Monday, April 26, 2010

MAADHIMISHO YA MIAKA 46 YA MUUNGANO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akipungia mkono wananchi mbalimbali waliojitokeza kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika leo kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam ambapo wakazi mbalimbali walijitokeza katika sherehe hizo, kulia ni mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange.
Viongozi wa vyama mbalimbali pamoja na maafisa kutoka serikalini nao walikuwepo katika maadhimisho hayo.
Wageni waalikwa mbalimbali na mabalozi wakifuatilia kwa karibu kila kilichokuwa kikendelea kwenye uwanja wa Uhuru leo jijini Dar es salaam.
Wanafunzi wa shule mbalimbali jijini Dar es salaam wakicheza halaiki wakati wa maadhimisho ya miaka 46 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika leo kwenye uwanja wa Uhuru leo.

Msomaji
Dar es salaam

Saturday, April 24, 2010

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AFUNGUA KONGAMANO LA MAKATIBU MUHTASI DODOMA LEO

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi Makatibu Muhtasi kabla ya kufungua Kongamano lao kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango Mjini Dodoma, Aprili 24, 2010 Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Celina Kombani.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akihutubia wakati alipofungua kongamano la Makatibu Muhtasi kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango Mjini DOdoma
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja baada ya kufungua Kongamano la Makatibu Muhtasi kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango Mjini Dodoma Aprili 24, 2010. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Celina Kombani, na Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ndugu Maswi.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja baada ya kufungua Kongamano la Makatibu Muhtasi kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango Mjini Dodoma Aprili 24, 2010. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Celina Kombani.

Msomaji
Dar es salaam

Friday, April 23, 2010

Matukio Bungeni Dodoma Leo

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Kulia akizungumza na Mbunge wa Kwela mkoani Rukwa Christant Mzindakaya leo katika vikao vya Bungeni vinavyoendelea mjini Dodoma.
Kiongozi wa Upinzani Bungeni (kushoto) Hamad Rashid akiongea na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa Bernald Membe ambaye pia ni mbunge wa jimbo la (Mtama) na Basil Mramba Mbunge wa jimbo la (Rombo).
Mbunge wa Kinondoni (kushoto) Idd Azzan akibadilishana mawazo na mbunge wa viti maalum kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Halima Mdee .

Msomaji
Dodoma

Viongozi wa Tanzania na Msumbiji wakagua maadalizi ya uzinduzi wa daraja la umoja

Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Omari Chambo akiwa ameongozana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi za Jamii na Maendeleo ya Makazi wa Msumbiji Bi. Maria Luisa Mathe(mwenye shati jeupe) na Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu Bi. Fatma Salum Ally wakielekea sehemu ya juu ya Daraja la Umoja kukagua maandalizi ya sherehe za Uzinduzi wa Daraja hilo tarehe 12 mwezi ujao jana katika eneo la Mtambaswala wilayani Nanyumbu mpakani mwa Tanzania na Msumbiji
Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Omari Chambo (katikati) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi za Jamii na Maendeleo ya Makazi wa Msumbiji (Mwenye shati jeupe) Bi. Maria Luisa Mathe na Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu Bi. Fatma Salum Ally(kushoto) wakikagua Daraja la Umoja eneo la Mtambaswala mpakani mwa Tanzania na Msumbiji katika maandalizi ya sherehe za Uzinduzi wa Daraja hilo mwezi ujao.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Omari Chambo akiwaongoza viongozi mbalimbali kutoka wilayani Nanyumbu na Msumbiji kukagua maandalizi ya sherehe za uzinduzi wa daraja hilo katika eneo la chini ya Daraja la Umoja lililojengwa kwa Ushirikiano kati ya Tanzania na Msumbiji katika eneo la Mtambaswala wilayani Nanyumbu jana.

Msomaji
Nanyumbu

Thursday, April 22, 2010

WANAVYUO DODOMA WAJIUNGA NA JUMUIYA YA WAZAZI YA CCM

Mwenyekiti wa Jumuia ya wazazi nchini balozi Athmani Mhina akimkaribisha makamu wa Rais Dk Ali Mohamed shein katika ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma ambapo Dk Shein alifungua mkutano Mkuu maalum wa Jumuia ya wazazi leo.
Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano mkuu maalum wa baraza la jumuia ya wazazi mjini Dodoma leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuia ya wazazi balozi Athumani Mhina na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuia hiyo Dogo Idd Mbarouk.
Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano mkuu maalum wa baraza la jumuia ya wazazi mjini Dodoma leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuia ya wazazi balozi Athumani Mhina na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuia hiyo Dogo Idd Mbarouk.

Msomaji
Dodoma

Matukio Bungeni Dodoma Leo

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mwantumu Mahiza (mwenyemiwani) akiwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) leo wakati wanafunzi hao walipokwenda kuangalia maeneo mbalimbali ya shughuli za Bunge mjini Dodoma leo. Mwenyekiti wa Kamati za Mahesabu za Mashirika ya Umma Zitto Kabwe leo Bungeni akitoa taarifa ya Kamati za Hesabu za Mashirika ya Umma pamoja na mapendekezo na maoni yaliyomo kwenye taarifa . Picha na Mwanakombo Jumaa.
Mbunge wa Mtera Johhn Malecela Akichangia sheria ya Malisho na vyakula vya mifugo
Mbunge wa Monduli Edward Lowassa (kulia) akimsikiliza Mbunge wa Kiteto Benedict Nangoro (kushoto) leo ndani ya Ukumbi wa Bunge -Dodoma. Picha na Mwanakombo Jumaa
waziri wa Madini na Nishati William Ngeleja (kulia) na Naibu Waziri wa Madini na Nishati Adam Malima wakizungumza leo katika viwanja vya Bunge Dodoma baada ya Waziri Ngeleja kuwasilisha Muswada wa Sheria ya Madini wa Mwaka 2010.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza Wa Rais (Muungano) Muhammed Seif Khatib (kushoto) akizungumza na waandishi wa Habari Dododma leo kuhusu mambo mbalimbali ya Muungano. Mwengine ni Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano.
Msomaji
Dodoma

Monday, April 12, 2010

Rais Jakaya Kikwete alipopokea ujumbe maalumu na mchango kutoka UVCCM mkoa wa Shinyanga

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akikabidhi kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete mchango wa jumla ya Tshs.1,482,200/- kutoka kwa jumuiya ya umoja wa vijana mkoa wa Shinyanga kwaajili ya fomu ya ugombea urais ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete.Makabidhiano hayo yalifanyika jana jioni ikulu jijini Dar es Salaam na kushudiwa na viongozi wote wa CCM mkoa wa Shinyanga.Kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Stephen Julius Masele amnaye pia alisoma ujumbe maalumu wa vijana wa mkoa wa Shinyanga.
Viongozi wa CCM Mkoa wa Shinyanga wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni

Msomaji
Dar es salaam
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete, katibu Mkuu wa CCM Yusuf Makamba(katikati) na makamu mwenyekiti CCM Bara Pius Msekwa(kulia) wakituma ujumbe mfupi sms kupitia simu zao ili kuchangia CCM wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia CCM kupitia simu za mikononi ulifanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar
Habari zaidi kutoka Magazetini:
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kinatarajia kutumia Sh bilioni 1.5 kukodishia helikopta na ndege katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Fedha hizo ni kati ya Sh bilioni 40 wanazotarajia kuchangisha kwa ajili ya uchaguzi huo kupitia wanachama wake kwa njia ya ujumbe mfupi, akaunti ya benki na harambee.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Rais Jakaya Kikwete wakati akizindua rasmi kampeni za uchangiaji wa chama katika hafla iliyofanyika juzi usiku na kuwashirikisha viongozi wa juu wa chama hicho.

Kikwete alisema wameamua kukodisha helikopta na ndege ili kuepuka adha walizokuwa wakikumbana nazo katika kampeni za uchaguzi uliopita.

Mbali na ndege, pia Kikwete alisema kuwa katika malengo yao ya kuchangisha Sh bilioni 40 tayari wamepata Sh bilioni 4.8 ambazo zimechangishwa kupitia akaunti namba 01j1005069306 katika Benki ya CRDB.

CCM inatarajia kukusanya Sh bilioni 4.4 kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS) ambapo muda mfupi baada ya kuzindua kampeni hiyo, SMS 20,000 zilitumwa katika kipindi kifupi kisichozidi saa nne.

Katika njia hiyo wachangiaji wanatakiwa kutuma neno CCM kwenda namba 15399 ambapo watakuwa wamechangia Sh 1000 na wakituma kwenda namba 15388 watachangia Sh 500 na kwenda namba 15377 watachangia Sh 300.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Uchangiaji na Katibu wa Uchumi na Fedha wa chama hicho, Amos Makala alisema kuwa CCM ina wagombea 2,932 katika ngazi zote nchi nzima.

Alisema kuwa kwa kuwa ndio chama pekee kinachosimamisha wagombea katika ngazi zote za uchaguzi, kinatarajiwa kutumia Sh bilioni 3 katika kuendesha shughuli za kuchagua wagombea watakaogombea nafasi mbalimbali.

Alisema kuwa Sh bilioni 5 zinahitajika kwa ajili ya kununulia magari 26 kwa Tanzania bara huku Zanzibar ikihitaji magari 60. Pia watanunua pikipiki elfu sabini pamoja na baiskeli elfu 25 ambapo kwa pamoja itagharimu Sh bilioni 2.5.

Makala alisema kuwa kwa ujumla gharama ilitakiwa kuwa Sh bilioni 50 lakini magari yaliyopo katika ngazi za wilaya yamepunguza gharama mpaka kufikia Sh bilioni 40.

" Najua kwa kuwa CCM ndio chama ambacho kimekuwa kikiongoza nchi kwa muda mrefu, naona kuwa inatakiwa wanachama na wale wanaokitakia mema chama kutumia njia zilizo sahihi kwao kutuchangia fedha kwa ajili ya uchaguzi huu,” alisema Makala.

Alifafanua zaidi kuwa Sh bilioni 10 zinahitajika kwa njia ya harambee ambapo alisema kuwa kampeni ya kupata fedha kwa njia hiyo itazinduliwa.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha, Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi na mawaziri wakuu wastaafu akiwemo Edward Lowassa, John Malecela na David Msuya.

UCHAGUZI 2010!!

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, akibonyeza kitufe kwenye kompyuta ndogo kuashiria uzinduzi wa uchangiaji kupitia simu za mikononi (CCM Mobile System) Dar es Salaam juzi usiku. Mfumo huo utawawezesha wanachama na wapenzi wa chama hicho kukichangia fedha kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao baadaye mwezi Oktoba kwa kujiunga na namba 15016. Kwa mujibu wa Kikwete, chama kimepanga kukusanya shilingi bilioni 40 kufanikisha uchaguzi mkuu. Anayeshuhudia ni Katibu Mkuu wa CCM-Taifa, Yusuf Makamba.

Friday, April 9, 2010

Rais Jakaya Mrisho Kikwete aongoza kikao cha pamoja cha wajumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa, wenyeviti na makatibu wa CCM wa wilaya

Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua kikao cha pamoja cha wajumbe wa Halmashauri kuu ya taifa, wenyeviti na makatibu wa CCM wa wilaya uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam leo asubuhi Baadhi ya wajumbe walioudhulia katika kikao cha pamoja cha wajumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa, wenyeviti na makatibu wa CCM wilaya

Msomaji
Dar es salaam

Thursday, April 8, 2010

Rais Kikwete aongoza kikao cha NEC Karimjee

Mwenyekiti a CCM, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya chipukizi wa CCM muda mfupi baada ya kuwasili katika viwanja vya Karimjee ambapo aliongoza kikao cha Halmashauri kuu ya taifa ya CCM (NEC).
Mwenyekiti wa CCm Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Zanzibar Amani Abeid Karume na Katibu mkuu wa CCM Bwana Yusuf Makamba wakiingia katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam tayari kuanza kwa kikao cha Halmashauri kuu ya taifa ya CCM (NEC).
Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM NEC wakiwa katika kikao chao leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam
Msomaji
Dar es salaam

Wednesday, April 7, 2010

Rais Jakaya Mrisho Kikwete(Watano kulia) Rais Wa Zanzibar Amani Abeid Karume (Wasita kulia),pamoja viongozi wengine wa kitaifa wakiomba dua katika kaburi la muasisi wa mapinduzi ya Zanzibar Hayati Mzee Abeid Amani Karume huko katika ofisi kuu ya CCm Kisiwandui Zanzibar leo asubuhi.wengine katika picha kutoka kushoto Naibu Waziri kiongozi wa SMZ Ali Juma Shamuhuna,Naibu Katibu mkuu CCM Zanzibar Salehe Ramadhani Feruzi,Waziri kiongozi wa SMZ Shamsi Vuai Nahodha, na makamu wa Rais Dr.Ali Mohamed Shein.
Maghorofa mpya yaliyopo mtaa wa Michenzani Zanzibar yaliyoanza kujengwa kwaajili ya makazi bora ya Wananchi wa Zanzibar na hayati Mzee Abeid Amani Karume na kukamilishwa na Rais wa sasa Amani Abeid Karume.Makazi hayo tayari yamenza kugawanywa kwa wananchi waliokusudiwa kwa utaratibu maalumu
Msomaji
Zanzibar

Rais Kikwete ayapokea maandamano ya UVCCM ya kumuenzi marehemu Mzee Abeid Karume Zanzibar


Rais Jakaya mrisho Kikwete, Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar(kulia) na Mwenyekiti wa jumuiya ya umojawa Vijana wa CCM Bwana Yusuf Masauni wakati wa mapokezi ya maandamano ya umoja wa vijana wa CCM mjini Zanzibar jana jioni.
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete Mwenyekiti wa Jumuiya ya umoja wa Vijana CCM Yusuf Masauni(wapili kushoto), Makamu mwenyekiti wa jumuiya hiyo Bwana Beno Malisa(kushoto), na katibu mkuu wa jumuiya ya umoja wa Vijana CCM Bwana Martin Shigela wakiyapokea maandamano ya vijana wa CCM katika viwanja vya CCM Maisara Zanzibar jana jioni.Rais Jakaya Kikwete ambaye ndiye aliyekuwa mgeni Rasmi katika maandamano hayo aliwahutubia vijana hao.
Baadhi ya vijana wananchama wa UVCCM wakishangilia hotuba ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliyoitoa wakati wa kilele cha maandamano yaliyoandaliwa na jumuiya hiyo mjini Zanzibar kumuenzi muasisi wa mapinduzi ya zanzibar marehemu Mzee Abeid Amani Karume.
Mjane wa Muasisi wa mapinduzi ya Zanzibar Mama Fatma Karume pamoja na mke wa Rais wa Zanzibar Mama Shadya Karume wakati wa dua ya kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliyosomwa wakati wa kilele cha maandamano ya UVCCM kumuenzi muasisi huyo jana mjini Zanzibar.
Msimaji
Zanzibar