Monday, March 16, 2009

JIONEE ZIARA YA WAZIRI MKUU MH. MIZENGO PINDA SOKONI KARIAKOO ILIVYOKUWA

Hili ndilo soko la Kariakoo Dar es salaam, siku hizi liko safi kwa nje maana wamachinga walifukuzwa mambo yote ndani.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwasili katika soko la Kariakoo akifuatana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Patrick Sere.
Ujio ulipokewa na mgomo wa wanafunzi wa Chuo Kikuu ambao walikuwa wanamkumbushia kauli yake kuhusu mauaji ya maalbino nchini, wakisisitiza kuwa kunatakiwa wanasheria kukabiliana na hili jambo. Hivyo basi wanafunzi wa sheria waliofukuzwa siyo stahili yao. Bango jingine linaonekana kwa mbali likisema "Mpaka sasa ni wanafunzi 70 tu ndio wako madarasani" lakini hakuna mtu aliyekuwa anawatiamaanani wanachokisema.
Waziri Mkuu akiwa katika ofisi ya soko la Kariakoo pamoja na mwenyekiti wa soko hilo(kati) na kulia kabisa ni Meya wa Jiji la Dar es salaam Adam Kimbisa.
Watu wanajaribukusikiliza kinachosemwa ndani ya ofisi hiyo
Kama vile Mkuu anauliza "Hii sio boshen?" kisha kijana anajibu "Mheshimiwa hamna boshen hapa, ukweli ni kuwa nyanya zimejaa" Ufafanuzi; boshen ni pale nyanya zinaweza kupangwa mpaka juu ukadhani kweli zimejaa lakini katikati kuna upepo. Kwa maana nyingine unaweza kwenda sokoni kununua nyanya au viazi vingi kisha ukifika nyumbani vikawa sio vingi kama ulivyoona. Unatakiwa kuwa makini ukinunua nyanya au viazi. Usimruhusu muuzaji akuwekee nyanya kwenye mfuko, weka mwenyewe au mwambie aweke moja moja.
Mmoja wa wafanyibiashara akilalamikia uwongozi wa soko.
Mwingine akilalamika kwa hasira sana nakutia msisitizo.
Soko hili la Kariakoo lina "underground vending stalls" huku chini kuna joto na uchafu sana. Siku hiyo Waziri Mkuu alijionea mwenyewe.
Kadiri ya malalamiko yalivyozidi kuja mwenyekiti wa soko(brue) alibadilika sura, anaona kama vile anaonewa.
Malalamiko yalivyomzidi mwenyekiti akaanza kujikuna kichwa.
Msomaji
Dar es salaam

3 comments:

Anonymous said...

Kweli kazi hipo

Anonymous said...

Wewe msomaji uliyetuma hizi picha mbona haukutueleza kama huo uchafu ndio andagraundi yenyewe au hapo nikwenye shimo la uchafu. Mungu waepushe watanzania wenzagu na mabalaa kama haya

Anonymous said...

Nimependa sana ufafanuzi juhuu ya boshen, kumbe kanyaboya

mteja
kariakoo