Ndugu wajumbe, nimeona niulete kwenu mjadala huu ili kwa pamoja tuweze kujadili;
Hivi karibuni rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. JK Kikwete akiwa ziarani Zanzibar aliwaambia ndugu zetu wa Pemba kwamba huenda ikawachukua muda mrefu wapinzani kuongoza dola visiwani humo.
Kwa mtazamo wangu, rais aliyasema hayo akijaribu kuwasihi jamaa zetu wa Pemba kushirikiana na serikali ya chama tawala yaani CCM katika shughuli za maendeleo kwani maendeleo hayo ni kwa ajili yao wao wenyewe na kutoyashughulikia ni kujirudisha nyuma wao wenyewe.
Lakini pia Mh. Kikwete kama mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Taifa anapaswa kuwa na ndoto hizo kwamba CCM itaongoza kwa muda mrefu, sio tu Zanzibar bali pia Bara kwani amekua akijaribu kutimiza ahadi na matarajio ya watanzania toka kuingia kwake madarakani akitambua kwamba hiyo ndio njia pekee wa kuifanya CCM kuwepo madarakani kwa muda mrefu.
Lakini baadhi yetu tumekuja juu na kudai kwamba kauli hii ni ya kibabe na mambo kadha wa kadha.
Wajumbe mna maoni gani katika hili?
Ndejembi Michael.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
15 comments:
Asante saaana ndugu mwenyekiti, sio tu kwa sababu umetukabisha katika mjadala huu bali bia kwa sababu umetoa maana yenye maana.
binafsi nadhani ndugu kikwete alichokifanya si kibaya na kamwe hakiwezi kulaumiwa kwani kama alivyosema mwenyewe wapemba hawajui ni lini vyama vya upinzani vitaingia madarakani, na nimakosa kusuburi kwani muda hauwasuri wao. kwa hiyo ni sawa na ikibidi wenye mdomo washughlikiwe.
Nadhani umenipata ndugu mwenye kiti.
dickon manji
Taiwan
hivi kuna ubaya gani kwa baba kuwaonya watoto watukutu?, ni mambo ya ajabu sana kuona wajinga fulani wana kuja juu kwa kauli yenye maana na faida kwa jamii yenyewe.
unajua bwana ndejembi nchi yetu ina matatizo mengi sana, we unajua.
nchi ile inahitaji udikteta wa hali ya juu sana ili watu wanyooke, wawe na nidhamu na pia wajue wajibu wao. ni lazima tuwe na rais ambaye kwanza atakuwa tayari kubeba mzingo wa lawama hasa kabla watanzania hawajamuelewa ila wakishamuelewa watampenda tena sana. lazima awe tayari kuwafunga wezi, wala rushwa, wavivu. lazima awe tayari kuona uchungu kwa mabalozi wasio elewa wajibu wao kama huyu wa hapa Marekani yupo yupo tu. Mdogo wangu bwana ndejembi nina uchungu sana na nchi ile na mimi nakusihi tu - tuombeane mmoja kati yetu awe walau waziri tuwaonyeshe maana uwaziri.
Endeleeni ndugu zangu kazi yenu ni nzuri mnajitahidi sana.
Mathias
Atlanta GEO
USA
saaaaaaaaaaafi sana! hii nimeipenda
tusipoteze muda,mwambie kikwete mwenye kidomodomo chuo cha mafunzo kinamsubili hatuwezi kuwa na watu wanaogomea kazi za maendeleo kisa hawaitaki CCM huu ni ujinga. teyari CCM iko madarakani then wanachogomea nini? nasema lazima wafanye kazi la sivyo mkono wa sheria uwaangukie.
mwananchi
kampala
uganda.
e bwana kwanini asiwaache tu na umasikini wao!?, awa watu wahovyo sana kwanza chama chenyewe ni cha kidini, kiko zanziibar pekee na ndi wanao shabikia kuvunjika kwa muungano we unazani wanamaana hawa?
Julius
oklahoma
united state of america.
mkuu asante kwa hoja haijalishi kuwa ni nzuri au vipi. jamani maendeleo hayata kuja mwa kubembelezana kama tunavyofanya, watu hawataki kufanya kazi kamata weka ndani kama marekani, Urus, ujeruman etc.
mkiwabeleza matokeo yake ndio haya mnaanza kurumbana kwenye viti visivyo na msingi sana.
Iddy
Dallas
mkuu serkali ya kikwete inajitahidi sana! lakini naomba kufafanua kidogo, rais kama taasisi nadhani inajitahidi sema kuna kutokuwa na uhakika lipi lianze na lipi lifuate, kama nguvu kubwa ipelekwe kwenye katika afya na next let say year nguvu kubwa ipelekwe kwenye ajira, etc.
kwa upande wizara huku ndugu mwenyekiti sisi ni mashahidi tusidanganyane mawaziri wetu wengi hawajui ni kwanini wamepewa nafasi walizopewa, haiwezekani kila waziri anaekuja hana jipya yaani aliyetoka na anaeingia hakuna tofauti wote wanachojua ni kuingia ofisini asubuhi na kutoka jioni, basii.
mwenzangu mmoja alitoa mfano wa balozi wetu hapa marekani, ndiyo yale yale ninayoyasema kwamba hawajui kwanini ni viongozi. ndejembi uongozi sio kujuana na rais wala sio shule-shule itakua na maana kwako kama utaitumia kubuni mambo kutegemea na mahitaji.
mimi nitolee mfano mdogo tu kwetu sisi wana ccm marekani tulitambua kwamba tunahitaji maoni tukaachia viongozi jukumu hilo ninyi viongozi iliwachukua siku kadhaa tu kututaalifu kwamba tutakuwa na kajimtandao kadogo sio kwa ajili ya kupata maoni bali pia kupeana taarifa mbalimbali kama jumuia fulani, huu ndio uongozi unavyotakiwa kuwa bwana mdogo Michael.
mchangiaji
alaska
wajumbe tunahutaji sana mijadala kama hii, lazima tuwenayo mingi sana ili tuweze kuchambua mambo kikamilifu. bwana ndejembi tunakushauri uweke mambo globally najua unaelewa kwa maana ya kwamba mtandao wetu ujulikane ili wachangiaji wawe wengi zaidi na kwa hilo tutapata mawazo mazuri zaidi. NAWAOMBA WAJUMBE TUSHIRIKIANE KUUTANGAZA MTANDAO NA PIA VINGOZI WETU WAAMBIE NYUMBANI TANZANIA KWAMBA TUNAHITAJI MSAADA KATIKA HILO.
Senio mchangiaji
cow boy
houston
texas
USA
mkuu tasmini yetu tuliyoifanya hapa washington kuhusu maendeleo ya mtandao huu yanaonyesha kwamba perfomance ni 74percent ya matarajio yetu, hii ni kwa mwezi December pekee.
mwenyekiti perfomance sio mbaya ila naomba tujitahidi walau kwa mwezi huu january tufikie 80percent.
mtafiti wa mambo
washington
USA
well tunachangia hoja kama ulivyosema heshimiwa mwenyekiti. alichosema kikwete sio kama ni kibaya tatizo letu watanzania ni kwamba tunazani tunajua kuliko ukweli wenyewe, ukweli wenyewe ni kuwa wanapaswa kushiriki kwa kazi za maendeleo kumbe wasipofanya nani awafanyie? hao wapinzani wanawashawishi kutoshiriki ili lawama za kutokuwepo kwa maendeleo ndani ya maeneo yao wairushie CCM sasa nazani kuna haja ya nguvu kubwa kutumika katika kuwashughulikia hawa viongozi wanaowashawishi wananchi kutoshirikiana na serikal.
keny
sweden
utaratibu wa maisha ya watanzania hayamfanyi mtu kushiriki katika kazi za maendeleo moja kwa moja hata kama hataki, pili tanzania bado tuna mawazo kwamba kutofanya kazi ni kuikomoa serikali hasa hawa wenzetu wa zanzibar. sasa katika mazingira kama haya lazima tuwe tayari kuchukua hatua ambazo wakati mwingine zitatufanya tuonekane tuna kiuka kile wanachokiita eti haki za binadamu.
chacha j.
georgia
usa
waheshimiwa nimerudi nilikuwa kijijini kwetu siunajua mitandao huko bado ni matatizo. but ninasalam nyingi sana toka huko, nako ni kigoma kule uzembe wetu ulikopelekea tukapoteza jimbo. lakini tayari wanahabari juu ya moto huu toka marekani, anyway mwenyekiti asante kwa hoja hiyo mimi maoni yangu hawa jamaa wanadhani wanamkomoa kikwete kwa hiyo tuwaache na ujinga wao.
pinko
virginia
united of state of america
jamani katibu miraji sijamsikia yupo? hawa ni wapemba wenzake azungumze nao si washatushinda ndo maana sasa tunataka kutumia nguvu na kikwete awaadhibu vilivyo.
Hao waliokuja juu ndugu mwenyekiti ni wale wanaodanganywa kwa pipi kama wanaombiwa kuwa ukiua albino unapata utajili. Jk ni mmoja wa maraisi wachache waliotokea Africa, najua wapuuzi wachache watapingana na mimi lakini ukweli wenyewe ndio
Kuhusu zanzibar nikweli kabisa ndugu zangu niwavivu, nakama mnavyojua tena sifa kubwa ya watu wavivu ni kupenda kula sana na majungu kwa wingi maana wanamda mwingi wa kupiga gumzo bila kufanya kazi.
Jk hulivyowambia ndugu zangu ni kweli kabisa
Miembini
Zanzibar
Jk your the men !!!. I am with u in all your decission
Watanzania kama kawaida yetu hatupendi kuelezwa ukweli.
Post a Comment