Tuesday, August 4, 2009

Rais Kikwete azindua ujenzi wa barabara ya Singida-Minjingu

Rais Kikwete azindua ujenzi wa barabara ya Singida-Minjingu
Zaidi ya Sh. bilioni 210 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa barabara ya Singida hadi Minjingu mkoani Manyara yenye urefu wa kilomita 224 kwa kiwango cha lami.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Omari Chambo, aliwaambia waandishi wa habari kuwa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi huo litawekwa na Rais Jakaya Kikwete.
Alisema ujenzi wa barabara hiyo umegawanywa katika awamu tatu. Awamu ya kwanza ya Singida- Katesh ina urefu wa kilomita 65, Katesh- Dareda kilomita 74 na Dareda Minjingu kilomita 85.
Alisema kuwa ujenzi huo wa barabara ya lami unagharamiwa na serikali kuu kwa mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya maendeleo ya Afrika (ADB). Ujenzi huo utakamilika ndani ya miezi 33.
Aidha, Chambo amewataka makandarasi waliopewa zabuni ya ujenzi wa barabara hiyo kuzingatia masharti yote muhimu yaliyomo kwenye mkataba ikiwemo kumaliza kazi kwa wakati.
Rais Kikwete alitarajiwa kuwasili hapa jana jioni kwa ziara ya siku tatu ambapo atazindua miradi mbalimbali ya mendeleo ikiwemo kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara hiyo.

Msomaji
Singida


2 comments:

Anonymous said...

Barara zote za nchi yetu inabidi zifanyiwe uzinduzi wa ujenzi mpya. Sijaona barabara hata moja iliyojengeka katika viwango vya kimataifa. Tatizo nisababu ya 10% inayotakiwa na waizinishaji wa mikataba

Simeon Sungi said...

Hongera Mh. Rais. Tukitaka kuinua uchumi wa nchi yetu, infrastructure, ikiwemo barabara ni jambo la muhimu sana. Rais Franklin Delano Roosevelt (FDR) asingefanya mapinduzi ya barabara Marekani, nchi hii isingekuwa na maendeleo kama iliyonayo sasa. FDR aliamini kwamba miundo mbinu, ikiwemo barabara itakuza uchumi (Roosevelt believed that improving the public infrastructure would put more money into the economy).