Mkurugenzi Mkuu wa Executive Solutions, Bw. Aggrey Marealle akiongea na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa mashindano ya Kombe la Chifu Marealle 2009 leo kwenye ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO.
Mashindano ya Kombe la Chifu Marealle II kwa mwaka 2009 yatazinduliwa rasmi Mjini Moshi tarehe 9 Disemba ili kwenda sambamba na sherehe za Siku ya Uhuru.Mkurugenzi Mkuu wa Executive Solutions, waandaaji wa mashindano hayo, Aggrey Marealle amesema mashindano hayo yatapambwa na maandamano yatakayozihusisha timu zote shiriki na washabiki kutoka kata 17 za Manispaa ya Moshi hadi Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara (MUCCOBS) ambapo mechi ya ufunguzi itachezwa.
Marealle amesema zaidi ya timu 20 za soka, na timu 10 za netiboli kutoka wilaya za Moshi Mjini, Moshi Vijijini, Siha, Hai na Vunjo zote za mkoa wa Kilimanjaro zinatarajiwa kushiriki kwenye mashindano hayo yanayofanyika kwa mwaka wa tatu. Mashindano hayo yatafanyika katika kata mbalimbali za manispaa ya Moshi kama vile Pasua, Ikulu KDC, Majengo na viwanja vya George Memorial.
Fainali zitafanyika katika uwaja wa MUCCOBS siku kumi baada ya uzinduzi.Marealle alimema washindi watapata zawadi kabambe na za kuvutia na akaongeza kuwa mashindano hayo yatahusisha watu kutoka Nyanja mbalimbali na watashiriki katika michezo ya vijana kama vile soka na netiboli pamoja na michezo ya kujifurahisha kwa ajili ya wazee kama kuvuta kamba, kukimbia na gunia na kufukuza kuku.
“Mashindano haya yana lengo la kumuenzi Chifu Marealle akiwa ni kati ya waliotetea uhuru wa Tanganyika na kama mwanamaendeleo aliyechangia kuleta maendeleo mkoani Kilimanjaro. Marealle pia ameongeza kuwa mashindano hayo yana lengo la kuwakutanisha vijana pamoja na kushiriki michezo ili kuweka afya zao katika hali nzuri, kuwa na nidhamu, kujifunza sifa za uongozi na kuendeleza michezo kati ya vijana nchini”, amesema Marealle.
Mashindano hayo pia yanatumika kutoa elimu kwa vijana kuhusu mapambano dhidi ya Ukimwi na kuwafundisha vijana jinsi ya kuishi maisha bora. "Tunaamini kuwa mashindano haya yataunganisha watu wa mkoa wa Kilimanjaro na kuweka msingi imara wa vijana na maendeleo ya michezo na kuchangia kutoa elimu kuhusu UkimwiMwaka 2008 maandamano ya uzinduzi na kufunga mashindano yalikuwa na wanamichezo zaidi ya 700 na wakati wa mashindano pamoja na fainali watazamaji wapatao 7,000 waliudhuria mashindano hayo ambapo Mkuu wa Mkoa wa wakati huo Mhe.
Mohammed Babu alikabidhi zawadi zikiwemo pesa taslimu shilingi 600,000, ng’ombe, vifaa vya mpira wa miguu, mipira na kombe la kifahari kwa wahindi.Zawadi na Wadhamini wa mashindano hayo watatangazwa taratibu za udhamini zikishakamilishwa.
Msomaji
Moshi
No comments:
Post a Comment