Wednesday, April 29, 2009

MABOMU YALETA KIZAAZAA JIJINI DAR ES SALAAM

Jinsi moshi mkubwa ulivyotanda katika eneo ilipotokea milipuko
Kamishna wa jeshi la polisi Paul Chagonja akitoa maelezo kwa waandishi wa habari kutokana na milipuko iliyotokea katika Ghala la Jeshi katika kambi iliyoko mbagala Zhakhem, Kamishna Chagonja akiwa katika eneo la tukio amesema wananchi wawe watulivu wakati jeshi hilo pamoja na Jeshi la wananchi JWTZ wakishirikiana kuchukua tahadhari ikiwa ni pamoja na kuzima moto unaowaka, Chagonja amesema watu wasisogee eneo la tukio kwani bado si salama kutokana na milipuko kuendelea kusikika mpaka hali itakapokuwa imetulia ameongeza kuwa ni mapema kueleza chanzo cha milipuko hiyo na hasara yake au madhara yaliyotokea kwa bidadamu, lakini wananchi wawe watulivu watapewa taarifa.
Askari wa Usalama Barabarani na Polisi wakiwa wametanda katika maeneo hayo ili kuangalia usalama wa watu na kuzuia watu kuenda eneo la Tukio.
Kamishna wa Oparesheni ya Polisi Paul Chagonja akiongea na vyombo mbalimbali vya kimataifa ikiwemo BBC na Dauch Welle.
Eneo la Mbagala Zhakem mahala ambapo kuna barabara inayoingia katika kambi ya jeshi ambako Ghala la kuhifadhia Silaha lielipuka likiwa limezungushiwa uzio milipuko hiyo imeleta Kizaazaa kwa wakazi wa jiji la Dar es alaam na , hakuna mtu wala Mwandishi wa habari aliyeruhusiwa kuingia katika eneo la tukio Vikosi vya jeshi la ulinzi, zimamoto na Polisi wote kwa pamoja wanajaribu kuzuia watu wasiende katika eneo la tukio.
Katikati ya tukio vibaka nao walikuwepo kufanya vitu vyao kama unavyojionea mwenyewe hawa vibaka wakiwa wamekamatwa na askasi wa polisi.
Hiki ni moja ya kipande cha bomu kilichoruka kutoka eneo la tukio na kutua katika Barabara ya Kirwa baada ya bomu kulipuka.
Na hivi ni vipande vya mabomu vilivyotua mbagala kizuiani baada ya mlipuko kama unavyoona wakazi wa maeneo hayo wakivishangaa.


Msomaji
Dar es salaam

2 comments:

Anonymous said...

hivi serikali yetu ni vipofu kwamba hawajui lile ni eneo la makaazi ya watu? na mbona hawakuchukua hadhari mapema, wanaccm lazima tuyapinge haya kwa nguvu zetu zote

Anonymous said...

jamani poleni sana ndugu zangu hawako salama sijui ninyi.

aika