Friday, November 20, 2009

RIPOTI YA ZOEZI LA UHAKIKI WA MADAI YA WALIMU HADHARANI

Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali Ludovick Utouh akionyesha ripoti ya ukaguzi wa madai ya walimu wa Sekondari na vyuo.

Zoezi la Uhakiki wa madai ya waalimu na watumishi walio chini ya wizara ya elimu
na mafunzo ya ufundi lakamilika.

Akitolea ufafanuzi zoezi hilo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali Ludovick Utouh amesema imegundulika kuwa katika idadi ya majalada 19,861 yaliyowasilishwa na yenye jumla ya Sh. bilioni 26.07 kati ya madai hayo yenye jumla ya shilingi bilioni 12.5 au asilimia 48 yamekubaliwa kwa malipo na madai ya shilingi bilioni 13.5 ambayo ni asilimia 52 yamekataliwa na kuonekana kuwa hayastahili kulipwa kwa sababu mbalimbali ikiwemo nyaraka za kughushi.

Baada ya zoezi zima la ukaguzi wa madai hayo na kugundua kuwa kuna dosari au udanganyifu katika majalada hayo Ofisi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa Serikali imeishauri serikali ishughulikie tatio hilo la malimbikizo ya madai ya watumishi ili lisijirudie lakini pia serikali itoe fursa kwa walimu ya kukata rufaa kwa yeyote atakayedhani kuwa hakutendewa haki, pia mkaguzi huyo mkuu wa serikali na ofisi yake amependekeza kuwa walioghushi nyaraka wachukuliwe hatua za kinidhamu

Zoezi hilo lilianza mwezi Agosti 23. 2009 na kumalizika oktoba 31. 2009

Msomaji
Dar es salaam

No comments: