Friday, November 27, 2009

OPERESHANI KIPEPEO NI KIBOKO, IMENASA MAJANGILI YASIYOPUNGUA 70

Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Shamsa Mwanguna akiongea na waandishi wa habari katika makao makuu ya Wizara hiyo Mtaa wa Samora, ambapo amesema Jitihada za serikali katika kudhibiti ujangili wa wanyamapori nchini hususan wa Tembo kupitia operesheni kipepeo iliyoanza rasmi tarehe novemba 8, 2009 ndani na pembezoni mwa pori la akiba la Selous zimefanikiwakwa kiasi kikubwa ambapo hadi kufikia novemba 25, 2009 jumla ya watuhumiwa 70 wamekamatwa kwa makosa mbalimbali.

Wamekamata mizoga 9 ya Tembo, 12 ya viboko ,16 ya Nyati, 2 ya kuro na mmoja wa mamba, pamoja na kuonekana kwa mizoga hiyo nyara zifuatazo zilikamatwa meno 8 na vipande 12 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 39, nyama ya Nyati na Swalapala, Ngozi moja ya Mbawala, na mkia mmoja wa nyumbu, pia kilo 20 za samaki wabichi.

Silaha zilizokamatwa ni Bunduki za kuwindia wanyama (RIFLE) 3 na ShotGun 15 , SMG 1, Magobole 2, risasi 114 kati ya risasi hizo 25 zimetengenezwa kienyeji, sumu aina ya Furudan itumikayo kuulia samaki, mamba hata viboko na kwa vile sumu hii huwekwa kwenye maji madahara yake yanampata pia binadamu anayetumia maji hayo.

Kwa maana hiyo basi Wizara itawashughulikia wahalifu ipasavyo vilevile itaendeleza doria za pamoja kati ya jeshi la polisi na idara ya wanyamapori, TANAPA,Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro(NCAA) na Taasisi nyingine za Kanda na Kimataifa katika kudhibiti Ujangili.
Operesheni imepewa jina la "Kipepeo" ktokana na kutumiwa kwa Helkopta na Ndge za kusafirisha askari katika vituo ndani ya pori ikiwa ni pamoja na kuhakikisha askari wanapatiwa mahitaji yote muhimu mahali popote walipo.

Msomaji
Dar es salaam

No comments: