MAUAJI YA WALEMAVU WA NGOZI (MAALUBINO).
Takwimu za jeshi la polisi zinaonyesha kuwa tangu mwezi Juni 2007 hadi Februari 2009, miezi takribani 18, walemavu wa ngozi 43 wameshauawa, hii ni sawa na wastani wa vifo vya walemavu wa ngozi watatu kwa kila mwezi. Kimkoa mauaji ya walemavu ya ngozi katika kipindi hicho yalikuwa kama ifuatavyo, Mwanza waliuawa walemavu 20 ,Kagera waliuawa 6, Shinyanga 4, Mara 4, Kigoma 3 na mbeya, Arusha na Mtwara mlemavu mmoja mmoja. Waziri Mkuu Mizengo, Pinda alieleza kuwa kutokana na tatizo hilo aliamua kutembelea katika Mikoa husika na kuwaitisha waganga wa kienyeji na kuamua kuwafutia leseni jambo ambalo waliafiki wote.
MAUAJI YA VIKONGWE
Mauaji ya vikongwe katika nchi yetu imekuwa ni tatizo la muda. Taifa limekuwa likipoteza vikongwe kwa imani za kishirikina jambo ambalo siyo la kweli. TAKWIMU ZINAONYESHA kuwa katika kipindi cha miaka Mitano kuanzia mwaka 2003 hadi Februari 2009 Mkoa wa Mwanza waliuawa vikongwe 696. Shinyanga 522, Tabora 508. Iringa 256, Mbeya 192, Kagera 186, Singida 120, na Rukwa 103, Jumla ya vikongwe waliouawa katika kipindi hicho ni 2,866 hii ni sawa na wastani wa mauaji ya vikongwe 573 kwa mwaka au 47 kwa mwezi.
Waziri Mkuu aliongeza kuwa Serikali haiwezi kukaa kimya, Hivyo Serikali imeamua kurejesha ulinzi wa sungu sungu na kuiboreshea uwezo wa kufanya kazi. Nia na madhumuni ya uzinduzi huu ni kuhakikisha wale wote wanaojihusisha na mauaji ya walemavu wa ngozi, wauaji wa vikongwe na wauza madawa ya kulevya wanafahamika. Hii itakuwa ni siri ya kila mtoa maoni ilitabainisha kuwa katika mchakato huo wananchi wasikomoane hata kama walikuwa wanachuki basi chuki hiyo isiwepo bali wafanye kazi kwa umakini.
Msomaji, Dar es salaam
No comments:
Post a Comment