Msomaji
Dar es salaam
Msomaji
Dar es salaam
Dk Ladislaus Komba
Katoro Wagonjwa wa kijiji cha Katoro kata ya Katoro Tarafa ya Katerero wilaya ya Bukoba vijijini wanaolazwa katika kituo cha afya Katoro wanakabiliwa na tatizo la kulala na maiti wodini kutokana na kituo hicho kutokuwa na chumba cha kuhifadhia maiti.
Mbunge wa Jimbo la Kigoma kaskazini bwana zito kabwe ameanza kulaumiwa na wapiga kura wake kwa madai kwamba hana msaada naona kwamba hajawatembelea tangu achaguliwe miaka minne iliyopita. habari zilizotufikia mchana wa leo zinadai kwamba wapiga kura hao walitoa shutuma hizo walipokuwa wakizungumza na wajumbe wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa kigoma ambao alikuwa katika vijiji kadha vya jimbo hilo la kigoma kaskazini.
Makamu wa kwanza wa rais wa Marekani bwana Joe Biden amesema kwamba nchi yake iko tayari kuiunga mkono Georgia katika vita yake na Urusi. Biden ametoa kauli hiyo akiwa mjini Tbilisi ambao ni mji wa Georgia, Urusi na Georgia zimekuwa na mapigano na malumbano kwa muda mrefu sasa hali inayosababisha kupotea kwa amani katika eneo hilo. Marekani ilikwisha iagiza serikali ya Urusi kuondoa majeshi yake katika eneo la mapigano lakini Urusi ilipuuza na kwamba bado majeshi ya nchi hiyo yapo katika maeneo ya Abkhazia na Ossetia ambayo ni maeneo ya Georgia.
Rais Jakaya Kikwete amemteua, Zahra Mwanasharif Nuru, kuwa Msaidizi wa Rais wa masuala ya diplomasia. Taarifa iliyotolewa alhamisi wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, na Katibu Mkuu, Ikulu, Michael Mwanda, kwa niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi, ilisema kuwa uteuzi huo ulianzia juzi (Jumanne).
Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM) unatarajiwa kufanyika Sharm El Sheikh,Misri tarehe 15 hadi 16 Julai, 2009.
Mkuu wa wa maswala ya kibiashara wa Benki ya Afrika Wasia Mushi (kulia) akiongea wakati wa hafla ya makubaliano ya ushirikiano huo baina ya Benki ya Afrika na Vodacom kuhusiana na M-pesa. Wateja wa benki ya BAO watapata huduma ya kutuma pesa na kupokea pesa kupitia simu zao za mikononi, M-PESA. kushoto ni Mkuu wa Udhamini na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza.akimsikiliza kwa makini katika hafla iliyofanyika katika ofisi za benki hiyo jijini.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kati) akiwa kwenye mkutano na Rais wa Zambia Rupiah Bwezani Banda (hayupo pichani) kushoto kwake ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko Dr. Mary Nagu na kulia kwake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Seif Ally Idd. Lengho la mkutano huo ilikuwa kujadili kuhusu Mamlaka ya Reli ya Tanzanzia na Zambia (TAZARA).
Wanachama wa CCM wakisherehekea ushindi walioupata katika uchaguzi ndogo wa mbuge wa wilaya ya Biharamulo Magharibi kuziba nafasi ya ubunge iliyoachwa wazi kutokana na kifo cha mbunge wake Phares Kabuye.
Wapigaji kura wa Biharamulo mkoani Kagera, wakitumbukiza kura zao katika kituo cha shule ya msingi Umoja Biharamulo ili kuziba nafasi ya ubunge iliyoachwa wazi kutokana na kifo cha mbunge wake Phares Kabuye.
Tanzanian President Jakaya Kikwete, center leaves after attending the closing session at the third day of the 13th African Union summit of heads of state and government in Sirte, Libya Friday, July 3, 2009. African Union leaders were debating Friday a hotly contested draft declaration that could deal a heavy blow to efforts by the International Criminal Court to prosecute war criminals from the continent.
Tanzania's President Jakaya Kikwete (C) talked with unidentified officials at the Southern African Development Community (SADC) special summit on Madagascar in Johannesburg on June 21, 2009. The summit, called over the army-backed ouster of Marc Ravalomanana, also resolved to expediate mediation efforts and facilitate talks. Madagascar, which was suspended from the bloc in March, had no official representation but fallen leader Ravolamanana held informal bilateral talks with several participants.