and resources from Tanzanians living and working abroad.
Addressing a series of campaign rallies in Arusha, Mr Bilal stated that there were more potential skills, resources and even wealth to be tapped from the Diaspora and should CCM win, then Mr Jakaya Kikwete’s government will ensure that all Tanzanians living overseas are fully involved in catalyzing the country’s development.
‘’It is high time that Tanzania started making use of her people spread around the globe, most of them are highly skilled people who could help in both leadership and executing development projects here, others have wealth and resources that they are eager to share with their countrymen but have no idea how to go about it, we intend to establish a special system that will connect us with them,’’ the CCM’s aspiring vice-president said.
Dr Bilal, who is a nuclear scientist by profession, knows how to go about it: ‘’We have already started working towards connecting Tanzania with the entire world digitally via fibre optic cable to enable faster and easy communications and already many regions have been connected while more efforts to network the rest are going on.
‘’We intend to ensure that young children attend kindergarten schools as the foundation for their early education, pupils who start learning from nursery level have better chances of being able to grasp lessons later in life,’’ stated Dr Bilal.
In most remote parts of Tanzania, children usually by-pass early childhood (kindergarten) level of education going straight to class one (primary), nursery schools are also lacking in rural areas but are abundant in towns.
Mr Bilal hinted that his government would increase the number of female students in higher institutions of learning to reach at least 45 per cent and he maintained that his government will be able to accomplish that by ensuring that the poor girls, who do well in school but lack money, are sponsored to pursue further education.

Tuesday, September 21, 2010

TOGETHER, WE STAND!!!


KADA MACHACHARI WA CCM FRED MWAKALEBELA ALIYESHINDA KURA ZA MAONI JIMBO LA IRINGA MJINI, HANA TAMAA YA UONGOZI ANAJALI MASLAHI YA CHAMA CHAKE KWA KUHAKIKISHA MGOMBEA WA CCM BIBI MONICA MBEGA ANASHINDA KWA KISHINDO

IRINGA - SAMORA YAFURIKA NA KUKOSA PA KUKANYAGA

KURA KWA CCM TU!!!!!!!!

ISIMANI NGOME IMARA YA CCM

ISIMANI WALIKWISHAAMUA KURA ZOTE NI KWA CCM, NA WAKATOA KIANZIO KWA KUMPITISHA MBUNGE WAO BILA YA KUPINGWA.

LUKUVI MBUNGE MTEULE ISIMANI-CCM

REKODI YAKE NZURI YA UTENDAJI JIMBONI IMEWAKIMBIZA WAPINZANI, AMEPITA BILA YA KUPINGWA.

NAMANGA NA CCM

UMATI MKUBWA WA WAKAZI WA NAMANGA WALIJITOKEZA KUMSIKILIZA JK NA KUKATA SHAURI KWA KUWAPA KURA YA NDIYO WAGOMBEA WA CCM

TOBIKO KIKWETE, TOBIKO!!

MONDULI NI MOJA KATI YA NGOME NYINGI NGUMU ZA CCM

MUHEZA OYEEEEEEE

MKUZI, KICHEBA, LUSANGA, KIWANDA, AMANI...'YES TO JK AND CCM'

KILINDI 'KURA YA NDIYO KWA CCM'


KILINDI WAMEAHIDI KUPIGA KURA YA NDIYO KWA WAGOMBEA WA CCM

Monday, September 20, 2010

Sunday, August 22, 2010

CCM yaanza kampeni kwa kishindo



Rekodi iliyowekwa na Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete katika kutimiza ahadi zake, ni kielelezo tosha cha kukichagua chama hicho kuendelea kuiongoza nchi. Hatua hiyo ndiyo inafanya mgombea urais wa chama hicho, Kikwete aamini, kwamba CCM safari hii itashinda kwa kishindo zaidi, katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 31, mwaka huu. Akizindua rasmi kampeni za uchaguzi za CCM katika viwanja vya Jangwani Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alisema: “Hatuwaangusha … tumetekeleza Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2005 kwa kiwango kikubwa sana, yapo machache ambayo hatujayakamilisha na ambayo tutayachukua ili kuyakamilisha katika Ilani ya 2010”. Alisema CCM ni chama kinachoaminika na Watanzania wengi kutokana na uimara na ubora wa sera, ubora wa muundo na ubora wa wagombea wake, na kuwataka wananchi kuendelea kukiamini kwa kuchagua wagombea wake katika uchaguzi mkuu ujao. “Vipo vyama saba ambavyo vimesimamisha mgombea kwa nafasi ya Rais wa Jamhuri, lakini mgombea wa CCM ni bora zaidi. Tumejaribu kuangalia sera za vyama vyote 13 vyenye usajili wa kudumu, tukagundua kuwa wanachukua sera zetu na kuzibadili kidogo tu kuzifanya kuwa zao. “Si jambo baya kuiga kitu kizuri kutoka CCM, lakini ni kwa nini wananchi wachague kitu fotokopi wakati orijino kipo?” alihoji Rais Kikwete. Alisema wakati CCM ilipoingia madarakani ilitoa ahadi ya kutetea na kulinda Muungano, kuboresha ulinzi na usalama wa nchi, kuimarisha utawala bora ili kuhakikisha sheria na haki za binadamu vinafuatwa. “Kuboresha nidhamu ya matumizi ya fedha za umma, kuimarisha mihimili ya Dola ya Bunge, Mahakama na Utawala, kulinda uhuru wa kuabudu na wa vyombo vya habari, ahadi ambazo alisema zimetekelezwa kwa mafanikio makubwa. Kuhusu amani na utulivu, mgombea huyo alisema Watanzania wameendelea kuwa wamoja bila kubaguana kwa misingi ya dini, ukabila wala rangi na kwamba juhudi za kuwatenganisha zimegonga mwamba na kamwe hazitafanikiwa chini ya utawala wa CCM. “Uhalifu na ujambazi vimepungua sana, wakati tulipoingia madarakani, wimbi la ujambazi lilikuwa kubwa, lakini kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na Polisi, ujambazi umepungua ingawa yapo matukio machache ya hapa na pale yanayojitokeza ambayo hata hivyo tunakabiliana nayo.” Alisema mapato ya Serikali yameimarika kutoka Sh bilioni 117.5 kwa mwezi mwaka 2005 hadi Sh bilioni 390 kwa mwezi hivi sasa, hatua ambayo alisema imepunguza utegemezi kutoka asilimia 42 hadi asilimia 28 na pesa hizo kwa kiasi kikubwa zinawafikia walengwa. Kuhusu rushwa, alisema Serikali ya CCM katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, imekuwa na dhamira ya dhati ya kukabiliana na vitendo vya rushwa kwa kuiongeza meno zaidi-Sheria ya Kupambana na Rushwa na kutungwa kwa Sheria ya Gharama za Uchaguzi na kuiboresha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru). “Watu wote ni mashahidi namna watu tena wengine mashuhuri walivyofikishwa mahakamani, kutokana na kuhusishwa na rushwa. Tufanye nini zaidi ya hapa?” alihoji Kikwete. Rais Kikwete alisema pia Serikali ya CCM imeboresha maslahi ya wafanyakazi kwa kupandisha mishahara ya watumishi. Alisema Serikali ilikuwa katika mgogoro na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) kutokana na kutaka malipo ya juu ya mishahara ingawa suala hilo limepatiwa ufumbuzi. “Kuhusu hili la mishahara si kama tunapuuza, tulichokubaliana nao ni kwamba tutalipa kwa kiwango tunachoweza na tusichoweza hatutalipa. Tumejitahidi pia kuboresha huduma nyingine muhimu kama maji, elimu, miundombinu, kilimo na afya. Tunaomba Watanzania watupigie kura katika uchaguzi mkuu ujao,” alimaliza Rais Kikwete. Awali kabla ya Rais Kikwete kuhutubia Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba alimkabidhi Rais wa Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar, Dk. Amani Abeid Karume, Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kitabu cha Mwelekeo wa Sera za CCM ambavyo baadaye Rais Karume alimkabidhi mgombea, Rais Kikwete. Rais Karume, Makamba na mgombea mwenza wa urais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, walihutubia hadhira hiyo na kuwataka wananchi kuendelea kuichagua CCM. Wana-CCM walianza kuwasili katika viwanja vya Jangwani mapema asubuhi na hadi saa tano viwanja hivyo vilikuwa vimefurika umati mkubwa wa watu. Wana CCM waliitafsiri hali hiyo kuwa ni ishara na nyota njema kwao kuibuka na ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu mwaka huu. Kabla ya viongozi kuanza kutoa hotuba, bendi na vikundi mbalimbali vya burudani karibu vyote maarufu vilitoa burudani katika hadhara hiyo.

Tuesday, August 17, 2010

Obama salutes Kikwete over Zanzibar


President, Barack Obama has saluted his Tanzanian counterpart, Jakaya Kikwete on the way he has been handling the reconciliation process in Zanzibar. In his special message delivered to President Kikwete by the US Ambassador in Tanzania, Mr Alfonso E. Lenhardt in Dar es Salaam on Tuesday, the US president said that President Kikwete’s efforts culminated in the successful holding of the referendum on the Government of National Unity (GNU) in Zanzibar. “On behalf of the American people, I am congratulating you personally, Zanzibar leaders and the people as well as all Tanzanians for holding a peaceful referendum on the formation of a GNU held on July 31”, President Obama said in the message. He added that President Kikwete was a man who lived by his word, recalling their talks at the White House in the US on May 21, last year, when he (Kikwete) expressed his desire for reconciliation among the warring Zanzibar politicians. “It's my pleasure indeed that in a very short period of time, your able leadership, the resolve by the Zanzibar Electoral Commission (ZEC), non-governmental organizations, religious institutions and political parties have all helped to make a notable step in bringing about lasting peace which was demonstrated in the referendum”, he said. During their talks at the White House, President Kikwete promised his counterpart that his government would deploy every effort towards ending the political tension in Zanzibar peacefully. However, President Obama said there are still challenges as the general elections in October approach. But he said he was optimistic about the government’s desire to elect their leaders peacefully. “Through your visionary leadership, I can see a ray of hope and I am hopeful we will continue working together for the good of our great countries,” President Obama said in the message to President Kikwete.

Dr Shein calls for unity among CCM members


CCM’s presidential candidate for Zanzibar, Dr Ali Mohamed Shein, has called on party members in the islands to unite in efforts to end rifts ahead of October 31 general elections.
Dr Shein said that unity within the party was crucial despite the fact that CCM victory in the elections was ‘certain.’ Addressing party supporters and members, Dr Shein asked them to support him and abandon conflicting groups for the interest of the party. “It is obvious that everyone has own preference for councillorship, House of Representatives, Union Member of the Parliament and Zanzibar presidency. “Fortunately, the process to choose our candidates is over, let us now unite with the desire to win the next elections,” Dr Shein told the gathering at Bwawani Hotel in the Stone Town. Dr Shein who is expected to pick nomination forms at the Zanzibar Electoral Commission (ZEC) today, said he was a person of few words but a committed person who shows his competency by practice. He warned he would not hesitate to fire any leader in his government who puts personal interest first. “I am not a person who speaks a lot. I am a man of actions. I am ready to serve Zanzibaris to their expectations as per the party manifesto which is ready and will be made public during campaign time,” said Dr Shein amid cheers from the gathering. “I am disturbed with news that some houses have been damaged by home made bombs, people are beaten or live in fear. Let us put aside our differences which emerged during the nomination period and work as a team for CCM’s victory,” he said. Several ministers from both union and Zanzibar governments attended the meeting.

Sunday, August 15, 2010

Endorsed CCM Paliamentary Candidates

Here is the whole list of the names of parliamentary aspirants endorsed by the CCM National Executive Committee:

ARUSHA
i. Arusha: Dr. Batilda BURIANIii. Arumeru East: Jeremiah SUMARIiii. Arumeru West: Goodluck Ole MEDEYEiv. Karatu: Dr. Wilbald LORRIv. Longido: Michael LAIZERvi. Monduli: Edward LOWASSAvii. Ngorongoro: Saning’o Ole TELELE
IRINGA
i. Iringa Urban Monica MBEGAii. Isimani: William LUKUVIiii. Kalenga: William MGIMWAiv. Kilolo: Prof. Peter MSOLLAv. Ludewa: Deo FILIKUNJOMBEvi. Makete: Dr. Binilith MAHENGEvii. Mufindi North: Mohamed MGIMWAviii. Mufindi South: Menrad KIGOLAix. Njombe North: Deo SANGA (Jah People)x. Njombe South: Anne MAKINDAxi. Njombe West: Gerson LWENGE
KAGERA
i. Nkenge: Assumpter MSHAMAii. Bukoba Urban: Khamis KAGASHEKIiii. Bukoba Rural: Jasson RWEIKIZAiv. Muleba North: Charles MWIJAGEv. Muleba South: Anna TIBAIJUKA vi. Chato: John MAGUFULIvii. Kyerwa: Eustace KATAGIRAviii. Karagwe: Gosbert BLANDESix. Biharamulo: Oscar MUKASAx. Ngara: Deogratias NTUKAMAZINA
KIGOMA
i. Kigoma Urban: Peter SERUKAMBAii. Kigoma South: Gulam KIFUiii. Kasulu Urban: Neka NEKAiv. Kasulu Rural: Daniel NSANZUGWANKOv. Manyovu: Albert NTABALIBAvi. Buyungu: Christopher CHIZAvii. Muhambwe: Jamal TAMIMUviii. Kigoma North: Rabinson LEMBO
KILIMANJARO
i. Moshi Urban: Justin SALAKANAii. Moshi Rural: Dr. Cyril CHAMIiii. Rombo: Basil MRAMBAiv. Same East: Anne MALECELAv. Same West: David DAVIDvi. Hai: Fuya KIMBITAvii. Vunjo: Chrispin MEELAviii. Mwanga: Prof. Jumanne MAGHEMBEix. Siha: Aggrey MWANRI
MANYARA
i. Babati Urban: Kisyeri CHAMBIRIii. Babati Rural: Jitu SONIiii. Hanang: Dr. Mary NAGUiv. Kiteto: Benedict Ole NANGOROv. Mbulu: Philip MARMOvi. Simanjiro: Christopher Ole SENDEKA
MARA
i. Musoma Urban: Vedasto MATHAYO Manyinyiii. Musoma Rural: Nimrod MKONOiii. Mwibara: Alphaxard LUGOLAiv. Bunda: Stephene WASSIRAv. Rorya: Lameck AIROvi. Tarime: Nyambari NYANGWINEvii. Serengeti: Dr. Stephene KEBWE
MBEYA
i. Mbeya Urban: Benson MPESYAii. Mbeya Rural: Luckson MWANJALAiii. Kyela: Dr. Harrison MWAKYEMBEiv. Mbarali: Dickson KILUFIv. Lupa: Victor MWAMBALASWAvi. Songwe: Philipo MULUGOvii. Rungwe East: Prof. Mark MWANDOSYAviii. Rungwe West Prof. David MWAKYUSAix. Ileje: Aliko KIBONAx. Mbozi Mashariki: Godfrey ZAMBIxi. Mbozi West: Dr. Luka SIAME
MOROGORO
i. Morogoro Urban: Aziz ABOODii. Morogoro South East: Dr. Lucy NKYAiii. Morogoro South: Innocent KALOGERISiv. Mvomero: Amos MAKALAv. Ulanga East: Celina KOMBANIvi. Ulanga West: Haji MPONDAvii. Gairo: Ahmed SHABIBYviii. Kilosa: Mustafa MKULOix. Mikumi: Abdulsalaam SULEIMANx. Kilombero: Abdul MTEKETA
MTWARA
i. Mtwara Urban: Murji MOHAMEDii. Mtwara Rural: Hawa GHASIAiii. Masasi: Mariam KASEMBEiv. Lulindi: Jerome BWANAUSIv. Tandahimba: Juma NJWAYOvi. Newala: George MKUCHIKAvii. Nanyumbu: Dunstan MKAPA
MWANZA
i. Ilemela: Anthony DIALLOii. Nyamagana: Laurence MASHAiii. Busega: Dr. Kamani MLENGENYAiv. Magu: Dr. Festus Limbav. Kwimba: Sharif MANSOORvi. Sumve: Richard NDASAvii. Geita: Donald MAXviii. Nyang’wale: Hussein AMARix. Sengerema: William NGELEJAx. Buchosa: Charles TIZEBAxi. Misungwi: Charles KITWANGAxii. Ukerewe: Getrude MONGELA.
RUVUMA
i. Songea Urban: Emmanuel NCHIMBIii. Peramiho: Jenister MHAGAMAiii. Namtumbo: Vita KAWAWAiv. Tunduru South: Mtutura MTUTURAv. Tunduru North: Ramo MAKANIvi. Mbinga West: Capt. John KOMBAvii. Mbinga East: Gaudence KAYOMBO
TABORA
i. Tabora Urban: Ismail RAGEii. Tabora North: Sumar MAMLOiii. Urambo East: Samuel SITTAiv. Urambo West: Prof. Juma KAPUYAv. Igunga: Rostam AZIZvi. Sikonge: Said NKUMBAvii. Igalula: Athuman MFUTAKAMBA viii. Bukene: Seleman ZEDIix. Nzega: Hamis KIGWANGALA
TANGA
i. Tanga: Omari Rashid NUNDUii. Kilindi: Beatrice Matumbo SHELUKINDOiii. Muheza: Herbert James MNTANGIiv. Mkinga: Danstan Luka KITANDULAv. Pangani: Salehe Ahmed PAMBAvi. Lushot: Henry Daffa SHEKIFU vii. Bumbuli: January MAKAMBAviii. Korogwe Urban: Yusuph A. NASRI ix. Mlalo: Brig. Gen. Hassan Athuman NGWILIZIx. Korogwe Rural: Stephen NGONYANIxxi. Handeni: Dr. Abdalah Omari KIGODA
DAR ES SALAAM
i. Kinondoni: Idd Mohamed AZZANii. Ubungo: Dr Hawa Mgonja NG’HUMBIiii. Kawe: Angella Charles KIZIGHAiv. Ilala: Mussa Azzan ZUNGUv. Ukonga: Eugen Elishiringa MWAIPOSAvi. Segerea: Dr Milton Makongoro MAHANGAvii. Temeke: Mtemvu Abbas ZUBERIviii. Kigamboni: Dr Ndugulile FAUSTINE
LINDI
i. Ruangwa: Kassim Majaliwa MAJALIWA ii. Nachingwea: Mathias Meinrad CHIKAWE iii. Kilwa North: Muraza Ali MANGUNGU iv. Lindi South: Madabida Ramadhani RASHID v. Liwale: Faith Mohamed MITAMBOvi. Lindi Urban: Mohamed ABDULAZIZI vii. Mchinga: Saidi M. MTANDAviii. Mtama: Benard Kamilius MEMBE
COAST REGION
i. Bagamoyo: Dr Shukuru J. KAWAMBWAii. Chalinze: Saidi Athuman BWANAMDOGOiii. Kisarawe: Seleman Saidi JAFOiv. Kibiti: Abdul MAROBWAv. Kibaha Rural: Mahamud Abuu JUMAAvi. Kibaha Urban: Silvester KOKAvii. Mkuranga: Adam Kighoma MALIMAviii. Rufiji: Dr Seif Seleman RASHIDix. Mafia: Abdulkarim E. SHAH
RUKWA
i. Kwela: Malocha Aloyce IGNACEii. Kalambo: Kandege Sinkamba JOSEPHATiii. Nkasi North: Ally Mohamed KESSY iv. Nkasi South: Deusderius MIPATA v. Mlele: Mizengo Kayanza Peter PINDAvi. Mpanda Central Urban: Sebastian Simon KAPUFI vii. Sumbawanga Urban: Aeshi Khalfan HILALYviii. Mpanda Rural: Moshi KAKOSO
SHINYANGA
i. Shinyanga Urban: Steven Julius MASELEii. Kahama: Nchambi Seleman MASOUDiii. Msalala: James Daudi LEMBELIiv. Solwa: Ezekiel MAIGEv. Bukombe: Ahmed Ally SALUM vi. Mbogwe: Emanuel Jumanne LUHAHULA vii. Bariadi East: Masele Agustino MANYANDA viii. Bariadi West: Makondo Martine KAUNDAix. Maswa East: Andrewx. Maswa West: Bunyongoli Peter EDWARDxi. Meatu: Kisena Robert SIMONxii. Kisesa: Salum Khamis SALUM, and Joelson Luhaga MPINA
SINGIDA
i. Singida Urban: Mohamed Gulam DEWJI ii. Manyoni East: Mr John CHILIGATI iii. Manyoni West: John Paul LWANJIiv. Iramba West: Mwigulu Lameck Nchemba MATELUv. Iramba East: Salome David MWAMBUvi. Singida North: Lazaro Samwel NYALANDUvii. Singida West: Alhaj Mohamed MISANGA viii. Singida East: Jonathan Andrew NJAU
ZANZIBAR
North Pemba
i. Konde: Salum Nafoo Omarii. Mgogoni: Mselem Rashid Mselemiii. Micheweni: Khamis Juma Omariv. Tumbe: Rashid Abdallah Khamisv. Wete: Ali Rashid Alivi. Mtambwe: Khamis Seif Alivii. Kojani: Hafidh Said Mohammedviii. Ole: Masoud Ali Mohamed ix. Gando: Haji Faki Juma
Urban West
i. Mtoni: Ussi Ame PANDU ii. Mfenesini: Nasib Suleiman OMARiii. Kiembesamaki: Waride Bakari JABUiv. Dole: Sylvester Massele MABUMBAv. Magogoni: Issa Abeid MUSSA vi. Bububu: Juma Sururu JUMA vii. Dimani: Abdallah Sheria AME viii. Mwanakwerekwe: Haji Juma SEWEREJIix. Fuoni: Said Mussa ZUBEIR x. Chumbuni: Perera Ame SILIMA xi. Kwahani: Dr Hussein Ali MWINYIxi. Mpendae: Salum Hassan ABDALLAH Turkeyxii. Stone Town: Nassor Juma MUGHEIRY xiii. Magomeni: Mohamed Amour CHOMBOxiv. Kikwajuni: Hamad Yussuf MASAUNI xv. Kwamtipura: Kheir Ali KHAMIS xvi. Amani: Mussa Hassan MUSSA xvii. Rahaleo: Abdallah Juma ABDALLAH xviii. Jang'ombe: Hussein Mussa MZEE
Unguja Northi.
Chaani: Ali Juma Haji[Chepe]ii. Matemwe: Kheir Khatib Ameiriii. Mkwajuni: Jaddy Simai Jaddyiv. Nungwi: Ame Pandu Ame,v. Tumbatu: Juma Othman Alivi. Bumbwini: Ramadhan Haji Salehvii. Donge: Sadifa Juma Khamisviii. Kitope: Ambassador Seif Ali Iddi
Pemba South
i. Chake Chake: Hamad Bakar Aliii. Chonga: Issa Ali Jumaiii. Wawi: Daudi Khamis Jumaiv. Ziwani: Juma Ali Jumav. Mkoani: Issa Mohamed Salumvi. Mkanyageni: Prof. Makame Mnyaa Mbarawavii. Chambani: Mohamed Abrahman Mwinyiviii. Mtambile: Yakoub Mohamed Shokaix. Kiwani: Rashid Abdallah Rashid
Unguja Southi.
Makunduchi: Samia Suluhu Hassaniii. Muyuni: Mahadhi Juma Maalimiii. Koani: Amina Andrew Clementiv. Uzini: Mohamed Seif Khatibv. Chwaka: Yahya Kassim IssaCandidates for the

Zanzibar House of Representatives:
Unguja North
i. Chaani: Ussi Jecha SIMANI i. Matemwe: Abdi Mossi KOMBOii. Mkwajuni: Mbarouk Wadi MUSSSA [Mtando]iii. Nungwi: Mussa Ame SILIMAiv. Tumbatu: Khaji Omar KHERI v. Bumbwini: Mlinda Mabrouk JUMAvi. Donge: Ali Juma SHAMHUNAvii. Kitope: Makame Mshimba MBAROUK
Pemba South
i. Chake Chake: Suleiman Sarhan SAIDii. chonga: Omar Khamis JUMA ii. Wawi: Hamad Abdallah RASHIDiii. ziwani: Mohamed Kombo JUMAiv. Mkoani: Abdallah Abbas OMAR v. Mkanyageni: Masoud M. ABDALLAHvi. Chambani: Bahati Khamis KOMBOvii. Mtambile: Mohamed Mgaza JECHAviii. Kiwani: Mussa Foum Mussa
Unguja South
i. Makunduchi: Haroun Ali SULEIMANii. Muyuni: Jaku Hashim AYOUBiii. Koani: Mussa ali HASSAN iv. Uzini: Mussa Khamis SILIMAv. Chwaka: Issa Haji USSI Gavu
Urban West
i. Mfenesini: Ali Abdallah ALIi. Mtoni: Khamis Jabir MAKAME ii. Kiembe Samaki: Mansoor Yussuf HIMIDIiii. Dole: Shawana Bukheti HASSAN iv. Magogoni: Asha Mohamed HILALIv. Bububu: Salum Amour MTONDOO vi. Dimani: Mwinyihaji M. MwWADINIvii. Mwanakwerekwe: Shamsi Vuai Nahodha viii. Fuoni: Thuwayba E. KISASIix. Chumbani: Machano Othman SAIDx. Kwahani: Ali Salum HAJIxi. Mpendae: Mohamed Said M. DIMWAxii. Mkongwe: Simai Mohamed SAIDxiii. Magomeni: Salmin Awadh SALMIN xiv. Kikwajuni: Mahmoud M. MUSSAxv. Kwamtipura: Hamza Hassan JUMA xvi. Amani: Fatma Mbarouk SAIDxvii. Rahaleo: Nassor Salum Alixviii. Jang'ombe: Suleiman Othman Nyanga
North Pemba
i. Konde: Ramadhan Omar AHMEDi. Mgogoni: Ismail Amour ISMAILii. Micheweni: Chumu Kombo KHAMISiii. Tumbe: Amour Khamis MBAROUKiv. Wete: Siasa Khamis MELEK v. Mtambwe: Mauwa Mbarouk SAIDvi. Kojani: Makame Said JUMAvii. Ole: Badria Ramadhan MOHAMEDviii. Gando: Suleiman Khamis MAKAME.

Monday, August 2, 2010

KIKWETE ACHUKUA FOMU ZA URAIS


Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete na mgombea mwenza Dr. Gharib Billal wakiinua fomu za uteuzi kwa wana CCM na wananchi waliofika kwenye ofisi ya Tume ya Uchaguzi jijini Dar es Salaam mara baada ya kuchukua fomu hizo jana.

Saturday, July 31, 2010

KURA YA MAONI ZANZIBAR


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume akipiga kura yake katika kituo cha kupigia kura cha skuli ya Kiembesamaki, ikiwa ni zoezi la kura ya maoni ya Uundwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.

Saturday, July 24, 2010

Kiongozi wa CCM tawi la Marekani akutana na Mh Rais Kikwete

Bi Zainab Janguo Katibu wa siasa na uenezi wa CCM tawi la Marekani akiwa katika picha na Mh Rais Jakaya Kikwete katika Ikulu ndogo ya Chamwino, Dodoma.

Friday, July 9, 2010

CCM has picked Dr Ali Mohamed Shein as the party's presidential candidate for Zanzibar.



THE National Executive Committee of Chama Cha Mapinduzi (CCM-NEC) Friday night overwhelmingly elected the Vice-President of the United Republic of Tanzania, Dr Ali Mohamed Shein, as the ruling party’s presidential candidate for Zanzibar. Dr Shein scooped 117 votes, beating by far the former Zanzibar Chief Minister, Dr Mohamed Gharib Bilal, who garnered 54 votes. The Chief Minister, Mr Shamsi Vuai Nahodha, managed 33 votes. The results culminated the hot race that involved 11 presidential nominees who were trimmed down to five before being pruned to three. Others in the list were the Deputy Chief Minister Ali Juma Shamuhuna, Zanzibar Education and Vocational Training Minister Haroun Ali Suleiman, prominent businessman Mohammed Raza Dharamshi, Chumbuni MP Omar Sheha Mussa and a civil servant, Mr Hamad Bakar Mshindo. The rest were Mr Mohamed Yussuf Mshamba, Ambassador Ali Karume and the Deputy Minister for East African Cooperation, Mr Mohamed Aboud Mohamed. Speaking shortly after the election, Dr Shein promised to strengthen the Union and promote unity and peace in the Isles. He also said that he would lead the country with wisdom, promising speedy development in Zanzibar in collaboration with President Jakaya Kikwete. Dr Shein thanked CCM members for electing him, saying all nominees had competence and merits to be flag bearers of the party in Zanzibar presidential race. He called for solidarity and unity among the party’s members to enable the party emerge with landslide victory in the forthcoming general elections in October. Dr Shein will be pitted in the Isles race against the Secretary General of the Civic United Front (CUF), Mr Seif Shariff Hamad. According to the CCM Publicity and Ideology Secretary John Chiligati, the party’s special congress, to be held today and tomorrow, is expected to endorse the name of President Jakaya Kikwete as the party’s presidential candidate for the presidency of the United Republic of Tanzania. Although Mr Kikwete, who is the incumbent president, has no opponent, the congress will still conduct a democratic vote. He also said that the running mate of the union presidential candidate is also going to be introduced to the party’s congress tomorrow evening. Mr Kikwete, who enjoys massive backing from the more than 2,000 ruling party delegates, is expected to get overwhelming support in the vote.


Source: DAILY NEWS in Dodoma

Thursday, July 8, 2010

Bi Zainab Janguo kuwakilisha CCM Marekani huko Dodoma

Katibu wa uenezi na siasa wa CCM tawi la Marekani Bi. Zainab Janguo ameondoka hapa nchini kuelekea mjini Dodoma kuhudhuria mkutano mkuu wa 9 wa CCM unaotarajiwa kuanza hapo Julai 10 na 11 mjini humo. Mwakilishi huyo wa CCM tawi la Marekani ameondoka hapa kufuatia mwaliko wa kuhudhuria mkutano huo katika barua iliyotumwa na kusainiwa na Katibu Mkuu wa CCM Mh. Yusuf R. Makamba.
Bi Janguo pia anatarajiwa kuanza ziara ya kimafunzo kwa vitendo katika idara mbalimbali za chama kwa muda wa wiki tatu baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu huo. CCM tawi la Marekani linamtakia mwakilishi wetu safari na uwakilishi mwema katika mkutano huo.

Monday, June 21, 2010


Mbio za urais zaanza, Kikwete wa kwanza

Jakaya Kikwete amechukua fomu ya kuwania kugombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa miaka mitano ijayo katika sherehe zilizopambwa na shamrashamra na vijembe vya Katibu Mkuu wa Chama hicho, Yusuf Makamba. Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, alikabidhiwa fomu yake saa 5.38 asubuhi makao makuu ya CCM mjini hapa na Msimamizi wa Uchaguzi wa CCM, Makamba aliyetabiri kuwa Mwenyekiti wake, anaweza kuwa mgombea pekee wa chama hicho. Makamba alisema kabla na baada ya kumkabidhi Rais Kikwete fomu kuwa anaweza kuwa mgombea pekee baada ya mwanachama mwingine aliyetangaza nia, Mbunge wa Maswa, John Shibuda, kujiondoa katika mchakato huo. “Hili ni tukio kubwa na ndiyo tumeanza safari ya kwenda Ikulu,” Makamba aliuambia mkusanyiko wa wana-CCM wakiwamo wabunge, mawaziri, wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM, wenyeviti wa mikoa na wananchi wengine. “Ipo dalili kuwa utakuwa peke yako, tutakutuma wewe, ipo dalili wengine hawatakuja,” alisema Makamba akimweleza Rais Kikwete kabla ya kueleza kuwa Shibuda alishaondoa nia yake na kutokana na hilo, mbunge huyo wa Maswa aliyekuwa kwenye shughuli ya jana, aliitwa mbele ya meza kuu na kupeana mkono na Rais Kikwete. Makamba hakuishia hapo kwa vijembe na kauli zake zilizosisimua uchukuaji huo wa fomu, kwani kabla ya Rais Kikwete kutoa hotuba yake, alitumia muda mwingi kujitetea katika rafu zilizoanza kuchezwa katika majimbo ya wabunge wa CCM, ambazo zililalamikiwa hivi karibuni katika kikao cha wabunge wa CCM kabla ya Bunge la Bajeti kuanza ambalo ni la mwisho kabla ya Uchaguzi Mkuu. Mtendaji huyo wa CCM licha ya kukiri kupokea malalamiko ya wabunge hao, lakini alisema si yeye wala Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara, Pius Msekwa au Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM anayewatia kiburi wanachama hao waliotangaza nia, hivyo taratibu za chama zitachukua mkondo wake na asilaumiwe yeye. “Chonde chonde akina Msekwa chukueni hatua…nami mwenzenu niokoeni, wapo waliotusaidia wameandika malalamiko, tuyafanyie kazi. Yapo kwa Msekwa, nimekupa (akimwambia Msekwa), wewe ni Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Maadili, yafanyie kazi. Mna haki ya kulalamika, kwani mkomamanga wenye makomamanga ndio unaopigwa mawe,” alisema Makamba. Lakini aliwataka wanaolalamika, wamtendee haki kwa sababu naye ni binadamu. “Ni vizuri mkayasema haya tarehe 23 (kesho) wakati wa kikao cha NEC, pale ndipo mahali pake, Mwenyekiti atakuwapo, kule (bungeni) hapana. Nami nikiulizwa, nitasema, Msekwa usikasirike,” aliongeza Makamba na kuwafanya waliohudhuria kuangua vicheko. Pia aliomba apewe nafasi ya kuzungumza katika Mkutano Mkuu wa CCM mwezi ujao kwa kumkaribisha Mwenyekiti, kwani ana ya kuzungumza kwa sababu ratiba iliyopangwa sasa, imemwengua. Rais amekubali awekwe, ndio utaratibu. Mara baada ya Makamba kumaliza kuzungumza, alimpa nafasi Rais Kikwete aliyezitaja sababu zilizomfanya awanie tena nafasi hiyo kuwa ni ushawishi wa Watanzania wengi; kufanya vizuri kwa Serikali yake katika miaka mitano iliyopita na Katiba kumruhusu kuwania tena urais. “Ushawishi wa Watanzania wengi, wana-CCM na wasiokuwa wana-CCM, wanawake kwa wanaume, vijana kwa wazee wa mikoa yote na wilaya zetu zote kwa kunitaka nigombee tena. “Pili, nimeridhika kwamba katika miaka mitano hii, pamoja na kukabiliana na changamoto nyingi, Serikali chini ya uongozi wangu imefanya kazi nzuri ya kusukuma maendeleo ya Taifa letu na kuimarisha umoja, amani na utulivu katika nchi yetu. “Na tatu, Katiba inaniruhusu, kwani naweza kuwa Rais kwa vipindi viwili mfululizo. Nimemaliza kimoja, hivyo naweza kuomba kupata kipindi kingine cha pili,” alisema Rais Kikwete ambaye kabla ya hotuba yake, kadi yake ilihakikiwa na Makamba kuona kama ni mwanachama hai na kisha akalipa papo hapo Sh milioni moja za kuchukulia fomu na hatimaye kukabidhiwa. Rais Kikwete alisema mwaka 2005 walimpa ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM na sasa anaiomba tena na kuahidi kuwa akiteuliwa, atafanya hivyo kwa dhati na hasa kama wana-CCM wakishikamana kama 2005, watapata ushindi mkubwa au kuzidi huo. Alisema Watanzania na wana-CCM ni mashahidi kwa kiasi gani amekuwa mwaminifu kwa ahadi ya kutekeleza mipango na programu mbalimbali za utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, aliyosema imetekelezwa kwa umakini mkubwa na matokeo yake yanaonekana pembe zote. Aliueleza mkusanyiko huo, kwamba amefarijika kuona kwamba wao, pamoja na wana-CCM wenzake wengine nchini, wanamwamini kwamba anafaa kuendelea kuliongoza Taifa kwa kipindi kingine cha miaka mitano. “Hayo yote ndiyo yaliyonishawishi nami kushawishika kujitokeza kuomba tena kupewa nafasi ya kuliongoza Taifa letu. Safari ile nilisema mkinichagua nitafanya kazi kwa Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya na matokeo yake tumeyaona. “Safari hii nasema mkinichagua nitawatumikia Watanzania kwa Ari Zaidi, Nguvu Zaidi na Kasi Zaidi katika dhamira yetu ya kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania. Kwa pamoja, tuzidi kusonga mbele,” alisema Rais Kikwete na kushangiliwa na watu waliokuwapo. Aliahidi kuwa akipewa nafasi ya kuwa mgombea wa CCM Oktoba mwaka huu, hatawaangusha na atatumia bidii yake yote kufanya kampeni ya kukipigania chama hicho tawala ili kipate ushindi mkubwa. Awali, kabla ya shughuli ya kukabidhi fomu kwa mgombea huyo, Makamba alisema dalili za kuomba dua ya kuwa Rais Kikwete awe mgombea pekee zilizotolewa na watu kadhaa akiwamo aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pancras Ndejembi, zimesikika. Mbali na Ndejembi, shughuli hiyo ya kuchukua fomu ilihudhuriwa pia na wazee wengine wa CCM wakiwamo Peter Kisumo, Balozi Job Lusinde na Isaac Mwisongo. Wabunge John Malecela (Mtera) ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa zamani wa CCM, Dk. Abdallah Kigoda (Handeni) na Waziri Profesa Mark Mwandosya (Rungwe Mashariki) ambao pia waliwania urais 2005, ni miongoni mwa waliokuwapo jana. Familia ya Rais Kikwete ikiongozwa na mkewe Mama Salma Kikwete na wanawe saba, wavulana wanne wakiongozwa na kaka yao, Ridhiwani Kikwete na wasichana watatu, pia walimsindikiza baba yao, kama ilivyokuwa kwa kaka yake Kikwete, Suleiman Kikwete ambaye aliongozana na mkewe, kushuhudia mwanzo wa safari ya mpendwa wao kuomba ridhaa ya kuendelea kuongoza nchi.

Sunday, June 13, 2010

Makamba warns unfaithful CCM members

CCM Secretary General Yusuph Makamba this week warned fellow members including district and regional leaders reportedly engaging in illegal distribution of membership cards, conducting underground campaigns, saying that they would be sanctioned.
“Our party’s manifesto, regulations and policy stress the need for solidarity, transparency… this is what all officials irrespective of their positions in the party should stand for,” Makamba said.
Speaking in Moshi he said such leaders could be expelled from the party, pointing out that he has received complaints, calling for solidarity and team work in strengthening the party from the grassroots level.
The Secretary General said: “Measures will be taken against those are out to tarnish the good reputation that CCM has been proud of for years.”
Makamba distributed CCM membership cards to some 152 new members who have joined the party from various parts of Kilimanjaro Region.
According to the party’s National Executive Committee( NEC) , members wishing to cast votes during the nomination process must possess the voter’s card provided by the National Electoral Commission (NEC).
The party organ said only active CCM members, implying those who have paid membership fees will be allowed to participate in the opinion poll in search for CCM candidates for elective posts during the general elections in October.
According to NEC, CCM members will cast votes to decide on their candidates on August 8 in all its branches. The ruling party has close to five million members.
The conditions have been set to enable all party members exercise their democratic right of participating in the nomination process but responsibly.

Monday, June 7, 2010

TAARIFA MAALUM YA KUSIMAMISHWA UONGOZI BW. MICHAEL NDEJEMBI




Ndugu Wanachama


Kwa niaba ya uongozi wa CCM tawi la Marekani, ninapenda kutoa taarifa kwenu kama ifuatavyo.


Siku ya tarehe 26 mei 2010 uongozi wa Chama Cha Mapinduzi Tawi la Marekani ulitoa tamko rasmi juu ya taarifa za kuitishwa kwa uchaguzi wa tawi letu hapa Marekani. Taarifa hiyo ilieleza wazi kuwa uchaguzi huo ni batili na haukutokana na maamuzi rasmi ya vikao halali vya uongozi wa tawi. Aidha, maamuzi hayo yalikua ni maamuzi ya mwenyekiti mwenyewe na hayakutokana na kikao chochote. Hata hivyo uongozi wenu wa tawi ulichukua hatua za kuwasiriana na mwenyekiti ili atoe ufafanuzi juu ya ukiukwaji wa katiba na utaratibu mzima wa uendeshaji wa tawi, kwa bahati mbaya sana mwenyekiti hakutoa ushirikiano kama ambavyo ulitarajiwa na badala yake alifanaya 'uchaguzi' wake kwa matakwa na maslahi yake yeye mwenyewe anayoyafahamu.
Kwa kuzingatia kuwa Chama Cha Mapinduzi ni taasisi na si mali ya mtu binafsi, uongozi wenu wa tawi ulikutana na kuchukua hatua kadhaa ikiwemo ya kumsimamisha uongozi Bw. Michael Ndejembi kabla hajafanya 'uchaguzi' wake na kumpa nafasi ya kujieleza dhidi ya vitendo alivyofanya.


Ndugu wanchama, taarifa hii inakazia maamuzi ya CCM tawi la Marekani ya kutoutambua 'uchaguzi' ule na hata matokeo yake. Pia tawi linawaomba radhi wanachama na wapenzi wake kwa usumbufu wowote uliojitokeza juu ya kuitishwa 'uchaguzi' huo.


Tawi lenu lipo katika mchakato wa kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi hapa Marekani ili kifikie malengo haya yafuatayo:


Kuliondoa tawi katika mtazamo wa sura ya kuwa ni mali ya mtu mmoja na kulifikisha mahali ambapo litakua ni tegemeo kubwa katika kutoa mchango wa maendeleo ya kisiasa Tanzania.


1). Kuimarisha tawi kwa kuongeza idadi ya wanachama wapya wa CCM.

2). Kueneza siasa ya Chama Cha Mapinduzi kwa wanachama na wapenzi wake.

3). Kipindi hiki kitasaidia kutoa elimu ya kutosha kwa wanachama wapya na wazamani kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo kujitayarisha kugombea nafasi za uongozi.

4). Ku-restructure kamati ya uongozi wa tawi iliyopo sasa hivi ijulikane kama 'kamati ya muda ya CCM tawi la Marekani' na kuipa ukomo usiozidi miezi 24.

5). Kuandaa uchaguzi wa viongozi wa Tawi la CCM Marekani ndani ya miezi 24 kuanzia Julai 1 mwaka huu. Hii itasaidia kutoa fursa sawa kwa wanachama mbalimbaliwaweze kushiriki siasa hata wakiwa nje ya Tanzania wanapata nafasi hiyo kwa uwazi na usawa bila ya mizengwe.


Kidumu Chama Chama Mapinduzi.

Zainab Janguo


Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi.



Sunday, June 6, 2010

MH. RAIS KIKWETE AMTEMBELEA JENERAL MSTAAFU.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya M.Kikwete jana alimtembelea mkuu wa majeshi na Jeneral mstaafu E. Mwita Kiaro aliyelazwa katika hospital ya Bugando Jijini jana. Mh rais yuko katika ziara ya siku mbili jijini humo kukagua shughuli mbali mbali za maendeleo.
Mh. Kikwete akimsikiliza Jeneral Kiaro

KARUME AFUNGUA MKUTANO WA ZNCCIA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume, akifungua Mkutano Mkuu wa mwaka Zanzibar National Chamber of Commerce Industries and Agriculture (ZNCCIA) katika Ukumbi wa Salama Hotel Bwawani, ambapo mkutano huo utakuwa na Uchaguzi wa kumpata Rais mpya wa Jumuiya hiyo. Kulia ni Rais wa Jumuiya hiyo anayemaliza muda wake, Abdallah Abass na (kushoto) ni Waziri wa Biashara,Uwekezaji na Utalii, Mh. Samia Suluhu Hassan.
Picha na Ramadhan Othman wa Ikulu, Zanzibar.

Saturday, June 5, 2010

MWAKILISHI WA ADB NA KIKWETE IKULU

Mwakilishi wa benk ya maendeleo ya Afrika Dr.Sipho Moyo amekutana na rais Kikwete leo Ikulu Jijini Dar es salaam kwa lengo la kumuaga. Dr. Sipho Moyo amemaliza muda wake wa kufanya kazi kama mwakilishi wa benk hiyo nchini Tanzania.

Monday, April 26, 2010

MAADHIMISHO YA MIAKA 46 YA MUUNGANO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akipungia mkono wananchi mbalimbali waliojitokeza kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika leo kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam ambapo wakazi mbalimbali walijitokeza katika sherehe hizo, kulia ni mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange.
Viongozi wa vyama mbalimbali pamoja na maafisa kutoka serikalini nao walikuwepo katika maadhimisho hayo.
Wageni waalikwa mbalimbali na mabalozi wakifuatilia kwa karibu kila kilichokuwa kikendelea kwenye uwanja wa Uhuru leo jijini Dar es salaam.
Wanafunzi wa shule mbalimbali jijini Dar es salaam wakicheza halaiki wakati wa maadhimisho ya miaka 46 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika leo kwenye uwanja wa Uhuru leo.

Msomaji
Dar es salaam

Saturday, April 24, 2010

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AFUNGUA KONGAMANO LA MAKATIBU MUHTASI DODOMA LEO

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi Makatibu Muhtasi kabla ya kufungua Kongamano lao kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango Mjini Dodoma, Aprili 24, 2010 Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Celina Kombani.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akihutubia wakati alipofungua kongamano la Makatibu Muhtasi kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango Mjini DOdoma
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja baada ya kufungua Kongamano la Makatibu Muhtasi kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango Mjini Dodoma Aprili 24, 2010. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Celina Kombani, na Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ndugu Maswi.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja baada ya kufungua Kongamano la Makatibu Muhtasi kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango Mjini Dodoma Aprili 24, 2010. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Celina Kombani.

Msomaji
Dar es salaam

Friday, April 23, 2010

Matukio Bungeni Dodoma Leo

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Kulia akizungumza na Mbunge wa Kwela mkoani Rukwa Christant Mzindakaya leo katika vikao vya Bungeni vinavyoendelea mjini Dodoma.
Kiongozi wa Upinzani Bungeni (kushoto) Hamad Rashid akiongea na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa Bernald Membe ambaye pia ni mbunge wa jimbo la (Mtama) na Basil Mramba Mbunge wa jimbo la (Rombo).
Mbunge wa Kinondoni (kushoto) Idd Azzan akibadilishana mawazo na mbunge wa viti maalum kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Halima Mdee .

Msomaji
Dodoma

Viongozi wa Tanzania na Msumbiji wakagua maadalizi ya uzinduzi wa daraja la umoja

Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Omari Chambo akiwa ameongozana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi za Jamii na Maendeleo ya Makazi wa Msumbiji Bi. Maria Luisa Mathe(mwenye shati jeupe) na Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu Bi. Fatma Salum Ally wakielekea sehemu ya juu ya Daraja la Umoja kukagua maandalizi ya sherehe za Uzinduzi wa Daraja hilo tarehe 12 mwezi ujao jana katika eneo la Mtambaswala wilayani Nanyumbu mpakani mwa Tanzania na Msumbiji
Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Omari Chambo (katikati) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi za Jamii na Maendeleo ya Makazi wa Msumbiji (Mwenye shati jeupe) Bi. Maria Luisa Mathe na Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu Bi. Fatma Salum Ally(kushoto) wakikagua Daraja la Umoja eneo la Mtambaswala mpakani mwa Tanzania na Msumbiji katika maandalizi ya sherehe za Uzinduzi wa Daraja hilo mwezi ujao.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Omari Chambo akiwaongoza viongozi mbalimbali kutoka wilayani Nanyumbu na Msumbiji kukagua maandalizi ya sherehe za uzinduzi wa daraja hilo katika eneo la chini ya Daraja la Umoja lililojengwa kwa Ushirikiano kati ya Tanzania na Msumbiji katika eneo la Mtambaswala wilayani Nanyumbu jana.

Msomaji
Nanyumbu

Thursday, April 22, 2010

WANAVYUO DODOMA WAJIUNGA NA JUMUIYA YA WAZAZI YA CCM

Mwenyekiti wa Jumuia ya wazazi nchini balozi Athmani Mhina akimkaribisha makamu wa Rais Dk Ali Mohamed shein katika ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma ambapo Dk Shein alifungua mkutano Mkuu maalum wa Jumuia ya wazazi leo.
Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano mkuu maalum wa baraza la jumuia ya wazazi mjini Dodoma leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuia ya wazazi balozi Athumani Mhina na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuia hiyo Dogo Idd Mbarouk.
Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano mkuu maalum wa baraza la jumuia ya wazazi mjini Dodoma leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuia ya wazazi balozi Athumani Mhina na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuia hiyo Dogo Idd Mbarouk.

Msomaji
Dodoma

Matukio Bungeni Dodoma Leo

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mwantumu Mahiza (mwenyemiwani) akiwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) leo wakati wanafunzi hao walipokwenda kuangalia maeneo mbalimbali ya shughuli za Bunge mjini Dodoma leo. Mwenyekiti wa Kamati za Mahesabu za Mashirika ya Umma Zitto Kabwe leo Bungeni akitoa taarifa ya Kamati za Hesabu za Mashirika ya Umma pamoja na mapendekezo na maoni yaliyomo kwenye taarifa . Picha na Mwanakombo Jumaa.
Mbunge wa Mtera Johhn Malecela Akichangia sheria ya Malisho na vyakula vya mifugo
Mbunge wa Monduli Edward Lowassa (kulia) akimsikiliza Mbunge wa Kiteto Benedict Nangoro (kushoto) leo ndani ya Ukumbi wa Bunge -Dodoma. Picha na Mwanakombo Jumaa
waziri wa Madini na Nishati William Ngeleja (kulia) na Naibu Waziri wa Madini na Nishati Adam Malima wakizungumza leo katika viwanja vya Bunge Dodoma baada ya Waziri Ngeleja kuwasilisha Muswada wa Sheria ya Madini wa Mwaka 2010.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza Wa Rais (Muungano) Muhammed Seif Khatib (kushoto) akizungumza na waandishi wa Habari Dododma leo kuhusu mambo mbalimbali ya Muungano. Mwengine ni Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano.
Msomaji
Dodoma