Thursday, January 8, 2009

MAMA SOPHIA SIMBA ASHINDA!

Mwenyekiti wa kamati kuu ya CCM Bw. Seif Khatibu amemtangaza mama Sophia Simba kuwa mwenyekiti mpya wa umoja wa wanawake Tanzania (UWT), Sophia pichani aliinuka kwa furaha kama inavyoonekana ktk picha mara tu matokea yalipotangazwa na yeye kuibuka mshindi.
Mama Sophia Simba alimshinda mpinzani wake kwa kura 470 ambazo nisawa na asilimia 54.5 wakati Janet Kahama alipata kula 383 ambazo ni sawa na asilimia 48.4. Nae Joyce Masunga alipata kula 10 ambazo ni sawa na asilimia 1.1

Ndejembi Michael.

6 comments:

Anonymous said...

nampongeza mama huyu kwa ushindi lakini kwanini anajilimbikizia madaraka kwani hakuna watu wengine wa kuongoza hiyo jumuia?
tuna matatizo ya ajira na hawa watu wanajua ndio maana tunawapa uongozi sasa badala ya kuvigawanya vijinafasi vichache vilivyopo wao wanajikusanyia wao na sina uhakika kama hawa viogozi wanalipa kodi ya maendeleo. JK tunaomba uwakague hawa watu

Jonson
Jerusalem,
Israel.

Anonymous said...

bwana na ndejembi naomba kwanza nikushukuru kwa mtandao huu, tutautumia kuishauri ccm kujirudi pale inapobidi.
mimi nataka kumpongeza kikwete sio huyu mama kwanza ni kwa kuwa kikwete amejitoa kwa ajili ya watanzani amefanya hivyo akitambua kwamba watanzania walishajitoa kwake ndio maana wakamchangua.
sasa namuomba asimame katika hilo kwa manufaa ya taifa na naaminiatakuwa salama hata mbele za mwenyezi MUNGU.

majaliwa
washington
United state of america

Anonymous said...

hongea mama simba!

jay jay
Dar es salaam university

Anonymous said...

ccm imedhihilisha democrasia kwa mara nyingine, ni uchaguzi wa haki na kweli hili ni funzo kwa vyama vingine kuiga.
ccm marekani dumisheni mtandao wetu

Anonymous said...

uwt ni sehemu ya ccm ninakila sababu ya kujidai kuona democrasia ikitendeka, bt jk nakelwa sana na ufisadi and fisad's hembu tuondolee

iddy
Russia

Anonymous said...

hizi ni moja kati blog baabu kubwa zinazomilikiwa na watanzania duniani kwa sasa, sina uhakuka na ujuzi ulio nao bwana ndejembi lakini nakukubali kwa uwezo na moyo wako wa kuitanabahisha jumuiya ya kitanzania duniani kuhusu mambo mbali mbali yanayoendelea nyumbani na ndani ya ccm. wito wangu kwa watanzania ni kuitumia web hii kwa manufaa yaliyokusudiwa.

Frank
Soweto
South Africa