Tuesday, April 7, 2009

JINSI UBALOZI WA RWANDA NCHINI ULIVYOKUMBUKA WALIOKUFA KATIKA MAUAJI YA KIMBARI MWAKA 1994

Huu ulikuwa ndiyo ulikuwa ujumbe wa leo kwa watu waliohudhuria maadhimisho hayo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini leo jioni pata matukiao mbalimbali katika picha
wageni mbalimbali wakisimama kwa dakika moja kuwakumbuka marehemu waliokuokufa katika mauaji ya kimbari ya Rwanda mwaka 1994 kumbukumbu hiyo imefanyika jioni hii kwenye ukumbi wa Karimjee jijini na kuhudhuriwa na mabalozi na wageni mbalimbalali.
Wanamuziki Lifunyo , Chid Benz, Nakaaya na Enika wakiwasha mishumaa kama ishara ya kuwakumbuka watu waliokufa katika mauaji ya kimbari nchini Rwanda miaka 15 iliyopita kumbukumbu hiyo imefanyika leo jioni katika ukumbi wa karimjee.
Katibu mkuu wa Wizara ya mbambo ya nje Balozi Francis Malmbugi aliyekuwa mgeni rasmi akisoma hotuba katika maadhimisho hayo.
Mwakilishi wa umoja wa mataifa nchini Oscar Frnandes Taranco kulia Balozi wa Rwanda Zeno Mutimura na Katibu mkuu wizara ya mabo ya nje Balozi Francis Malambugi wakiwasha mishumaa kama ishara ya kuwakumbuka marehemu wa mauaji ya kimbari katika ukumbi wa Karimjee jioni leo.
Mwanamuziki Nakaaya Sumari akichangisha fedha kwa ajili ya kusaidia yatima waliotokana na mauaji hayo zaidi ya shiligi 600000 zimepatikana katika harambee hiyo na uchangiaji unaendelea kwa mtu yeyote atakayejisikia kuchangia.
Mwanamuziki Nakaaya Sumari watatu kutoka kushoto akiongoza wenzake katika kuimba wimbo Iam an Afrika unahamasisha waafrika kuwa kitu kimoja katika kupambana na machafuko kama yaliyotokea nchini Rwanda Miaka 15 iliyopita katika maadhimisho ya kuwakumbuka waliokufa katika machafuko hayo.
Sekretari wa Ubalozi wa Rwanda nchini Christin Bagumo kulia na katibu mkuu wa ubaliozi huoAmutonyi Shakila wakibadilishana mawazo mara baada ya kumalizika kwa shughuli hiyo katika ukumbi wa Karimjee jijini.

Msomaji, Dar

No comments: