MABADILIKO ya muundo mpya wa Wizara ya Miundombinu, umewaweka kando vigogo wawili wa wizara hiyo kutoka katika nafasi walizokuwa wakishikilia.
Wiki hii Rais Jakaya Kikwete, aliidhinisha mabadiliko ya muundo wa Wizara ya Miundombinu, ikiwemo kuanzishwa Idara mpya ya Miundombinu ya Usafiri inayojumuisha usimamizi wa Reli na Bandari.
Kwa mujibu wa muundo huo mpya, aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchukuzi, Dk Bathlomew Rufunjo, ameondolewa katika nafasi hiyo.
Idara hiyo sasa inaitwa ya Huduma za Uchukuzi ambayo inaongozwa na Dk William Nshama, ambaye alikuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Msemaji Mkuu wa Wizara hiyo Patrick Ntemo, alipoulizwa jana, alisema mabadiliko tayari yalizungumzwa na Katibu Mkuu, Mhandisi Omari Chambo , hivyo hana la kusema.
Hata hivyo, duru nyingine za habari ziliweka bayana kwamba, Dk Rufunjo huenda akapangiwa kazi nyingine.
Katika muundo huo, Elius Mwakalinga ambaye alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Nyumba, naye anasubiri ama kupangiwa kazi nyingine.
Akitangaza muundo huo, Katibu Mkuu Mhandisi Chambo, alisema Idara ya Huduma za Ufundi na Umeme itakuwa na sehemu za Ufundi na Umeme na Majengo ya umma.
Idhini hiyo ya rais imekuja katika kipindi ambacho wizara hiyo imekuwa ikiweka mipango ya kupatia ufumbuzi matatizo makuu ikiwemo ya Shirika la Reli (TRL), Bandari na usimamizi wa majengo ya serikali.
Katibu Mkuu Chambo, alifafanua kwamba, lengo la muundo huo ni kuongeza tija na ufanisi katika utendaji kazi wa wizara.
Msomaji
Dar es salaam
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment