Sunday, July 19, 2009

RAIS JAKAYA KIKWETE AMEMTEUA MSAIDIZI WAKE KATIKA DIPLOMASIA

Rais Jakaya Kikwete amemteua, Zahra Mwanasharif Nuru, kuwa Msaidizi wa Rais wa masuala ya diplomasia. Taarifa iliyotolewa alhamisi wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, na Katibu Mkuu, Ikulu, Michael Mwanda, kwa niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi, ilisema kuwa uteuzi huo ulianzia juzi (Jumanne).

Taarifa hiyo ilisema kuwa Zahra Nuru anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Andrew Daraja ambaye alihitimisha mkataba wake wa utumishi wa umma.

Ilisema Zahra Nuru amepata kuajiriwa na Umoja wa Mataifa. Kabla ya kuhitimisha mkataba wake na Umoja wa Mataifa, Zahra Nuru alikuwa mtaalam na Mshauri Mwandamizi wa Katibu Mkuu Msaidizi na Mshauri Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Afrika.

Msomaji
Dar es salaam

5 comments:

Anonymous said...

sawa bwana mpeni pongezi

Anonymous said...

aaalah! kumbe hakuwa na msaidizi? so nani alikuwa akifanya kazi hiyo before? ccm nijibuni.

Anonymous said...

nyinyi mnamatatizo gani, mbona hamtoi maoni yetu?

Anonymous said...

Nampongeza mama Zahra Nuru kuchaguliwa kuwa msaidizi wa Raisi kwa masuala ya Diplomasia. Anastahili. Ni mchapakazi na mtu mwenye msimamo. Nilimfahamu tangu akiwa kama Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Watoto. Kwa nini usigombee ubunge kama rafiki yako Mama Fatma Said Ally? Unamkumbuka ee! Hongera sana.

Anonymous said...

Jk kaza buti tutafika