Tuesday, August 4, 2009

UNHCR YAKABIDHI MAGARI NA PIKIPIKI KWA WIZARA YA MAMBO YA NDANI

Mwakilishi wa shirika linaloshughulikia wakimbizi nchini Tanzania UNHCR Bw. Yakoub El Hillo akikata utepe kama ishara ya makabidhiano ya magari na pikipiki kwa jeshi la polisi nchini ili kusaidia kupambana na uhalifu, wanaoshuhudia kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Rawlence Masha, kushoto ni Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Said Mwema na katikati ni Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya Jinai, DCI Robelt Manumba, makabidhiano hayo yamefanyika katika Makao makuu ya Wizara ya Mambo ya ndani ambapo UNHCR imekabidhi magari aina ya Toyota Prado 2 Toyota Hardtop 6 na pikipiki 10 vyote vikiwa na thamani ya Dola za kimarekani 241.000
Baadhi ya Magari na pikipiki yakiwa yameegeshwa katika Wizara ya mambo ya ndani leo Magari hayo yametolewa na Yakoub El Hillo Mwakilishi mkazi wa shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia wakimbizi nchini UNHCR kama msaada kwa Jeshi la Polisi nchini katika kupambana na uhalifu mbalimbali.


Msomaji
Dar es salaam

No comments: