Thursday, January 8, 2009

Ndugu watanzania,

Kama ilivyo ada kwetu watanzania kupongezana pindi mmoja wetu ama kikundi miongoni mwetu kinapofanya na kufanikiwa katika jambo fulani, leo kwa mara nyingine tena napenda kumpongeza mama Sophia Simba kwa ushindi mkubwa alioupata jana katika uchaguzi wa jumuia ya wanawake Tanzania (UWT) uliofanyika Dodoma.

Salam hizi si zangu pekee bali ni za viongozi na wanachama wa CCM Marekani ambao kwa dhati kabisa tunampongeza tukiamini kwamba ushindi huo ni ishara tosha kwamba kina mama na watanzania kwa ujumla tuna imani na mama Sophia Simba na kwamba ataifanya kazi aliyoiomba kwa uadilifu mkubwa kabisa na ufanisi litakuwa ni moja ya vipimo vya utendaji wa uongozi wake.

Mwisho tunakutakia kila la kheri ili matokeo ya uadililifu na ufanisi vikufikishe kwenye nafasi zingine za uongozi ukiwa na uwezo nazo, na pia zikufikishe kuwa nembo ya utambulisho kama mama miongoni mwa kina mama wanaoheshimika Tanzania, Afrika na Duniani.

Ndejembi Michael,

Mwenyekiti.

7 comments:

Anonymous said...

Mbona ccm wenyewe hapa bongo hawampongezi au ndio mambo ya utamaduni wetu wa kotokupongezana mwenzetu anapofanikiwa. Kwetu sisi majungu, sasa hivi utasikia huyu mama kaiba kula.

mwanachama
ccm

Anonymous said...

You're kidding me. Huyu mama si waziri, sasa katika watanzania takribani millioni 39 hatuna mtu mwingine wa kuongoza mpaka hawe huyu. Does that mean the normal tanzania who were born and raised in a normal family has no chance of perticipating in politics?

What ???

Anonymous said...

Tunawashukuru kwa pongezi zenu.

Anonymous said...

Mama nakupongeza sana kwa ushindi wako, pia nakutakia afia njema. Sisi wote ni watanzania na tunapomchagua mtu maana yake anauwezo wa kukabiliana na majukumu tuliyomkabizi.

NAWAPONGEZA CCM HUU MTANDAO UNATUWEZESHA SISI KUTOA MAWAZO YETU.

Anonymous said...

asanteni kwa pongezi, vijana wa marekani mnajitahidi sana. hongereni tutakuja kuwatembelea hivi karibuni

nathan
uvccm
dar es salaam

Anonymous said...

mimi najua kwamba kupongezana ni utamaduni wetu so kama hawajampongeza pole!
sisi wamarekani hatupaswi kuiga mifano mibaya ndio maana mwenyekiti wetu amempongeza mama sophia simba kama mwenyewe anavyopenda kumwita maana mwenyekiti huanza kwa kumwita eti 'mama' sijui ni mama wa nani.
anyway najua ndejembi utakasirika na hauta toa haya maoni yangu.

khaji
dallas
usa

Anonymous said...

Hivi huu niumoja wa wanawake wa Tanzania au wanawake wa CCM mimi sielewi jamani wadau naomba nieleweshwe...