Friday, January 16, 2009

Ndege mali ya shirika la ndege la US Air ways flight 1549 imeanguka dakika tatu tu toka ilipokuwa ikipaa ikitokea La Gardian kuelekea North Carolina jana. Ndege hiyo ilyoangukia Hudson River New york city ilikuwa na abiria takribani 148 ambao wote wameokolewa na hakuna aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa.

10 comments:

Anonymous said...

tanzania inapaswa kuiga mfano wa marekani, ajari kuwa kama hii iawezekanaje isipoteze japo mtu mmoja? wala kujeruhi? kuna umuhimu mkubwa wa sisi watanzania kujifunza katika kuwajibika.

iddy
new york city

Anonymous said...

eeh? poleni jamani ingawa hamjapoteza mtu katika hiyo ajari.

Anonymous said...

hivi kweli hawa jamaa inawezekana vipi wakafanikiwa kwa kiwango hiki wakati tanzania bado ajari za bara barani zinatusumbua, jamani lazima tujifunze kwa wanaojua kikwete waambie mawaziri wajifunze kazi siyo majungu na kujiona kama miungu watu.

hamza
tumaini university
iringa

Anonymous said...

uwezo wa kukabiliana na majanga kama haya upo lakini serikali bado ni tatizo hasa upande wa mawaziri, unajua bwana ndejembi, mawaziri ndi watendaji kwa hiyo lazima wajue ni kwanini wamepewa hizo nafasi kisha wajue namna wanavyoweza kutimiza hizo kazi na ikiwa wanamatatizo lazima wayaseme mapema ili wapatiwe misaada. ona ajari za barabarani ni kama zimeumbwa kwa ajili yetu, inakela sana

james,
rome
italy

Anonymous said...

waelimishwe watendaji wote wa serikali juu ya majukumu yao sio wanapewa kwa kuwa ni watoto wa vigogo ndio maana wanashindwa kufanya kazi, na wenye moyo wanakosa motisha kwani hao watoto wa vigogo sio tu kwamba hawajui kazi bali pia ni wavivu na hawana nidhani ya kazi kwani hawana wanachokiogopa na hivyo kuwavunja moyo wenye moyo wa kuwajibika.

steve
DC
usa

Anonymous said...

Mnakumbuka ajari ya MV Bukoba. watu zaidi ya helfu moja walipoteza maisha yao. Hakuna hata mtu mmoja aliyeokolewa.

Hapa ndio unagundua kuwa tupo ulimwengu wa tatu.

Masanja
Mwanza

Anonymous said...

hivi viongozi wetu wanaona wenzao wanavyofanya au wao ni kufikiria 10%. tunataka viongozi wetu waone na kujifunza hawa wenzetu wanavyofanya. nawapongeza ccm usa.

dada rose
australia

Anonymous said...

asante baba ndejembi, naona jitihada zako lazima waone eidha kwa maandishi au kwa picha, wasipoelewa tuta find other altenative.

kipingu
dar es salaam

Anonymous said...

ccm oyeeeeeeee! nimependa saaaana shughuli zenu wa ccm marekani

johnson
nigeria

Anonymous said...

naomba kujua huyu ndejembi michael ni yule aliyekuwa akisoma cbe dar es salaam? maana kuna jamaa namfahamu alikuwa pale cbe anaitwa michael ndejembi.

suzana mangembe

russia.