Friday, April 3, 2009

MSHITAKIWA WA 11 KESI YA AKINA ZOMBE AMEFARIKI DUNIA

Marehemu Rashid Lema akichechemea huku akisaidiwa na mtuhumiwa mwenzake (ambaye yuko huru sasa) alipokuwa anatoka mahakamani Februari 3 mwaka huu.

SHAHIDI muhimu katika kesi ya mauji ya wafanyabiashara watatu kutoka Mahenge mkoani Morogoro na dereva taxi mmoja DC Rashid Lema amefariki dunia leo alfajiri katika hospitali ya saratani Ocean Road jijini Dar es Salaam. Taarifa zilizopatika katika hospitali hiyo kupitia Mkurugenzi wa Tiba hospitalini hapo Dk. Hamza Maunda alisema Lema alifariki majira ya saa kumi alfajiri ambapo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa saratani. Habari zilizofikia mwandishi wa habari hii inasemekana kuwa taratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwake Osterbay jijini Dar es Salaam.
Msomaji
Dar es salaam

No comments: