Tuesday, March 10, 2009

MKUTANO MKUU WA IMF WAFUNGULIWA DAR ES SALAAM- TANZANIA.

DAR ES SALAAM.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimtaifa la Fedha, IMF, Dominique Strauss-Kahn amesema kuwa mgogoro mkubwa wa kiuchumi duniani unahatarisha kuyatumbukiza mataifa masikini katika hali mbaya zaidi ya mizozo na umasikini.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kimataifa ulioandaliwa na shirika hilo mjini Dar es Salaam, Tanzania, mkuu huyo wa IMF amesema kuwa hali ya kuyumba kwa uchumi inatishia kuwarejesha mamilioni ya watu katika ufukara uliyotopea.

Kwa upande wake, Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, akifungua rasmi mkutano huo, alizungumzia umuhimu kwa nchi za Afrika kutojisahau katika kujiandaa na hali ya kuyumba kwa uchumi duniani.

Mkutano huo wa siku mbili unawajumuisha pamoja zaidi ya washiriki mia tatu wakiwemo mawaziri, magavana wa benki kuu na wadau wengine wa sekta za fedha na uchumi kutoka Afrika.

1 comment:

Anonymous said...

k\KWELI UTAWALA WA JK NI BARAKA KUBWA KWA NCHI YETU