Monday, July 13, 2009

Waziri wa mambo ya nchi za nje Mh. Bernard K. Membe Kumwakilisha Rais Jakaya Kikwete Kwenye Mkutano wa NAM,Misri..

Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM) unatarajiwa kufanyika Sharm El Sheikh,Misri tarehe 15 hadi 16 Julai, 2009.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mhe. Bernard K.Membe atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete katika mkutano huo.

Mkutano huo utatanguliwa na mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za NAM unaofanyika tarehe 13 na 14 Julai,2009.Maudhui ya mkutano huo ni pamoja na Mtikisiko wa Kiuchumi Duniani;Mageuzi katika Vyombo vya Fedha Duniani; Mageuzi katika Umoja wa Mataifa na Migogoro ya Kisiasa Duniani.

Aidha, mkutano huo unategemewa kupitisha maazimio mbalimbali yaliyopendekezwa na mkutano wa Mawaziri huko Tehran, Iran mwaka 2008 na ule wa Havana,Cuba mwezi Mei, 2009.Mhe.Waziri Membe ataambatana na Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, Mhe. Dkt.Augustine Mahiga Na Balozi wa Tanzania nchini Misri,Mhe.Ali Shauri Haji.

IMETOLEWA NA:
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO
WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM

No comments: