Friday, July 24, 2009

MAREKANI YASEMA IKO TAYARI KUIUNGA MKONO GEORGIA

Makamu wa kwanza wa rais wa Marekani bwana Joe Biden amesema kwamba nchi yake iko tayari kuiunga mkono Georgia katika vita yake na Urusi. Biden ametoa kauli hiyo akiwa mjini Tbilisi ambao ni mji wa Georgia, Urusi na Georgia zimekuwa na mapigano na malumbano kwa muda mrefu sasa hali inayosababisha kupotea kwa amani katika eneo hilo. Marekani ilikwisha iagiza serikali ya Urusi kuondoa majeshi yake katika eneo la mapigano lakini Urusi ilipuuza na kwamba bado majeshi ya nchi hiyo yapo katika maeneo ya Abkhazia na Ossetia ambayo ni maeneo ya Georgia.

Msomaji
Rusia



1 comment:

Anonymous said...

hawa jamaa ni wanafiki sana, juzi tu rais obama alikuwa na rais wa rusia mama nani sijui pale white house na wamekubaliana kusaidiana leo biden yuko huko georgea anawaambia eti marekani itawaunga mkono huu si unafiki jamani.

anthony
london