Sunday, June 28, 2009

PROFESA HAROUB OTHMANI AFARIKI DUNIA!?

Aliyekuwa mmoja wa waandamizi wa chuo kikuu cha Dar es salaam pro. Haroub Othmani amefariki dunia asubuhi hii (East African Time) jijini Dar es salaam. taarifa tutawaletea kadri tutakavyokuwa tukizipata.....

Saturday, June 27, 2009

MKUTANO WA KWANZA WA KIISLAMU WAFUNGULIWA UJERUMANI

Mkutano wa kwanza wa jumuia za kiislamu umefunguliwa leo na waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo bwana Wolfgang Schauble. Mkutano huo unalengo la kujadili mambo mbalimbali yanayowahusu waislamu ambao wengi wao wanaamini hawajapata uwakilishi wa kutosha katika mabo kadhaa nchi ujerumani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.JK akifunua kitambaa kuashilia uzinduzi rasmi wa Shule ya sekondari ya Sekwai iliyoko kata ya Gairo wilaya ya Kilosa akiwa katika ziara ya siku moja jimboni Gairo Mkoani Morogoro jana.
Aliyekuwa kaimu Sheikh mkuu Suleiman Gorogosi enzi za uhai wake. Hapa ni mjini Dodoma katika moja ya sherehe za Maulid hivi karibuni kabla ya kifo chake kilichotokea leo mchana.

KAIMU SHEIKH MKUU WA TANZANIA AFARIKI DUNIA.

Aliyekuwa kaimu sheikh mkuu wa Bakwata mzee Suleiman Gorogosi amefariki dunia kwa ajali ya gari iliyotokea leo mchana (EastAfrican Time) akiwa njiani kwenda Lindi. Sheikh Gorogosi alikuwa akitokea Mtwara ambapo alikuwa amewasili muda mchache kwa ndege toka Dar es salaam, hata hivyo taarifa hiyo haikusema mzee Gorogosi alikuwa katika safari binafsi au ni ya kikazi na kama gari hilo lilikuwa ni binafsi au ni la jumuia (private car or public trasport). tutawaletea taarifa zaidi pindi zitakapo tufikia.

Friday, June 26, 2009

Michael Jackson Dies

Pop icon Michael Jackson has died after suffering from a cardiac arrest in the early afternoon of 25th June 2009.TMZ were the first to publish news of Jackson's death, hours before any other news body would risk confirming. It is said that Michael was already dead when paramedics arrived at his Holmby Hills home. He was rushed to UCLA Medical Center. More later.........

Thursday, June 25, 2009

Tanzania’s Power Utility to Spend $1.48 Billion to Boost Service

Tanzania Electric Supply Co. Ltd. Headquaters (Ubungo)
Tanzania Electric Supply Co. Ltd. will spend 1.95 trillion shillings ($1.48 billion) in the next five years to boost power supply in the East African country, the company said.
The Tanzanian government will contribute 289.6 billion shillings towards the program, the Millennium Challenge Corp. 280 billion shillings and the World Bank 243.4 billion shillings, while the utility will spend 652 billion shillings of its own funds, Tanesco spokman said in a report given out yesterday in the commercial capital, Dar es Salaam.

Msomaji
Dar es salaam

Thabeet grateful for opportunity

Wednesday, June 24, 2009

Thabeet, Kolikoli Tanzanians born set for NBA slots

Excitement has gripped the local basketball fraternity ahead of the National Basketball League Association (NBA) draft which will see Tanzanian duo Hasheem Thabeet and Martin Kolikoli competing with other budding stars for the NBA selection tonight.

The entire basketball family in the country of Tanzania was eagerly waiting for the draft to be conducted between 2:00 am to 7:00am (local time) at the Madison Square Garden in the USA.

“This is a historic moment for our country; it’s a very big thing….a very significant event for our country and for the sports sector than what most people think. We know even the President (Jakaya Kikwete) and the US embassy in Tanzania are waiting for it. “We don’t think if there’s any other athlete since Filbert Bayi in the 1970s who could match the success that could be attained by these two players.

NBA is the leading professional league in the world, in which players are paid bigger wages than professional footballers. If Thabeet and Koli both selected to join NBA the duo would completely change the face of the country, hence the need for them to grab with both hands the opportunity to impress. We urged local basketball players to follow in the path of Thabeet who has been a big hit in the US basketball College league,

“He has done it, and it’s up to young players to trace his course. “They need to work hard to get where he is, most often things don’t come on a silver platter. Thabeet could open the doors for other players from our country,”. Should Thabeet and Kolikoli excel in the draft they would become the first basketball players from Tanzania to play in the NBA.

NBA draft is an annual North American event in which the NBA’s thirty teams can select players who wish to join the league. Thabeet decided to forgo his senior season and declare for the 2009 NBA Draft on April 14 this year. He was named First Team All-American in 2008-09 by the NABC and the John R. Wooden Award.

He was the NABC National Defensive Player of the Year and BIG EAST Defensive Player of the Year in each of the past two seasons and was the 2008-09 BIG EAST Co-Player of the Year. He averaged 13.6 points, 10.8 rebounds and 4.2 blocked shots per game (No. 2 nationally) in 2008-09 and helped lead the Huskies the 2009 NCAA Final Four and a 31-5 final record.

As for Kolikoli, he has spent his career playing for Pazi Basketball Team. He is 6'2" tall and weighs 189 pounds. Last year he represented the country at the 2008 Basketball Without Borders Programme, held at American International School of Johannesburg and organized by the NBA and International Basketball Federation where he was among the outstanding performers.

KoliKoli comes from a family filled with basketball; his cousin Louis Charles Ngonyani played for Pazi for four seasons between 1994 and 1998 but stopped to focus more on studying. His other cousin David Wilbard Ngonyani is still an active player in the ACAMIS and ISAC league of Beijing, China

CCMMAREKANI WISH THEM ALL THE VERY BEST FOR THE FUTURE !!!!

Tuesday, June 23, 2009

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAKURUGENZI WA MAKAMPUNI YA SIMU ZA MIKONONI NCHINI

Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wakurugenzi watendaji wa simu za mikononi za Zantel, Tigo na Zain leo jijini Dar es salaam. Kutoka kushoto ni bwana Nabil Tofilis wa kampuni ya Zantel, Pablo Guardia Vasquez kapuni ya Tigo, Khaled Muhtadi kampuni ya Zain, na Rais Kikwete mwenyewe wakwanza kutoka mkono wa kulia.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ya Teknolojia ya Kompyuta – National Fibre Optic – unaojengwa nchini utakuwa na shabaha kuu ya kusukuma mbele maendeleo ya taifa.

Aidha, Rais Kikwete ameelekeza Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kukaa chini na makampuni binafsi ya simu nchini na kuangalia jinsi pande hizo zinavyoweza kushirikiana katika ujenzi wa mkongo huo utakaokuwa na urefu wa kilomita 7,000 ukisambaza mtandao wake katika nchi nzima.

Rais Kikwete ametoa maelekezo hayo leo, Jumanne, Juni 23, 2009 wakati alipokutana na kuzungumza na viongozi wa makampuni ya simu ya Tigo, Zantel na Zain, Ikulu, mjini Dar Es Salaam.

Rais Kikwete amesema Serikali yake inataka kuyashirikisha makampuni hayo katika ujenzi wa mkongo huo badala ya kila kampuni kufikiria kujenga njia yake yenyewe kwa sababu mkongo huo ni kwa manufaa ya pande zote.

Ujumbe huo ulionana na Rais Kikwete kumweleza nia ya makampuni hayo kutaka kushirikiana na Serikali katika ujenzi huo baada ya makampuni hayo kusita kwa muda mrefu kushirikiana na Serikali katika ujenzi wa mkongo huo.

Mkongo huo unalenga unalenga kuiwezesha teknolojia ya mawasiliano ya kompyuta kutumika kikamilifu na kwa ufanisi zaidi kwa maendeleo ya taifa.

"Yalikuwa maelekezo yangu na nia yangu tokea mwanzo kushirikisha wadau wote katika ujenzi wa mkongo huo kwa nia ya kupunguza mzigo kwa kila upande kwa sababu mkongo huo utatumiwa na sisi sote," amesema Rais na kuongeza:

"Hayo ndiyo yalikuwa maelekezo yangu kwa Wizara husika, lakini naona awali nyie mlisita kushirikiana na Serikali katika hili," amesisitiza Rais na kuongeza:

"Lakini sasa maadamu mko tayari basi kaeni chini ya wizara husika na kuangalia jinsi ya kukamilisha ujenzi wa mkongo huo."

Mkongo huo unatarajiwa kugharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 170. Serikali imeamua kuzikopa fedha hizo kutoka China ambayo imekubali kutoa mkopo huo.

Rais amewasisitizia viongozi hao wa simu za mkononi kuwa ni muhimu kwa Serikali kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa mkongo huo kwa sababu Serikali inataka mkongo huo utumike kwa ajili ya maendeleo ya taifa na siyo kwa ajili ya faida tu.
"
Tunataka mkongo huu utumike katika kuboresha huduma za elimu, huduma za afya, shughuli za utalii katika kila ncha ya nchi yetu, katika mikoa yote, iwe mijini ama vijijini.

Kwetu sisi ni wajibu wa kitaifa kwa sababu kwa Serikali nia yake kubwa ya kujenga mkongo huu ni kuhakikisha unatumika kwa maendeleo ya nchi." amesema JK.

Msomaji
Dar es salaam

Monday, June 22, 2009

WATAALAMU WAZUNGUMZIA UTATUZI WA MIGOGORO AFRIKA.

Mkurugenzi wa Taasisi ya amani na utatuzi wa migogoro barani Afrika (IPCS) Cosmas Bahali akifungua mafunzo ya kutunza amani barani Afrika(leo) katika ukumbi wa mikutano hoteli ya Beach Komba jijini Dar es Salaam.Washiriki kutoka nchi 19 barani Afrika wanashiriki mafunzo hayo yaliyofadhiriwa na serikali ya Norway.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kutunza amani barani Afrika wakifuatilia mafunzo yaliyoandaliwa na Taasisi ya amani na utatuzi wa migogoro barani Afrika (IPCS) yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano katika hoteli ya Beach Komba jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa mafunzo ya kutunza amani kutoka katika nchi 19 barani Afrika wakiwa katika picha ya pamoja nje ya ukumbi wa mikutano wa hotel ya Beach Komba jijini Dar es Salaam.

Msomaji
Dar es salaam

Sunday, June 21, 2009

Tanzania mbioni kufunga kambi zote za wakimbizi nchini


SHIRIKA la kimataifa la kuhudumia wakimbizi nchini (UNHCR) linajiandaa kufunga ofisi zake nchini baada ya wakimbizi wote kuondoka katika kambi za kuhifadhi wakimbizi.

Shirika hilo limefikia hatua hiyo baada ya zoezi la kurejesha wakimbizi katika nchi zao kuendelea vizuri.

Akizungumza na Mwaandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya siku ya wakimbizi dunia inayoadhimishwa Juni 20 kila mwaka Mwakilishi wa Shirika hilo nchini Yacoub El hillo alisema kambi hiyo itafungwa mara baada ya wakimbizi kuondoka.

Maadhisho hayo yatatanguliwa na matembezi yatakayoanzia viwanja vya Mnazi mmoja hadi ukumbi wa Kareem Jee na mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Laurence Masha.

Mwakilishi huyo wa UNHCR nchini alisema baada ya kambi zote kufungwa ofisi pamoja na vifaa vyote vya kuhudumia wakimbizi zitakabidhiwa serikali ya Tanzania.

Alisema kambi hizo zitafungwa kwa sababu suala la wakimbizi si la kudumu na wala haifahamiki ni lini wakimbizi watapatikana.

“Hatuwezi kuendelea na kambi hizi wakati wakimbizi wamerudi kwao wala hatuwezi kusema kwamba huo ndiyo mwisho wa kuhudumia wakimbizi kwa sababu suala la wakimbizi linatokana na vurugu za kisiasa hivyo siku ya kupatikana kwao haifahamiki”alisema El Hillo.

Alisema mwanzoni mwa mwaka 2007 kulikuwa na wakimbizi 300,000 kutoka Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na walihifadhiwa katika kambi 11 za Mikoa ya Kigoma na Kagera.

“Leo hii tumebakiza wakimbizi 100,000 wanaohifadhiwa kwenye kambi tatu Mkoani Kigoma ambazo ni Mtabila ambapo kuna wakimbizi wa Burundi, Lugufu na Nyarugusu zenye wakimbizi kutoka Congo” aliongeza El Hillo .

Kuhusu wakimbizi 220,000 waliokimbilia nchini mwaka 1972 na kuishi katika kambi za Ulyankulu, Katumba na mishamo katika mikoa ya Tabora na Rukwa, aliasema 40,000 kati yao walisaidiwa na UNHCR kurejea Burundi kwa hiyari mwaka 2008.

“Mbali na jitihada hizo za UNHCR kurejesha wakimbizi hao nchini Burundi tumeandaa mikakati ya kurejesha wakimbizi wengine 15,000 ifikapo Oktoba Mwaka huu" El Hillo aliendelea kufafa zidi.

Msomaji
Dar es salaam

Saturday, June 20, 2009

Kampeni zaendelea Biharamulo

Mgombea wa CCM Oscar Rwegasira Mukasa akiendeleza kampeni kwa wapiga kura katika Kijiji cha Mavota wilaya Biharamulo katika moja ya mikutano ya CCM ya kampeni kuwania kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Biharamulo Magharibi.

Msomaji
Biharamulo

President Obama hosted a BBQs Party for farther's Day weekend!!!

President Obama BBQs With The Fellas
President Obama hosted a Father’s Day Weekend BBQ at the White House yesterday afternoon. And he invited several celebrity fathers, influential men, and local teen boys over for some chit chat about the responsibility of men and fathers…and some BBQ.

Dwyane Wade, Alonzo Mourning, Etan Thomas, the President of Motorola, the President of Morehouse, and many other men were in attendance. And of course, the BBQ master himself Bobby Flay was there to get steaks and burgers poppin’ for everybody while Prez Obama served them up.

Tuesday, June 16, 2009

UN to assist Tanzania's general elections in 2010

The United Nations has offered to assist next year's general elections in Tanzania, the local daily the African reported on Tuesday.

The support of 23 million U.S. dollars from the UN is a complementary initiative to the on-going national efforts to plan and implement elections, the report quoted the statement released on Monday from the UN offices in Dar es Salaam as saying.

The Elections Support Project 2010 is expected to start to assist the National Electoral Commission (NEC) and the Zanzibar Electoral Commission (ZEC) and will continue until after the elections, expected in October 2010, according to the statement after the signing ceremony of the three parties of the UN, the NEC and the ZEC.

At the signing ceremony, UN Resident Coordinator Oscar Fernandez-Taranco made the introduction to the project, which will help the Commissions plan for and manage some technical needs of the elections process including voter registration, voter education, coordinating election observers and communications, the statement said.

Fernandez-Taranco quoted the statement as saying that the main goal is to further strengthen national capacities for the implementation of free, fair and credible elections with a focus on increasing the capacity of the NEC and ZEC as well as further engaging national stakeholders such as political parties, the media and other civil society actors.

The project will be managed directly by the United Nations Development Programme (UNDP). Funding for the projects is provided by the UNDP and other donor partners including Denmark, Finland, Netherlands, Norway, Sweden, Switzerland, Britain and the European Commission.

In Tanzania, general elections are organized in every five years whereby the President, the Members of Parliament and Councilors for local authorities are elected to public offices through a competitive electoral process that involve multi-party contests by the electorates.

President’s special offer message to Tanzania tourist sector

DAR ES SALAAM, Tanzania - Good news reached Tanzania tourism when President Jakaya Kikwete announced what could be a special offer to rescue the sector from the global falling economy.

In his public address last week, Mr. Kikwete said his government is taking serious measures to rescue Tanzania’s tourism sector, which has recorded a sharp drop in tourist arrivals due to global economic downturn.

He said between seven and 18 percent of tourists once planned to visit Tanzania canceled their trips while 20 to 30 percent of employees lost their jobs in the Indian Ocean tourist Island of Zanzibar.

Measures to be taken with immediate effect were the cutting down visa fees from US$100 to US$50 per a tourist entering Tanzania.

Cutting down or reviewing visa fees would make Tanzania compete with other African safari destinations including neighboring Kenya, which had slashed its visa fees to US$25 per a visitor.
Mr. Kikwete further said tourists who are currently looking at possible means to save money would look for alternative and cheap destinations to spend their holidays if Tanzania fails to review its entry visa regulations by cutting down the fees.

“A tourist would prefer to go where is cheap,” he said. “Tanzanian animals are similar to those in other African destinations, so no reason for a tourist to come here if finds our visa rates higher. We must review the fees to attract more tourists.”

He added, “Just imagine a tourist coming to Tanzania in a company of five children and think the amount of money he/she has to pay to get visas for all.

”Other measures in his SOS message to the tourist stakeholders including temporary taxation review to hotel operators and a two-year holiday for hotel operators with bank loans. This SOS will allow hotel proprietors holding bank loans to be exempted from bank interest from the amount they borrowed and extend the period to re-pay their loans for two more years under protection of the Tanzania government.

The Tanzania Association of Tour Operators (TATO) had earlier advised the government of Tanzania to review visa entry and park fees, at least, to give a relief to holiday makers visiting Tanzania’s premier tourist attractive sites.

Monday, June 15, 2009

BEI ZA MAFUTA ZAPANDA NCHINI TANZANIA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) Haruna Masebu akionyesha wandishi wa habari dokomenti ambayo inaonyesha namana walivyo jipanga kuthibiti uuzwaji wa mafuza kwa bei ya juu ambayo ni kinyume na taratibu.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) Haruna Masebu akifafanua jambo juu ya mwenendo wa bei za mafuta hapa nchini kwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali jana katika ofisi za mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (EWURA) Haruna Masebo amesema kuwa kutokana na biashara ya mafuta hapa nchini ni huria mamlaka imepewa jukumu la kufuatilia mwenendo wa biashra hiyo kwa karibu zaidi lengo kuu ni kujiridhisha kuwa nchi inakuwa na akiba ya ziada ya mafuta. Mafuta kwa sasa hivi yameanza kupanda bei kwa baadhi ya vituo. Azma ya EWURA ni kuhakikisha mafuta yanauzwa kwa bei ya kawaida kulingana na soko na kwa kutumia miundo mbinu salama hii inatokana na unyeti wa bidhaa za mafuta na umuhimu wake katika maendeleo.
Masebo alisema mwenendo wa bei za mafuta hapa nchini na katika soko la Dunia kwa kipindi cha mwezi Januari hadi juni 2009 bei za mafuta ya aina ya zote nchini zimekuwa za zikipanda japo si kwa kasi kubwa kama ilivyokuwa kwa mwaka jana. Kupanda kwa bei za mafuta kumetokana na sababu kuu mbili ambazo aalizitaja. Moja ni ongezeko la bei kununulia mafuta kwenye soko la dunia kwa Petroli bei imepanda asilimia 46.31,dizeli asilimia 11.98 na mafuta ya taa asilimia 6.42 katika kipindi cha kati ya mwezi Januari na mwishoni mwa mwezi Mei 2009. Mfumuko wa bei hapa nchini ni 13.3 %
Msomaji
Dar es salaam

Sunday, June 14, 2009

SERIKALI YATOA KIPAUMBELE ELIMU YA UTUNZAJI MAZINGIRA

Dk Batilda Buriani akizungumza katika moja ya mikutano mbalimbali aliyowahi kuhutubia kuhusa suala la mazingira.

Serikali imekuwa ikilipa umuhimu mkubwa suala la elimu kwa umma katika kufanikisha programu ya kuhifadhi na kutunza mazingira kwa kutekeleza programu nyingi za elimu ya mazingira kuanzia ngazi ya taifa hadi ngazi ya vijiji.

Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Dkt. Batilda Burian wakati akifungua kituo cha elimu na mafunzo ya Mazingira kilichojengwa na kampuni ya Glumeti Fundi kilichopo katika hifadhi ya Serengeti Mkoani Mara.

“Lengo la kutoa programu hizo ni kuielimisha jamii juu ya kuyaelewa mazingira wanayoishi, uhusiano wa shughuli zake za kila siku na ustawi wa mazingira hayo pamoja na kujadili uwiano wake”, alisema Dk. Batilda Burian.

“Grumeti Fund wamefikiria maendeleo ya vizazi vyetu vijavyo hivyo wameamua kuielisha jamii katika kujenga kituo hiki ili rasilimali ya ajabu na ya kipekee iliyopo katika Mbuga ya Serengeti pekee hapa Duniani isiweze kupotea” aliongeza Dk Batilda Buriani.

Akimkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Mstaafu Enos Mfuru alisema kuwa kampuni ya Glumeti Fundi imekuwa ikiwasaidia wananchi wa mkoa huo kwa kuwapatia huduma mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kujenga barabara, kuchimba visima na kutoa elimu kwa jamii

Akieleza nia ya kujengwa kwa kituo hicho Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa maendekeo ya jamii wa Grumeti Grian Harris alisema kuwa kituo cha mazingira ni uwekezaji katika rasilimaliwatu, yaani elimu ya vijana ambapo vijana kumi na wawili pamoja na walimu wao wawili watapata mafunzo kwa muda wa siku tano.

“Baada ya mafunzo ya nadharia na vitendo watakuwa wahamasishaji wa klabu za mali hai kwenye shule yao. Walimu waliioongozana nao watakuwa wasimamizi wao. Wanafunzi wataingia kila wiki na nyakati za likizo, tutaandaa utaratibu wa kuwafunza viongozi wa maeneo ya jirani na hifadhi ya akiba ya Grumeti”, alisema Harris.

Alisema,“Ili kuweza kuyaelewa, kuyakubali na kuishi maisha yanayodumisha mazingira endelevu na yenye tija elimu ni silaha muhimu sana. Kituo cha mazingira kitatoa mchango wake katika kufanikisha ndoto hii”,.Mkurugenzi huyo alimalizia kwa kusema kuwa , wanafunzi wengi kutoka wilaya ya Serengeti na Bunda wamenufaika na wanaendelea kunufaika kielimu kutokana na ufadhili wa Mfuko wa maendekeo ya jamii wa Grumeti.

Tunaahidi kuendelea kufanya hivyo kama sehemu ya wajibu wetu kwa jamii lakini pia kama njia ya endelevu ya kudumisha uhifadhi endelevu.Vijana watakaohudhuria mafunzo kwenye kituo hicho watateuliwa kulingana na ufanisi wao katika masomo yote lakini zaidi elimu viumbe, jiografia na kemia.

Kituo kitawapa changamoto, wakifanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho wachache watafadhiliwa kusomea utalii ama mazingira katika ngazi za vyuo.Gharama ya ujenzi wa kituo hicho ni Shilingi milioni mia nne kumi na mbili na laki tatu za kitanzania. Ikiwa ni gharama ya ujenzi na vifaa vyote katika kuwezesha kituo kiweze kuanza kufanya kazi.

Msomaji
Dar es salaam

WATAALAM KUTOKA JAPAN WALIVYOAGWA NA KAIMU KATIBU MKUU MENEJIMENTI YA UTUMISHI

Mmoja wa wataalamu wa kujitolea katika fani mbalimbali waliokuja nchini kutoka Japan Yuka Nakayama akifurahia Zawadi yake aliyokabidhiwa na Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma Mathias Kabunduguru baada ya kumaliza muda wa miaka miwili ya kujitolea nchini Tanzania.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma Mathias Kabunduguru akiongea na wataalam wa fani mbalimbali kutoka nchini Japan waliokuja nchini kujitolea.Wataalamu hao walikuwa wakijitolea katika nyanja mbalimbali za sayansi ikiwemo ualimu wa shule za sekondari,sekta ya afya, masuala ya jamii na fani za mawasiliano na wanatarajia kuondoka nchini tarehe 17 mwezi huu.

Msomaji
Dar es salaam

Friday, June 12, 2009

SALAAM KUTOKA KWA MSOMAJI WETU DAR ES SALAAM

Msomaji wetu wa dar amendelea kutuma salaam kwa watanzania wote waliopo nje na ndani ya nchi na anependa kwa wote waliopo nje ya jiji la dar es salaam wajionee jii kulivo kwa sasa. Pia amehaidi kuwa ataendele na utaratibu huu wa kuwatumia picha za jiji la dar hili mkumbuke nyumbani
BONYEZA KWENYE PICHA HILI UJIONEE VIZURI
Maeneo ya akiba karibu na makitaba kuu ya taifa
Maeneo ya Victoria karibu na makumbusho
Jengo la NMB
Hotel ya peacockJengo la wizara ya viwanda biashara na masoko
jngo la benki ya stanbick pale karibu na ulipokuwepo ubarozi wa Marekani zamani
Imala seko supermarket, mbezi beach tangi bovu
Alfa house
Jengo la kitega uchumi
Bustani Jiji ni dar es salaam
CCM nchini Marekani inatoa shukrani kwa niaba ya wasomaji na watanzania wote kwa ujumla

BAJETI YA TANZANIA 2009/10

Bajeti ya Serikali 2009/10.
Waziri wa Fedha na Mipango ya uchumi Mhe Mustafa Mkulo akiwasili bungeni kwa ajili ya kusoma bajeti. Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo akisoma bajeti bungeni.
Msomaji

WAZIRI BERNARD MEMBE AWASHUKURU MABALOZI

Waziri wa Mambo ya Nche na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe akiwashukuru mabalozi wanaofanya kazi hapa nchini wakati alipowaandalia chakula cha jioni katika ukumbi wa st Gasper Dodoma.
Baadhimya Mabalozi wanaofanya kazi hapa nchini wakimsikiliza Waziri wa Ushirikiano wa Mambo ya Nche na ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe wakati alipowaandalia chakula cha jioni katika ukumbi wa ST Gasper Mjini Dodoma baada ya kumaliza kusomwa kwa bajeti.
Red wine na mazungumzo yanaenda safi kabisa.

Msomaji

Wednesday, June 10, 2009

KESI ZA MAUAJI YA ALBINO ZIMEANZA KUSIKILIZWA

Wakili wa utetezi katika kesi ya mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) na vikongwe Bw. Feran Kweka akiongea na watuhumiwa kabla ya kuanza kwa kesi inayowakabili chini ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma Gadi Mjemas. Kikao hicho kimeaza juzi (Juni 8, 2009) mjini Shinyanga.Kesi za mauaji ya Ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi ama Albino zilianza jana katika mahakama kuu za kanda ya ziwa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi, Kesi hizo zinatarajiwa kusikilizwa mfululizo kwa siku 35.
Msomaji
Dar es salaam

Tuesday, June 9, 2009

HOTUBA YA RAIS JAKAYA KIKWETE WAKATI AKIWAHUTUBIA WANANCHI WA DODOMA, NA WABUNGE KWENYE UKUMBI WA KILIMANI,

JK akihutubia katika ukumbi wa Kilimani Dodoma
Waheshimiwa Wabunge;
Ndugu wananchi;
Nawashukuru kwa dhati wazee wangu, Waheshimiwa Wabunge na wananchi wenzangu wa Dodoma, kwa kuitikia wito wangu wa kuja kukutana na kuzungumza nanyi. Nakushukuru Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa na Katibu wa Baraza la Wazee kwa maandalizi mazuri.

Mara kadhaa katika hotuba zangu za siku za nyuma, nimekuwa nikielezea jinsi ambavyo uchumi wa dunia unavyopita katika misukosuko mikubwa na jinsi ambavyo mtikisiko huo unavyoweza kuathiri uchumi wetu pia. Tayari athari zake tumezipata na tunaendelea kuathirika nazo.

Nilifanya uamuzi siku za nyuma wa kuunda kikundi kazi chawatalaam chini ya uongozi wa Gavana wa Benki Kuu, Profesa Benno Ndulu, kufanya uchambuzi wa hali ilivyo ili kubaini athari tulizopata na kushauri hatua za kunusuru uchumi wetu na kujenga uwezo wa kujihami na kukuza uchumi.

Ndugu Wananchi;Wenzetu hao wamemaliza kazi yao na taarifa yao imeshajadiliwa na Baraza la Mawaziri na maamuzi kufanywa. Matokeo yake ni kuwepo kwa mkakati wa Kunusuru Uchumi wa Tanzania dhidi ya Msukosuko wa Uchumi wa Duniani. Katika mkakati huo mpango wa utekelezaji wa malengo na hatua mbalimbali za kuchukua zimeanishwa.


Mtikisiko Katika Mfumo wa Fedha Duniani
Ndugu Wananchi;
Uchumi wa dunia unakabiliwa na matatizo makubwa sana ambayo hayajawahi kutokea kwa zaidi ya miaka 60. Mara ya mwisho uchumi wa dunia ulikuwa na matatizo makubwa katika miaka 1930 lakini nayo hayakuwa makubwa kama ilivyo safari hii. Matatizo ya uchumi wa dunia yana sura mbili. Upande mmoja lipo tatizo la kuvurugika kwa masoko na mfumo wa fedha wa kimataifa. Na, upande wa pili kudorora kwa uchumi wa duniakulikosababishwa na kuanguka kwa masoko ya fedha na mitaji.

Tatizo hili limeanzia Marekani kutokana na udhaifu katika usimamizi wa mfumo wa fedha na hasa mikopo. Baadae ukaenea Ulaya Magharibi na hatimaye dunia nzima na siye tukiwemo. Kiwango cha athari kinatofautiana kutoka nchi moja na nyingine. Mataifa makubwa kiuchumi ya Marekani, Ulaya na Asia yameathirika zaidi kuliko nchi maskini za Afrika. Hata hivyo, mataifa makubwa yana uwezo mkubwa zaidi wa kukabiliana na athari hizo pamoja na ukubwa wake.

Mataifa maskini kama yetu hayana uwezo wa kukabiliana hata na hizi athari ndogo zinazotukabili. Kinachoonekana kidogo kwao, kwetu sisi ni kikubwa.Mabenki mengi, makubwa kwa madogo, na asasi za fedha kubwa na ndogo katika mataifa tajiri zimeshashuhudiwa zikianguka kibiashara au kufilisika. Masoko ya hisa na mitaji nayo hivyo hivyo yameanguka kwa kiasi ambacho hakijawahi kufikiwa.

Makampuni mengi madogo na makubwa yameanguka. Watu wengi wenye hisa wamejikuta wakiharibikiwa na hata kuwa maskini bila kutazamia. Makampuni mengi yameanguka kibiashara na kufilisika. Watu wamepoteza ajira kwamamilioni na wengi wamepoteza nyumba na mali walizozipata kwa mikopo kwa sababu ya kushindwa kulipa mikopo. Kwa ujumla hali ya kiuchumi na kimaisha katika nchi hizo ni ngumu kwa makampuni mengi na watu wengi.

Kutokana na hali hii, uwekezaji umepungua, biashara ya ndani na nje imeshuka, uzalishaji viwandani umepungua sana na kwingine umesimama, makampuni madogo na hata makubwa na yenye heshima yamefilisika, ununuzi wa bidhaa umepungua, watu kwa mamilioni wakakosa ajira katika nchi kubwa kiuchumi. Athari hizo bado zinaendelea na matokeo yake ni kuzorota kwa ukuaji wa uchumi wa mataifa hayo makubwa na uchumi wa dunia kwa ujumla.

Mwaka 2008, uchumi wa nchi hizi ulikua kwa asilimia 0.9. na mwaka huu inatarajiwa utapungua kwa asilimia 3.8. Hali hii imezilazimisha Serikali za nchi hizo kuingilia kati na kutumia fedha za Serikali kuokoa makampuni binafsi, kinyume kabisa na falsafa ya soko huria.
Vilevile, Serikali za nchi hizo zikalazimika kukopa fedha nyingi kwa ajili ya miradi mingi mikubwa ili kuchochea shughuli za kiuchumi.


Athari kwa Tanzania
Ndugu Wananchi,
Kwa upande wetu hapa nchini mabenki yetu yako salama kwa vile hatujafungamanishwa na masoko ya fedha ya kimataifa. Lakini, kibiashara na baadhi ya shughuli za kiuchumi, tumeathirika hasa zile zinazotegemea masoko ya kimataifa hususan ya mataifa tajiri ya Marekani, Ulaya na Asia.

Athari kubwa ya kwanza ni ile ya kupungua kwa bei na masoko ya bidhaa zetu tunazouza nje ya nchi hususan mazao ya kilimo, madini na bidhaa za viwandani. Kadhalika, sekta ya utalii nayo imeathirika na kupungua kwawatalii wanaokuja nchini. Vilevile uwekezaji wa kutoka nje umepungua.Kwa upande wa mauzo ya mazao ya kilimo napenda nitoe mifano ya pamba, kahawa na hata maua na karafuu.

Kwa pamba, kwa kipindi kifupi cha miezi minne kuanzia Septemba2008 bei ya pamba ilianguka kutoka senti 82 za dola kwa paundi moja mpaka senti 40. Hivyo pamba iliyonunuliwa kwa bei ya juu toka kwa wakulima, ghafla ilibidi iuzwe kwa bei ya chini na nyingine kukosa soko kabisa.
hadi mwezi Aprili 2009 marobota 124,344 ya pamba yalikuwa bado hayajauzwa.

Inakadiriwa kuwa hasara iliyopatikana kwa kuuzapamba nje kwa bei chini ya bei ya kununulia ni kadiri ya shilingi bilioni 15 na 18. Unapochanganya tatizo hili na lile la pamba kutokuuzwa, shilingi bilioni 93.6 zilizokopeshwa na CRDB peke yake (bila kujumuisha riba) hazijarejeshwa. Kati ya madeni hayo, shilingi bilioni 4.6 ni ya vyama vya ushirika na TSh bilioni 81.9 ni ya makampuni 24 makubwa yanayofanya biashara ya pamba.

Vilevile, kwa upande wa zao la kahawa, kutoka mwezi Oktoba, 2008 bei zilianzakushuka kutoka wastani wa US$ 140 kwa gunia la Arabica hadi wastani wa US$ 104.21. Robusta nayo ilishuka toka wastani wa US$ 91 kwa gunia hadi dola za Marekani 64 ilipofika mwezi Machi 2009, ikiwa ni anguko la bei la asilimia 26 kwa Arabica na asilimia 29 kwa Robusta. Kahawa iliyokumbwa na msukosuko huo ni kiasi cha kilo 26,645,439 za Arabica zenye thamani ya US$ 55,536,099 na kilo 11,981,710 za Robusta zenye thamani ya US$ 15,469,353.

Kutokana na bei za kununulia kahawa hizo kwa mkulima (farm gate price) kuwa za juu kuliko ile ya kuuzia kwenye soko la dunia, vyama vya ushirika vya kahawa na wafanyabiashara walionunua kahawa wamepata hasara inayokadiriwa kuwa TSh bilioni 4.85.

Ndugu Wananchi;
Hasara waipatayo wanunuzi na ugumu waupatao kuuza mazao yao kunasababisha washindwe kulipa madeni yao Benki na kuwaweka kwenye hatari ya kufilisiwa mali zao walizoweka dhamana. Aidha, kwa ukubwa wa mikopo ambayo haijalipwa na ambayo huenda isilipwe itayafanya mabenki yaliyokopesha kupata hasara. Pia mabenki hayo yanaweza kukataakuwakopesha wanunuzi wa mazao na kusababisha mgogoro mwingine mkubwa wa mazao ya wakulima kutokununuliwa msimu ujao. Jambo hilo likitokea litafanya wakulima kula hasara na kuwa maskini zaidi. Shabaha ya mkakati wetu ni kumpunguzia mnunuzi mzigo wa hasara na madeni, kuiepusha benki na hasara na kuwezesha mazao ya mkulima kuendelea kununuliwa.

Kwa upande wa kilimo cha maua na mboga mambo ni hayo hayo. Bei imeshuka kwa asilimia 25 na mauzo yamepungua kwa sababu mahitaji katika masoko ya nje yamepungua kutokana na hali mbaya ya uchumi katika nchi hizo. Kuna hatari kwamba wakulima wa maua watashindwa kulipa mikopo ya mabenki ya Tshs. bilioni 43.4, ajira za watu zitapotea (tayari Mount Meru Flowers imepunguza watumishi 36). Sekta hii inaajiri watu 3,000 na wengi wao ni wanawake. Ni dhamira yetu pia hapa kuwanusuru wakulima, mabenki na ajira.

Madini
Ndugu Wananchi;
Hali ni mbaya pia kwa upande wa bei na masoko ya vito hasa almasi na Tanzanite. Bei ya Tanzanite imeshuka kwa asilimia hamsini na kufikia US$200 kwa karati. Bei ya almasi imeshuka kwa asilimia 26 na kuwa US$8,870 mwezi Septemba. Wachimbaji na wanunuzi wa almasi, Tanzanite na vito vinginevyo wanakabiliwa na tatizo kubwa la madini ambayo wanapata taabu kuyauza.Bahati nzuri dhahabu haina matatizo hayo. Soko lake ni zuri na bei ni nzuri sana.

Mkakati wetu unalenga namna ya kuwasaidia wachimbaji wa vito ambao tusipowasaidia wao na serikali tutaendelea kukosa mapato na wakati huo watu wengine watakosa ajira kwa sababu ya shughuli za uchimbaji kupungua.


Viwanda na Utalii
Ndugu Wananchi;
Viwanda vyetu navyo hasa vya nguo, nyuzi, mavazi na vile vya ngozi vimeathirika na msukosuko wa uchumi wa dunia. Mauzo nje yamepungua sana na kusababisha hasara kubwa. Uzalishaji umepungua, ajira nazo hali kadhalika. Sekta ya Utalii ambayo ndiyo sekta kiongozi kwa mapato ya fedha za kigeni nayo imebanwa pia.

Idadi ya Watalii wanaokuja nchini inapungua. Takwimu zinaonyeshaidadi hiyo kupungua kwa asilimia 10. Mapato yatokanayo na utalii ya mwezi Januari – Aprili, 2009 nayo yamepungua na kufikia US$302.1 kutoka US$388.2 milioni mwaka 2008. Hali hiyo inaathari kubwa kwa wawekezaji na kwa mapato ya Serikali na fedha za kigeni hivyo nayo tumeipa uzito stahiki katika mkakati wa kunusuru uchumi.

Mapato ya Ndani
Ndugu wananchi,
Kutokana na matatizo ya kupungua mauzo nje, utalii, uwekezaji n.k mapato ya ndani ya Serikali nayo yameathirika. Sasa hivi, tunakusanya mapato kutoka ushuru wa forodha, kodi za ndani n.k yako chini ya kiwango tulichotarajia. Kama mwenendo wa makusanyo ya kodi utaendelea kama ulivyo sasa, makusanyo ya kodi kwa mwaka 2008/09 yatakuwa chini ya makadirio ya bajeti kwa asilimia 10. Kwa maneno mengine, tutashindwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 472.9 ambazo matumizi yake tulishayapangia kwenye bajeti.

Katika mkakati huo tumeweka mipango ya kuikabili hali hiyo katika mwaka huu wa fedha na mwaka ujao pia ambapo tunadhani athari zitakuwepo au hata kuzidi.

Mapato ya Fedha za Kigeni
Ndugu Wananchi;
Kwa sababu ya kupungua kwa mauzo ya mazao yetu nje, mapato yetu ya fedha za kigeni yatapungua pia. Inakadiriwa kuwa thamani ya mauzo nje itapungua kutoka US$ 2,891 milioni mwaka 2008/09 hadi US$2,860 milioni mwaka 2009/10.
Wakati huo huo mapato ya fedha za kigeni kutokana na utalii yatapungua kwa US$ 186 milioni. Katika mkakati wetu tunayo mipango ya kuziba pengo hilo ili kuepuka matatizo ya upatikanaji wa fedha za kigeni kwa ajili ya manunuzi yetu ya


Uwekezaji kutoka nje
Ndugu Wananchi;
Kwa sababu ya matatizo ya uchumi uwekezaji wa vitega uchumi kutoka nje umepungua. Wawekezaji wamekuwa wanakosa fedha kutoka mabenki na masoko ya mitaji. Matokeo yake ni kuchelewa au kukosa kabisa au kuahirishwa miradi mikubwa ambayo ingetoa mchango muhimu kwa ukuaji wa uchumi wetu na ajira.

Kwa mfano: Mradi wa umeme wa MW 300 kule Mtwara kwa sababu ya Barrick Gold Ltd. kujitoa na Artumas peke yake haina uwezo wa kifedha; mradi wa nickel Kabanga, mradi wa aluminium smelter, Mtwara; mradi wa usambazaji umeme mkoani Mtwara, miradi ya viwanda vya saruji na mbolea Mtwara na uwekezaji katika utafutaji wa madini umepungua kutoka US$90 mpakaUS$40 milioni.

Ajira
Ndugu Wananchi;
Hali ya ajira nchini nayo itakuwa mbaya kutokana na matatizo haya. Mwaka 2009 ni mwaka ambao athari za msukosuko zimeanza kujitokeza kwa nguvu katika masoko ya ajira na kusababisha watu wengi kupoteza kazi na hivyo kuongeza umas wa kipato.
Hadi kufikia Aprili 2009 jumla ya wafanyakazi 48,000 walikuwa wamepoteza ajira zao nchini. Kutokana na kutarajiwa kupungua kwa idadi ya watalii wanaokuja nchini, baadhi ya hoteli zilizotarajiwa kuwapokea watalii hao zimelazimika kupunguza wafanyakazi wao kutokana na kupungua kwa biashara. Kati ya asilimia 20-30 za ajira katika sekta ya utalii Zanzíbar ziko hatarini kupotea kutokana na upungufu wa utalii. Vivyo hivyo, katika sekta ya kilimo, viwanda na madini, watu wengine wanatarajiwa kupoteza kazi zao.

Kupungua kwa ukuaji wa uchumi

Waheshimiwa Wabunge,
Ndugu Wananchi,
Matokeo ya athari zote hizi ni kupungua kwa kasi ya ukuaji wa uchumi nchini. Kama mjuavyo, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, uchumi wetu umekuwa ukikua kwa kiwango cha juu cha wastani wa asilimia 7.2. Tulitegemea mwaka huu uchumi wetu ungekuwa kwa zaidi ya asilimia 8 na kufikia asilimia 10 mwaka 2010 kama tulivyoahidi kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2005.

Lakini kama wasemavyo Waswahili, ng’ombe wa maskini hazai. Msukosuko wa fedha na uchumi duniani umesababisha ukuaji wa uchumi wa Tanzania kupungua kutoka asilimia 7.4 mwaka jana hadi kati ya asilimia 5-6 mwakahuu. Kwa upande wa Zanzibar, uchumi wao unategemewa kukua kwa asilimia 4.5 mwaka huu ukilinganisha na asilimia 5.4 mwaka jana.

Mkakati wa Kuhami na Kuunusuru Uchumi
Ndugu Wananchi;
Baada ya kutafakari hali hii, na kuchambua athari hizi nilizobainisha kwa uchumi, ustawi na mipango ya muda mrefu ya maendeleo ya Taifa letu, na kwa kuzingatia azma yangu niliyoitangaza kwenye salamu ya mwaka mpya wa 2009, kwamba mwaka huu ni mwaka wa kuhami na kukuza uchumi, tumebuni na tutatekeleza Mkakati Maalum wa Kuhami na Kuunusuru Uchumi wa Tanzania.
Mkakati huu unazingatia ukweli kuwa msukosuko wa uchumi duniani ni wa kupita. Changamoto ya muda mfupi ni jinsi ya kujinusuru na hatimaye kudumisha juhudi za maendeleo baada ya msukosuko kupita.
Katika kukabili athari hizi nilizozitaja, tunalenga mambo mawili makuu. Kwanza ni kupunguza makali ya msukosuko, na pili, kulinda uwekezaji ambao ni muhimu katika kudumisha ukuaji endelevu wa uchumi katika kipindi cha muda wa kati. Mkakati wetu wa kuhami na kuunusuru uchumi unalenga kukabili matatizo ya mpito na dharura – hasa ya ukwasi (liquidity) na siyo ufilisi (solvency).
Mkakati huu sio mbadala wa mipango ya maendeleo na bajeti ya Serikali ya kila mwaka. Chini ya mkakati huu Serikali imepima matatizo kwa uzito wake na kushughulikia yale tu yaliyojitokeza hivi karibuni kutokana na msukosuko wa uchumi na siyo vinginevyo.
Ndugu Wananchi;
Tumetengeneza Mkakati huu kutimiza malengo makubwa manne:1. Kulinda ajira na vipato vya wananchi;2. Kuhakikisha upatikanaji wa chakula;3. Kulinda uwekezaji muhimu katika miradi ya maendeleo, hususan miundombinu, na4. Kulinda programu muhimu za kijamii
Ndugu Wananchi;
Kama nilivyosema, lengo kuu la kwanza la mkakati huu ni kupunguza makali au kuhimili shinikizo la msukosuko, hususan kuwalinda wananchi walio katika hatari kubwa zaidi ya kimaisha. Katika kutekeleza hili lengo yako mambo kadhaa ambayo tutayafanya:
(i) Kufidia hasara waliyopata wanunuzi wa mazao msimu wa 2008/09Serikali imeamua kufidia vyama vya ushirika na makampuni yaliyonunua mazao ya wakulima na kuyauza kwa hasara. Hasara hiyo inayokisiwa kufikia shilingi 21.9 bilioni imepatikana kutokana na bei ya kuuzia mazao hayo kuwa chini sana ya gharama iliyotumika kuyanunua. Serikali italipa madeni yenye thamani ya hasara hiyo, moja kwa moja kwa mabenki yaliyokopesha vyama na makampuni hayo. Lakini tutafanya uhakiki kabla ya kulipa. Napenda kusisitiza kuwa hatutalipa madeni ya zamani ambayo hayahusiki na msukosuko wa uchumi wa dunia.

(ii) Kutoa udhamini wa kuahirisha mikopo ya waathirikaYapo madeni ambayo wakopaji kwa sababu ya msukosuko wa uchumi wa dunia wanapata matatizo kulipa kwa wakati. Kundi hili linawajumuisha wengi wenye viwanda, wenye shughuli za utalii, kilimo n.k. Madeni hayo yanafikia Shs.270 bilioni. Serikali itayadhamini madeni na kuyataka mabenki kuahirisha ulipaji wa mikopo hiyo na riba yake wa miaka miwili.
Udhamini wa Serikali utatolewa kwa uwiano wa kila shilingi moja kwa shilingi tano na Serikali ikidhamini asilimia 70 ya mkopo. Kwa uwiano huu, fedha zitakazohitajika katika dhamana hiyo ni TSh 45 bilioni. Pamoja na kutoa nafuu kwa makampuni lakini hatua hii pia itayawezesha mabenki kuendelea kutoa mikopo na hivyo shughuli za kiuchumi na biashara hazitaisimama.
(iii) Kutoa mitaji ya uendeshaji (working capital) kwa riba nafuuTumeamua vilevile kuchukua hatua za kupunguza upungufu wa mitaji ya uendeshaji (working capital).

Kwa ajili hiyo Serikali itayakopesha mabenki fedha kwa riba nafuu ya asilimia 2 ili na wao wawakopeshe wafanyabiashara fedha za mitaji ya uendeshaji kwa riba nafuu.

Lengo ni kusaidia walioko kwenye sekta zinazokumbwa na msukosuko wa uchumi waweze kuhimili vishindo. Kwa kila shilingi moja tutakayotoa sisi Serikali, benki husika itatakiwa itoe shilingi moja na nusu (1:1½).

Kwa madhumuni haya, tutaanzisha mfuko maalumu wenye shilingi bilioni 80 ambao utasimamiwa na Benki Kuu na mabenki yatakayoshiriki yatatakiwa kutoa shilingi 120 bilioni. Viwango vya riba kwa wakopaji vitapangwa kwa maelewano ya pamoja baina ya BoT na mabenki na itategemea sekta na shughuli yenyewe.

(iv) Kuboresha Mifuko ya Dhamana:
Chini ya mkakati huu tutaiboresha na kuiongezea fedha mifuko ya kudhamini mikopo (credit guarantee schemes). Mifuko hiyo ni pamoja na Mfuko wa Udhamini wa Uuzaji wa Mazao Nje ya Nchi (Export Credit Guarantee Scheme -ECGS) na Mfuko wa Udhamini wa Mikopo kwa Wajasiliamali Wadogo na wa Kati (SME Credit Guarantee Scheme).
Tutaongeza mtaji wa shilingi bilioni 10 kwa kila mfuko katika mwaka wa fedha wa 2009/10. Nyongeza hii itawezesha kuongeza dhamana ya mikopo ya shilingi bilioni 65 kwenye Mfuko wa Udhamini wa Uuzaji wa Mazao Nje ya Nchi na shilingi bilioni 60 kwenye Mfuko wa Udhamini wa Mikopo kwa Wajasiliamali Wadogo na wa Kati katika kuchochea mauzo ya bidhaa nje na uzalishaji. Hivi sasa mfuko wa ECGS una mtaji wa Shs.32.5 bilioni na umekopesha Shs.161.5 bilioni na ule wa SME una Shs.500 milioni na umeshakopesha Shs.6.5 bilioni.
(v) Kupunguza gharama za vito vya thamani:
Katika sekta ya vito vilivyoshuka bei kwa kiasi kikubwa, kama vile Tanzanite na almasi, tunaangalia uwezekano wa kuahirisha ulipaji wa mrahaba (royalty) kwa wachimbaji wa vito. Lengo ni kuwapa muda wa kupumua na kujijenga. Chini ya mpango huu Serikali itaahirisha mapato ya kiasi cha US$ milioni 0.5 kutoka almasi na US$ milioni 2.5 kutoka tanzanite.
(vi) Kuongeza uzalishaji wa Chakula
Ndugu Wananchi;Lengo lingine muhimu la mkakati huu ni kuinusuru nchi kutokana na athari za upungufu wa chakula duniani zilizochochewa na msukosuko. Katika kutekeleza hili, mkakati huu utahakikisha kuwa miradi yote ya kilimo, hususan ile ya uzalishaji wa mazao ya chakula, inaendelea kugharimiwa bila kuathiriwa na msukosuko. Lengo la kwanza ni kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula ili kujitosheleza kwa chakula na kuuza ziada nje na hivyo kutumia ipasavyo fursa inayotokana na kuadimika kwa chakula duniani.

Chini ya mkakati huu, pamoja na kuendelea kuhimiza na kusimamia yale mambo yote ya kuongeza tija na uzalishaji kwenye kilimo, tumeamua katika kipindi hiki kufanya yafuatayo:
(i) kutoa mikopo nafuu na ya muda mrefu ya shilingi 20 bilioni kupitiaTIB kwa sekta binafsi kwa ajili ya kuendeleza kilimo
(ii) kutoa shilingi bilioni 20 kwa ajili ya mkopo wa riba nafuu kwa zana za kilimo kama matrekta madogo kupitia mpango wa karadha (lease finance), ambapo, kwa kila shilingi ambayo serikali itatoa, mabenki yatakayoshiriki katika mkakati huu itabidi nayo yatoe shilingi moja: na
(iii) Kuongeza kiasi na idadi ya wakulima watakaopata mbolea ya ruzuku kwa utaratibu wa vocha. Benki ya Dunia watatupa mkopo wa US$46 milioni na sisi tutatoa kiasi hicho hicho kwenye mfuko wa mbolea katika mwaka ujao wa fedha (2009/10).
Aidha tumeamua sasa tutumie Hifadhi ya Chakula ya Taifa kusaidia kutuliza bei za vyakula kwa walaji. Tunaiboresha sera ya sasa ambapo Hifadhi hungojea ilani ya njaa. Tumesema kupanda sana kwa bei za vyakula vikuu katika soko ni dalili ya upungufu hivyo kupunguza makali kila inapowezekana.
Chini ya mkakati huu, tutatoa shilingi bilioni 20 kwa Hifadhi ya Chakula ya Taifa kwa ajili ya kuongeza akiba ya chakula na kudhibiti mfumuko wa bei.

Miundombinu

Ndugu Wananchi,
Kuhusu lengo la kulinda uwekezaji muhimu, hasa katika miundombinu, ya umeme na reli tumekubaliana kuwa tuendeleze juhudi za kutafuta mikopo kutoka Benki ya Dunia na mashirika mengine ya fedha. Kwa ajili hiyo tutatumia fedha za IMF kukwamua mradi wa usambazaji umeme Mtwara. Zinatakiwa US$ 7 milioni.
Kuhusu Shirika la Reli, sisi tuchangie sehemu yetu, yaani US$43 milioni, kuongezea US$ 40milioni za Benki ya Dunia kuimarisha reli yetu. Wakati huo suala la uendeshaji tulitafutie jawabu muafaka.
Kadhalika tumekubaliana kuwa taendelee kuwekeza katika ujenzi wa barabara na miradi ya elimu, afya na maji. Suala la hati-fungani ambalo liliahirishwa kwa sababu ya matatizo ya soko la fedha tulitafutie vyanzo mbadala.
Ndugu Wananchi;
Tumekubaliana pia katika mkakati huu, kuwa lazima kuhakikisha kuwa utulivu wa uchumi unakuwepo ili kuhimiza ukuaji endelevu wa uchumi na kuvutia sekta binafsi kushiriki. Vilevile tuongeze kasi ya kuharakisha uimarishaji wa TIB na uanzishwaji wa Agricultural Development Bank.
Ndugu Wananchi;
Kuhusu lengo la Mkakati la kulinda programu muhimu za kijamii, Serikaliitahakikisha kuwa mipango yote ya kijamii haitaathirika, hata ile ambayo itakosa fedha za kutosha kutoka kwa wafadhili. Hii inajumuisha mipango ya utoaji wa ruzuku kwa dawa za kurefusha maisha kwa wagonjwa wa UKIMWI, vyandarua vya kuzuia malaria, programu za kifua kikuu, na nyingine za kusaidia juhudi za vijana na kulinda makundi ya wanyonge.
Ndugu Wananchi;
Pia zipo hatua kadhaa nyingine za kisera ambazo Serikali inaziandaa katikakukabiliana na athari za msukosuko huu. Katika miezi inayokuja, Wizara mbalimbali zitatangaza hatua za kisera zenye nia ya kuzihami sekta hizo na athari hizi na kuchochea ukuaji wa sekta mbalimbali kama vile utalii na viwanda.
Miongoni mwa hatua tunazoziandaa sasa ni kupunguza gharama za visa kwa watalii kutoka dola 100 na 200 na kuwa dola 50. hazina inaangalia uwezekano wa kufanya hivyo.

Hitimisho

Ndugu Wananchi,
Sasa nimefika mwisho wa hotuba yangu. Nawashukuru tena kwa kukubali wito wangu. Kwa nchi yetu ambayo bado ina safari ndefu katika maendeleo, hatua tuliyochukua hapa ni kubwa na ya kihistoria.
Katika kuchukua hatua hii, tumezingatia mahitaji ya dhamana tuliyopewa na wananchi katika kuwaongoza na kusimamia maendeleo na ustawi wao na wanchi yetu. Lakini vilevile, tumezingatia mafundisho ambayo historia ya nchi yetu imetupatia.
Kwa mkakati huu, tumedhamiria kuepuka hali iliyojitokeza miaka ya 1980 ambapo kutokana na kushindwa kukabili kwa dhati na wakati muafaka, athari za kupanda kwa bei za mafuta na hali mbaya ya uchumi wa dunia iliyofuatia, zilisababisha nchi kupoteza miongo miwili ya ukuaji wa uchumi na mafanikio yaliyokuwa yamepatikana katika nyanja za jamii na miundombinu.
Mwisho kabisa,
Nawasihi viongozi wenzangu na wananchi kwa ujumla, tuwe wavumilivu na tuiunge mkono Serikali katika kutekeleza mkakati huu. Tangu mwaka 2006, mambo hayakuwa mepesi sana, tumepitia misukosuko mikubwa kwa uchumi wetu: mgao mkubwa wa umeme, njaa, bei kubwa ya mafuta na bei kubwa za vyakula na sasa msukosuko huu wa aina yake. Kwa kila tatizo tumepambana nalo kiume na kwa umakini mkubwa na kuvukasalama. Mshikamano wetu, umoja wetu ndiyo uliotufikisha hapo.
Napenda kuwahakikishia wananchi wa Tanzania kwamba Serikali yao inawajali na inafanya kila lililo ndani ya uwezo wake kutimiza wajibu wake katika kuwatumikia. Sisi katika Serikali tupo kwa ajili yenu na tutaendelea kuwatumikia kwa nguvu zetu zote. Tutaendelea kutengeneza mipango na mikakati ya kukabiliana na matatizo na changamoto zinazowakabili wananchi wa
Tanzania walioko katika kila kona ya nchiyetu.

Tuliyaweza yale naamini na haya tutayamudu!!
Asanteni sana kwa kunisikiliza!
Mungu Ibariki Afrika!
Mungu Ibariki Tanzania!

Maandamano Makubwa yafanyika Mkoani Iringa ya kumpongeza Rais Jakaya Kikwete

Umoja wa Vijana-CCM mkoa wa Iringa wanakubali kuwa mkoa huo una imani na Rais Jakaya Kikwete na unamtaka kuendelea kuwa mgombea pekee kwa mwaka 2010 kutokana na kuonyesha uwezo mkubwa wa kiutendaji nje na ndani ya nchi
Mkuu wa mkoa wa Iringa Bw Mohamed Abdulaziz(katikati )akiwa na kamanda wa umoja wa vijana mkoa wa Iringa Salim Abri Asas(kushoto), na mwenyekiti wa umoja huo mkoani Iringa Bw Fadhil Ngajilo (Kulia).

Msomaji
Iringa

Rais Kikwete apata mwaliko wa Kutembele nchi ya Cuba

Barozi wa Cuba Nchini Tanzania Mh.Ernesto Gomezi Diaz akimkabidhi rasmi Rais Jakaya Kikwete (Ikulu jijini Dar es salaam) mwaliko wa kutembelea nchi ya Cuba. Rais Kikwete alikubali mwaliko huo na kumwahidi barozi huyo kuwa tarehe na maandalizi ya kutembelea nchi hiyo yatafanywa Mapema iwezekanavyo

Msomaji

Monday, June 8, 2009

Mama Kikwete achangia shilingi Milioni Mbili Kwaya ya Mtakatifu Kizito, Makuburi, Ubungo

Mtoto Rayness Venance(5) kutoka katika parokia ya Mwenyeheri Anwarite, Ubungo Makuburi akimkaribisha kwa Maua Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati alipowasili katika parokia hiyo kuongoza sherehe za kuadhimisha miaka ishirini(20) ya kwaya ya Mtakatifu Kizito.sherehe hizo zilifanyika jana(Jumapili) ambapo Mama Salma kupitia taasisi yake ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) alichangia kwaya ya Mtakatifu Kizito jumla ya shilingi milioni mbili
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiagana na wanaparokia wa Mwenyeheri Anwarite,Makuburi, Ubungo bada ya kuongoza sherehe za kuadhimisha miaka ishirini tangu ilipoanzishwa Kwaya ya Mtakatifu Kizito jana jumapili mchana

Msomaji
Dar es salaam

Thursday, June 4, 2009

RAIS JAKAYA KIKWETE AKIZINDUA KIVUKO CHA MV MAGOGONI

Hiki ndiyo kivuko cha MV Magogoni kilichozinduliwa leo na Rais jakaya Mrisho Kikwete
Rais jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kama ishara ya kuzindua kivuko cha MV Magogoni Tayari kwa kuanza Rasmi kazi ya kuvusha abiria na mizigo kati ya Kigamboni na Posta, Kivuko hicho kilianza kujengwa mwaka 2007 na kilikamilika mwaka 2008 kina uwezo wa kubeba tani 500, ujenzi wake umegharimu jumla ya shilingi za kitanzania bilioni 8.3 huku kikiwa na Uwezo wa kuchukua watu 2000 na magari 60, katika picha kushoto ni Waziri wa Wizara ya Miundombinu Mh. Shukuru Kawambwa na kulia ni Mkuu wa mkoa wa Dar es alaam William Lukuvi na anayefuata ni Naibu Waziri wa Wizara ya Miundombinu Ezekiel Chiburunje Uzinduzi huo umefanyika leo asubuhi eneo la Ferri.
Rais Jakaya Kikwete akishuka kutoka ndani ya Kivuko mara baada ya kukizindua rasmi huku akiongozwa na wasaidizi wake, kulia ni Waziri wa Ardhi na Makazi Mh. John Chiligati na Nyuma ya Rais jakaya kushoto ni Waziri wa Miundombinu Mh. Shukuru kawambwa wananchi wa mkoa wa Dar es alaam wakiwa wamekusanyika eneo la Kigamboni tayari kwa kumpokea Mh. Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya kuzindua kivuko cha MV. Magogoni leo.
Kap. John Komba na kundi zima la TOT wakitumbuiza kwa nyimbo za kwaya kabla ya mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kuwasili eneo la Ferri Kigamboni tayari kwa kuzindua Kivuko cha MV Magogoni leo asubuhi.
Msomaji
Dar es salaam