Chama Cha Mapinduzi nchini Marekani kinapenda kuwajulisha watanzania wote kuwa kimekamilisha mipango yake ya kuonyesha sinema zenye lengo la kuitangaza tanzania katika kumbi mbali mabali nchini Marekani. Sinema ya kwanza itaonyeshwa katika kumbi la AMC lililopo katikati ya jiji la Kansas City, Missouri siku ya Alhamisi ya tarehe 23/ 04/2009 kuanzia saa 1:45 usiku.
Kabra ya sinema hiyo video ifuatayo http://www.tanzaniatouristboard.com/pages/ttb_video.php itaonyeshwa. Uongozi wa ccm nchini Marekani unatoa pongezi kwa wote walioshiriki katika kufanikisha mpango huu.
Address kamili ya ukumbi huo wa AMC ni:
AMC Theatres
1400 Main Street.
Kansas City, MO 64105
Pia tunapenda kuwafamisha kuwa CCM nchini marekani imefanikisha Tanzania kujiunga na shirika la Ethnic Enrichment Commissiner linalotumika kuzitangaza nchi mbali mbali wanachama katika nyanja za kiuchumi, utamaduni, na mambo yote yanayousiana na nchi mwanachama. Kwa taharifa zaidi kuhusiana na hili shirika tembelea tovuti yao na ukibonyeza pale panaposema Countries utakuta bendera ya Tanzania tayari imeshatundikwa na ukibonyeza kwenye bendera ya nchi yetu basi utakutana na mambo yote yanayohusu tanzania. Tovuti yao ni www.eeckc.org
Kwa taharifa na maelezo zaidi wasiliana na wafuatao hapa chini
Michael Ndejembi--Mwenyekiti CCM makao makuu nchini Marekani 713 384 4567
Miraji Malewa--Katibu mkuu CCM makao makuu nchini Marekani 832 741 4452
Deogratias Rutabana--Mwenyekiti CCM shina la Kansas City, Missouri - Marekani 816 812 5495
Mungu Ibariki Tanzania.
Taarifa hii imeletwa na uongozi wa CCM nchini Marekani
No comments:
Post a Comment