Monday, June 7, 2010

TAARIFA MAALUM YA KUSIMAMISHWA UONGOZI BW. MICHAEL NDEJEMBI




Ndugu Wanachama


Kwa niaba ya uongozi wa CCM tawi la Marekani, ninapenda kutoa taarifa kwenu kama ifuatavyo.


Siku ya tarehe 26 mei 2010 uongozi wa Chama Cha Mapinduzi Tawi la Marekani ulitoa tamko rasmi juu ya taarifa za kuitishwa kwa uchaguzi wa tawi letu hapa Marekani. Taarifa hiyo ilieleza wazi kuwa uchaguzi huo ni batili na haukutokana na maamuzi rasmi ya vikao halali vya uongozi wa tawi. Aidha, maamuzi hayo yalikua ni maamuzi ya mwenyekiti mwenyewe na hayakutokana na kikao chochote. Hata hivyo uongozi wenu wa tawi ulichukua hatua za kuwasiriana na mwenyekiti ili atoe ufafanuzi juu ya ukiukwaji wa katiba na utaratibu mzima wa uendeshaji wa tawi, kwa bahati mbaya sana mwenyekiti hakutoa ushirikiano kama ambavyo ulitarajiwa na badala yake alifanaya 'uchaguzi' wake kwa matakwa na maslahi yake yeye mwenyewe anayoyafahamu.
Kwa kuzingatia kuwa Chama Cha Mapinduzi ni taasisi na si mali ya mtu binafsi, uongozi wenu wa tawi ulikutana na kuchukua hatua kadhaa ikiwemo ya kumsimamisha uongozi Bw. Michael Ndejembi kabla hajafanya 'uchaguzi' wake na kumpa nafasi ya kujieleza dhidi ya vitendo alivyofanya.


Ndugu wanchama, taarifa hii inakazia maamuzi ya CCM tawi la Marekani ya kutoutambua 'uchaguzi' ule na hata matokeo yake. Pia tawi linawaomba radhi wanachama na wapenzi wake kwa usumbufu wowote uliojitokeza juu ya kuitishwa 'uchaguzi' huo.


Tawi lenu lipo katika mchakato wa kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi hapa Marekani ili kifikie malengo haya yafuatayo:


Kuliondoa tawi katika mtazamo wa sura ya kuwa ni mali ya mtu mmoja na kulifikisha mahali ambapo litakua ni tegemeo kubwa katika kutoa mchango wa maendeleo ya kisiasa Tanzania.


1). Kuimarisha tawi kwa kuongeza idadi ya wanachama wapya wa CCM.

2). Kueneza siasa ya Chama Cha Mapinduzi kwa wanachama na wapenzi wake.

3). Kipindi hiki kitasaidia kutoa elimu ya kutosha kwa wanachama wapya na wazamani kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo kujitayarisha kugombea nafasi za uongozi.

4). Ku-restructure kamati ya uongozi wa tawi iliyopo sasa hivi ijulikane kama 'kamati ya muda ya CCM tawi la Marekani' na kuipa ukomo usiozidi miezi 24.

5). Kuandaa uchaguzi wa viongozi wa Tawi la CCM Marekani ndani ya miezi 24 kuanzia Julai 1 mwaka huu. Hii itasaidia kutoa fursa sawa kwa wanachama mbalimbaliwaweze kushiriki siasa hata wakiwa nje ya Tanzania wanapata nafasi hiyo kwa uwazi na usawa bila ya mizengwe.


Kidumu Chama Chama Mapinduzi.

Zainab Janguo


Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi.



No comments: