Tuesday, August 11, 2009

SERIKALI YATOA UFAFANUZI WA UUZAJI WA MAGOGO NJE YA NCHI

Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki Wizara ya Maliasili na Utalii ndugu Ernest Kilahama
Serikali imewataka wafanyabishara wa mazao ya misitu kuwekeza hapa nchini kwa kujenga viwanda vitakavyosaidia kukuza ajira na kuongeza pato la taifa badala ya kukimbilia kuuza mazao ya misitu hususan magogo nje ya nchi kinyume cha sheria. Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Felician Kilahama wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoa ufafanuzi kuhusu madai ya usafirishaji wa magogo nje ya nchi.
Dk. Kilahama amesema sheria Misitu ya Tanzania Namba 14 ya mwaka 2002 ambayo ilianza kutumika rasmi Julai 2004 inazuia na kupiga marufuku uuzaji na biashara ya aina yoyote ya magogo nje ya nchi.“Sheria yetu ya mwaka 2002 iliyoanza kutumika Julai 2004 hairuhusu kwa namna yoyote kufanyika kwa biashara ya magogo nje ya nci na anayeuza magogo na rasilimali za misitu nje ya nchi ni mwizi, rasilimali ya misitu imehifadhiwa kisheria na ipo kwa ajili ya watanzania” Amesema.
Tanga kwenda Morogoro bali tunazuia wale wasiolipia ushuru na kukiuka masharti na leseni za biashara” Aliendelea kufafanua Dkt. Kilahama. Akitoa taarifa za baadhi ya matukio ya uharibifu wa misitu hapa nchini Dk. Kilahama amesema bado kuna wananchi ambao wanaendelea kufanya biashara ya magogo kinyume cha sheria akiitaja baadhi ya mikoa hapa nchini kama Rukwa, Kigoma ,Ruvuma, Tabora na Pwani kuwa wananchi walio wengi hawana uelewa wa kutosha wa utunzaji wa misitu.
Msomaji
Dar es salaam

No comments: