Thursday, November 19, 2009

RAIS JAKAYA AWALAANI TFF KWA KUWAFUNGIA WACHEZAJI MIEZI SITA!!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amelinyanyua juu kombe la FIFA la dunia wakati alipozindua rasmi ziara ya kombe hilo hapa nchini na kupiga nalo picha jioni hii kwenye uwanja wa taifa rais aliingia kwenye kibada maalum kilichojengwa kwenye uwanja huo kwa ajili ya kuhifadhia kombe hilo akalibeba na kulinyanyua juu huku akilibusu kombe hilo , Rais Jakaya amemtaka rais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Rodger Tenga pamoja na kamati zake kufanya kazi ya kusimamia na kuinua kiwango na vipaji vya mpira wa miguu nchini badala ya kusimamia timu ya taifa tu na mapato ya milangoni kwani hawako TFF kwa ajili ya kujenga nyumba zao Binafsi bali wapo kwa ajili ya kuendeleza na kukuza soka nchini, Rais Jakaya amelaani kitendo cha shirikisho hilo kuwapa adhabu ya kuwafungia muda mrefu hadi miezi sita wachezaji na kusema hiyo ni kuwakomoa na kudidimiza vipaji vyao badala ya kuviendeleza ziara ya kombe la FIFA la dunia inaratibiwa na wadhamini wa kombe hilo Cocacola na linatembezwa nchi mbalimbali Duniani, aliyeko kulia katika picha ni Hedi Hamer mwakilishi wa FIFA.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katikati akiwasili kwenye uwanja wa taifa jioni hii ili kuzindua rasmi ziara ya kombe hilo nchini kushoto ni mke wake Mama Salma Kikwete na kulia ni Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Mh. Joel Bendera wakiiwa wameongozana na rais.
Ndege iliyobeba kombe hilo ikiwasili kwenye uwanja wa mwalimu J.K. Nyerere.
Msomaji
Dar es salaam

No comments: