Thursday, March 19, 2009
SERIKALI imebainisha sababu za kutwaa sehemu ya eneo la Kigamboni kwa ajili ya ujenzi wa mji mpya.
Akizungumza na wakazi wa mji wa Kigamboni jana Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi John Chiligati amesema Serikali imefikiria kwa kina kabla ya kutoa uamuzi huo.Akizitaja baadhi ya sababu Waziri alisema mji wa Kigamboni unaeneo refu la bahari ambalo bado halijatumika sawasawa na kuongeza kuwa fukwe hizo zikitumika sawasawa zitaweza kuleta maendeleo makubwa.
Aidha Waziri alisema mji wa Kigamboni upo kariku na jiji la Dar es salaam ambalo ni kitovu cha biashara nchini hivyo kujengwa kwake kutasaidia katika kuongeza uchumi mara dufu.Waziri Chiligati pia alisisitiza kuwa mradi huo utaleta taswira nzuri ya mji huo wa Kigamboni na kuwa utakuwa ni mji wa kuigwa na nchi nyingine ukiwa katika mfumo mzuri wa majengo.
“Mradi huu utakuwa na manufaa makubwa kwa Taifa na kwa wanakigamboni wenyewe kwani Serikali itahakikisha kuwa wakazi wa Kigamboni ni sehemu ya mradi” Alisema Waziri.
Alisema ili kuhakikisha kila mtu anapata fidia sahihi elimu ya sheria za fidia itatolewa kwa wakazi wote na kueleza kuwa fedha za fidia zitatoka kwa wawekezaji watakao kuja katika maeneo hayo na hakuna mtu atakayepoteza haki yake katika mradi huo.Waziri hata hivyo alisisitiza kuwa ujenzi wa mradi huo hauta fanyika mpaka pale Serikali itakapoona elimu ya kutosha imekwisha kutolewa kwa wananchi wote ili kuepuka matatizo hapo baadae.
”Elimu hii ndiyo kwanza tumeianza ninauhakika mtaelewa tu kwani Serikali haina nia mbaya ila kuleta mabadiliko tutahakikisha tutaendelea kuwaelimisha” Alisema WaziriKatika kutekeleza mradi huo Serikali imewaomba wakazi wa maeneo hayo kusimamisha shughuli zote za ujenzi walizonazo mpaka pale ramani ya mji huo itakapokamilika.Mradi huo unahusisha maeneo ya Kigamboni, Vijibweni,Kibada na Mjimwema.
Msomaji
Dar es salaam
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment