Mwakilishi wa uongozi wa CCM - Marekani ambae pia ni mwenyekiti wa CCM - Shina la Missouri bwana Deogratias Rutabana (katikati) alipokutana na Mh.balozi Ombeni Y. Sefue jijini Washington D.C jumatano wiki hii. Kulia ni Mh. balozi Sefua na kushoto ni mmoja wa maafisa waandamizi wa ubalozi bwana Dr. Switbert Z. Mkama
Monday, August 31, 2009
Uandikishaji wapiga Kura Pemba!!
Kina mama wakaazi wa Chake Chake Pemba wakionyesha fomu zao za kuzaliwa nje ya Afisi ya Mkuu wa Wilaya. Bila ya kuwa na cheti cha kuzaliwa huwezi kupata kitambulisho cha uraia.
Moja ya fomu inayojazwa kwa ajili ya kupata kitambulisho cha uraia huko Pemba.
Wakaazi wa Chakechake wakiwa katika foleni wakisubiri kujiandikisha katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chakechake iliwawezekupewa kitambulisho cha uraia. Kitambulisho cha uraia huko Zanzibar humuwezesha mkaazi kupata kitambulisha cha kupiga kura.
Kitambulisho cha uraia kimekuwa dili huko Pemba maana ni nguzo kuu ya mwananchi huko kupata haki yake ya kupiga kura mwakani.
Msomaji
Zanzibar

Friday, August 28, 2009
Vigogo wawili miundombinu waondolewa katika nyadhifa zao
MABADILIKO ya muundo mpya wa Wizara ya Miundombinu, umewaweka kando vigogo wawili wa wizara hiyo kutoka katika nafasi walizokuwa wakishikilia.
Wiki hii Rais Jakaya Kikwete, aliidhinisha mabadiliko ya muundo wa Wizara ya Miundombinu, ikiwemo kuanzishwa Idara mpya ya Miundombinu ya Usafiri inayojumuisha usimamizi wa Reli na Bandari.
Kwa mujibu wa muundo huo mpya, aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchukuzi, Dk Bathlomew Rufunjo, ameondolewa katika nafasi hiyo.
Idara hiyo sasa inaitwa ya Huduma za Uchukuzi ambayo inaongozwa na Dk William Nshama, ambaye alikuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Msemaji Mkuu wa Wizara hiyo Patrick Ntemo, alipoulizwa jana, alisema mabadiliko tayari yalizungumzwa na Katibu Mkuu, Mhandisi Omari Chambo , hivyo hana la kusema.
Hata hivyo, duru nyingine za habari ziliweka bayana kwamba, Dk Rufunjo huenda akapangiwa kazi nyingine.
Katika muundo huo, Elius Mwakalinga ambaye alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Nyumba, naye anasubiri ama kupangiwa kazi nyingine.
Akitangaza muundo huo, Katibu Mkuu Mhandisi Chambo, alisema Idara ya Huduma za Ufundi na Umeme itakuwa na sehemu za Ufundi na Umeme na Majengo ya umma.
Idhini hiyo ya rais imekuja katika kipindi ambacho wizara hiyo imekuwa ikiweka mipango ya kupatia ufumbuzi matatizo makuu ikiwemo ya Shirika la Reli (TRL), Bandari na usimamizi wa majengo ya serikali.
Katibu Mkuu Chambo, alifafanua kwamba, lengo la muundo huo ni kuongeza tija na ufanisi katika utendaji kazi wa wizara.
Msomaji
Dar es salaam

Thursday, August 27, 2009
SERIKALI YAKANUSHA MADAI YA TBC KUUZWA
Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo MH. George Mkuchika akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.
Serikali imekanusha madai ya shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kuuzwa kinyemela kama ilivyoonyeshwa katika taarifa iliyotolewa na chombo kimoja cha habari hapa nchini.Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar esa Salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo George Mkuchika wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu hatua iliyochukuliwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kuunda kampuni mpya iitwayo Star Media (Tanzania) Limited kwa ubia na mwekezaji.
Amesema Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kama shirika la umma halijauzwa na kuwataka wananchi kutoamini taarifa zozote zinazotolewa kuhusu kuuzwa kwa namna yoyote kwa shirika hilo.
“ Nawathibitishieni leo kuwa shirika la Utangazaji (TBC) halijauzwa ,bado ni la wananchi na kamwe halitauzwa” amesisitiza.Ameongeza kuwa TBC ni mali ya umma na itaendelea kuwa hivyo kama shirika la umma linalomilikiwa na serikali kwa asilimia 100 na kuongeza kuwa Star Media Tanzania Limited ni Kampuni tanzu ya TBC.
Amefafanua kuwa TBC imeunda kampuni hiyo mpya kwa ubia na mwekezaji aliyeteuliwa kihalali ili kutekeleza mabadiliko ya Digitali na kuendesha mitambo ya kurushia matangazo yake nchi nzima kazi ambayo itakamilika mwaka 2012 kwa gharama ambazo TBC isingeweza kuzimudu yenyewe kutokana na jukumu hilo kuhitaji utaalam mkubwa wa kiufundi ili kukamilisha ufanisi.
Msomaji
Dar es salaam
Wednesday, August 26, 2009
Rais Kikwete alivyoshiriki Mazishi ya Askofu Antony Mayala
Rais jakaya Kikwete akimpa pole Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Mhashamu Yuda Thadei Ruwaichi wakati wa ibada ya mazishi ya aliyekuwa askofu mkuu jimbo Katoliki la Mwanza,iliyofanyika katika makazi easmi ya askofu mkuu huko Kawekamo mjini Mwanza Rais Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma wakitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Askofu Mkuu Jimbo Katoliki la Mwanza Marehemu Mhashamu Antony Mayala wakati wa ibada ya Mazishi iliyofanyika nyumbani kwake eneo la Kawekamo,Mwanza na baadaye kuzikwa katika kanisa kuu la Epifania mjini Mwanza.
Msomaji
Dar es salaam
Msomaji
Dar es salaam
Maadhimisho ya JWTZ kutimiza miaka 45 ilivyofana
Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya mambo ya nje Ulinzi na Usalama Wilison Masilingi mara baada ya ufunguzi wa maadhimisho ya JWTZ kutimiza miaka 45. Mh. Masilingi alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa Maadhimisho hayo yanayoendelea katika kikosi cha 603 cha jeshi eneo la Airwing ,Ukonga jijini Dar es salaam.Wa kwanza Kulia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein mwinyi ambaye aliambatana na Naibu wake Dkt. Emannuel Nchimbi (wa kwanza kushoto).
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya mambo ya nje, Ulinzi na Usalama Mh. Wilson Masilingi akipata ufafanuzi kutoka kwa Luten Kanali Anselum Bahati kuhusu bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na JWTZ kikosi cha Nyumbu wakati wa maonyesho ya miaka 45 ya JWTZ.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye maonyesho ya JWTZ kutimiza miaka 45 wakipata huduma za tiba na ushauri leo katika mabanda ya Maonyesho katika viwanja vya kikosi cha 603 cha Jeshi la wananchi Air wing,Ukonga jijini Dar es salaam.
Monday, August 24, 2009
Kura Za Maoni !!
WAISLAMU NCHINI WATAKIWA KUACHA MAOVU
Waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda kulia akisalimiana na Waziri wa Kazi Ajira na Vijana katika moja ya matukio waliokuwa pamaoja.
Waislamu nchini wametakiwa kutenda matendo yaliyo mema na kujiepusha na maovu katika maisha yao ili waweze kupata thawabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Wito huo umetolewa hivi karibuni na Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana Prof. Juma Kapuya wakati akiongea na Waislamu wa Mkoa wa Dar es Salaam katika kongamano la kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani lililofanyika viwanja vya Mnazi Mmmoja.
Waziri Kapuya ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika kongamano hilo aliwataka waislamu hao pia kufuata nguzo tano za imani yao ambazo ni kutoa shahada, kusimamisha swala, kufunga mwezi wa Ramadhani, kutoa zaka na kwenda kuhiji Makka kwa wale wenye uwezo.
"Watukufu Waislamu ninachosema hapa ni kwamba binadamu ameumbwa, ataishi, atakufa, atafufuka, atahukumiwa na baada ya hapo ataishi katika raha au mateso kutokana na vitendo vyake hapa Duniani hivyo basi ni wajibu wenu kuishi kadri ya neno la Mungu linavyosema", alisema.
Akiongelea umuhimu wa kufunga wakati wa Mwezi wa Ramadhani Waziri Kapuya alisema kuwa kufunga ni amri na lazima kwa kila muislamu kama Mwenyezi Mungu anavyosema katika aya ya 183 ya Surat Al-Bakara.
Msomaji
Dar es salaam
Wahanga wa mabomu Mbagala Walipwa !!
Mmoja wa wazee Mussa Mgeni akionyesha hundi yake yenye thamani ya shilingi 168,000 alizolipwa kama fidia kutokana na nyumba yake kuathilika na mabomu hata hivyo mzee huyo asiyeweza kutembea ana umri wa miaka 76 alilia sana kutokana na kuwa nyumba yake ilikuwa ya gharama zaidi ya hiyo pesa aliyopewa.
Thursday, August 20, 2009
KONGAMANO LA KUJADILI ATHARI ZA UANDIKISHWAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA PEMBA LAENDELEA JIJINI!
Wanasiasa Mashuhuri nchini wakielekea kwenye ukumbi wa mkutano mara baada ya mapumziko mafupi katika kongamano la kujadili Athari za Uandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura Kisiwani Pemba lililofanyika Karimjee Hall.
Viongozi na wadau mabalimabli wa siasa wakiwemo wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanahudhuria Kongamano hilo, ambapo mada mbalimbali zitawasilishwa kwa wajumbe na kujadiliwa katika kongamano hilo na kutolewa mapendekezo ya hatua zitakazochukuliwa , kutoka kulia ni Waziri Mkuu wa zamani Joseph Sinde Warioba, Katibu Mkuu wa chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad ,Katibu mkuu wa Zamani wa AU amabyo zamani ilijulikana kama OAU Salim A. Salim na Mwenyekiti wa Chama hicho Prf. Ibrahim Lipumba.

NAIBU WAZIRI KIONGOZI WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR ALLY J.SHAMHUNA ATEMBELEA TSN
Naibu WaZiri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Ally Juma Shamhuna akisaini kitabu cha wageni wakati alipowasili katika ofisi za magazeti ya Serikali TSN leo asubuhi kwa ziara fupi kushoto ni Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo na kulia ni Katibu mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Muungano Dr. Florens Turuka.
Naibu Waziri Kiongozi wa Saerikali ya Mapinduzi Zanzibar na waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Ally Juma Shamhuna akitoka katika ofisi za TSN mtaa wa Samora baada ya kutembelea Ofisi Hizo tayari kwa kuendelea na Ziara yake ambapo, alienda kutembelea mtambo wa kuchapia magazeti wa shirika hilo uliopo maeneo ya Tazara Jijini Dar es salaam, gazeti la DailyNews ndiyo gazeti kongwe kuliko yote nchini ambapo lilianzishwa mwaka 1972 na kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa kwa mgeni huyo na uongozi wa TSN Daily News
Naibu Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Zanzibar Mh. Ally Juma Shamhuna akitoka mara baada ya kutembelea ofisi za Magazeti ya Serikali.
Msomaji
Tuesday, August 18, 2009
EVANCE MHANDO WA TBC1 AKIZUNGUMZA NA HASHEEM THABEET.
Mchezaji mpira wa kikapu (NBA) Hasheem Thabeet anaecheza huko nchini Marekani kwenye ligi ya NBA katika timu ya MEMPHIS GRIZZLES ya Tenesse akihojiwa na mwandishi na Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Evance Mhando.Mahojiano hayo yalifanyika kwenye ofisi za TBC1 Mikocheni Jijini Dar es salaam siku ya jumapili August 16/ 2009 saa nane mchana ambapo Hasheem alienda kutembelea ofisi hizo na kushiriki kwenye kipindi cha wiki cha Michezo kinachoitwa Michezo Yetu kilichoendeshwa na Evance Mhando (Mr Names).
Pamoja na yote Hasheem aliwataka vijana wa Kitanzania kujitahidi kwenye michezo pia na kutilia mkazo suala la Elimu na kutokata tamaa mapema kwenye kila jambo wanalolitaka katika Maisha yao.

Thursday, August 13, 2009
Hospitali ya Ludewa !!
Mfanyabiashara ya Dagaa wa ziwa Nyasa katika soko kuu la Songea Ruvuma Editha Kiwila akipanga bidhaa yake ambao kisado kimoja huaza shilingi 2000 hadi 4000.
Akina mama ambao wanawauguza ndugu zao katika hosptali ya Wilaya ya Ludewe wakisonga Ugali nje ya wodi ya akina mama wanaosubiri kujifungua,kati ya akina mama 100,000.wajawaito 200 hupoteza maisha katika Wilaya hiyo kutokana na ukosekanaji wa miundombinu.
Wanawake wajawazito toka katika vijiji 76 vinavyo zunguka Wilaya ya Ludewa wakiwa wamelala na wengine wakila chakula huku wakiwa wamesubilia siku zao za kujifungua katika hospitali ya Wilaya ya Ludewa Mkoa wa Iringa kati ya akina mama 100,000 wajawazito 200 hufariki kutokana na ukosefu wa huduma.
Baadhi ya akina mama wajawazito wakiwa nje ya wodi ya wazazi katika hospitali ya Wilaya ya Ludewa ambapo jengo hilo lina vitanda 6 na kila kitanda hutumiwa na akina mama wajawazito wawili. Wengine hulazimika kulala chini.
Msomaji
Mbeya

Wednesday, August 12, 2009
Tanzania to Spend $5 Billion on Transport Upgrade
Tanzania will spend $5 billion over the next five years to upgrade its transport system, Infrastructure Development Minister Shukuru Kawambwa said.
The project is part of the East African nation’s transport investment program, which will run over two five-year phases and will develop roads, ports, railways, airports and ferries, Kawambwa said at a conference in the commercial capital Dar es Salaam today.
“It is expected that by 2018, all trunk roads will be paved, thus enabling all regional centers to be linked with paved roads and all district headquarters to be linked with all weather roads,” he said.
Due to low levels of investment, Tanzania’s transport infrastructure is inadequate to cope with growing demand, Kawambwa said.
The government can “ill afford” to develop the system alone, and needs to partner with the private investors, he said, without adding more detail.
The country is in talks with the Japanese government to secure funds to build flyovers in Dar es Salaam to ease traffic congestion, Prime Minister Mizengo Pinda said on July 27.

Tanzania to Halt Power Utility’s 41-Year Monopoly by Year-End
Energy Minister William Ngeleja
Tanzania plans to enact a law allowing private companies to provide electricity in the East African nation by the end of the year, halting a four decade- long monopoly held by the Tanzania Electric Supply Company Ltd.
Tanzania will publish the Electricity Act, which enables other providers to generate power, in the government gazette by year-end, Deputy Energy Minister Adam Malima said on the sidelines of a conference in the commercial capital Dar es Salaam today.
“The private sector is more than welcome to invest by doing it alone or by partnering with the public sector,” Energy Minister William Ngeleja said at the convention.
Tanzania suffers from recurring power shortages due to insufficient investment in its electricity-generating capacity. The government approved a 300 billion-shilling loan for the state-owned power utility, known as Tanesco, to help it upgrade its infrastructure, Ngeleja said. The funds form part of a 1.95 trillion-shilling recovery plan announced in June, with the World Bank and Millennium Challenge Corp. contributing to the project.
Ngeleja said the government “was aware” of barriers which deter private capital from the industry and that it was changing its power-industry reform plan, first released in 1999, to make it more conducive to investment, he said

Tuesday, August 11, 2009
SERIKALI YATOA UFAFANUZI WA UUZAJI WA MAGOGO NJE YA NCHI
Serikali imewataka wafanyabishara wa mazao ya misitu kuwekeza hapa nchini kwa kujenga viwanda vitakavyosaidia kukuza ajira na kuongeza pato la taifa badala ya kukimbilia kuuza mazao ya misitu hususan magogo nje ya nchi kinyume cha sheria. Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Felician Kilahama wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoa ufafanuzi kuhusu madai ya usafirishaji wa magogo nje ya nchi.
Dk. Kilahama amesema sheria Misitu ya Tanzania Namba 14 ya mwaka 2002 ambayo ilianza kutumika rasmi Julai 2004 inazuia na kupiga marufuku uuzaji na biashara ya aina yoyote ya magogo nje ya nchi.“Sheria yetu ya mwaka 2002 iliyoanza kutumika Julai 2004 hairuhusu kwa namna yoyote kufanyika kwa biashara ya magogo nje ya nci na anayeuza magogo na rasilimali za misitu nje ya nchi ni mwizi, rasilimali ya misitu imehifadhiwa kisheria na ipo kwa ajili ya watanzania” Amesema.
Tanga kwenda Morogoro bali tunazuia wale wasiolipia ushuru na kukiuka masharti na leseni za biashara” Aliendelea kufafanua Dkt. Kilahama. Akitoa taarifa za baadhi ya matukio ya uharibifu wa misitu hapa nchini Dk. Kilahama amesema bado kuna wananchi ambao wanaendelea kufanya biashara ya magogo kinyume cha sheria akiitaja baadhi ya mikoa hapa nchini kama Rukwa, Kigoma ,Ruvuma, Tabora na Pwani kuwa wananchi walio wengi hawana uelewa wa kutosha wa utunzaji wa misitu.
Msomaji
Dar es salaam
Mazishi ya makamu wa rais wa Zimbabwe Mrehemu Joseph Wilfred Msika
Jeshi la Wananchi wa Zimbabwe likiwa limebeba jeneza lenye mwili wa Marehemu Joseph Msika(85) aliyekuwa Makamu wa Rais Wa zimbabwe tayari kwa maziko katika makamburi ya mashujaa wa Zimbabwe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliiwakilisha serikali katika Maziko hayo yakiyofanyika jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Ali Mohamed Shein akitoa heshima za mwisho kwa Marehemu Joseph Wilfred Msika nyumbani kwake kabla ya maziko ambayo yamefanyika jana katika makaburi ya mashujaa wa Zimbabwe. Nyuma ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Mwanamwema Shein. Dk Shein ameiwakilisha serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Maziko hayo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Ali Mohamed Shein akimfariji Mjane wa Marehemu wa Makamu wa Rais wa Zimbabwe Mama Mai Maria Msika wakati alipomtembelea nyumabni kwake nje kidogo ya Mji wa Harare kutoa salamu za ploe kufuatia kifo cha Makamu wa Rais wa Zimbabwe Joseph Wilfred Msika. Katikati ni Mama Mwanamwema Shein.
Msomaji
Monday, August 10, 2009
Taifa Stars itaelekea Rwanda.
Naibu mkurugenzi wa Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Bwana Charles Matoke na kocha mkuu wa timu ya Taifa Marcio Maximo wakiwa pamoja na wadhamini katika hafla fupi ya kukabidhi bendera kwa timu ya Taifa inayoelekea Rwanda kwa mechi ya kimataifa ya kirafiki na Rwanda.
Msomaji
Dar es salaam
Saturday, August 8, 2009
MAMA SALMA KIKWETE ALIVYOPEWA ZAWADI NA MWAKILISHI WA UNICEF
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete akimshukuru Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mambo ya watoto (UNICEF) Heimo Laakkonen mara baada ya kupewa zawadi ya kanga iliyoandikwa “Tuungane kwa ajili ya watoto”.
Laakkonen pamoja na Makamishina wenzake walitembelea ofisi za WAMA kwa ajili ya kutoa mrejesho wa shughuli ya ziara yao ya wiki moja waliyoifanya hapa nchini baada ya kupata mwaliko kutoka wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia na watoto.

Friday, August 7, 2009
WAZIRI WA NISHATI NA MADINI WILLIAM NGELLEJA AKIFUNGUA BARAZA LA WAFANYAKAZI
Waziri wa Nishati na Madini William Ngelleja akifungua mkutano wa kwanza kwa mwaka 2009/10 wa baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) uliopo katika jengo la Water Front jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria mkutano wa kwanza kwa mwaka 2009/10 wa baraza la wafanyakazi wa wizara ya Nishati na Madini uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) uliopo katika jengo la Water Front jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria mkutano wa kwanza kwa mwaka 2009/10 wa baraza la wafanyakazi wa wizara ya Nishati na Madini uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) uliopo katika jengo la Water Front jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja na waziri wa Wizara hiyo William Ngelleja (watatu kushoto) akifuatiwa na Katibu Mkuu wa wizara Athur Mwakapugi (kushoto)
Msomaji
Tuesday, August 4, 2009
N. Korea says 2 U.S. journalists will be freed
Announcement of pardon comes after Bill Clinton meets with Kim Jong Il
North Korean leader Kim Jong Il, left, speaks with former President Bill Clinton in Pyongyang on Tuesday.
North Korean leader Kim Jong Il has pardoned two jailed American journalists and ordered their release following an unannounced meeting with former President Bill Clinton, the North's state media said Wednesday.
The release of Laura Ling and Euna Lee was a sign of North Korea's "humanitarian and peace-loving policy," the Korean Central News Agency reported.
Clinton met with the reclusive and ailing Kim on Tuesday, shortly after landing in the capital Pyongyang. It was Kim's first meeting with a prominent Western figure since his reported stroke nearly a year ago.
SEOUL,
South Korea
Rais Kikwete azindua ujenzi wa barabara ya Singida-Minjingu
Rais Kikwete azindua ujenzi wa barabara ya Singida-Minjingu
Zaidi ya Sh. bilioni 210 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa barabara ya Singida hadi Minjingu mkoani Manyara yenye urefu wa kilomita 224 kwa kiwango cha lami.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Omari Chambo, aliwaambia waandishi wa habari kuwa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi huo litawekwa na Rais Jakaya Kikwete.
Alisema ujenzi wa barabara hiyo umegawanywa katika awamu tatu. Awamu ya kwanza ya Singida- Katesh ina urefu wa kilomita 65, Katesh- Dareda kilomita 74 na Dareda Minjingu kilomita 85.
Alisema kuwa ujenzi huo wa barabara ya lami unagharamiwa na serikali kuu kwa mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya maendeleo ya Afrika (ADB). Ujenzi huo utakamilika ndani ya miezi 33.
Aidha, Chambo amewataka makandarasi waliopewa zabuni ya ujenzi wa barabara hiyo kuzingatia masharti yote muhimu yaliyomo kwenye mkataba ikiwemo kumaliza kazi kwa wakati.
Rais Kikwete alitarajiwa kuwasili hapa jana jioni kwa ziara ya siku tatu ambapo atazindua miradi mbalimbali ya mendeleo ikiwemo kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara hiyo.
Msomaji
Singida

Rais Kikwete Ashauri Watanzania Kununua Matrekta Badala Magari Ya Anasa
RAIS Jakaya Kikwete ametaja anasa za Watanzania kuwa moja ya mambo yanayofanya sekta ya kilimo kushindwa kufikia malengo ya kuwa uti wa mgongo kwa uchumi wa Tanzania.
Akizungumza katika uzinduzi wa maonyesho ya Nanenane katika viwanja vya Nzuguni nje kidogo ya mji wa Dodoma , Rais Kikwete alisema baadhi ya Watanzania wanapenda zaidi kununua magari ya kifahari badala ya matrekta kwa ajili ya kilimo.Rais Kikwete alitaja sababu zingine zinazofanya kilimo kisifanikiwe kuwa ni pamoja na ukosefu wa wataalamu wa kufanya utafiti katika sekta ya kilimo
“Watafiti wengi wanaamini kuwa mbegu nzuri ya kupandwa ni ile iliyozalishwa katika maeneo husika sio ya kuagiza kutoka nje, sasa sisi tunaagiza nje asilimia 75 ya mbegu bora zote tunazopanda hapa nchini hiyo ni hatari kwetu” alisema Kikwete.
Katika maonyesho hayo ambayo kaulimbiu yake ni ‘Kilimo kwanza’Mapinduzi ya kijana uhakika wa chakula na kipato,rais alisema haiwezekani kukosa chakula kila mwaka kana kwamba Watanzania wamelaaniwa.
Alisema kila mwaka Tanzania imekuwa ikikosa chakula wakati ardhi ya kutosha ipo pamoja na baadhi ya maeneo kuwa na mvua za uhakika kitu ambacho ni ndoto katika maeneo ya nchi nyingine duniani lakini bado wanazalisha chakula cha kutosha.
Hata hivyo aliponda kwa Watanzania kuendelea kutumia jembe la mkono na akasema kuwa hicho ni kikwazo kingine cha kuwafanya waendelee kubaki katika hali ya umasikini mkubwa ambao utaendelea kuisumbua nchi.
Pamoja na kusema kuwa kilimo cha jembe la mkono kimepitwa na wakati, aliwaacha hoi wakulima pale aliposema kuwa hata kilimo cha jembe la kukokotwa na ng’ombe ni cha zaidi ya miaka 2000 iliyopita.
“Sisi tunahimiza kilimo cha jembe la kukokotwa na wanyama huku tukisahahu kuwa kilimo hicho kilikuwepo tangu hata kabla ya Yesu Kristo kuzaliwa ambayo ni zaidi ya miaka 2000 iliyopita, lakini sisi ndio kwanza tunaanza”
Katika hatua nyingine rais Kikwete amesema Benki ya Wakulima nchini itaanzishwa kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya China na tajiri maarufu wa Kimarekani Bill Gates.
Rais Kikwete alisema, mkakati huo umekuja kutoka na ukosefu wa vyombo vya fedha vya uhakika vya kutoa mitaji kwa wakulima hapa nchini.
Kikwete alisema serikali imeamua kuchukua hatua hiyo kwa kuwa ukosefu wa mitaji kwa wakulima umekuwa ni kikwazo kikubwa kinarudisha nyuma maendeleo ya kilimo nchini.
Aliongeza kuwa wakulima wengi hawana uwezo wa kununua matrekta kutokana na kuuzwa kwa bei ya juu pamoja na serikali kuondoa kodi kwenye nyenzo hiyo ya kilimo.
“Serikali iligundua uwezo mdogo wa wakulima kununua matreka.Pamoja na kuondoa kodi katika matrekta ili kuwasaidia wakulima lakini bei bado iko juu” alisema Rais Kikwete.
Habari hii imeandaliwa na Habel Chidawali, Patricia Kimelemeta,Dodoma na Hussein Kauli, Dar
Msomaji
Dodoma
UNHCR YAKABIDHI MAGARI NA PIKIPIKI KWA WIZARA YA MAMBO YA NDANI
Mwakilishi wa shirika linaloshughulikia wakimbizi nchini Tanzania UNHCR Bw. Yakoub El Hillo akikata utepe kama ishara ya makabidhiano ya magari na pikipiki kwa jeshi la polisi nchini ili kusaidia kupambana na uhalifu, wanaoshuhudia kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Rawlence Masha, kushoto ni Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Said Mwema na katikati ni Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya Jinai, DCI Robelt Manumba, makabidhiano hayo yamefanyika katika Makao makuu ya Wizara ya Mambo ya ndani ambapo UNHCR imekabidhi magari aina ya Toyota Prado 2 Toyota Hardtop 6 na pikipiki 10 vyote vikiwa na thamani ya Dola za kimarekani 241.000
Msomaji
Baadhi ya Magari na pikipiki yakiwa yameegeshwa katika Wizara ya mambo ya ndani leo Magari hayo yametolewa na Yakoub El Hillo Mwakilishi mkazi wa shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia wakimbizi nchini UNHCR kama msaada kwa Jeshi la Polisi nchini katika kupambana na uhalifu mbalimbali.
Msomaji
Dar es salaam
Subscribe to:
Posts (Atom)