Balozi wa Rwanda Nchini Zeno Mutimura alizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya habari maelezo leo juu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini humo mwaka 1994 miaka 15 iliyopita yanayotarajiwa kufanyika kesho kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam
Katika maadhimisho hayo pia kutakuwa na wimbo maalum uliotungwa na mwanamuziki Nakaaya Sumari unaoitwa I am in Africa kuachana na mambo ambayo yanaweza kuchochea kwa mauaji kama yaliyotokea Rwanda laakini pia unaozungumzia kampeni ya kuwasaidia yatima walioko nchini Rwanda waliopoteza wazazi kutokana na mauaji hayo watu mbalimbali na mashirika wameombwa kuchangia kuazia dola moja na kuendelea.
Balozi Mutimura amezitaja akaunti zitakazotumika kukusanya michango hiyo kuwa ni National Bank of Commerce Emassy of Rwanda Acc No. USD:012105025668 na Acc no: Tsh: 012103016937 kampeni hii itaendeshwa kwa muda wa siku 100 ili kukusanya michango hii katika picha kushoto ni Usia Nkhoma afisa habari wa umoja wa mataifa.
Msomaji
Dar es salaam
No comments:
Post a Comment