Saturday, July 24, 2010

Kiongozi wa CCM tawi la Marekani akutana na Mh Rais Kikwete

Bi Zainab Janguo Katibu wa siasa na uenezi wa CCM tawi la Marekani akiwa katika picha na Mh Rais Jakaya Kikwete katika Ikulu ndogo ya Chamwino, Dodoma.

Friday, July 9, 2010

CCM has picked Dr Ali Mohamed Shein as the party's presidential candidate for Zanzibar.



THE National Executive Committee of Chama Cha Mapinduzi (CCM-NEC) Friday night overwhelmingly elected the Vice-President of the United Republic of Tanzania, Dr Ali Mohamed Shein, as the ruling party’s presidential candidate for Zanzibar. Dr Shein scooped 117 votes, beating by far the former Zanzibar Chief Minister, Dr Mohamed Gharib Bilal, who garnered 54 votes. The Chief Minister, Mr Shamsi Vuai Nahodha, managed 33 votes. The results culminated the hot race that involved 11 presidential nominees who were trimmed down to five before being pruned to three. Others in the list were the Deputy Chief Minister Ali Juma Shamuhuna, Zanzibar Education and Vocational Training Minister Haroun Ali Suleiman, prominent businessman Mohammed Raza Dharamshi, Chumbuni MP Omar Sheha Mussa and a civil servant, Mr Hamad Bakar Mshindo. The rest were Mr Mohamed Yussuf Mshamba, Ambassador Ali Karume and the Deputy Minister for East African Cooperation, Mr Mohamed Aboud Mohamed. Speaking shortly after the election, Dr Shein promised to strengthen the Union and promote unity and peace in the Isles. He also said that he would lead the country with wisdom, promising speedy development in Zanzibar in collaboration with President Jakaya Kikwete. Dr Shein thanked CCM members for electing him, saying all nominees had competence and merits to be flag bearers of the party in Zanzibar presidential race. He called for solidarity and unity among the party’s members to enable the party emerge with landslide victory in the forthcoming general elections in October. Dr Shein will be pitted in the Isles race against the Secretary General of the Civic United Front (CUF), Mr Seif Shariff Hamad. According to the CCM Publicity and Ideology Secretary John Chiligati, the party’s special congress, to be held today and tomorrow, is expected to endorse the name of President Jakaya Kikwete as the party’s presidential candidate for the presidency of the United Republic of Tanzania. Although Mr Kikwete, who is the incumbent president, has no opponent, the congress will still conduct a democratic vote. He also said that the running mate of the union presidential candidate is also going to be introduced to the party’s congress tomorrow evening. Mr Kikwete, who enjoys massive backing from the more than 2,000 ruling party delegates, is expected to get overwhelming support in the vote.


Source: DAILY NEWS in Dodoma

Thursday, July 8, 2010

Bi Zainab Janguo kuwakilisha CCM Marekani huko Dodoma

Katibu wa uenezi na siasa wa CCM tawi la Marekani Bi. Zainab Janguo ameondoka hapa nchini kuelekea mjini Dodoma kuhudhuria mkutano mkuu wa 9 wa CCM unaotarajiwa kuanza hapo Julai 10 na 11 mjini humo. Mwakilishi huyo wa CCM tawi la Marekani ameondoka hapa kufuatia mwaliko wa kuhudhuria mkutano huo katika barua iliyotumwa na kusainiwa na Katibu Mkuu wa CCM Mh. Yusuf R. Makamba.
Bi Janguo pia anatarajiwa kuanza ziara ya kimafunzo kwa vitendo katika idara mbalimbali za chama kwa muda wa wiki tatu baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu huo. CCM tawi la Marekani linamtakia mwakilishi wetu safari na uwakilishi mwema katika mkutano huo.

Monday, June 21, 2010


Mbio za urais zaanza, Kikwete wa kwanza

Jakaya Kikwete amechukua fomu ya kuwania kugombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa miaka mitano ijayo katika sherehe zilizopambwa na shamrashamra na vijembe vya Katibu Mkuu wa Chama hicho, Yusuf Makamba. Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, alikabidhiwa fomu yake saa 5.38 asubuhi makao makuu ya CCM mjini hapa na Msimamizi wa Uchaguzi wa CCM, Makamba aliyetabiri kuwa Mwenyekiti wake, anaweza kuwa mgombea pekee wa chama hicho. Makamba alisema kabla na baada ya kumkabidhi Rais Kikwete fomu kuwa anaweza kuwa mgombea pekee baada ya mwanachama mwingine aliyetangaza nia, Mbunge wa Maswa, John Shibuda, kujiondoa katika mchakato huo. “Hili ni tukio kubwa na ndiyo tumeanza safari ya kwenda Ikulu,” Makamba aliuambia mkusanyiko wa wana-CCM wakiwamo wabunge, mawaziri, wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM, wenyeviti wa mikoa na wananchi wengine. “Ipo dalili kuwa utakuwa peke yako, tutakutuma wewe, ipo dalili wengine hawatakuja,” alisema Makamba akimweleza Rais Kikwete kabla ya kueleza kuwa Shibuda alishaondoa nia yake na kutokana na hilo, mbunge huyo wa Maswa aliyekuwa kwenye shughuli ya jana, aliitwa mbele ya meza kuu na kupeana mkono na Rais Kikwete. Makamba hakuishia hapo kwa vijembe na kauli zake zilizosisimua uchukuaji huo wa fomu, kwani kabla ya Rais Kikwete kutoa hotuba yake, alitumia muda mwingi kujitetea katika rafu zilizoanza kuchezwa katika majimbo ya wabunge wa CCM, ambazo zililalamikiwa hivi karibuni katika kikao cha wabunge wa CCM kabla ya Bunge la Bajeti kuanza ambalo ni la mwisho kabla ya Uchaguzi Mkuu. Mtendaji huyo wa CCM licha ya kukiri kupokea malalamiko ya wabunge hao, lakini alisema si yeye wala Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara, Pius Msekwa au Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM anayewatia kiburi wanachama hao waliotangaza nia, hivyo taratibu za chama zitachukua mkondo wake na asilaumiwe yeye. “Chonde chonde akina Msekwa chukueni hatua…nami mwenzenu niokoeni, wapo waliotusaidia wameandika malalamiko, tuyafanyie kazi. Yapo kwa Msekwa, nimekupa (akimwambia Msekwa), wewe ni Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Maadili, yafanyie kazi. Mna haki ya kulalamika, kwani mkomamanga wenye makomamanga ndio unaopigwa mawe,” alisema Makamba. Lakini aliwataka wanaolalamika, wamtendee haki kwa sababu naye ni binadamu. “Ni vizuri mkayasema haya tarehe 23 (kesho) wakati wa kikao cha NEC, pale ndipo mahali pake, Mwenyekiti atakuwapo, kule (bungeni) hapana. Nami nikiulizwa, nitasema, Msekwa usikasirike,” aliongeza Makamba na kuwafanya waliohudhuria kuangua vicheko. Pia aliomba apewe nafasi ya kuzungumza katika Mkutano Mkuu wa CCM mwezi ujao kwa kumkaribisha Mwenyekiti, kwani ana ya kuzungumza kwa sababu ratiba iliyopangwa sasa, imemwengua. Rais amekubali awekwe, ndio utaratibu. Mara baada ya Makamba kumaliza kuzungumza, alimpa nafasi Rais Kikwete aliyezitaja sababu zilizomfanya awanie tena nafasi hiyo kuwa ni ushawishi wa Watanzania wengi; kufanya vizuri kwa Serikali yake katika miaka mitano iliyopita na Katiba kumruhusu kuwania tena urais. “Ushawishi wa Watanzania wengi, wana-CCM na wasiokuwa wana-CCM, wanawake kwa wanaume, vijana kwa wazee wa mikoa yote na wilaya zetu zote kwa kunitaka nigombee tena. “Pili, nimeridhika kwamba katika miaka mitano hii, pamoja na kukabiliana na changamoto nyingi, Serikali chini ya uongozi wangu imefanya kazi nzuri ya kusukuma maendeleo ya Taifa letu na kuimarisha umoja, amani na utulivu katika nchi yetu. “Na tatu, Katiba inaniruhusu, kwani naweza kuwa Rais kwa vipindi viwili mfululizo. Nimemaliza kimoja, hivyo naweza kuomba kupata kipindi kingine cha pili,” alisema Rais Kikwete ambaye kabla ya hotuba yake, kadi yake ilihakikiwa na Makamba kuona kama ni mwanachama hai na kisha akalipa papo hapo Sh milioni moja za kuchukulia fomu na hatimaye kukabidhiwa. Rais Kikwete alisema mwaka 2005 walimpa ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM na sasa anaiomba tena na kuahidi kuwa akiteuliwa, atafanya hivyo kwa dhati na hasa kama wana-CCM wakishikamana kama 2005, watapata ushindi mkubwa au kuzidi huo. Alisema Watanzania na wana-CCM ni mashahidi kwa kiasi gani amekuwa mwaminifu kwa ahadi ya kutekeleza mipango na programu mbalimbali za utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, aliyosema imetekelezwa kwa umakini mkubwa na matokeo yake yanaonekana pembe zote. Aliueleza mkusanyiko huo, kwamba amefarijika kuona kwamba wao, pamoja na wana-CCM wenzake wengine nchini, wanamwamini kwamba anafaa kuendelea kuliongoza Taifa kwa kipindi kingine cha miaka mitano. “Hayo yote ndiyo yaliyonishawishi nami kushawishika kujitokeza kuomba tena kupewa nafasi ya kuliongoza Taifa letu. Safari ile nilisema mkinichagua nitafanya kazi kwa Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya na matokeo yake tumeyaona. “Safari hii nasema mkinichagua nitawatumikia Watanzania kwa Ari Zaidi, Nguvu Zaidi na Kasi Zaidi katika dhamira yetu ya kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania. Kwa pamoja, tuzidi kusonga mbele,” alisema Rais Kikwete na kushangiliwa na watu waliokuwapo. Aliahidi kuwa akipewa nafasi ya kuwa mgombea wa CCM Oktoba mwaka huu, hatawaangusha na atatumia bidii yake yote kufanya kampeni ya kukipigania chama hicho tawala ili kipate ushindi mkubwa. Awali, kabla ya shughuli ya kukabidhi fomu kwa mgombea huyo, Makamba alisema dalili za kuomba dua ya kuwa Rais Kikwete awe mgombea pekee zilizotolewa na watu kadhaa akiwamo aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pancras Ndejembi, zimesikika. Mbali na Ndejembi, shughuli hiyo ya kuchukua fomu ilihudhuriwa pia na wazee wengine wa CCM wakiwamo Peter Kisumo, Balozi Job Lusinde na Isaac Mwisongo. Wabunge John Malecela (Mtera) ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa zamani wa CCM, Dk. Abdallah Kigoda (Handeni) na Waziri Profesa Mark Mwandosya (Rungwe Mashariki) ambao pia waliwania urais 2005, ni miongoni mwa waliokuwapo jana. Familia ya Rais Kikwete ikiongozwa na mkewe Mama Salma Kikwete na wanawe saba, wavulana wanne wakiongozwa na kaka yao, Ridhiwani Kikwete na wasichana watatu, pia walimsindikiza baba yao, kama ilivyokuwa kwa kaka yake Kikwete, Suleiman Kikwete ambaye aliongozana na mkewe, kushuhudia mwanzo wa safari ya mpendwa wao kuomba ridhaa ya kuendelea kuongoza nchi.

Sunday, June 13, 2010

Makamba warns unfaithful CCM members

CCM Secretary General Yusuph Makamba this week warned fellow members including district and regional leaders reportedly engaging in illegal distribution of membership cards, conducting underground campaigns, saying that they would be sanctioned.
“Our party’s manifesto, regulations and policy stress the need for solidarity, transparency… this is what all officials irrespective of their positions in the party should stand for,” Makamba said.
Speaking in Moshi he said such leaders could be expelled from the party, pointing out that he has received complaints, calling for solidarity and team work in strengthening the party from the grassroots level.
The Secretary General said: “Measures will be taken against those are out to tarnish the good reputation that CCM has been proud of for years.”
Makamba distributed CCM membership cards to some 152 new members who have joined the party from various parts of Kilimanjaro Region.
According to the party’s National Executive Committee( NEC) , members wishing to cast votes during the nomination process must possess the voter’s card provided by the National Electoral Commission (NEC).
The party organ said only active CCM members, implying those who have paid membership fees will be allowed to participate in the opinion poll in search for CCM candidates for elective posts during the general elections in October.
According to NEC, CCM members will cast votes to decide on their candidates on August 8 in all its branches. The ruling party has close to five million members.
The conditions have been set to enable all party members exercise their democratic right of participating in the nomination process but responsibly.

Monday, June 7, 2010

TAARIFA MAALUM YA KUSIMAMISHWA UONGOZI BW. MICHAEL NDEJEMBI




Ndugu Wanachama


Kwa niaba ya uongozi wa CCM tawi la Marekani, ninapenda kutoa taarifa kwenu kama ifuatavyo.


Siku ya tarehe 26 mei 2010 uongozi wa Chama Cha Mapinduzi Tawi la Marekani ulitoa tamko rasmi juu ya taarifa za kuitishwa kwa uchaguzi wa tawi letu hapa Marekani. Taarifa hiyo ilieleza wazi kuwa uchaguzi huo ni batili na haukutokana na maamuzi rasmi ya vikao halali vya uongozi wa tawi. Aidha, maamuzi hayo yalikua ni maamuzi ya mwenyekiti mwenyewe na hayakutokana na kikao chochote. Hata hivyo uongozi wenu wa tawi ulichukua hatua za kuwasiriana na mwenyekiti ili atoe ufafanuzi juu ya ukiukwaji wa katiba na utaratibu mzima wa uendeshaji wa tawi, kwa bahati mbaya sana mwenyekiti hakutoa ushirikiano kama ambavyo ulitarajiwa na badala yake alifanaya 'uchaguzi' wake kwa matakwa na maslahi yake yeye mwenyewe anayoyafahamu.
Kwa kuzingatia kuwa Chama Cha Mapinduzi ni taasisi na si mali ya mtu binafsi, uongozi wenu wa tawi ulikutana na kuchukua hatua kadhaa ikiwemo ya kumsimamisha uongozi Bw. Michael Ndejembi kabla hajafanya 'uchaguzi' wake na kumpa nafasi ya kujieleza dhidi ya vitendo alivyofanya.


Ndugu wanchama, taarifa hii inakazia maamuzi ya CCM tawi la Marekani ya kutoutambua 'uchaguzi' ule na hata matokeo yake. Pia tawi linawaomba radhi wanachama na wapenzi wake kwa usumbufu wowote uliojitokeza juu ya kuitishwa 'uchaguzi' huo.


Tawi lenu lipo katika mchakato wa kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi hapa Marekani ili kifikie malengo haya yafuatayo:


Kuliondoa tawi katika mtazamo wa sura ya kuwa ni mali ya mtu mmoja na kulifikisha mahali ambapo litakua ni tegemeo kubwa katika kutoa mchango wa maendeleo ya kisiasa Tanzania.


1). Kuimarisha tawi kwa kuongeza idadi ya wanachama wapya wa CCM.

2). Kueneza siasa ya Chama Cha Mapinduzi kwa wanachama na wapenzi wake.

3). Kipindi hiki kitasaidia kutoa elimu ya kutosha kwa wanachama wapya na wazamani kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo kujitayarisha kugombea nafasi za uongozi.

4). Ku-restructure kamati ya uongozi wa tawi iliyopo sasa hivi ijulikane kama 'kamati ya muda ya CCM tawi la Marekani' na kuipa ukomo usiozidi miezi 24.

5). Kuandaa uchaguzi wa viongozi wa Tawi la CCM Marekani ndani ya miezi 24 kuanzia Julai 1 mwaka huu. Hii itasaidia kutoa fursa sawa kwa wanachama mbalimbaliwaweze kushiriki siasa hata wakiwa nje ya Tanzania wanapata nafasi hiyo kwa uwazi na usawa bila ya mizengwe.


Kidumu Chama Chama Mapinduzi.

Zainab Janguo


Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi.



Sunday, June 6, 2010

MH. RAIS KIKWETE AMTEMBELEA JENERAL MSTAAFU.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya M.Kikwete jana alimtembelea mkuu wa majeshi na Jeneral mstaafu E. Mwita Kiaro aliyelazwa katika hospital ya Bugando Jijini jana. Mh rais yuko katika ziara ya siku mbili jijini humo kukagua shughuli mbali mbali za maendeleo.
Mh. Kikwete akimsikiliza Jeneral Kiaro

KARUME AFUNGUA MKUTANO WA ZNCCIA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume, akifungua Mkutano Mkuu wa mwaka Zanzibar National Chamber of Commerce Industries and Agriculture (ZNCCIA) katika Ukumbi wa Salama Hotel Bwawani, ambapo mkutano huo utakuwa na Uchaguzi wa kumpata Rais mpya wa Jumuiya hiyo. Kulia ni Rais wa Jumuiya hiyo anayemaliza muda wake, Abdallah Abass na (kushoto) ni Waziri wa Biashara,Uwekezaji na Utalii, Mh. Samia Suluhu Hassan.
Picha na Ramadhan Othman wa Ikulu, Zanzibar.

Saturday, June 5, 2010

MWAKILISHI WA ADB NA KIKWETE IKULU

Mwakilishi wa benk ya maendeleo ya Afrika Dr.Sipho Moyo amekutana na rais Kikwete leo Ikulu Jijini Dar es salaam kwa lengo la kumuaga. Dr. Sipho Moyo amemaliza muda wake wa kufanya kazi kama mwakilishi wa benk hiyo nchini Tanzania.

Monday, April 26, 2010

MAADHIMISHO YA MIAKA 46 YA MUUNGANO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akipungia mkono wananchi mbalimbali waliojitokeza kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika leo kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam ambapo wakazi mbalimbali walijitokeza katika sherehe hizo, kulia ni mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange.
Viongozi wa vyama mbalimbali pamoja na maafisa kutoka serikalini nao walikuwepo katika maadhimisho hayo.
Wageni waalikwa mbalimbali na mabalozi wakifuatilia kwa karibu kila kilichokuwa kikendelea kwenye uwanja wa Uhuru leo jijini Dar es salaam.
Wanafunzi wa shule mbalimbali jijini Dar es salaam wakicheza halaiki wakati wa maadhimisho ya miaka 46 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika leo kwenye uwanja wa Uhuru leo.

Msomaji
Dar es salaam

Saturday, April 24, 2010

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AFUNGUA KONGAMANO LA MAKATIBU MUHTASI DODOMA LEO

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi Makatibu Muhtasi kabla ya kufungua Kongamano lao kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango Mjini Dodoma, Aprili 24, 2010 Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Celina Kombani.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akihutubia wakati alipofungua kongamano la Makatibu Muhtasi kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango Mjini DOdoma
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja baada ya kufungua Kongamano la Makatibu Muhtasi kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango Mjini Dodoma Aprili 24, 2010. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Celina Kombani, na Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ndugu Maswi.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja baada ya kufungua Kongamano la Makatibu Muhtasi kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango Mjini Dodoma Aprili 24, 2010. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Celina Kombani.

Msomaji
Dar es salaam

Friday, April 23, 2010

Matukio Bungeni Dodoma Leo

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Kulia akizungumza na Mbunge wa Kwela mkoani Rukwa Christant Mzindakaya leo katika vikao vya Bungeni vinavyoendelea mjini Dodoma.
Kiongozi wa Upinzani Bungeni (kushoto) Hamad Rashid akiongea na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa Bernald Membe ambaye pia ni mbunge wa jimbo la (Mtama) na Basil Mramba Mbunge wa jimbo la (Rombo).
Mbunge wa Kinondoni (kushoto) Idd Azzan akibadilishana mawazo na mbunge wa viti maalum kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Halima Mdee .

Msomaji
Dodoma

Viongozi wa Tanzania na Msumbiji wakagua maadalizi ya uzinduzi wa daraja la umoja

Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Omari Chambo akiwa ameongozana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi za Jamii na Maendeleo ya Makazi wa Msumbiji Bi. Maria Luisa Mathe(mwenye shati jeupe) na Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu Bi. Fatma Salum Ally wakielekea sehemu ya juu ya Daraja la Umoja kukagua maandalizi ya sherehe za Uzinduzi wa Daraja hilo tarehe 12 mwezi ujao jana katika eneo la Mtambaswala wilayani Nanyumbu mpakani mwa Tanzania na Msumbiji
Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Omari Chambo (katikati) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi za Jamii na Maendeleo ya Makazi wa Msumbiji (Mwenye shati jeupe) Bi. Maria Luisa Mathe na Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu Bi. Fatma Salum Ally(kushoto) wakikagua Daraja la Umoja eneo la Mtambaswala mpakani mwa Tanzania na Msumbiji katika maandalizi ya sherehe za Uzinduzi wa Daraja hilo mwezi ujao.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Omari Chambo akiwaongoza viongozi mbalimbali kutoka wilayani Nanyumbu na Msumbiji kukagua maandalizi ya sherehe za uzinduzi wa daraja hilo katika eneo la chini ya Daraja la Umoja lililojengwa kwa Ushirikiano kati ya Tanzania na Msumbiji katika eneo la Mtambaswala wilayani Nanyumbu jana.

Msomaji
Nanyumbu

Thursday, April 22, 2010

WANAVYUO DODOMA WAJIUNGA NA JUMUIYA YA WAZAZI YA CCM

Mwenyekiti wa Jumuia ya wazazi nchini balozi Athmani Mhina akimkaribisha makamu wa Rais Dk Ali Mohamed shein katika ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma ambapo Dk Shein alifungua mkutano Mkuu maalum wa Jumuia ya wazazi leo.
Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano mkuu maalum wa baraza la jumuia ya wazazi mjini Dodoma leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuia ya wazazi balozi Athumani Mhina na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuia hiyo Dogo Idd Mbarouk.
Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano mkuu maalum wa baraza la jumuia ya wazazi mjini Dodoma leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuia ya wazazi balozi Athumani Mhina na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuia hiyo Dogo Idd Mbarouk.

Msomaji
Dodoma

Matukio Bungeni Dodoma Leo

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mwantumu Mahiza (mwenyemiwani) akiwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) leo wakati wanafunzi hao walipokwenda kuangalia maeneo mbalimbali ya shughuli za Bunge mjini Dodoma leo. Mwenyekiti wa Kamati za Mahesabu za Mashirika ya Umma Zitto Kabwe leo Bungeni akitoa taarifa ya Kamati za Hesabu za Mashirika ya Umma pamoja na mapendekezo na maoni yaliyomo kwenye taarifa . Picha na Mwanakombo Jumaa.
Mbunge wa Mtera Johhn Malecela Akichangia sheria ya Malisho na vyakula vya mifugo
Mbunge wa Monduli Edward Lowassa (kulia) akimsikiliza Mbunge wa Kiteto Benedict Nangoro (kushoto) leo ndani ya Ukumbi wa Bunge -Dodoma. Picha na Mwanakombo Jumaa
waziri wa Madini na Nishati William Ngeleja (kulia) na Naibu Waziri wa Madini na Nishati Adam Malima wakizungumza leo katika viwanja vya Bunge Dodoma baada ya Waziri Ngeleja kuwasilisha Muswada wa Sheria ya Madini wa Mwaka 2010.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza Wa Rais (Muungano) Muhammed Seif Khatib (kushoto) akizungumza na waandishi wa Habari Dododma leo kuhusu mambo mbalimbali ya Muungano. Mwengine ni Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano.
Msomaji
Dodoma

Monday, April 12, 2010

Rais Jakaya Kikwete alipopokea ujumbe maalumu na mchango kutoka UVCCM mkoa wa Shinyanga

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akikabidhi kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete mchango wa jumla ya Tshs.1,482,200/- kutoka kwa jumuiya ya umoja wa vijana mkoa wa Shinyanga kwaajili ya fomu ya ugombea urais ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete.Makabidhiano hayo yalifanyika jana jioni ikulu jijini Dar es Salaam na kushudiwa na viongozi wote wa CCM mkoa wa Shinyanga.Kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Stephen Julius Masele amnaye pia alisoma ujumbe maalumu wa vijana wa mkoa wa Shinyanga.
Viongozi wa CCM Mkoa wa Shinyanga wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni

Msomaji
Dar es salaam
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete, katibu Mkuu wa CCM Yusuf Makamba(katikati) na makamu mwenyekiti CCM Bara Pius Msekwa(kulia) wakituma ujumbe mfupi sms kupitia simu zao ili kuchangia CCM wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia CCM kupitia simu za mikononi ulifanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar
Habari zaidi kutoka Magazetini:
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kinatarajia kutumia Sh bilioni 1.5 kukodishia helikopta na ndege katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Fedha hizo ni kati ya Sh bilioni 40 wanazotarajia kuchangisha kwa ajili ya uchaguzi huo kupitia wanachama wake kwa njia ya ujumbe mfupi, akaunti ya benki na harambee.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Rais Jakaya Kikwete wakati akizindua rasmi kampeni za uchangiaji wa chama katika hafla iliyofanyika juzi usiku na kuwashirikisha viongozi wa juu wa chama hicho.

Kikwete alisema wameamua kukodisha helikopta na ndege ili kuepuka adha walizokuwa wakikumbana nazo katika kampeni za uchaguzi uliopita.

Mbali na ndege, pia Kikwete alisema kuwa katika malengo yao ya kuchangisha Sh bilioni 40 tayari wamepata Sh bilioni 4.8 ambazo zimechangishwa kupitia akaunti namba 01j1005069306 katika Benki ya CRDB.

CCM inatarajia kukusanya Sh bilioni 4.4 kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS) ambapo muda mfupi baada ya kuzindua kampeni hiyo, SMS 20,000 zilitumwa katika kipindi kifupi kisichozidi saa nne.

Katika njia hiyo wachangiaji wanatakiwa kutuma neno CCM kwenda namba 15399 ambapo watakuwa wamechangia Sh 1000 na wakituma kwenda namba 15388 watachangia Sh 500 na kwenda namba 15377 watachangia Sh 300.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Uchangiaji na Katibu wa Uchumi na Fedha wa chama hicho, Amos Makala alisema kuwa CCM ina wagombea 2,932 katika ngazi zote nchi nzima.

Alisema kuwa kwa kuwa ndio chama pekee kinachosimamisha wagombea katika ngazi zote za uchaguzi, kinatarajiwa kutumia Sh bilioni 3 katika kuendesha shughuli za kuchagua wagombea watakaogombea nafasi mbalimbali.

Alisema kuwa Sh bilioni 5 zinahitajika kwa ajili ya kununulia magari 26 kwa Tanzania bara huku Zanzibar ikihitaji magari 60. Pia watanunua pikipiki elfu sabini pamoja na baiskeli elfu 25 ambapo kwa pamoja itagharimu Sh bilioni 2.5.

Makala alisema kuwa kwa ujumla gharama ilitakiwa kuwa Sh bilioni 50 lakini magari yaliyopo katika ngazi za wilaya yamepunguza gharama mpaka kufikia Sh bilioni 40.

" Najua kwa kuwa CCM ndio chama ambacho kimekuwa kikiongoza nchi kwa muda mrefu, naona kuwa inatakiwa wanachama na wale wanaokitakia mema chama kutumia njia zilizo sahihi kwao kutuchangia fedha kwa ajili ya uchaguzi huu,” alisema Makala.

Alifafanua zaidi kuwa Sh bilioni 10 zinahitajika kwa njia ya harambee ambapo alisema kuwa kampeni ya kupata fedha kwa njia hiyo itazinduliwa.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha, Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi na mawaziri wakuu wastaafu akiwemo Edward Lowassa, John Malecela na David Msuya.

UCHAGUZI 2010!!

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, akibonyeza kitufe kwenye kompyuta ndogo kuashiria uzinduzi wa uchangiaji kupitia simu za mikononi (CCM Mobile System) Dar es Salaam juzi usiku. Mfumo huo utawawezesha wanachama na wapenzi wa chama hicho kukichangia fedha kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao baadaye mwezi Oktoba kwa kujiunga na namba 15016. Kwa mujibu wa Kikwete, chama kimepanga kukusanya shilingi bilioni 40 kufanikisha uchaguzi mkuu. Anayeshuhudia ni Katibu Mkuu wa CCM-Taifa, Yusuf Makamba.