Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Kikwete, leo anatarajia kuzindua rasmi Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Uzinduzi huo utafanyika Makao Makuu ya Kamandi eneo la Msangani, Kibaha Mkoa wa Pwani na Rais Kikwete atatumia nafasi hiyo kuzungumza na maafisa, wapiganaji na wananchi wa maeneo hayo.
Taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Uhusiano ya JWTZ jijini Dar es Salaam jana, ilisema kamandi hiyo inajumuisha vyuo, shule na vikosi vyote vya nchi kavu vikiwemo vifaru, mizinga, askari wa miguu na wahandisi wa medani.
Ilisema kuzinduliwa kwa kamandi hiyo kutafanya JWTZ kuwa na kamandi tatu;
Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu (LFC),
Kamandi ya Ulinzi wa Anga (AFC) na
Kamandi ya Wanamaji (Navy).
Wakati huohuo, Kamanda aliyeongoza Majeshi ya Tanzania kusaidia Msumbiji kupambana na waasi wa Renamo mwaka 1986-87, Brigedia Jenerali mstaafu, Simon Amri Makaranga, amefariki dunia.
Makaranga alifariki dunia Machi Mosi, mwaka huu katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro alikokuwa amelazwa na alitarajiwa kuzikwa jana mkoani Morogoro kwa heshima zote za kijeshi. Makaranga alistaafu jeshi kwa heshima mwaka 1997 baada ya kulitumikia kwa miaka 34. Alijiunga na JWTZ mwaka 1963.
msomaji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
good job Dr.
Post a Comment