Uongozi ulio bora na wenye tija, siku zote ni ule wa wale wenye Dola (wananchi) kuwa na maamzi ya namna dola yao wenyewe iendeshwe katika ngazi mbalimbali za kisiasa, kiuchumi na hata kiutamaduni.
Kwa maana halisi ni kwamba misingi imara ya uchumi bora na endelevu itatoka kwa wananchi wenyewe kwa kupitia viongozi wale waliowachagua wenyewe, toka katika hatua za awali na maamuzi yao kueshimika mpaka katika hatua za kitaifa. Hii itamfanya kiongozi huyo kuwajibika ipasavyo kwa wananchi.
Kwa njia hi itapelekea wananchi kueshimiwa na viongozi wao, kwa kuwa wao ndio watakuwa wenye mamlaka ya kupendekeza viongozi wao kupitia matawi yao.
Napenda kutoa pongezi kwa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Mh. Mrisho Jakaya Kikwete kwa kuwa na mwelekeo mzuri kwenye hatua za kupata viongozi wa kitaifa wa CCM au wagombea wa kitaifa wa CCM. Hii inaonyesha wazi jinsi gani serikali ya CCM ilivyodhamilia kuwapa wananchi wenyewe nguvu ya kuendesha dola yao kwa kuteua na kupendekeza viongozi wao kuanzia hatua ya Matawi na Mashina.
Hivyo basi napenda kuwaomba wananchi wote kuunga mkono hoja hii kwa vitendo yaani;
(1) Kuhakikisha viongozi watakao wapendekeza wasiwe ni wale ambao wanatoa mlungula (rushwa) ili waweze kupendekezwa na kigezo cha kutoa mlungula kiwe ni sababu mojawapo ya kumnyima kabisa uongozi mtu wa namna hiyo kwani uongozi ni kipawa kutoka kwa Mungu, hivyo kipawa huwa hakiuzwi bali kinajinadi kwa sera nzuri na endelevu.
(2) Kwa kuwa hatua hii inakusudia kabisa kuletwa kwenye matawi, hivyo basi kiongozi atakayeteuliwa awe ni mtu mwenye sifa nzuri kwenye familia yake na si kwa sababu anapesa nyingi la hasha, bali ni kwa uwezo wake wa kuweza kuitunza familia yake kwa misingi ya usawa kielimu, kijinsia, kiuchumi na kimaradhi. Hii ni rahisi kwa wananchi walio karibu na mgombea huyo kuyafahamu yote hayo kwa kuwa ni majirani zake.
(3) Kama mgombea huyo anafanya biashara binafsi wananchi wa eneo husika Pendeni kufahamu kuwa hizo biashara zake ni za kihalali kwa kuzingatia vipengele vifuatavyo;
a. Zimesajiliwa na zina leseni
b. Je analipia kodi ipasavyo
c. Mahusiano yake na wafanyakazi ni mazuri.
Kwa kufanya hivyo itawasaida kupendekeza viongozi waadilifu ambao wataweza kusimamia kodi zetu ipasavyo, miradi mbalimbali pia itaweza kusimamiwa na kukamilika ipasavyo.
(4)Wananchi pia wawe makini kuangalia je kiongozi watakaowachagua wanayo sifa ya kushirikiana vizuri na majirani zake, hasa katika nyanja za kijamii kama misiba, sherehe za harusi, harambee mbalimbali na shughuli za uzalishaji katika jumuia zetu.
Kwa njia hizi chache na nyinginezo nyingi, zikizingatiwa zitaweza kujenga CCM imara yenye viongozi bora na kama ilivyozoeleka kuwa na majina yale yale yaliyowaletea tija wananchi. Tafadhali wananchi tuwe makini kwenye jambo hili, kwani lina manufaa kwa nchi, na hasa ikizingatiwa kuwa viongozi bora watatoka CCM. Hivyo tuunge mkono hoja hizo za Mwenyekiti wa CCM Taifa Mh. J.M Kikwete vitendo, kwa kuchagua viongozi walio bora, ili waweze kushirikiana na waweze kuliletea tija taifa letu.
Napenda kutanguliza shukrani zangu za dhati kwa viongozi wa CCM kwa ushirikiano wenu mzuri kwa Mwenyekiti wa taifa wa CCM -
Nasema, kidumu Chama Cha Mapinduzi.
Anthony N. Rugimbana
Houston Tx
USA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment