Thursday, March 12, 2009

MAGUFULI AKAMATA MELI YA MAHARAMIA TOKA VIETNAM WALIOKUWA WAKIIBA SAMAKI WA TANZANIA

Meli hiyo ya uvuvi haramu ikiwa chini ya ulinzi makali
Ulinzi kama kawaida hakuna kuchekeana Wavuvi haramu wakiwa wamepozi bila wasi wasi.
Msafara wa magari ya polisi wakiwapeleka maharamia hao mahakama ya kisutu tayari kwa kufunguliwa mashitaka Maharamia hao toka Vietnam wakiwa kizimbani tayari kusomewa mashitaka yao Kiongozi wa Departnent Envolomet bw. Keith Govender akipewa zawadi na Waziri John Pombe Magufuli baada ya kufanikisha zoezi la kukamata meli hiyo

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi ikiongozwa na Waziri wake machachari Mheshimiwa John Pombe Magufuli wiki moja iliyopita alizindua mradi huo ambao umeshirikisha nchi ya Afrika Kusini. Mradi huu ni kwa ajili ya kukamata uvuvi haramu. Baada ya mradio huo kuzinduliwa haikupita siku nyingi matunda yake kuonekana kama unavyoona hapo juu meli ya maharamia kutoka Vietnam imekamatwa
Katika meli hiyo kulikuwa na wafanyakazi 35 ambao wengi wao wanatoka nchi za vietinam.
Magufuli aliwapongeza askari wa Tanzania na wale wa Afrika Kusini kwa kuwazawadia vitu mbalimbali. Oparesheni hiyo ilifanywa na meli ya Sahar baartman ya Afrika kusini baada ya kukodiwa na Wizara ya Uvuvi na Mifugo kwa ajili ya kukomesha wizi wa samaki unaofanywa na mataifa matajiri duniani. Kwa muda wa miaka hamsini haikuwahi mkukamatwa kwa meli yoyote pamoja na kuwa tayari Tanzania ina rada ya kuweza kuona uhalifu baharini, lakini ilikuwa inashidwa namna ya kuweza kupata vifaa vya kuweza kuwafikia maharamia hao. Rais Jakaya Kikwete amewapongeza mashujaa hao waliofanikiwa kukamtwa kwa wahalifu hao, pia ametoa onyo kali kwa maharamia hao na kubainisha kuwa nchi ya Tanzania, Kenya, Msumbiji hazitakubali kuona vitendo hivyo vinaendelea.
Msomaji
Dar es salaam

2 comments:

Anonymous said...

Je Mh. John Pombe Magufuli naye alikuwemo kwenye hiyo meli iliyowakamata hao maharamia?. Huyu jamaa uwa anajiamini sana na shughuli yake si mchezo

Anonymous said...

Kweli serikali yetu ikipata mawaziri kama huyu bwana nchi itabadilika.