Monday, April 13, 2009

WATOTO WA MAHASIMU WAKUBWA WAKUTANA BUTIAMA

WATOTO wawili wa viongozi wa zamani wa Uganda na Tanzania waliandika historia mpya baada ya kukutana kwenye kijiji cha Butiama alikozaliwa na kuzikwa Rais Julius Nyerere na kukubaliana kuanza umoja mpya.

Watoto hao, Madaraka Nyerere kulia na Jaffar Amin, ambao baba zao walionekana kuwa mahasimu wakubwa katika vita vya mwaka 1978 baina ya nchi hizo mbili, walionyesha kusikitikia vita hiyo, huku mtoto wa Idd Amin wa Uganda akisema "ilisababisha maafa makubwa" kwa wananchi wa Tanzania na Uganda.

"Vita ile ilisababisha maafa makubwa kwa wananchi," alisema Jaffar akionekana kusikitikia kitendo cha baba yake ambaye alikuwa chanzo cha vita hiyo kwa kuishambulia Tanzania kabla ya Nyerere kuamua kujibu mapigo kwa kuiondoa serikali yake madarakani habari na picha kwa msaada wa Mwananchi.

Msomaji
Msoma

No comments: